Nipe hereni na shanga nikupe watu, muafrika asivyothamini utajiri wake

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Simulizi nyingi za kihistoria zinatuambia kwamba machifu waliwauza vijana wengi wenye nguvu kwa wakoloni wa kizungu kwa kuwabadilisha na hereni/shanga na vitu vingine vyenye kuwakawaka machoni.

Nabakia nikijiuliza hata baada ya miongo mingi kupita, hivi kwa asili muafrika hakithamini cha kwake au kuna tatizo gani ndani kabisa ya ufikiriaji wetu?.

Chifu mmoja anawatoa mamia ya vijana wenye nguvu na kuwakabidhi kwa mzungu ambaye anampatia shanga, hereni na vitu vidogo sana kama malipo!.

Na siwezi sana kuwalaumu mababu zetu waliokuwa na mamlaka kwenye jamii zetu, mpaka leo hii Afrika imegawa bure kabisa rasilimali nyingi kwa wageni kwa kupewa shanga/hereni na vidani.

Mirahaba ya mauzo ya madini ambayo huenda kwenye serikali za kiafrika ambayo ni asilimia ndogo ya fedha kulinganisha na thamani halisi ya mzigo unaouzwa, ina tofauti gani na shanga/hereni walizopewa machifu nyakati hizo?.

Utayari wetu kupunjwa kwenye miradi mikubwa ya uwekezaji, utayari wetu katika kuwafaidisha wageni kutoka mabara mengine, ni kielelezo cha kuendelea kuishi kwa akili zile zile za kuchekelea shanga na hereni wakati mgeni kutoka mbali akitegemea kufaidika mara elfu kumi kulinganisha na kitu alichompa chifu wetu fulani.

Ninamuunga mkono yoyote yule asiyezuzuliwa na shanga pamoja na hereni anazopewa na mwekezaji, akijivunia utajiri halisi alionao, na akiwa tayari kuumiza kichwa katika kuupandisha thamani ili faida na ubora utakaopatikana baada ya kazi nzito, iweze kutuongezea utajiri.
 
Hope umesoma sehemu, umeshawahi kufanya kautafiti kidogo kujiridhisha na ulichokisoma na kukiandika humu?
 
Kaka siku zote Historia inamfavour anayeiandika, usitegemee kusoma kinyume na hicho ulichokisoma na kukiamini kwenye historia ukiyoandikiwa,

Kesho utaambiwa Wasukuma walikuwa wajinga wanachezea bao Almasi, na wewe ukaamini kweli walikuwa wajinga

Kwa taarifa yako vita zilipiganwa na Waafrika walijihami sana tu mpaka walifikia hatua ya kuchimba mahandaki kujificha
 
Angalia nilichokiandika halafu kitafakari kwa undani sana, maneno yangu yana maana nyingi unaweza kuyaongelea katika muktadha zaidi ya mmoja. Naheshimu sana historia ya nchi zote za Afrika.

Lakini ujumbe wangu ni tahadhari kwa jamii ya leo na ya kesho, tusijetukateleza tena. Najua kuwa wazee wetu walipigana dhidi ya ukoloni lakini wapo walioingia mkenge wa kudanganyika na zawadi ndogo ndogo.
 
Nimesoma kwingi sana mkuu, historia ni yetu iwe tunataka kuisoma au hatutaki.

Mkuu Phillipo tatizo liko kwetu sisi waafrika, kuanzia waliosoma mpaka wasio na elimu, bora hata wasio na elimu wana cha kujitetea. Umesikia kwamba Tazara anapewa mchina kuiendesha? Sasa katika mazingira haya huwezi kuona sisi wote ni mabwege wa kutosha?
 
Kulikubali tatizo siku zote ni mwanzo wa michakato ya utatuzi wake. Nashukuru kwa maoni yako mazuri.
 
Mama Tanzania ameshindwa kulisha watoto wake, mbali na utajiri alionao watoto wamedhoofu hawana afya wala amani ndio maana haoni thamani yao, wamedumaa kiakili wanashindwa kuindesha nyumba yao ndio maana wanatolewa zawadi nafasi ya kuleta mtoto toka jirani aliekula vizuri akapanua akili aje atuletee mafanikio, ipatikane.
 
Back
Top Bottom