Nipo njia panda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nipo njia panda

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Amelie, Oct 13, 2008.

 1. A

  Amelie Senior Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 195
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapendwa wana JF naombeni msaada wenu katika hili;

  Mimi nipo kwenye ndoa ni mwaka mmoja sasa lakini matatizo ndani ya hii ndoa hayaishi.Mimi na mme wangu wote tunafanya kazi ila kuna mambo nashindwa kuyaelewa na ninabaki njia panda!

  Mwezi uliopita nilikwenda likizo nyumbani cha ajabu wakati najiandaa kuondoka asubuhi mme wangu akaninyang'anya card yangu ya benki eti akifikiria nitakwenda kuwapa pesa nyumbani kwetu!

  Kwa kweli tulibishana sana hadi nikafanikiwa kuondoka na card yangu ila alikasirika sana hadi akasema nikirudi nije na wazazi wangu eti hanitaki tena!

  Nimeenda likizo nimerudi yakawa yameisha cha ajabu tukawa tumetoka out na waliokuwa washenga wetu wa harusi acha aanze kusimulia yaliyotokea!

  Mimi ninaamini katika kusamehe na kusahau lakini mwenzangu ukifanya kosa anakumbushia na makosa yaliyopita nashindwa kuelewa ni kwa nini?

  Kwa kweli mimi inaniuma sana na kuna kipindi najiuliza hivi kweli huyu mme wangu ananipenda kweli?

  Naombeni mnisaidie katika hili kutokana na hizi tabia za mme wangu mimi nifanye nini?
  Amelie!
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Amelie,

  Ngoja nijaribu kuwa mshauri wenu kidogo...

  Matatizo ya namna hii hayakuandami wewe pekee, wapo wengi wa namna yako.

  Amelie, wewe ni mkristu? Mkatoliki? Mlienda semina ya ndoa kabla ya kufikia maamuzi ya kufunga ndoa kanisani? Kama si mkatoliki basi uliikosa fursa hii ya kipekee ambapo ungemsikiliza mfundishaji ungeweza kuchukua maamuzi kabla ya kuingia katika ndoa ambayo kwa mwaka mmoja tu unaanza kuhisi ni ndoano.

  Ndoa ni kitu cha heri kabisa na wala usikijutie, kughafirika ni kwa kila binadamu na kubadilika inawezekana!

  Kwanza:
  Kuna ilani mliyojiwekea kuhusiana na masuala ya benki? Simu? Akaunti za barua pepe n.k? Kama hapana basi hili ni tatizo ila hujachelewa, mnaweza kuelewana mapema tu juu ya nini kifanyike na kivipi.

  Pili:

  Una kawaida ya kugawa ngawira mbele za mmeo haswa ukiwapa wadogo zako na ndugu za upande wako huku wa kwake ukiwapiga 'kibuti'? Kama ndiyo basi wewe ndiye tatizo na kama hapana basi kuna zaidi ambacho inabidi kueleweshana ili tuone pa kuanzia.

  Tatu:
  Una hakika ni mumeo tu au ni mume wenu? I mean, wewe ni mke wa ndoa halali ambapo una kila haki katika ndoa au mmeaminiana na kuamua kuanza kuishi pamoja? Kama hakuna ndoa baina yenu (inayotambuliwa na serikali) nitachemsha kwani huenda mwenzio ndo sasa kampata anayeona anamfaa kuwa mke... Hii inaweza kuwa habari mbaya kwako lakini bado si mwisho wa mahusiano yenu!

  Nne:
  Je washenga unaowaongelea ni watu wazima? Namaanisha ni watu wa makamo? Wakati anawasimulia ulitia neno? Wao walichukuliaje hali hiyo? Walitoa ushauri wa maana? Nini ulijifunza toka kwao?

  Mara nyingi watu katika hali ya uchumba na wanapokaribia kuoana hukurupuka kutafuta washenga na kujikuta hawapati washenga sahihi na hivyo kubeba mamluki juu kwa juu na madhara yake mbeleni huwa makubwa. Aidha, matron na patron ni vema wawe watu wenye ndoa ili waweze kuwashauri kulingana na wao wanavyoyaishi maisha ya ndoa. Kama mlikosea na kutafuta wasela wataalam wa maneno tu hii inaweza kuwaathiri siku za usoni, washenga wakionekana si mali kitu msikimbilie kwa wazazi, kutana na matron au patron wanaweza kusaidia kabla hamjafikia pabaya.

  Mwisho:
  Ninaamini una mengi ya ziada na nilichoandika hakijakutosheleza, natambua wazi kuwa kuna chanzo cha yote haya, hii inawezekana kuwa imechochewa na masuala yenu binafsi (chumbani) ambayo yamepelekea hasira za mmeo naye anajikuta anakuwa mbogo. Kuwa mpole kwa mmeo, onyesha kumjali katika kipindi hiki ambacho mmetofautiana kidogo, mwambie mmeo ni jinsi gani unampenda, mweleze ni namna gani uliumizwa na kitendo cha yeye kukosa imani na wewe juu ya kitabu chako cha benki, usimwonee aibu kwani huyo ni mmeo!

  Jaribu kuwa muwazi kwake, mpe 'account details' za benki na mwombe kama anaweza kukupa zake pia. Usimfiche password (neno au namba ya siri) ya akaunti yako! Penda kutumia hela yako kwa matumizi ya nyumbani na mfahamishe mmeo pindi ufanyapo hivyo, hii itamfanya aelewe mchango wako katika umoja wenu.

  Nasisitiza: Ndoa si kitu kibaya, ni jambo la heshima na kusambaratika kwake ni dhahma kubwa kwa wapendanao. Kukosea ni jambo la kawaida na kuombana radhi hurejesha penzi lililoingia kiza.

  Nakutakia tafakuri njema!
   
 3. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2008
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  usishangae sana miaka ya kwanza kwanza kwenye ndoa nyingi ndio hivyo mamaa, unajua mkiwa kwenye uchumba /honeymoon mnakuwa mpo mbigu ya tisa tisa hivi ...hamuishi kwenye reality...pretending kibao... lakini sasa baada ya muda inabidi tu mshuke huku duniani na kuanza kuishi kwenye reality...hapo sasa ndio inakuwa kazi maana muda si muda mnagundua kuwa kumbe mlikuwa hata hamjuani vizuri...

  cha muhimu muwe werevu katika kudeal na hizo conflicts for example msipigane physically.. msitukanane matusi au kuitana bad names.. hakikisheni mnasolve conflict moja baada ya nyingine hata kama itabidi mdiscuss overnight...conflicts zinaonekana bitter kwa sasa lakini ndio hizo zitakazowafanya mfahamiane vizuri... mwenzangu hapendi au anapenda nini, au yuko sensitive ktk ishu zipi...mkiwin hapo mtaanza kucompliment each other...and eventually get better and better...by the way, conflicts will never end as long as both of you are imperfect human beings...it can only get better
   
 4. BiMkubwa

  BiMkubwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2008
  Joined: Jan 9, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Amelie nitajitahidi kujibu maswahibu yanayokupata katikati ya maandishi yako binafsi. Ila kwa mujibu ya maelezo yako ningependa kukueleza yote uliyotupa hapa leo kwa kuomba ushauri ni hadithi ya upande mmoja- ambao ni wako wewe. Ila pia katika maelezo yako ninaona kuna walakini katika attitude ya huyo mumeo.

  Mosi, ndio kwanza mko katika stage ya kufahamiana zaidi kwa hiyo kuna mengi madogo ambayo yatatokea na yatakusononesha na kumsononesha yeye. Ila jitahidini kutafuta njia muafaka wa kuyatatua na pia kuhakikisha kila mmoja wenu anaelewa kuwa nyie ndio watatuzi wa mwanzo na hakuna kinachoshindikana kutatua. Msiweke issues zenu kiporo hata siku moja, hakikisha mnayatatua kabla hamjalala maana hakuna kitu kibaya kama kuweka matatizo kiporo maana ndio yanatoa nafasi kwa mawazo potofu.

  Kauli aliyotoa mumeo kuhusu wewe kuja na wazazi wako ni kauli yenye kuonyesha kuwa bado ni 'mtoto' katika haya maswala ya ndoa na hafahamu ni kiasi gani yeye anapaswa kuweka heshima upande wa wazazi wako na vivyo hivyo wewe upande wa wazazi wake. Asifikiri kuwa yeye ana mamlaka kubwa sana katika kukuoa wewe kiasi kwamba anaweza kuwaita wazee wako kwa suala dogo mno kama hilo YEYE ndio anapaswa kuwafuata wao ikiwa ana chochote chenye kumsumbua. Nakuasa mdogo wangu (I assume hivyo maana nimeishi ndani ya ndoa zaidi ya miaka 12) hata upande wako wewe usije ukafunga safari za kijinga kwenda kwa wakwe kumshitaki mumeo. Kumbuka kwa kuoana kwenu mumeonyesha walimwengu kuwa nyie ni watu wazima ambao mnaweza kujitegemea kimawazo na kutatua matatizo yenu bila kuingiliwa na mtu yeyote. Mosi, Kadi ya benki ni yako na siyo yake, kama alikuwa na wasiwasi alipaswa kukueleza na siyo kukunyang'anya. Nachelea kusema kuwa hiyo ni dalili mbaya sana maana inaonyesha kuwa ikiwa kuna chochote kitakachotokea baina yenu, mwanaume wa aina hiyo anaweza akanyanyua mkono na kukupiga. mdogo wangu that is the reality. Mkae chini mkubaliane matumizi yenu yatakuwaje. Na ikiwa wewe unajichukulia mamlaka fedha zako kumbuka uko kwenye ndoa na inapswa mkubaliane mambo ya kifedha yataendaje. Usitumie nafasi hii kudai kuwa kila mmoja anafanyakazi, hilo halitoshi. kwa hiyo mkae myatatue hayo
  Bibi mumeo anakupenda na ndio maana kakuchagua wewe kuwa mwenzi wake. Ila naona tatizo lake ni kwamba hajui namna ya kutatua matatizo yenu. Anasahau kuwa yeye ndio kichwa na anapaswa kuonyesha njia. Pia anasahau kuwa nyinyi ni mwili mmoja na ikiwa mmoja wenu ameenda mrama basi wote mtaonekana wa ovyo tu. hakuna wa kumshika mwenzie mkono. katika hili suala lenu sioni haja ya mtu mwingine kuja kuwasaidia kulitatua bali nyie wenyewe mkae chini muelezane ukweli pasipo kuficha. na kama hawezi basi wewe chukua jukumu la kumweleza yale unayofikiria. Atajifanya pengine hakusikii na wala hakuelewi ila my dear, as long as you tell him in the best way, message itakuwa delivered. Atajisuasua kuja karibu ila he will come around.

  Amelie,
  Kumbuka hakuna kisichokuwa na mwisho. Huyo mumeo atajifunza taratibu ujifunze uvumilivu huku pia ukijitahidi kuonyesha best practices.
   
 5. A

  Amelie Senior Member

  #5
  Oct 13, 2008
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 195
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana Invisible kwa ushauri wako!

  Mimi ni Mkristo lakini si mkatoliki ni Mpentecoste hatukuwa na semina kabla ya ndoa ila mchungaji alitupa mawaidha siku ya ijumaa kabla ya ndoa!

  Kwa kweli kuhusu mambo ya benki kila mmoja wetu anafahamu password ya mwenzake!Pia kuhusu simu hatuna mipaka yani akikuta simu yangu anaweza akaperuzi kama anavyotaka pia mimi nikiamua nachukua simu yake naiperuzi!pia kuhusu barua pepe kila mtu anapassiword ya mwenzake tuko huru kwa hilo halina tatizo!

  mimi nikiwa na ngawira nasaidia pande zote mbili sibagui na wakati mwingine nasaidia ndungu wa mme wangu kuliko hata wangu!Nikisafiri nje ya Tz nikirudi naleta zawadi za pande zote ila mwenzangu akisafiri nje analeta za upande wa ndugu zake tu!

  Ni mme wangu kabisa tulifunga ndoa kanisani kwa baraka zote za wazazi wa pande mbili na ilikuwa ni baada ya kufuata taratibu zote pamoja na kutoa mahali!

  Washenga ninaowaongelea namaanisha Patron na Matroni ni wanandoa wameoana tangu 2004!
  Patron na Matron walituambia wao wanavyoishi na walivyoelewana katika mambo yao ya kipato!sasa wao ni tofauti na sisi maana Matron ni mama wa nyumbani!wao Patroni akipata mshahara anaweka mezani then wanapanga na mke wake!Sisi kwa kweli mimi nikiwa na pesa huwa nanunua matumizi yote ya nyumbani!

  Tatizo mme wangu alishanitamkia kuwa anataka anicontrol na mimi kwa kweli nilimjibu hataweza kunicontrol maana hata mimi nina haki zangu naomba uniambie labda nilikosea kumjibu kuwa hawezi kunicontrol!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,599
  Trophy Points: 280
  Hongera sana kwa hilo, kwa maoni yangu hukukosea chochote kujibu kwamba hawezi kucontrol. Katika ndoa hakuna yeyote anayestahili kumcontrol mwenziye. Mmeamua kuingia kwenye ndoa hii kwa mapenzi yenu hivyo hakuna yeyote ambaye ana haki ya kumcontrol mwenziye kwenye lolote lile. Haya uliyaandika hapa kama wewe ukisafiri unaleta zawadi kwa pande zote mbili za familia zenu ni muhimu pia kuzungumza na mwenzako juu ya hili. Katika maswala ya pesa za matumizi yenu ya kila siku nyumbani kwenu ni vizuri mkafungua account ya pamoja na kama matumizi yenu ni shilingi laki moja kwa mwezi basi kila mmmoja wenu akaweka nusu au vyoyote myakavyokuabaliana wenyewe. Na hii account itakuwa ni kwa ajili hiyo tu. Uwe na account yako binafsi ambayo mume wako hana access nayo wala hajui password yako. Mwaka mmoja katika ndoa maharusi bado wanakuwa kwenye honeyomoon na siyo matatizo kama haya. Nakutakia kila la heri katika ndoa yenu, lakini yape uzito mkubwa haya niliyoyaandika.
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Oct 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Amelie, I once was a teacher... Nitajaribu kukusaidia kadiri nitakavyoangaziwa na Muumba.

  Usijali mamangu, tupo kushirikishana maisha ya kila siku.

  Kutokuwa mkatoliki hakujakupunguzia ulichotakiwa kupata japo ungeenda hizo semina huwa kuna mengi ambayo wanandoa hufundwa kabla ya ndoa ili wachukue maamuzi sahihi. Mabadiliko unayoyaona kwa mumeo ni ya ghafla au hali hii uliihisi tangia mwanzo wakati wa uchumba? Kama ni mabadiliko ya ghafla kuna kitu naweza kugusia zaidi.
  Umenena vema, mnafanya jambo zuri japo upande wa simu na barua pepe najua kuna risking kubwa sana. Wapo wanaodhamiria kuharibu ndoa za wenzao nao wanaweza kutengeneza anuani pepe au sms na kutuma kama vile ni wapenzi wa mmoja wenu na kuwagombanisha kisawasawa! Kuwa makini katika hili!
  Wewe ni mwanamke wa kipekee basi, wachache wa aina yako! Mungu akupe moyo na uendelee hivi!

  Ni vema, lakini uchumba wenu ulidumu kwa muda gani? I mean, kabla hamjaoana mlifahamiana kwa muda gani? Ulimkatalia kushiriki naye tendo la ndoa hadi muoane? *Naelewa wachache wanaojua nini nalenga* Kama mlifahamiana kwa zaidi ya miaka walau miwili au mwaka mmoja unusu kabla ya kuchukua maamuzi ya kuoana basi mtakuwa mlipata muda wa kufahamiana kwa karibu na hivyo unaweza kutambua kuwa tabia hii mpya ya mumeo ni ya ghafla na ina chanzo, dawa tunaweza kukupa hapa! Kama ulikuwa 'unambania' basi jamaa alikuwa na hamu na 'mchezo' na baada ya kuonja akakuta si sawa na matarajio yake anaanza zake. Ukweli ni kwamba vijana wengi hupenda kuanza kujuana kimwili kabla ya ndoa, ndiyo maana wengi hujikuta wanafunga ndoa wako na vi-friji. Hakukuwa na uharaka wa kufunga ndoa? Najua ni gumu hili kujibika hapa, lakini kama unaelewa kuwa ID unayotumia si real name yako basi unaweza kutusaidia kwa kuuanika ukweli hapa ili wengi wetu wafahamu athari za mambo haya!

  Washenga si Patron na Matron, washenga ni wazee (yule mzee/kijana alokuja kwenu akakutana na wazazi/walezi kusema jamaa anataka kumposa binti yao) ambao hushughulikia masuala ya mahari na mambo mengine ya kimila.

  Oh, kuna utofauti katika familia zenu mbili then! Lakini bado walitakiwa wawili hao kutumia busara zao kuwaweka sawa. Ndoa yenu changa na naionea huruma, ningefurahi kuona unatufahamisha kuwa ndoa yako ina miaka 10 hivi na mnaendelea vema na mnazidi kupendana kadiri siku zinavyokwenda. Si kweli kuwa ndoa huanza kwa mapenzi matamu na baadae kuwa ndoano, usiamini hivi kwani itakuandama sana akilini... Hao wasemao hivyo hufahamiana na wenza wao kwa miezi kadhaa (hata mwaka haufiki kwa wengine) na kukimbilia kudai wako tayari kwa ndoa.

  Ulikosea mama, hamtakiwi kupanda nyote. Akipanda shuka, kuna siku yako ya kupanda. Kila mwanaume anapenda awe juu... Asikudanganye mtu! Tunatambua haki ya kila mwanamke lakini ukichanganya kisomo cha mkeo (sema Masters tu) na akawa ana chenji nzuri, halafu akujibu kama ulivyomjibu basi mwenzio anaona heri atafute binti wa la 7 huenda wakaelewana kuliko wewe.

  Ndoa ni furaha, Ndoa si pingu za maisha kama wasemavyo wengi... Ni furaha ya maisha! Kutoelewana kupo na kutoelewana huko kutumie kama changamoto kwa maisha yenu katika ndoa. Mumeo anakupenda sana, anapenda awe juu yako... Kuku-control alikokwambia sidhani kama alilenga pabaya bali alitaka awe mwenye sauti katika familia. Anastahili, mpe heshima ya mume na mwambie yeye ndiye kichwa cha familia, ni maneno machache tu lakini yatamfanya ajione mfalme katika ndoa yenu.

  Kama wengine walivyokuasa, jaribuni kuyamaliza ninyi bila kwenda kwa wazazi, huko hapatatua tatizo kirahisi. Hili ni tatizo dogo ambalo ukweli linaweza kupelekea kubwa. Jazba, hasira ni jambo la kawaida, kiepushe kinywa chako na majibizano na mumeo nawe utaifurahia ndoa.

  Nakutakia kila la kheri katika ndoa yako na Mungu awape mwanga zaidi mpendane zaidi na kushirikiana kwa karibu!
   
 8. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hypothetically speaking ikitokea siku identity za watu huku jf zinajulikana au watu wote wanakutana itakuwa very interesting. Inaelekea profession zote ziko represented. Nilikua sijaifikiria ila leo nimeona mpaka marriage counsellors are in the house!!!!!!!!! Secret agents najua wapo, mapadri na wachungaji mpo?
   
 9. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135  Nimekukubali mzee, nami nitakuwa nautumia huo mfano. Umeweza kueleza jambo pana kwa mstari mmoja tu.
  .
   
 10. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Amelie,
  huyo tayari ni mume wako.Si fahamu u muumini wa wapi lakini kwa Wakristo ukishafunga ndoa ndo umeweka kitanzi.KUTOKANA NA UKWELI KUWA HUYU NI MUME WAKO NA ANAJUA IN AND OUT YA MAISHA YAKO,MPENDE.
  Pili haiwezekani akawa ameanza vituko bila sababu.Ipo.Nakushauri wewe kama mwanamke tumia ufahamu wako wote kujua kwanini ameanza hivyo.Then mnaweza mkayazungumza kwa njia mnayoona kuwa inafaa.Kumbuka wewe mwenyewe unaweza kuwa sababu ya mmeo ama kukupenda au kukuchukia.Anza sasa.
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Oct 15, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Nani huyo? BiMkubwa sio?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Amelie,

  Rules for a Happy Marriage


  1. Never both be angry at the same time.

  2. Never yell at each other unless the house is on fire.

  3. If one of your has to win an argument, let it be your mate.

  4. If you have to criticize, do it lovingly.

  5. Never bring up mistakes of the past.

  6. Neglect the whole world rather than each other.

  7. Never go to sleep with an argument unsettled.

  8. At least once every day try to say one kind or complimentary thing to your life's partner.

  9. When you have done something wrong, be ready to admit it and ask for forgiveness.

  10. It takes two to make a quarrel, and the one in the wrong is the one who does the most talking.

  Ukipata nafasi zisome hizo rules mara mbili kila week, zinafanya kazi vizuri sana. Ukisoma comment za watu hapo juu zina-appy kwenye hizo rules. Try them out
   
 13. A

  Amelie Senior Member

  #13
  Oct 15, 2008
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 195
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika Urafiki hadi uchumba tulidumu miaka mitano!ndani ya hii miaka mitano!kusema ukweli tulishirikiana kimwili!Tuliamua kuoana kabisa wala hakuna aliyemshurutisha mwenzake!
  Ngoja niwe muwazi hapa kusema kweli baada ya kuoana nikawa mvivu sana natoka kwenye shughuli za kutafuta mkate wa kila siku nakuwa nimechoka kweli akiniomba "mchezo"kweli nikawa namnyima namwambia nimechoka!
  Ila hili limekwisha baada ya kuhudhuria semina ya wanandoa iliyofanyika kwa Gamanywa kweli ilinisaidia ni nilimuomba MUNGU anitie nguvu ili nisimnyime mwenzangu!
   
 14. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2008
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  Dada Amelie kwanza pole pili usifikiri kuwa hilo ni tatizo la kuvuruga ndoa yako, hapana.

  Kama alivyoeleza mchangiaji mmoja NDOA ni jambo la kheri tele kama tu mtelewana kwenye masuala ya msingi na mkiwa na nia thabiti ya kuifanya iwe paradiso.

  Hili wala halihitaji mtu kuwa wa dini au mwenye imani sana.

  Wengi wetu tunasahau kuwa nguzo kuu za mahusiano ni wakati wa uchumba na pale mambo muhimu yaainishwe kabla ya kuishi, badala yake uchumba huwa juu juu kupeana zawadi,ahadi na kusahau jukumu lililo mbele. Mambo muhimu kabisa ya kuwekana wazi ili yasilete matatizo ni Matumizi ya pesa, idadi ya watoto, misingi ya malezi, masuala ya extended families, nk. Na ni vyema wote yani mume na mke wajue kila jinsia ina mtazamo kwenye mambo mbalimbali na kila mmoja akubali tofauti za mwenzake.

  Nina imani kuwa ujenzi wa familia ni jukumu la wote. Tena hapo awali huduma kuu za familia zilifanywa na mume. Mume alihakikisha familia ina mahitaji muhimu. Nina kumbuka miaka hiyo kwenye semina ya ndoa kuna majukumu muhimu ya mume na mke na moja ya jukumu kuu la mume ni "provide for his wife and the children" na hili ni agizo la biblia ila sikumbuki mstari but will check it out.
  Ila kwa kuwa siku hizi wote wawili wanaweza kuwa wanafanya kazi na maisha yamekuwa juu familia haina budi kujengwa na wote wawili. La muhimu ni kuongea kw autaratibu kabisa kuwa vipato vyetu ni hivi- tuna majukumu a,b,c,d sasa tufanyeje kukabili haya.

  Pili endelea kuwa mfano bora wa kuwapenda ndugu zake sana bila ubaguzi, na kama ni mtu wa kujifunza atajifunza kutoka kwako.

  Muweke wazi mumeo kuwa ni jukumu lako kuwasaidia wazazi,wala usiwasaidie kwa uficho.

  Napendekeza dada yangu muyaongelee haya mambo mapema yasije waletea tabu huko mbele. Mna mengi mtapata watoto nani atalipa school fees? mtahitaji kujiendeleza n.k

  La muhimu zaidi mwombe Mungu akupe busara unapoongea na mumeo, usiongee ukisukumwa na superiority bali humbleness na hakika kwa busara utaweza kumuelewesha mambo mengi naye atajifunza na kama nafsi yake i wazi ataomba msamaha.

  Hujachelewa kuchukua hatua,ichuke sasa na utaishi na amani-ni mapema mno kuwafuata councelors ambao nao wameoana juzi tu.

  Good Luck.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapo ndo penye tatizo kubwa kuliko yote.
  Jifunze kunyenyekea hata kama umemzidi jamaa kipato mheshimu mmeo mtii ulikubali yote ukiweka sera za ladies first mmh utaugulia kila siku.
  Tatizo la wanawake wenye elimu na kipato juu ni hili tu kuwa juu hawataki kujishusha kwa waume zao kila kukicha matatizo ndani ya nyumba.
  Ndo maana mimi sitaki kabisa kuoa na wala sioi leo wala kesho haya matatizo nayaona sana kwa jamaa zangu...
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Jamani kuna father mmoja alitulisha neno kuhusu matatizo ya NDOA nyingi yanasababishwa na vitu hivi hapa ukivishinda hivi basi utakuwa mwenye fraha sana katika ndoa yako navyo ni;- 1.RELATIVES FACTOR 2.FINANCE 3.BED ROOM.
  Fatilia matatizo ya ndoa nyingi hapa na pale yanasababishwa na hivyo vitu hapo juu.
  Unaweza ukavichambua kwa undani zaidi na unaweza kusight mifano kibao na kadha wa kadha.
   
 17. C

  Chuma JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  1-Akipanda shuka...cool...(Invible katangulia kusema!!!)..Mkipanda wote hapo tatizo,the same mwanaume anatakiwa akiona mke anapanda yeye anashusha!!!

  2- Kama mlionjana kabla ya Ndoa, ujue ndoa yenu itakuwa ktk mashaka throughout, otherwise mnatakiwa mtubu na msirudie makosa. Ubaya wa kuonjana kabla ya Ndoa, kuna uwezekano mkubwa wa kuenda Nje ya Ndoa baada ya Ndoa...

  3-Ndugu, Pesa, Kitandani (Fidel katangulia) ni mambo ya kuyaangalia sana. Ni Ngumu kuya control na hasa hutegemea BACKGROUND ya kila mmoja wenu ipoje...na Hasa Ndugu zetu wengi hupenda tuwatreat the same kama tunavyowa treat wake zetu. so Mme asipokuwa makini anaweza kuyumbishwa na Ndugu zake...Wao wanaona wivu kwanini mali ya kaka yetu......so both take care!!! kwani kila mmoja atapenda asaidie Nduguze...ndio inavyotakiwa ila tuwe makini...Tupende kutoa kwa SIRI kuepusha HASADI...Kwani Kila NEEMA hufanyiwa HUSUDA...

  4- Ushauri wangu mambo ya email na simu jiweke mbali usije kuumia roho bure... Kila mmoja ajiweke mbali na mwenzake...believe ukiona email/sms ya ajabu ya mumeo au Mkeo....from that point utaanza kuwa na waswas na mwenzako...Kila mmoja amtrust mwenzake...
   
 18. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #18
  Oct 15, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hehehe, yani hapa dadangu ndipo ulikoroga mambo! Nakusihi sana, ulimzoesha kumpa 'haki' yake na sasa gharama yake ndiyo hii.

  Yote uliyodhania yanaanzia HAPA! Ni vema ukae chini naye, mwambie hivi:

  "Mume wangu nakupenda sana, natambua kuwa unanipenda pia na hilo linathibitika kwa yote ufanyayo kwangu mkeo. Najua nakukosea sana mume wangu kwa kutokuridhisha kipindi unapohitaji hivyo, naomba unielewe kuwa si mapenzi yangu na naelemewa na kazi lakini bado nakuhitaji sana. Nitajitahidi kupunguza kazi zangu na kupangilia namna ya kuzifanya kwa mpangilio mzuri ili nipate fursa ya kuilinda ndoa yangu.

  Sipendi hali inakoelekea lakini naomba unipe ushauri wewe juu ya nini nifanye."

  Hapo mpe fursa yeye kuona anasemaje, msikilize kwa karibu sana ili uweze kutambua nini anafikiria. Bibie katika mapenzi/ndoa ni muhimu sana kutenganisha muda wa kazi na mahaba kwa mwenzio. Wengi hujilaumu kwa kosa la namna hii. Ndoa nyingi zimevunjika kwa u-bize wa wanandoa na wengi hujikuta wakijutia kukuta wanandoa wenzao wakiamua kwenda nje ya ndoa/mapenzi kusaka kile wanachodhani wanakosa.

  Aidha mwenzio anadhani umemchoka, nakushaurini fanya kuwa na mpangilio wa kushirikiana kimwili walau mara 3 kwa wiki na ikishindikana kabisa basi mara 2. Itapendeza sana mkiwa mnabadili mazingira ya kufanya hivyo (isiwe nyumbani tu) ili kupata ladha ya kufanya tendo hili takatifu mkiwa maeneo tofauti tofauti. Usisubiri mmeo akutoe 'auti' bali kwakuwa inaonesha nyote mna kipato wewe pangilia vema ratiba yako, andaa kila kitu nyumbani kuhakikisha usalama wa maskani kwenu, mpe taarifa ya mapema kabisa kwa kumwambia kuwa kuna siku ungependa kutoka naye 'auti' kisha hakikisha unaenda hoteli yenye hadhi ya kuitwa hoteli (japo mara mbili kwa mwaka).

  Hii inaweza kuonekana kuwa ni kichekesho lakini imewasaidia wengi! Nimeijaribu hii na nimeshaona matunda yake kwa mwenzi wangu :).

  Kisha hakikisha unakuwa msafi, usafi ni kitu muhimu sana katika mapenzi/ndoa. Kumbuka kuwa huyu ndiye aliyekuona wewe bora kuliko wote! Amekuridhia na yuko tayari kufa nawe! Mpe kila unachodhani anastahili lakini kuwa makini usije mzoesha vibaya. Epuka kufanya kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu! Itakugharimu si duniani pekee hata siku ya Kiama.

  Bibie ni hili tu tatizo kubwa ninaloliona kwako ambalo wanandoa wengi linawakabili. Si rahisi kutambua athari yake, mbaya zaidi ukikuta mwenzi wako ni mkimya na anaamua ku-'riakti' anavyodhani ni sawa. Jazba za ghafla, maamuzi yasiyotarajiwa na vitu kama hivyo hutokana na mwenzi mmojawapo kuacha ama kupunguza 'makasheshe'. Najaribu kupunguza ukali wa maneno lakini naamini kama mwanandoa unanielewa.

  Kama ulikuwa msafi endelea kuwa msafi, kama ulikuwa ukirudi/mkirudi kutoka kazini LAZIMA kubusiana basi fanya kumbusu. Kama ilikuwa kawaida yenu kuambiana 'nakupenda mme/mke wangu' usiache kwani ataamini sasa humpendi ama umeshapata 'kifaa' kingine mbadala. Mfanye ajisikie mfalme naye atakufanya malkia! Kuna vijizawadi vingine ni vidogo na havina thamani kwako lakini kwake vitakuwa na thamani. Hakuna cha dawa wala uchawi, atanasika tu!

  Bibie, nakuomba kukiwa na tatizo zaidi tushirikishe. Akionekana kutoelewa somo tafadhali rejea hapa na kutufahamisha nini tatizo nasi tutajitahidi kuiweka sawa ndoa yako.

  Umesahau, hata elimu haina nafasi. Ni kama wote mnakuwa watoto vile!
  Na hasa wanawake hujisahau na kuhamisha mapenzi yao yote kwa watoto wakisahau nani anastahili kuwa 'festi boni' wao.

  Well said! Usishauri tu... Hata wewe mkuu teh teh teh!

  Good point!

  Councelling ya online inakuwa rahisi kwake kwani identity yake inabaki kuwa siri yake! Muhimu apate ujumbe.

  Oa wewe! Usiogope elimu ya mwanamke. Usiparamie wanawake, tafuta mke. Wanawake ni wengi lakini wa kuwa mke ni mmoja naye akija huna ujanja huo wa Mwana-FA! It's the matter of time.

  Mkuu Chuma, haya mambo kwa nyakati za sasa ni kama hayakwepeki tu. Asilimia 90 na zaidi ya wanandoa ambao wamefunga ndoa zao kuanzia miaka ya 90 wametembea pamoja kabla ya ndoa. Yani mtu akishapeleka posa na kumvalisha pete ya uchumba basi shughuli inakuwa kama ndio imepata baraka zote!

  Hii inategemea na tabia zenu! Kama mnaaminiana na ni wakweli basi mke au mme hana haja ya kuficha Email wala sms. Yani kwangu huwa naona kawaida kabisa, labda issues za kikazi, issues za kibiashara hizo ndizo unatakiwa unamweleza ukweli mwenzako lakini hatakiwa kuwa na access ya kazi zako. Hii ni muhimu kikazi! Hata mwenza wangu anajua najihusisha na JF lakini hajui password yangu! Nilimwambia "Kumradhi, hilo siwezi!"
   
 19. E

  Endaku's JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2008
  Joined: May 25, 2007
  Messages: 322
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mama Tulia na ndoa na uwe mvumilivu lakini haki yako ya msingi usikubali kunyang'anywa kabisa hata na mumeo with time akuelewa tuu !

  Sijui mnaishije lakini fanya manunuzi ya vitu hapo nyumbani hasa kama una kazi usimuachie mwenzako tuu ,na kama anapenda kitu fulani na wewe uwe unamnunulia siku mojamoja its all about caring each other !Speaking from experience my wife is doing that and is perfectly working !

  Usipovumilia utakaribisha MAFISADI mama itakuwa balaa!
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,599
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu mume ndani ya nyumba anaweza kabisa kupewa nafasi na mke wake ‘kuwa juu" au kuwa kiongozi ndani ya nyumba kutokana na matendo yake ndani ya familia yake na pia upendo wa kweli anaouonyesha katika familia zote mbili, na siyo kwa vitisho vya kumtamkia mkewe kwamba anataka ‘kumcontrol". Hii mwanaume anaweza kuifanya kama mkewe ni mama wa nyumbani 24/7 lakini siyo kwa mke ambaye ana kazi na kipato kizuri tu. Hebu imagine kama huyo njemba angetamka maneno hayo wakati wa uchumba wao, basi nina hakika kabisa kwamba Amelie angeingia mitini siku nyingi sana. Ingekuwa vizuri tungepata definition ya huyu bwana ana maana gani anaposema anataka ‘kumcontrol mkewe" maana anaweza kabisa akawa na maana tofauti na tunayoifikiria sisi.
   
Loading...