Nipo njiapanda, msaada wenu wanaJF

trica

Member
Aug 31, 2020
73
154
Wakuu nilimaliza chuo mwaka 2018, nilitafuta ajira mpaka nikahisi kukata tamaa, Mungu amtupi mja wake nikabahatika kupata kazi katika kampuni binafsi uko mkoani (nje ya Dar es Salaam) hiyo kazi ni project tu ya miaka miwili, ile kazi nilifanya vizuri mpaka ikaisha kwa uaminifu mkubwa kabisa, katika kujichanga changa mpaka project inamalizika nikawa nimejichanga changa mpaka kupata kiasi flani cha pesa, nilikuwa na kiwanja maeneo ya Dar nikaweka msingi wa nyumba ya ramani niliokuwa nayo (nyumba simple, ambayo naamini uko mbeleni haiwezi nisumbua kujenga kwa kudunduliza).

Ndugu zangu nadhani mnajua sisi vijana tunakuwa na matamanio mengi sana kwenyee hii dunia, ususani sisi vijana wenye hizi age za miaka 25s-35 kunakuwa na matamanio makubwa ya kumiliki gari na nyumba nzuri, sasa kilichofuata pesa nyingine nikanunua gari aina ya IST niliagiza from japan (online buy).

Wakuu mpaka nakuja kuomba ushauri kwenu ni ili suala, Kwa sasa sina tena kazi yoyote ile ya kuniingizia kipato kabisa, maana ile project imesha isha kabisa, na kwenye account yangu nina shilingi milion moja tuu.

Naombeni ushauri wenu wa dhati kabisa, nifanyeje ili niweze japo kuiona kesho yangu ikiwa njema, sijui hii milion moja nafanyia nini ili niweze kutoka, na sijajua hii gari naifanyeje ili iweze kunitoa kimaisha, nimebaki kwenye wimbi kubwa la mawazo (kuna muda najutia kununua gari, ila imesha tokea na kuna muda mwingine nikiliangalia gari yangu naona kama sijafanya maamuzi baya sana maana nalipenda).

Sina mke wala mtoto, na nipo Dar es Salaam kwa sasa, niliwaza kuliingiza gari kwenye uber.. uko nako sijui kukoje

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu ambao siku nikikaa ntaona kabisa kweli jamiiforum ilinitoa sehemu mmoja kunipeleka sehemu nyingine, mbalikiwe sana.

Karinuni
 
Ulisomea fani mkuu? Kama ni ujenzi usiuze gari fanyia kazi kupata kazi,
Kama ni fani nyingine pia usiuze gari kwa hali uliyonayo maana utauza kwa shida n hela itakua ndogo
 
Usiuze gari ,ingia barabarani mwenyewe ,watu wanakodi magari kwa maboss kufanya taxi au Uber na Kila mwezi wanapeleka mahesabu na familia zao zinaishi na mipango inaenda sembuse we mwenye gari na boss ni wewe mwenyewe ,endesha mwenyewe usione aibu kuwa dereva taxi maana wasomi wengi wanaona aibu na wanachagua kazi ndo maana wanafeli .

Piga kazi ya kuendesha tafuta maeneo yenye abiria kama bandarini ,ukijali wateja watakuzoea utakuwa unapigiwa simu kutoa huduma ,huku ukiendelea kutafuta kazi nyingine
 
sijasema naogopa mkuu, ila sijajua ipoje iyo biashara, nayo pia napokea mawazo ya iyo biashara mkuu
Sasa usiogope basi mkuu, hiyo gari uliyonayo ndio mtaji pekee ulionao sasa hivi, hiyo milioni moja iache kama ilivyo bank, pambana ujifunze biashara ya uber kisha ingia barabarani. Uzuri huna mke wala mtoto unaweza fanya kazi hata masaa 23 kwa siku na ukapumzika kesho yake kutwa. Baada ya mwaka utajikuta hela benki zimeongezeka na gari bado unayo. Utakuwa katika nafasi ya kuamua biashara ingine.
 
Usiuze gari ,ingia barabarani mwenyewe ,watu wanakodi magari kwa maboss kufanya taxi au Uber na Kila mwezi wanapeleka mahesabu na familia zao zinaishi na mipango inaenda sembuse we mwenye gari na boss ni wewe mwenyewe ,endesha mwenyewe usione aibu kuwa dereva taxi maana wasomi wengi wanaona aibu na wanachagua kazi ndo maana wanafeli .

Piga kazi ya kuendesha tafuta maeneo yenye abiria kama bandarini ,ukijali wateja watakuzoea utakuwa unapigiwa simu kutoa huduma ,huku ukiendelea kutafuta kazi nyingine
asante sana mkuu kwa maoni yako, ntafanyia kazi mkuu
 
Mkuu mimi naona uza gari tafuta biashara nzuri, Kiwanja ni asset usiuze, biashara ikifanikiwa utajenga
 
Sasa usiogope basi mkuu, hiyo gari uliyonayo ndio mtaji pekee ulionao sasa hivi, hiyo milioni moja iache kama ilivyo bank, pambana ujifunze biashara ya uber kisha ingia barabarani. Uzuri huna mke wala mtoto unaweza fanya kazi hata masaa 23 kwa siku na ukapumzika kesho yake kutwa. Baada ya mwaka utajikuta hela benki zimeongezeka na gari bado unayo. Utakuwa katika nafasi ya kuamua biashara ingine.
asante sana kaka kwa mawazo yako, ubarikiwe sana mkuu
 
Gari ulinunua ili uendee wapi ikiwa kazi ilishaisha au kutembea ndugu.

We need to create channels first then to buy motorcar for reaching those channel Fred Vunjabei, Diamond, MO wanahitaji gari.
Mkuu ni ujana tuu, ndio maana nikaelezea sana hapo juu, sitaki kuanza kujutia kwa maamuzi nilio chukua ila ndio imetokea tayari inatakiwa nitoke hapa nilipo nisogee mbele zaidi kwa kutatua tatizo
 
Back
Top Bottom