Nipo njia panda

Wapendwa wana JF naombeni msaada wenu katika hili;

Mimi nipo kwenye ndoa ni mwaka mmoja sasa lakini matatizo ndani ya hii ndoa hayaishi.Mimi na mme wangu wote tunafanya kazi ila kuna mambo nashindwa kuyaelewa na ninabaki njia panda!

Mwezi uliopita nilikwenda likizo nyumbani cha ajabu wakati najiandaa kuondoka asubuhi mme wangu akaninyang'anya card yangu ya benki eti akifikiria nitakwenda kuwapa pesa nyumbani kwetu!

Kwa kweli tulibishana sana hadi nikafanikiwa kuondoka na card yangu ila alikasirika sana hadi akasema nikirudi nije na wazazi wangu eti hanitaki tena!

Nimeenda likizo nimerudi yakawa yameisha cha ajabu tukawa tumetoka out na waliokuwa washenga wetu wa harusi acha aanze kusimulia yaliyotokea!

Mimi ninaamini katika kusamehe na kusahau lakini mwenzangu ukifanya kosa anakumbushia na makosa yaliyopita nashindwa kuelewa ni kwa nini?

Kwa kweli mimi inaniuma sana na kuna kipindi najiuliza hivi kweli huyu mme wangu ananipenda kweli?

Naombeni mnisaidie katika hili kutokana na hizi tabia za mme wangu mimi nifanye nini?
Amelie!


Amelia pole sana .. this is the true him resurfacing .. guess you still have a lot to learn from him

You better show him your stand now otherwise ukikubali from the beginning then thats it you have no time to raise your head again kwani the next step ni beating
 
Kwakweli Invisible no doubt na bora uendeleee kuwa invisible mkuu,wewe lazima uwe qualified counsellor ila ndio safi.

I hope dada yetu atakua amepata auheni sana baada ya kupata maoni yako.
 
sasaaa Amelia pole tu endelea kuomba Mungu na kumheshimu mumeo...
 
Oa wewe! Usiogope elimu ya mwanamke. Usiparamie wanawake, tafuta mke. Wanawake ni wengi lakini wa kuwa mke ni mmoja naye akija huna ujanja huo wa Mwana-FA! It's the matter of time.

Mkuu unaona sasa ishu hii ya Amerie yeye hataki kujishusha ndo maana jamaa anakuwa mbogo.Lakini akijifanya mjinga mambo yanakuwa shwali kabisa.
Lakini ni wachache sana ambao wana roho za kujishusha lakini ukipata mwanamke mwenye Masters au PHD na kwendelea huko wewe una kabachara au kadiploma mkuu walahi nyumba itakuwa ndogo hapatoshi.....mmh mimi bado nipo nipo kwanza nyie tangulieni kwanza...
 
Amelie Pole sana na hongera kwa kupata ushauri.
Kwa upande wangu kama ningekuwa nikupe ushauri ningepata wakati mgumu SANA, au ningekupa ushauri kwa kurefer kwenye incidence nyingine. sababu ni kwamba siamini kama kutofautiana siku moja tu tena kwenye kitu kidogo ndio ingepelekea wewe uombe msaada wa mawazo unless narudia UNLESS kama kuna vituko vingine vimetokea.

kama kweli mnashare kuanzia password, simu, pin card, puk card na vitu vingine vya namna hiyo huoni kuwa alikuwa na HAKI YA KUZUIA VITU VYENU visitumike pasipokuwa na ridhaa ya pande zote mbili?

Vipi wewe na yeye nani ana kipato zaidi na katika kutoa misaada uliyoisema nani anatoa zaidi na kwa upande wa nani?
NI HAYO TU.
 
Mkuu unaona sasa ishu hii ya Amerie yeye hataki kujishusha ndo maana jamaa anakuwa mbogo.Lakini akijifanya mjinga mambo yanakuwa shwali kabisa.
Lakini ni wachache sana ambao wana roho za kujishusha lakini ukipata mwanamke mwenye Masters au PHD na kwendelea huko wewe una kabachara au kadiploma mkuu walahi nyumba itakuwa ndogo hapatoshi.....mmh mimi bado nipo nipo kwanza nyie tangulieni kwanza...

Ndugu mpendwa hapa swala sio kujishusha, ni kwamba mtu ameamua kutafuta ushauri wa haki yake. Masters au ukapuku (no education)haviingiliani na haki ya mtu hata siku moja. You have your rights with you everytime. Ina maanisha ok umeo Phd na wewe Diploma, then Phd akakutwanga mwiko kichwani pwaaa! ukakudhuru (faint or colapse), you mean hutatafuta your rights bcoz she is Masters. Tafuta MKE umeshaambiawa and with time, marriage has its respects too. Unless may be you have problems also. All the best lakini.
 
Amelia pole sana .. this is the true him resurfacing .. guess you still have a lot to learn from him

You better show him your stand now otherwise ukikubali from the beginning then thats it you have no time to raise your head again kwani the next step ni beating

Thank you!!!!
 
Amelie,

Ngoja nijaribu kuwa mshauri wenu kidogo...

Matatizo ya namna hii hayakuandami wewe pekee, wapo wengi wa namna yako.

Amelie, wewe ni mkristu? Mkatoliki? Mlienda semina ya ndoa kabla ya kufikia maamuzi ya kufunga ndoa kanisani? Kama si mkatoliki basi uliikosa fursa hii ya kipekee ambapo ungemsikiliza mfundishaji ungeweza kuchukua maamuzi kabla ya kuingia katika ndoa ambayo kwa mwaka mmoja tu unaanza kuhisi ni ndoano.

Ndoa ni kitu cha heri kabisa na wala usikijutie, kughafirika ni kwa kila binadamu na kubadilika inawezekana!

Kwanza:
Kuna ilani mliyojiwekea kuhusiana na masuala ya benki? Simu? Akaunti za barua pepe n.k? Kama hapana basi hili ni tatizo ila hujachelewa, mnaweza kuelewana mapema tu juu ya nini kifanyike na kivipi.

Pili:

Una kawaida ya kugawa ngawira mbele za mmeo haswa ukiwapa wadogo zako na ndugu za upande wako huku wa kwake ukiwapiga 'kibuti'? Kama ndiyo basi wewe ndiye tatizo na kama hapana basi kuna zaidi ambacho inabidi kueleweshana ili tuone pa kuanzia.

Tatu:
Una hakika ni mumeo tu au ni mume wenu? I mean, wewe ni mke wa ndoa halali ambapo una kila haki katika ndoa au mmeaminiana na kuamua kuanza kuishi pamoja? Kama hakuna ndoa baina yenu (inayotambuliwa na serikali) nitachemsha kwani huenda mwenzio ndo sasa kampata anayeona anamfaa kuwa mke... Hii inaweza kuwa habari mbaya kwako lakini bado si mwisho wa mahusiano yenu!

Nne:
Je washenga unaowaongelea ni watu wazima? Namaanisha ni watu wa makamo? Wakati anawasimulia ulitia neno? Wao walichukuliaje hali hiyo? Walitoa ushauri wa maana? Nini ulijifunza toka kwao?

Mara nyingi watu katika hali ya uchumba na wanapokaribia kuoana hukurupuka kutafuta washenga na kujikuta hawapati washenga sahihi na hivyo kubeba mamluki juu kwa juu na madhara yake mbeleni huwa makubwa. Aidha, matron na patron ni vema wawe watu wenye ndoa ili waweze kuwashauri kulingana na wao wanavyoyaishi maisha ya ndoa. Kama mlikosea na kutafuta wasela wataalam wa maneno tu hii inaweza kuwaathiri siku za usoni, washenga wakionekana si mali kitu msikimbilie kwa wazazi, kutana na matron au patron wanaweza kusaidia kabla hamjafikia pabaya.

Mwisho:
Ninaamini una mengi ya ziada na nilichoandika hakijakutosheleza, natambua wazi kuwa kuna chanzo cha yote haya, hii inawezekana kuwa imechochewa na masuala yenu binafsi (chumbani) ambayo yamepelekea hasira za mmeo naye anajikuta anakuwa mbogo. Kuwa mpole kwa mmeo, onyesha kumjali katika kipindi hiki ambacho mmetofautiana kidogo, mwambie mmeo ni jinsi gani unampenda, mweleze ni namna gani uliumizwa na kitendo cha yeye kukosa imani na wewe juu ya kitabu chako cha benki, usimwonee aibu kwani huyo ni mmeo!

Jaribu kuwa muwazi kwake, mpe 'account details' za benki na mwombe kama anaweza kukupa zake pia. Usimfiche password (neno au namba ya siri) ya akaunti yako! Penda kutumia hela yako kwa matumizi ya nyumbani na mfahamishe mmeo pindi ufanyapo hivyo, hii itamfanya aelewe mchango wako katika umoja wenu.

Nasisitiza: Ndoa si kitu kibaya, ni jambo la heshima na kusambaratika kwake ni dhahma kubwa kwa wapendanao. Kukosea ni jambo la kawaida na kuombana radhi hurejesha penzi lililoingia kiza.

Nakutakia tafakuri njema!

Invisible!
Hii imetulia sana. Nadhani wengi humu JF watafaidika na ushauri huu wa kina.
 
wapendwa wana jf naombeni msaada wenu katika hili;

mimi nipo kwenye ndoa ni mwaka mmoja sasa lakini matatizo ndani ya hii ndoa hayaishi.mimi na mme wangu wote tunafanya kazi ila kuna mambo nashindwa kuyaelewa na ninabaki njia panda!

Mwezi uliopita nilikwenda likizo nyumbani cha ajabu wakati najiandaa kuondoka asubuhi mme wangu akaninyang'anya card yangu ya benki eti akifikiria nitakwenda kuwapa pesa nyumbani kwetu!

Kwa kweli tulibishana sana hadi nikafanikiwa kuondoka na card yangu ila alikasirika sana hadi akasema nikirudi nije na wazazi wangu eti hanitaki tena!

Nimeenda likizo nimerudi yakawa yameisha cha ajabu tukawa tumetoka out na waliokuwa washenga wetu wa harusi acha aanze kusimulia yaliyotokea!

Mimi ninaamini katika kusamehe na kusahau lakini mwenzangu ukifanya kosa anakumbushia na makosa yaliyopita nashindwa kuelewa ni kwa nini?

Kwa kweli mimi inaniuma sana na kuna kipindi najiuliza hivi kweli huyu mme wangu ananipenda kweli?

Naombeni mnisaidie katika hili kutokana na hizi tabia za mme wangu mimi nifanye nini?
Amelie!

mumeo anakabiliwa na tatizo la ugonjwa wa wivu yaani ana wivu kupita kiasi. Tena wivu wenyewe si ule wa maendeleo ! Wivu uliochanganyika na roho mbaya ! Kaanae chini mueleze kwa utaratibu mno. Tena siku ambayo unaona anafuraha ! Pole sana !
 
Kwakweli Invisible no doubt na bora uendeleee kuwa invisible mkuu,wewe lazima uwe qualified counsellor ila ndio safi.

I hope dada yetu atakua amepata auheni sana baada ya kupata maoni yako.

Ni kweli kabisa mawazo yaliyotolewa lazima yataleta matunda mazuri. wasiwasi wangu ni mmoja. Kwenye game kuna two housemates( mume+ mke), Sasa mmoja amehisi sheria za game hazifuatwi vizuri au hana hakika na rules za game. Kajitahidi kucheza kaona analemewa, akaomba msaada kwa muamuzi.

Then refa/ muamuzi anamchukua huyo mmoja na kwenda kumuelekeza vizuri sana masharti au sheria za mchezo na jinsi ya kucheza bila kumdhuru mwenzie. Je kweli hilo game nitakuwa Fair? nini kifanyike? ushauri mwingi umetolewa kwa dada, sasa jamaa naye si anahitaji dozi? tutampata wapi tumpatie time-out ili naye apate mawili matatu?

Some men do take advantage of their wives. akiona mke amechange na kuanza kunyenyekea/ good behavior, sasa ndio kabisaaa anaona wewe bwege mtozeni !! subiria majibu yake sasa.

Ni mawazo tu msinipige mawe
 
Amelia, hakuna jambo zuri japo gumu kama kujadiliana kabla, baada kuhusu jinsi ambavyo mgependa mahusiano yawe na ni nini mnaweza kushirikiana pasi mipaka na ni nini na wapi kuna mipaka.

Wewe na mumeo mmetoka kwenye mazingira na malezi tofauti, hivyo hamna budi kujaribu kuleta mahusiano yenu kwenye level ambayo itawawezesha nyote kuhusiana pasipo mmoja kuona anaonewa au anadharauliwa.

Maswala ya pesa yamekuwa magumu sana katika mahusiano na nyumba nyingi, hivyo ni vizuri mkayaangalia kwa undani na mkayatolea uamuzi thabiti na mzuri kwa kuzingatia hali zenu halisi.

Dunia imebadilika na mahitaji yamekuwa makubwa na mengi hivyo ni vizuri pia kukubali kusaidiana kuyaendesha maisha yenu kukawa ni moja ya lengo lenu. Kwa kufanya hivyo ninaamini mtafanikiwa kufikia makubaliano wa jinsi ya kuendesha nyumba/ndoa yenu.

Ndoa ikiwa na mpangilio mzuri na maelewano ni jambo zuri na utaliifurahia.
 
Nashukuru sana Invisible kwa ushauri wako!

Mimi ni Mkristo lakini si mkatoliki ni Mpentecoste hatukuwa na semina kabla ya ndoa ila mchungaji alitupa mawaidha siku ya ijumaa kabla ya ndoa!

Kwa kweli kuhusu mambo ya benki kila mmoja wetu anafahamu password ya mwenzake!Pia kuhusu simu hatuna mipaka yani akikuta simu yangu anaweza akaperuzi kama anavyotaka pia mimi nikiamua nachukua simu yake naiperuzi!pia kuhusu barua pepe kila mtu anapassiword ya mwenzake tuko huru kwa hilo halina tatizo!

mimi nikiwa na ngawira nasaidia pande zote mbili sibagui na wakati mwingine nasaidia ndungu wa mme wangu kuliko hata wangu!Nikisafiri nje ya Tz nikirudi naleta zawadi za pande zote ila mwenzangu akisafiri nje analeta za upande wa ndugu zake tu!

Ni mme wangu kabisa tulifunga ndoa kanisani kwa baraka zote za wazazi wa pande mbili na ilikuwa ni baada ya kufuata taratibu zote pamoja na kutoa mahali!

Washenga ninaowaongelea namaanisha Patron na Matroni ni wanandoa wameoana tangu 2004!
Patron na Matron walituambia wao wanavyoishi na walivyoelewana katika mambo yao ya kipato!sasa wao ni tofauti na sisi maana Matron ni mama wa nyumbani!wao Patroni akipata mshahara anaweka mezani then wanapanga na mke wake!Sisi kwa kweli mimi nikiwa na pesa huwa nanunua matumizi yote ya nyumbani!

Tatizo mme wangu alishanitamkia kuwa anataka anicontrol na mimi kwa kweli nilimjibu hataweza kunicontrol maana hata mimi nina haki zangu naomba uniambie labda nilikosea kumjibu kuwa hawezi kunicontrol!


Nadhani mumeo bado hajakua, ameingia kwenye ndo na lile andiko 'Mume ni kicha cha Mke'. Nadhani you need to help him, ndo si utumwa, ndoa si ubawana na utwana.

Mkumbushe kuwa Kichwa bila mwili si kichwa na hakina maana. Kichwa bila mwili hakina uhai, kichwa kinaonekana kichwa kwa kuwa kimebebwa na mwili na ukweli ni kuwa kichwa hakiwezi kwenda popote pasipokuwa na mwili.

Nadhani mnahitajika kuwa na joint bank akaunti itawasaidia kuondoa mizozo isiyokuwa na maana , hiyo itawasaidia kuwa na equal say and decision kwenye masuala ya pesa. Nakwambia kuwa ikiwa mtakuwa sawa kwenye maswala ya pesa basi mmevuka kikwazo muhimu sana katika ndoa na vikwazo vingine vitakuwa si vigumu kama cha pesa.
 
Amelie,

Rules for a Happy Marriage


  1. Never both be angry at the same time.

  2. Never yell at each other unless the house is on fire.

  3. If one of your has to win an argument, let it be your mate.

  4. If you have to criticize, do it lovingly.

  5. Never bring up mistakes of the past.

  6. Neglect the whole world rather than each other.

  7. Never go to sleep with an argument unsettled.

  8. At least once every day try to say one kind or complimentary thing to your life's partner.

  9. When you have done something wrong, be ready to admit it and ask for forgiveness.

  10. It takes two to make a quarrel, and the one in the wrong is the one who does the most talking.

Ukipata nafasi zisome hizo rules mara mbili kila week, zinafanya kazi vizuri sana. Ukisoma comment za watu hapo juu zina-appy kwenye hizo rules. Try them out
mgiriki njooo uone hiii huku... mshana jr mambo hayo, MO11 njoo ukenue basi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom