Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Wakati tunapita JKT miaka 80+ kigezo Cha uaskari kilipimwa Kwa mambo yafuatayo;
1. Urefu
2. Mwonekano wa umbo
3. Uwezo wa kupiga paredi
4. Smartness Kwa maana ya unadhifu wa mavazi.
5. Unoko
Watu wenye sifa zilizoelezwa hapo juu bila kujali uwezo wao wa kufikiri,kupambanua mambo na kufanya maamuzi sahihi ambavyo ni vigezo visivyoonekana Kwa macho walipata Nafasi ya kujiunga kwenye Jeshi,polisi na vyombo vingine
Kwa mazingira ya kipindi kile walikuwa sahihi lakini miaka ilivyokwenda mbele watu wakaanza kujiuliza maswali yaliyopelekea reform isiyo rasmi. Swali la kwanza likawa, Ni ipi Nafasi ya mtu mfupi kwenye Nafasi ya kijeshi?
Ikabainika kumnyima mtu Nafasi ya kujiunga Jeshi lolote Kwa sababu ya ufupi nikuwanyanyapaa watu wafupi ambao vimo vyao ni chini ya vimo vilivyowekwa. Lakini pia ikabaini kigezo Cha urefu kiliwekwa na wazungu na wakati huo wazungu wakoloni awakutaka watu wenye akili maana wao walikuwa na akili,walitaka watu wenye nguvu na maumbo ya kutisha. Wadadisi walihoji endapo Jeshi linakitengo Cha ukachero,je makachero lazima wawe warefu na walioshiba?
Je, urefu na mwili uliojaa haviwezi kuwa vigezo vyakukwamisha ukachero? Wakazidi kuhoji mafundi cherehani na mafundi wengine lazima wawe warefu na wenye nguvu? Madaktari lazima wawe warefu na wenye misuli?
Waimbaji wa bendi lazima wawe warefu? Maswali haya na mengine yakawafanya watoa ajira hasa kwenye majeshi ya Nchi nyingi Afrika wakaondoa kigezo cha urefu nakutruhusu wafupi nao kupata nafasi japo sijui Tanzania kama mifumo yetu inaruhusu wafupi jeshini.Matangazo yetu Bado yameandikwa awe ana urefu 5.7ft Kwa wanaume wanawake nadhani 5. Najiuliza tunaajiri vimo au tunaajiri akili na maarifa yaliyopo kwenye vimo tofauti?
Dhana ya unoko nayo ikawa inatumika kupata maafisa inteligensia, yaani mkiwa JKt watu wanoko na wambea wakawa Wana nafasi kubwa yakupata kazi ya ushushu. Watu wasio na makoromeo wakapita mlango wa unoko wakaajiriwa.Tukumbuke dhana hii ilirithiwa kutoka Kwa wakoloni, wao walitaka watu wambea wawe viongozi Ili waweze kuwaletea majungu. Walitaka watu waoga wawe sehemu ya Jeshi Ili wakitishwa basi wajitokeze kusema "Afande Mimi sijashiriki walioshiriki ni flani n flani" .
Mifumo yetu ikaacha kuchukua IQ Kwa maana ya intelligent wakakusanya wanoko na wambea , watu intelligent wakaachwa Kwa sababu TU hakuna wanaposikika. Hawa watu walipopata ajira wakaingiza jeshini umbea wakakosesha majeshi mengi ubunifu na hivyo kukazaliwa mafarakano na kutoelewana, kukazaliwa ushirikana kwenye Kambi na kukazaliwa chuki na kutokuaminia.
Finally kota za majeshi mengi Zika sehemu yakuzalisha watu maskini na wasioelewa maana ya maendeleo. Kama mnakumbuka wakati wa mwalimu na Mzee Mwinyi mashushu walikuwa na kazi yakuhesabu umekunywa bia ngapi na kulinganisha salary Yako. Wakatoka makambini wakaingia mtaani nakuanza Kuanza kuangalia Nani amejenga wakiona nyumba nzuri ya mtu mweusi wakawa wanawapelekea taarifa wakubwa na bila analysis yoyote na kuhojiwa watu wakawa wanaishia mikononi mwa manjagu kwa visingizio kadhaa. Mashushu wa aina hii wakawafanya watumishi wa umma wawe walisha tumbo, wazinzi, watapanyaji wa Fedha wakiogopa kufanya maendeleo Kwa sababu wataulizwa umepataje Fedha
Hali hii yakuajiri wambea na wanoko ikazalisha wanasiasa wanaoiba Fedha Afrika na kwenda kuzificha nje bara la Afrika. Fedha zikajaa Uswiz bila kazi Kwa sababu wanasiasa hao hao ndio mashushu walioajiriwa kwa unoko na umbea. Wakazaliwa Waze ambao wanalipwa mishahara mikubwa lakini awawezi kujenga Wala kuishi maisha ya thamani au hafhi zao, wanatembelea gari zimechakaa kuaminisha wananchi kwamba wao ni wazalendo bila kujiuliza wana maawara wangapi na wanaonga kiasi gani? Wananchi nao wakawa wanasifia watu maskini kuwa ni wazalendo. Hii mentality imekwenda mbali Hadi Leo hii 2022 wapo watu nimeona Jana wanasema Bashingwa ni mtu humble na may be mzalendo kisa amepanda mwendokasi huko Dsm kutoka point Moja na nyingine. Inshort ushushu ukawa chanzo Cha umasikini na kudumaza fikra za viongozi wengi. Viongozi wanaotumia pesa kwenye anasa wakashindwa kufanya maendeleo wakawa wanaaminika wao ni wazalendo.
Hali hii yakuajiri watu kwenye vyombo nyeti wakiwa na uwezo mdogo nikaamini iliisha may be miaka ya tisini huko lakini Leo Mahakamani unamsikia kijana mdogo less than 45yrs kutoka kwenye chombo nyeti hajui maana sober, aelewi chochote kuhusu inteligensia, anashindwa kufanya analysis lakini kimwonekano na matamshi yake unabaini kama siyo mnoko basi ni mbea. Anatamka adharani mbele ya wanaume Kwa "NILISHINDWA KUKAA NALO ROHONI". Na mtu wa aina hii Yupo eneo nyeti na inlongrun anaweza akakabidhiwa watu awaongoze njia. What do you expect such kind of people.
Mazingira haya na muundo wa Jeshi la kikoloni ndio umenifanya nijiulize endapo Kuna uhusiano wowote baina ya wanaoteuliwa kwenye Nafasi ya ukomando na uwezo mkubwa wa IQ? Au Bado makomando wanatokana na sifa Tano zilizotajwa hapo juu?
Duniani Kwa Sasa let say America, watu wanaopewa nafasi yakwenda mafunzo ya ukomando asilimia kubwa ni wale wenye IQ kubwa si ya darasani TU Bali yakuchanganua mambo. Technologia na mbinu za kupambana na adui Dunian Kwa Sasa hazihitaji watu warefu na wenye nguvu zinahitaji uwezo wakutumia vifaa vya kisasa kupambana. Maisha yamebadilika Sana, mapigano mengi si ya silaha Bali mapigano mengi ni ya matumizi ya akili. Economic war.
Niwaombe Watanzania tutumie baraka iliyopo mbele yetu kuwakazania watoto wetu wenye akili kubwa waingie jeshini na kwenye vyombo vya dola wakaondoe gap lililopo. Tuamke, tulazimishe watoto wenye first class waende jeshini, watoto wenye vipaji waende jeshini naamini wingi wao utaondoa mashushu wenye vigezo vya umbea na uchonganishi na kuzalisha mashushu wanaowekeza kuzima majaribio ya wageni kujinufaisha na rasilimali zetu na kuwafungulia fursa hata kwakuwalinda watanzania wanaotaka kukua kiuchumi. Machinga wanapopigwa mabomu na kuibuka shushushu anayesema mateja wamewasha mishumaa nimatokeo yakukosekana Kwa watu wanaongalia changamoto ya machinga na kupush wanasiasa watengeneze solution kabla moto kuwaka na kutegemea watu ambao kwao wanapambana na janga linapotokea.
Tusipokubali kupeleka watoto wetu wenye uwezo mkubwa kwenda kutulinda tukategemea watoto wetu wenye sifa Tano nilizozitaja hapo juu huko tuendako Hawa watoto wenye maumbo makubwa, warefu na wanoko watashindwa kutulinda sisi na viongozi wetu na matokeo yake watageuka kuwalinda mabeberu kama walivyokuwa wanafanya babu zetu enzi za ukoloni.
Nadhani hata Sasa mnaweza mkaona Kati ya watu weusi na watu wenye rangi nyingine ni wapi walikaa mahabusu kwa wingi kipindi Cha uhujumu uchumi! Ni mabeberu wangapi walikamatwa na kupitia magumu kipindi Cha awamu ya Tano? Wenye rangi walitupia pesa Kwa DPP wakaondoka kwenda nje, vijana wetu wakabaki nasisi magerezani na kwenye surveillance huku tukiumizwa Sana. Sidhani kama kuna beberu aliyepotezwa na watu wasiojulikana, tulikuwa sisi weusi.
Na kizuri zaidi walipotumwa kuadhibu na kukamata walikamata wa CCM na wasio wa CCM. Means Hawa watu tunaoruhusu wakakae kwenye dola nakuacha vijana wetu wenye IQ nzuri IPO Siku watatukamata sisi wazazi wao Kwa maelekezo ya mabeberu.
Nimeandika maneno haya kuwafikirisha wanasiasa, wafanyabiashara, watumishi wa umma, wakulima na wafugaji kwamba kipindi cha kusema mwanangu amefaulu vizuri asiende jeshi kimepitwa na wakati. Kama tunahitaji walinzi wazuri kwetu na kwa Mali zetu tunahitaji tukubali watoto wetu wakalitumikie Taifa kupitia vyombo vya ulinzi na usalama waweze kutulinda kesho tutakapotajirika au Taifa litakapotaka kusimama bila wahisani.
Mwisho, ni fedhea kubwa Sana Kwa kiongozi aliyetengeneza Carrie yake for more than 30yrs, au mfanyabiashara aliyetengeneza utajiri wake for years, au mwanadiasa aliyejiimatrisha for years anashindwa kusherekea mafanikio yake Kwa sababu TU alishindwa kuandaa structure nzuri ya yeye kuishi Kwa heshima na haki mbeleni. Furaha ya maisha inaanzia kwenye usalama wa afya, Mali na Nchi unayokaa. Tuwasaidie waajiri kuondoa mfumo wa mabavu kwa kuajiri wenye uwezo wa kufanya analysis juu ya tafsiri ya ulinzi wa raia na Mali zake au ulinzi wa mipaka.