Nipo Njia Panda Naomba Mnishauri

Nipo Njia Panda Naomba Mnishauri

Acha nyodo wewe, kwani demu unayemtafuta hajatafunwa na wengine? Huyo unamwogopa kisa katafunwa na rafikiyo? Mtoto kajileta usilazie damu. Unataka upewe gunia la chawa au Mungu ashuke toka juu akukabidhi Mke?. Shauri yako ukimwacha huyo demu abadili mawazo.
 
Hii hali ishanitokea, in fact inaniathiri hadi leo wakati nilifanya hivo zaidi ya miaka minne ilopita.
Well, mi nilifanya hivo kama kulipiza kisasi kwa ex wangu...nahisi na huyo dada atakuwa anajaribu kukutumia wewe kama mimi nilivofanya...nikuhakikishie kuwa athari ni nyingi kuliko faida, na kumbuka undugu ni hazina...hivi umefikiria siku mkiachana na huyo dada??!
Usiruhusu kutumika kama chambo, kama kweli unampenda huyo rafiki ako hii kitu itakuathiri maana nikuhakikishie kuwa urafiki wenu ndo utakuwa umefika mwisho.
 
Wakuu habari za mda huu. Kwanza kabisa TGIF.

Naomba niende kwenye mada moja kwa moja bila kupoteza wakati. Mimi ni kijana bado yanki kidogo nimehitimu chuo kikuu mwaka juzi. Sasa tatizo langu lipo kuwa kuna mdada ambaye tulisoma nae chuo ambaye wakati tukiwa chuoni alikuwa mpenzi wa rafiki yangu wa karibu sana.

Yani rafiki wa karibu kiasi cha kutosha maana tullikuwa tuna share mambo yetu na hata kusaidiana kwa hali na mali. Huyu shemeji wameachana kwa mda sasa tokea tukiwa chuoni lakini juzi hapa amenitafuta akaniambia amenimiss anaomba tuonane.

Kweli tumeonana na katika kukaa kwetu akaanza vijitabia ambavyo sikuvielewa elewa (kurembua rembua na mikonyezo mingi) ila nikajiongeza kusingizia dharura nikaondoka. Baadae usiku akanitumia sms kuwa kwanini namfanyia makusudi sitaki kukaa nae sijui anaumia moyo, nikashtuka sana. Kiukweli kwangu mimi naona kama jambo la ajabu ukizingatia alishawahi kuwa mpenzi wa rafiki yangu japo ni miaka kama mitatu imepita tokea walipoachana.

Naona kama kitendo cha kuwa nae ni kama usaliti kwa msela wangu japo sijui kama yeye atachukulia vipi au jamii mnachukuliaje swala kama hilo. Huyu binti ananitafuta kila wakati sio asubuhi mchana wala jioni, kisingizio ni kuwa anasema najali na alinipenda mda tokea chuoni ila ni baada ya kuwa alishakuwa na rafiki yangu.

Anadai alipenda jinsi nilivyokuwa mcheshi, ninaejali na nimaejituma kwenye masomo kuanzia ngazi ya mimi mwenyewe hadi kwenye group ambalo tulikuwa nae group moja na mara nyingi nilikuwa namsaidia assignments hata kama hakuwepo chuoni nilimfanyia na mwisho akapata na yeye GPA nzuri tu.

Tatizo kubwa jingine linakuja kuwa anajiamini kuwa ataninasa kutokana na hali mbaya ya ajira na maisha kuwa magumu na yeye kwao ulimbo upo na hata hiyo degree alisoma tu ili apate kujua masuala ya usimamizi wa biashara za nyumbani kwao, hivyo anatumia nguvu ya ulimbo kuninasa maana mpaka sasa nipo mtaani natangatanga sina hata shilingi.

Wakuu hali hii kusema kweli imenifanya nizidiwe na msongo wa mawazo ukizingatia kuwa mimi naona kama nitakuwa nimemsaliti mwana alafu kwa upande mwingine naona kama ndio sehemu ya kujifariji maana sina hata demu kila ninaemtaka anaringa kisa sina hela. Wakati hapa mbele yangu naona kabisa kuna faraja lakini nikimfikiria msela nakosa kabisa la kufanya.

Naombeni ushauri wenu wakuu nifanyeje.
PUMBAV KABISA,UMESHAPATA KAZI?
 
Mbali uoga kuhusu jamaa yako akijua... We unaonaje,ukiwa na huyo dada nafsi yako itaridhika?
Mimi hofu yangu kubwa ni jamaa kujua, je urafiki wetu utakufa kwasababu hiyo?
 
Acha nyodo wewe, kwani demu unayemtafuta hajatafunwa na wengine? Huyo unamwogopa kisa katafunwa na rafikiyo? Mtoto kajileta usilazie damu. Unataka upewe gunia la chawa au Mungu ashuke toka juu akukabidhi Mke?. Shauri yako ukimwacha huyo demu abadili mawazo.
Dah mkuu mbona mkali sana
 
Hii hali ishanitokea, in fact inaniathiri hadi leo wakati nilifanya hivo zaidi ya miaka minne ilopita.
Well, mi nilifanya hivo kama kulipiza kisasi kwa ex wangu...nahisi na huyo dada atakuwa anajaribu kukutumia wewe kama mimi nilivofanya...nikuhakikishie kuwa athari ni nyingi kuliko faida, na kumbuka undugu ni hazina...hivi umefikiria siku mkiachana na huyo dada??!
Usiruhusu kutumika kama chambo, kama kweli unampenda huyo rafiki ako hii kitu itakuathiri maana nikuhakikishie kuwa urafiki wenu ndo utakuwa umefika mwisho.
Asante kwa ushauri mkuu. Hebu naomba niambie nini kilitokea mkuu ili nipate funzo.
 
Asante kwa ushauri mkuu. Hebu naomba niambie nini kilitokea mkuu ili nipate funzo.
Narudia tena...kuna ushikaji na urafiki!! Mi naweza kumsaidia mshikaji wangu kama kuna tatizo na ninao uwezo wa kumsaidia.
Kuishi na mtu hostel au room moja hakuwafanyi muwe marafiki. Unaweza kuwa mlikuwa washkaji tu na huyo mtu aloachana na huyo dada.
ILA kama mlikuwa marafiki, yaani wale wa kushibana...wazungu wanasema BFF, yaani mkafikia undugu...trust me, hii kitu itakutafuna.
Inshort urafiki wenu utavunjika.
 
Mimi hofu yangu kubwa ni jamaa kujua, je urafiki wetu utakufa kwasababu hiyo?
Usihofu kuhusu jamaa kama unaona ukiwa na huyo binti nafsi yako itaridhika do it without any fearing...

Mengine yatakayojitokeza mbeleni uwezo wa kukabiliana nayo utakua nao just follow ur heart....
 
Narudia tena...kuna ushikaji na urafiki!! Mi naweza kumsaidia mshikaji wangu kama kuna tatizo na ninao uwezo wa kumsaidia.
Kuishi na mtu hostel au room moja hakuwafanyi muwe marafiki. Unaweza kuwa mlikuwa washkaji tu na huyo mtu aloachana na huyo dada.
ILA kama mlikuwa marafiki, yaani wale wa kushibana...wazungu wanasema BFF, yaani mkafikia undugu...trust me, hii kitu itakutafuna.
Inshort urafiki wenu utavunjika.
Mtihani huu mkuu
 
Binafsi nakushauri baki na msimamo wako tu,hata ukifanya naye lolote haiwez kuwa solution ya shida zako,we endelea kupambana utafanikiwa na kumpata wa kufanana naww
 
Mimi kwakweli kuwa na mahusiano na mtu aliyekuwa na mahusiano na rafiki angu naona ni usaliti.

Mimi mwenyewe rafiki angu akitembea na aliyekuwa mpenzi wangu, sitakaa nimtazame vizuri.
 
Usihofu kuhusu jamaa kama unaona ukiwa na huyo binti nafsi yako itaridhika do it without any fearing...

Mengine yatakayojitokeza mbeleni uwezo wa kukabiliana nayo utakua nao just follow ur heart....
Unanishawishi mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom