Nipo njia panda wandugu

yorkshire

JF-Expert Member
Sep 9, 2016
2,508
3,110
Habarini wana jf,
Naomba niende moja kwa moja kwenye point....

Usiku wa kuamka leo nimekosa amani totally na nimewaza sana lakini nakosa majibu nikaona ni bora niombe msaada kwenu.

Ni kwamba mimi ninaishi na binti mmoja ambaye mwanzoni tulikuwa na mahusiano mazuri tu lakini sasa hivi nipo dilemma kutokana na mwenendo wake jana nilimtia kibao kibao kimoja baada ya kunifyonza kiukweli hasira zilinipanda sana nikamnasa na siyo mara moja wala mara mbili kunifyonza na maneno mengine ya kejeli hasa anapokuwa na hasira.

Sasa baada ya tukio hilo alilia sana na kudai anataka aondoke kwamba hajawahi kupigwa na mwanaume yeyote ambaye atampiga hata kama ana makosa basi ni lazima amwache nilimbembeleza sana pasipo mafanikio baadae sana akakubali ingawa bado ana fundo moyoni.Shida ina kuja kwamba katika kupekua pekua simu yake nimeona namba fulani nadhani ndio inayompa kiburi ingawa sina uhakika maana huwa anafuta ushahidi na anapopigiwa hapokei ninapomuuliza kwa nini hapokei anadai hajisikii kupokea lakini nilipotazama zile call logs inaonyesha huwa anapokea mara kwa mara hiyo namba.

Shida nyingine dini zetu ni tofauti ingawa kweli nampenda kwa dhati kabisa nina mpango nae sasa mara kwa mara ninakuwa nina mashaka naye hasa anapokuwa anachart nimebaki najiuliza nifanye nini lakini nakosa cha kuamaua ...

Wazo jingine linaniambia nitemane naye na jingine linaniambia niwe na subira ...naombeni ushauri wenu hasa jinsi ya kuachana naye kwa amani zaidi pasipo mimi kuhisi maumivu kwani bado nampenda sna ila kuzungukwa ndiko kunakonifukuza
 
we kama unakazi zako nenda mwache hm mwachie ela yamatumizi,ukiludi jion utapata jibu kama wakuondoka ataondoka kama,kama sio wakuondoka utamkuta,alafu jikaze kiume usioneshe unamjali sana,yani fanya kama akitaka kwenda poa,uone moto wake,anatikisa kiberiti,akikaa ndio uanze kufatilia kimya kimya kama anamausiano ya nje,anaweza akawa nishoga yake tu wanapigaga umbea sana we ukaisi nimwanaume,lakin pia mabint wengi wakisha kaa na mtu mda mrefu huwa wanabadilika bila wenyewe kujijua aidha kwasababu wanaiga kwa wenzao au wewe unaweza kuwa chanzo cha tatizo mpaka yeye kubadilika,ugomvi ukiisha anza kuyajenga taratibu kwamazungumzo yataratibu tu kama niwako mtaelewana namaisha yatakuwa poa,utaacha wangapi mwl,wao kipofu nikazi yako kumfanya aone unachokiona wewe mbele.@mawazo yangu tu.
 
Ukiwa unatunga uongo ujitahidi kuwa na sanaa ya bongo movie,uongo wako utakubalika haraka. Umetiririka pumba weee ukaja jazia mashudu ati dini yenu tofauti,muda wote ulioishi nae ulikua wapi kufahamu tofauti ya dini? Si useme tu ukweli umemtumia binti wa watu vya kutosha,umemchoka unaanza visingizio ati kakufonya mara namba ngeni inayompa kiburi kisha ukakumbuka dini tofauti

Hapa kinachokusumbua sio utoto bali ni ujinga na sifa za mitandaoni uonekane kidume kinachopiga mwanamke kisa kakufyonza.
 
mkuu unaweza kuona kama nimemtumia vile lakini hilo si lengo langu hata kidogo hizi ni baadhi ya changamoto zake nimefupisha sana maelezo lakini ni mengi mno ninayoyavumilia ila ukweli nimefikia mahali nimechoka kuwa mtumwa wake maaana hata sasa bado amenuna tu na majibu yake ni shortcut
 
we kama unakazi zako nenda mwache hm mwachie ela yamatumizi,ukiludi jion utapata jibu kama wakuondoka ataondoka kama,kama sio wakuondoka utamkuta,alafu jikaze kiume usioneshe unamjali sana,yani fanya kama akitaka kwenda poa,uone moto wake,anatikisa kiberiti,akikaa ndio uanze kufatilia kimya kimya kama anamausiano ya nje,anaweza akawa nishoga yake tu wanapigaga umbea sana we ukaisi nimwanaume,lakin pia mabint wengi wakisha kaa na mtu mda mrefu huwa wanabadilika bila wenyewe kujijua aidha kwasababu wanaiga kwa wenzao au wewe unaweza kuwa chanzo cha tatizo mpaka yeye kubadilika,ugomvi ukiisha anza kuyajenga taratibu kwamazungumzo yataratibu tu kama niwako mtaelewana namaisha yatakuwa poa,utaacha wangapi mwl,wao kipofu nikazi yako kumfanya aone unachokiona wewe mbele.@mawazo yangu tu.
yupo mpaka sasa hivi ukweli ni kwamba hana hela ya kurudi hostel cuz ni mwanachuo chuo kimoja cha ualimu ...toka tuanze kuishi tuna mwaka mmoja now ina maana akipata hela anytime ni wa kuondoka huyo
 
Kwa nini usichukue hiyo namba na kumpigia huyo mwanaume na kumkataza kuwasiliana na mchumba wako?
 
kuishi na mwanamke unae muhitaji sana kuliko anavyokuhitaji wewe ,ni kujitengezea utumwa

ona amekukosea Adabu mmemkanya mwisho wa siku ww ndo unaomba msamaha

sasa nani hapo alomkosea mwenzie
mkuu umepigilia msumari yaani ni mtu anayejiona malaika hapendi umkosoe hata kama unaona kabisa jambo fulani lina dosari ya moja kwa moja yeye huona unambishia na humuungi mkono
 
Kwa nini usichukue hiyo namba na kumpigia huyo mwanaume na kumkataza kuwasiliana na mchumba wako?
nahofia huenda nikamchochea yeye kuongeza moto makusudi maana namba zake ni dhahiri ni za mwanaume
 
Sasa compact kwani manzi hajui yeye ni mchumba wa mtu!
anajua cuz si mara ya kwanza kumuonya juu kitendo kama hicho ila ana tabia ya kupuuzia pia hutumia kama njia ya kuniumiza kisaikolojia
 
anajua cuz si mara ya kwanza kumuonya juu kitendo kama hicho ila ana tabia ya kupuuzia pia hutumia kama njia ya kuniumiza kisaikolojia
Binafsi kama unauhakika namba ni ya mwanaume na umemwonya hataki kwangu naona achana naye... ila mengine jiongeze mwenyewe maana wew unayajua vizuri kuliko mimi.
 
Back
Top Bottom