zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,935
Katika jumla jamala ya kutimiza krismasi, nimejishtukia nikialikwa kwenda kusherehekea krismasi Arusha. Kwa bahati nzuri (au mbaya?), mwenyeji wangu aliyenialika, kwao ni uso kwa uso na KIA na hapa kwao panaitwa KIA. Duh!
Cha kustaajabisha na ambacho "si kawaida", wenyeji wangu wamenitoa "outing".
Wenyeji wangu wamenileta kwenye "kumbi ya starehe" kwa jina panaitwa "kwa godi". Toka tumefika hapa saa moja kamili ya usiku huu mpaka nnapoandika haya, tunastareheshwa kwa nyimbo za taarabu. Si maajabu hayo? KIA na taarab wapi na wapi? Hususan Wameru! Amma kweli Kikwete ana shani yake na asifiwe. Nakumbuka "baniani mbaya kiatu chake dawa".