Nipo njiapanda, msaada wenu wanaJF

Nipo njiapanda, msaada wenu wanaJF

Wakuu nilimaliza chuo mwaka 2018, nilitafuta ajira mpaka nikahisi kukata tamaa, Mungu amtupi mja wake nikabahatika kupata kazi katika kampuni binafsi uko mkoani (nje ya Dar es Salaam) hiyo kazi ni project tu ya miaka miwili, ile kazi nilifanya vizuri mpaka ikaisha kwa uaminifu mkubwa kabisa, katika kujichanga changa mpaka project inamalizika nikawa nimejichanga changa mpaka kupata kiasi flani cha pesa, nilikuwa na kiwanja maeneo ya Dar nikaweka msingi wa nyumba ya ramani niliokuwa nayo (nyumba simple, ambayo naamini uko mbeleni haiwezi nisumbua kujenga kwa kudunduliza).

Ndugu zangu nadhani mnajua sisi vijana tunakuwa na matamanio mengi sana kwenyee hii dunia, ususani sisi vijana wenye hizi age za miaka 25s-35 kunakuwa na matamanio makubwa ya kumiliki gari na nyumba nzuri, sasa kilichofuata pesa nyingine nikanunua gari aina ya IST niliagiza from japan (online buy).

Wakuu mpaka nakuja kuomba ushauri kwenu ni ili suala, Kwa sasa sina tena kazi yoyote ile ya kuniingizia kipato kabisa, maana ile project imesha isha kabisa, na kwenye account yangu nina shilingi milion moja tuu.

Naombeni ushauri wenu wa dhati kabisa, nifanyeje ili niweze japo kuiona kesho yangu ikiwa njema, sijui hii milion moja nafanyia nini ili niweze kutoka, na sijajua hii gari naifanyeje ili iweze kunitoa kimaisha, nimebaki kwenye wimbi kubwa la mawazo (kuna muda najutia kununua gari, ila imesha tokea na kuna muda mwingine nikiliangalia gari yangu naona kama sijafanya maamuzi baya sana maana nalipenda).

Sina mke wala mtoto, na nipo Dar es Salaam kwa sasa, niliwaza kuliingiza gari kwenye uber.. uko nako sijui kukoje

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu ambao siku nikikaa ntaona kabisa kweli jamiiforum ilinitoa sehemu mmoja kunipeleka sehemu nyingine, mbalikiwe sana.

Karinuni
Uza gari
 
Usiuze gari ,ingia barabarani mwenyewe ,watu wanakodi magari kwa maboss kufanya taxi au Uber na Kila mwezi wanapeleka mahesabu na familia zao zinaishi na mipango inaenda sembuse we mwenye gari na boss ni wewe mwenyewe ,endesha mwenyewe usione aibu kuwa dereva taxi maana wasomi wengi wanaona aibu na wanachagua kazi ndo maana wanafeli .

Piga kazi ya kuendesha tafuta maeneo yenye abiria kama bandarini ,ukijali wateja watakuzoea utakuwa unapigiwa simu kutoa huduma ,huku ukiendelea kutafuta kazi nyingine
afuate ushauri huu, hii komenti imefunga uzi
 
Mbona bado upo kwenye nafasi nzuri tu kiongozi, achilia mbali sisis ambao tulifanya project na kudhurumiwa tukatoka mikono mitupu ila wewe umebakiwa na mtaji, milioni ni kubwa sana, chukua laki 5 nunua photocopy machine hata kwa mtu, chukua laki mbili nunua computer hata kwa mtu fungua stationary hii inaleta faida asikwambie mtu nimeifanya kwa mda inafaida yake
 
gari usiuze asiliani, utauza bei ya njaa sana, ingiza gari kwa uber na uendeshe mwenyewe, usimpe mtu, NIMEKUONYA
 
Back
Top Bottom