Nipo njiapanda, msaada wenu wanaJF

Nipo njiapanda, msaada wenu wanaJF

Mfate mancity ashinde na goli mbili against Tottenham weka hiyo milion unapata milioni mbili

Jumanne kuna UEFA na Europa

Ndani ya week mbili unaingiza milion 3
 
duuh mkuu, aya bwana
 
duuh mkuu, aya bwana
mkuu hela ya kamari haina longo longo, ukipata umepata, ukikosa umekosa do your math well kutafuta namba za uhakika
japo hakuna hela rahisi, kwenye uwekezaji kibongobongo lazima uteseke sana
nchi ngumu sana hii
 
Igeuze hio gari uwe kama dereva taxt hio million moja utaitumia kuongezea mafuta utakuja kunishukuru 🙏
 
Hiyo milioni tengeneza business card kwa 40,000 kanunue manukato mazuri 50,000 ukipata perfume inaitwa tool Box itapendeza zaidi, nunua barakoa safi tano za light blue na nyeupe 5,000.Sanitizer 10,000.Then 5000 kanyoe usipauke. Alaf 50, 000 weka mafuta kwenye gari zunguka ofisi kubwa unazozijua muone mtu wa mapokezi mwambie wewe unatoa usafiri binafsi kama anamjua mtu hapo ofisini ambaye huwa anakodi tax mara kwa mara Kwani wewe unatoa huduma hiyo, kwa bei nafuu. Wagawie hao watu business kadi, uwaambie unatoa huduma ya usafiri binafsi kwa uaminifu,. Kuzunguka kugawa hizo business cards hadi kupata wteja na mahitaji hapo juu matumizi hayatazidi 400,000.Baada ya mwezi nenda TRA kabadilishe plate number ingia Uber. Kama wewe ni muoga wa kwenda maofisi mkubwa kagawe hizo cards chuo chochote ila jihadhari na mambo ya madem Kwani ukimtogoza tuu gari inakuwa yake na mashost zake biashara inakufa. Usitafute kijiwe cha kudum, fanya Kazi kwa sim kwanza. Kila la kheri ukipata hela unikumbuke
 
asante sana mkuu, ubarikiwe sana kwa ushauri wako.
 
Wakuu nilimaliza chuo mwaka 2018, nilitafuta ajira mpaka nikahisi kukata tamaa, Mungu amtupi mja wake nikabahatika kupata kazi katika kampuni binafsi uko mkoani (nje ya Dar es Salaam) hiyo kazi ni project tu ya miaka miwili, ile kazi nilifanya vizuri mpaka ikaisha kwa uaminifu mkubwa kabisa, katika kujichanga changa mpaka project inamalizika nikawa nimejichanga changa mpaka kupata kiasi flani cha pesa, nilikuwa na kiwanja maeneo ya Dar nikaweka msingi wa nyumba ya ramani niliokuwa nayo (nyumba simple, ambayo naamini uko mbeleni haiwezi nisumbua kujenga kwa kudunduliza).

Ndugu zangu nadhani mnajua sisi vijana tunakuwa na matamanio mengi sana kwenyee hii dunia, ususani sisi vijana wenye hizi age za miaka 25s-35 kunakuwa na matamanio makubwa ya kumiliki gari na nyumba nzuri, sasa kilichofuata pesa nyingine nikanunua gari aina ya IST niliagiza from japan (online buy).

Wakuu mpaka nakuja kuomba ushauri kwenu ni ili suala, Kwa sasa sina tena kazi yoyote ile ya kuniingizia kipato kabisa, maana ile project imesha isha kabisa, na kwenye account yangu nina shilingi milion moja tuu.

Naombeni ushauri wenu wa dhati kabisa, nifanyeje ili niweze japo kuiona kesho yangu ikiwa njema, sijui hii milion moja nafanyia nini ili niweze kutoka, na sijajua hii gari naifanyeje ili iweze kunitoa kimaisha, nimebaki kwenye wimbi kubwa la mawazo (kuna muda najutia kununua gari, ila imesha tokea na kuna muda mwingine nikiliangalia gari yangu naona kama sijafanya maamuzi baya sana maana nalipenda).

Sina mke wala mtoto, na nipo Dar es Salaam kwa sasa, niliwaza kuliingiza gari kwenye uber.. uko nako sijui kukoje

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu ambao siku nikikaa ntaona kabisa kweli jamiiforum ilinitoa sehemu mmoja kunipeleka sehemu nyingine, mbalikiwe sana.

Karinuni
anza biashara ya mtumba au chakuala, kwa kutumia gari yako. Tafuta sehemu ajiri dada awe anapika chakula then mnaenda kuuza kwenye maofisi makubwa, au mtumba unaweka kwa gari yako vizia wakati wa mchana au jioni then thanx me later in the name of Jesus
 
Nilisoma Bsc in computer science mkuu
Kazi hyo haikuwa mpango wa Allah, hasa kama ulifanya kwa uangalizi wa jicho la Mungu so fear not another chance iz coming but hold for a while
 
itoshe tu kusema.hiyo gari haina kaz kwa Sasa ukiikumbatia inaenda kula hiyo 1M dakika 0 kama huna nia ya kufanya Uber uza haraka sana na ufanye biashara unayoweza kuimudu na uisimamie mwenyewe
 
anza biashara ya mtumba au chakuala, kwa kutumia gari yako. Tafuta sehemu ajiri dada awe anapika chakula then mnaenda kuuza kwenye maofisi makubwa, au mtumba unaweka kwa gari yako vizia wakati wa mchana au jioni then thanx me later in the name of Jesus
ubarikiwe sana mkuu
 
itoshe tu kusema.hiyo gari haina kaz kwa Sasa ukiikumbatia inaenda kula hiyo 1M dakika 0 kama huna nia ya kufanya Uber uza haraka sana na ufanye biashara unayoweza kuimudu na uisimamie mwenyewe
asante kwa mawazo yako ndugu yangu
 
Wakuu nilimaliza chuo mwaka 2018, nilitafuta ajira mpaka nikahisi kukata tamaa, Mungu amtupi mja wake nikabahatika kupata kazi katika kampuni binafsi uko mkoani (nje ya Dar es Salaam) hiyo kazi ni project tu ya miaka miwili, ile kazi nilifanya vizuri mpaka ikaisha kwa uaminifu mkubwa kabisa, katika kujichanga changa mpaka project inamalizika nikawa nimejichanga changa mpaka kupata kiasi flani cha pesa, nilikuwa na kiwanja maeneo ya Dar nikaweka msingi wa nyumba ya ramani niliokuwa nayo (nyumba simple, ambayo naamini uko mbeleni haiwezi nisumbua kujenga kwa kudunduliza).

Ndugu zangu nadhani mnajua sisi vijana tunakuwa na matamanio mengi sana kwenyee hii dunia, ususani sisi vijana wenye hizi age za miaka 25s-35 kunakuwa na matamanio makubwa ya kumiliki gari na nyumba nzuri, sasa kilichofuata pesa nyingine nikanunua gari aina ya IST niliagiza from japan (online buy).

Wakuu mpaka nakuja kuomba ushauri kwenu ni ili suala, Kwa sasa sina tena kazi yoyote ile ya kuniingizia kipato kabisa, maana ile project imesha isha kabisa, na kwenye account yangu nina shilingi milion moja tuu.

Naombeni ushauri wenu wa dhati kabisa, nifanyeje ili niweze japo kuiona kesho yangu ikiwa njema, sijui hii milion moja nafanyia nini ili niweze kutoka, na sijajua hii gari naifanyeje ili iweze kunitoa kimaisha, nimebaki kwenye wimbi kubwa la mawazo (kuna muda najutia kununua gari, ila imesha tokea na kuna muda mwingine nikiliangalia gari yangu naona kama sijafanya maamuzi baya sana maana nalipenda).

Sina mke wala mtoto, na nipo Dar es Salaam kwa sasa, niliwaza kuliingiza gari kwenye uber.. uko nako sijui kukoje

Ndugu zangu naombeni ushauri wenu ambao siku nikikaa ntaona kabisa kweli jamiiforum ilinitoa sehemu mmoja kunipeleka sehemu nyingine, mbalikiwe sana.

Karinuni
Kijana, sajili gari lako kwenye kampuni za Uber, bolt, taxify na little ride. Kwa kuwa huna ajira rasmi ni vema uendeshe mwenyewe, ukipata ajira inaliopa vizuri uza Hilo gari na uendelee na ujenzi.

Vv
 
Back
Top Bottom