Nipo Njia Panda Naomba Mnishauri

Nipo Njia Panda Naomba Mnishauri

Sababu ya yeye kuachana nae uliijua?
Kulala na ex wa rafiki yako ni tabia mbaya.. yaani wewe ni utakuwa bomu usiyejiheshimu. Kichefuchefu kuwa hata unafikiria kufanya hivyo..
Sababu sijui mkuu maana nilikua sitaki kujiingiza kwenye ugomvi wao. Ila mkuu ndio hivyo mda huu tu nimetoka kuongea nae ananisisitiza kesho tutoke jioni
 
Mkuu for the sake of your friendship na mwana. Jikatae mbaba usile huyo shem wa kale.
Ila kama huna option kill the friendship beba huyo mtoto.
Option ya pili naitamani sana lakini moyo wa kuua huo urafiki na msela nao unaniwia vigumu
 
Sababu sijui mkuu maana nilikua sitaki kujiingiza kwenye ugomvi wao. Ila mkuu ndio hivyo mda huu tu nimetoka kuongea nae ananisisitiza kesho tutoke jioni

Kaa utulie tafuta wako.. tabia mbaya kushare
 
Huyo mchizi wako kama akaimaindi atakuwa boya....na wewe acha uboya kula huyo demu...nakumbuka nilikuwa na mchizi wangu very close friend kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari mpaka mtaani ....mi nikila demu na yeye anamvizia anagonga..na yeye akila demu nafanya hivyo hivyo....na wote tunakua tunajua....hakuna anaye mind...siku nyingine tukiamua tulikuwa tunapiga collabo(mtungo) hasa tukishamlewesha demu...na mambo yalikuwa yanaenda...mpaka nilkuja kuoa demu ambae pia alimkosa kosa kidogo...kwa hiyo nyie wote nawaona ni maboya kama mnamaind vitu vidogo namna hii,hao viumbe hawahitaji staha yeyote
Mnagongean mpaka Wake???? Aisee huo ni usela mav....
 
Walishaachana toka mkiwa chuo na alikuwa demu wa mchizi wako sio mchumba, hapo ulipo una magundi kitambo hujaosha rungu bibie kajileta mixer ulimbo upo.. nafikiri hauhitaji ushauri bali kofi la uso uamke
Dah
 
Wakuu habari za mda huu. Kwanza kabisa TGIF.

Naomba niende kwenye mada moja kwa moja bila kupoteza wakati. Mimi ni kijana bado yanki kidogo nimehitimu chuo kikuu mwaka juzi. Sasa tatizo langu lipo kuwa kuna mdada ambaye tulisoma nae chuo ambaye wakati tukiwa chuoni alikuwa mpenzi wa rafiki yangu wa karibu sana.

Yani rafiki wa karibu kiasi cha kutosha maana tullikuwa tuna share mambo yetu na hata kusaidiana kwa hali na mali. Huyu shemeji wameachana kwa mda sasa tokea tukiwa chuoni lakini juzi hapa amenitafuta akaniambia amenimiss anaomba tuonane.

Kweli tumeonana na katika kukaa kwetu akaanza vijitabia ambavyo sikuvielewa elewa (kurembua rembua na mikonyezo mingi) ila nikajiongeza kusingizia dharura nikaondoka. Baadae usiku akanitumia sms kuwa kwanini namfanyia makusudi sitaki kukaa nae sijui anaumia moyo, nikashtuka sana. Kiukweli kwangu mimi naona kama jambo la ajabu ukizingatia alishawahi kuwa mpenzi wa rafiki yangu japo ni miaka kama mitatu imepita tokea walipoachana.

Naona kama kitendo cha kuwa nae ni kama usaliti kwa msela wangu japo sijui kama yeye atachukulia vipi au jamii mnachukuliaje swala kama hilo. Huyu binti ananitafuta kila wakati sio asubuhi mchana wala jioni, kisingizio ni kuwa anasema najali na alinipenda mda tokea chuoni ila ni baada ya kuwa alishakuwa na rafiki yangu.

Anadai alipenda jinsi nilivyokuwa mcheshi, ninaejali na nimaejituma kwenye masomo kuanzia ngazi ya mimi mwenyewe hadi kwenye group ambalo tulikuwa nae group moja na mara nyingi nilikuwa namsaidia assignments hata kama hakuwepo chuoni nilimfanyia na mwisho akapata na yeye GPA nzuri tu.

Tatizo kubwa jingine linakuja kuwa anajiamini kuwa ataninasa kutokana na hali mbaya ya ajira na maisha kuwa magumu na yeye kwao ulimbo upo na hata hiyo degree alisoma tu ili apate kujua masuala ya usimamizi wa biashara za nyumbani kwao, hivyo anatumia nguvu ya ulimbo kuninasa maana mpaka sasa nipo mtaani natangatanga sina hata shilingi.

Wakuu hali hii kusema kweli imenifanya nizidiwe na msongo wa mawazo ukizingatia kuwa mimi naona kama nitakuwa nimemsaliti mwana alafu kwa upande mwingine naona kama ndio sehemu ya kujifariji maana sina hata demu kila ninaemtaka anaringa kisa sina hela. Wakati hapa mbele yangu naona kabisa kuna faraja lakini nikimfikiria msela nakosa kabisa la kufanya.

Naombeni ushauri wenu wakuu nifanyeje.
Tumia akili. Ukishindwa, jiulize ungekuwa wewe unafanyiwa hivyo na rafiki yako ungejisikiaje. Simpo mwanangu.
 
Tumia akili. Ukishindwa, jiulize ungekuwa wewe unafanyiwa hivyo na rafiki yako ungejisikiaje. Simpo mwanangu.
Nilisha solve. Siku hizi kaolewa na ni best yangu sana haipiti siku hajanitafuta.
 
Sijaona mahali umesema unamuogopa mungu kama utembea naye so na conclude huna hofu ya Mungu, hivyo nakushauri kagonge ila tumia Combat ya Jeshi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom