NIPASHE Wamshukia mbunge Madabida (CCM)

NIPASHE Wamshukia mbunge Madabida (CCM)

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,392
[h=2]Ukweli ambao Madabida amelificha Bunge[/h]
Juzi jioni wakati wa mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Zarina Madabida, alitumia fursa adhimu ya kujadili masuala ya kitaifa kuhusu afya ya Watanzania kushambulia watu na taasisi nyingine ambazo haziwezi kufika bungeni kujibu tuhuma hizo.

Miongoni mwa walioshambuliwa vibaya kabisa ni gazeti la NIPASHE. Alilitolewa maneno ya kashfa kubwa. Alisema gazeti hili linaandika habari za uongo.

Kilichomfanya mbunge huyo afure kiasi hicho ni habari tuliyoandika Alhamisi Februari 14 mwaka huu ikiwa na kichwa cha habari ‘Kada wa CCM akamatwa na shehena ya sukari mbovu.’

Katika habari hiyo pamoja na mambo mengine, tulisema hutumika kutengeneza dawa za kurefusha maisha kwa walioathirika na Ukimwi (ARV).

Alisema NIPASHE wamesema uongo, ni wazandiki, wanagombanisha CCM na wagonjwa wa Ukimwi, na kulitaka gazeti hili kuandikisha chama cha siasa kama linataka au vinginevyo liseme linatete chama gani.

Kwa kifupi, maneno ya mbunge huyu yametushitua sana, siyo kwa sababu nyingine yoyote ila kwa sababu kuu moja, kwamba ni maneno ya ovyo mno yanayotamkwa na mbunge kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chombo chenye wajibu mkubwa wa kusimamia serikali na kuwakilisha wananchi.

Siyo nia yetu hata kidogo kuendeleza malumbano katika suala hili kwa sababu tayari liko mahakamani.

Kuna kesi ya jinai namba 158/2013 iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Mkurugenzi wa Kiwanda cha Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI) kwa kosa la kuuza sukari iliyoharibika.

Kesi hii iko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive, itatajwa tena Mei 14, mwaka huu. Mara ya kwanza ilifikishwa hapo Machi 18, mwaka huu.

Kabla kufikishwa mahakamani kwa suala hilo, NIPASHE iliandika habari ya kuwako kwa sukari mbovu, ikimilikiwa na mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda hicho ambaye Madabida anamfahamu vizuri kwa kuwa ni mwandani wake, kama alivyothibitisha bungeni mwenyewe, Madabida ana maslahi na suala hili.

Katika habari hiyo, Madabida alitafutwa na kuulizwa juu ya kuwako kwa sukari hiyo ambayo ilikuwa inatoroshwa kutoka kwenye ghala la kuhifadhia bidhaa, alithibitisha kuwako kwa sukari hiyo, ingawa alimkejeli mwandishi wetu kwamba anachotafuta wala siyo habari, na kusisitiza kwamba hayo ni matokeo ya kufungwa kwa kiwanda chao.

Tuliripoti kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani na tumeendelea kuripoti na tutaendelea kuripoti hadi mwisho wake utakapofika kwa kuwa ni wajibu wetu kama chombo cha habari kufanya hivyo

Hatuhitaji kumuomba Madabida wala mtu mwingine awaye yeyote ruhusa ya kuripoti habari zinazohusu jamii, hasa inapokuwa ni suala la afya ya jamii kama ilivyo kwa sukari hii ambayo inamfanya Madabida afure bungeni, kwa bahati nzuri Madabida analijua hili, hatuombi ruhusa kufanya kazi yetu, na tutaendelea kuifanya hata kama akitaka kufura hadi apasuke!

Pamoja na kujua ukweli huo ambao hauna hata chembe ya uongo kama ambavyo anataka kuusadikisha umma, lakini kibaya zaidi akitumia nafasi yake kama mbunge kutushambulia mahali anapojua fika hatuwezi kufika kutoa majibu haya, basi nasi tumeamua kutumia fursa hii kuweka msimamo wetu sawa mbele ya jamii.

Kwamba amejaribu kututukana, kwamba amejaribu kujenga picha kwamba sisi tuliandika habari ile kwa sababu ya msukumo wa kisiasa na kwamba sisi siyo ‘Mwanga wa Jamii’ kama kauli mbiu yetu inavyosema ila ni ‘giza la jamii’, haya yote ni maneno ya ovyo na ni bahati mbaya yametoka kinywani kwa mbunge.

Hata hivyo, pamoja na kuzungumza maneno ya ovyo, bado hayawezi kumuondolea wajibu wa kusema ukweli na kwa kweli kuwajibika kama kiongozi wa nchi hii juu ya mwenendo mzima wa suala alilotumia muda mrefu mno kujitakasa la kuhusika kuanzia sukari mbovu na dawa feki za ARV ambayo yote yangali kwenye mchakato wa kisheria.

Tunajua ubunge ni utumishi, ni kuwatumikia wananchi, lakini hakika kama mbunge atafuta nafasi hiyo ili kukimbizana na maslahi yake binafsi kama alivyofanya Madabida juzi bungeni huku akijaribu kutuchafua, siyo jambo linaloweza kuachwa lipite hivi hivi tu.

Madabida anajua kwamba NIPASHE ni gazeti huru lisilofungamana na chama chochote cha siasa, anajua wamiliki wa NIPASHE, anajua zilipo ofisi za NIPASHE na anajua NIPASHE kwa miaka yote tangu lianzishwe mwaka 1994 limekuwa linaandika nini.

Ni kulionea na kupotosha umma kutaka usadiki kwamba eti lina malengo au mwelekeo fulani wa kisiasa kwa kuwa tu liliripoti tuhuma zinazomkabili mmiliki wa kiwanda cha dawa ambaye pia ni kada mwandamizi wa CCM.

Huu ni ukweli ambao hautafutwa na kebehi na matusi ya Madabida. Itabaki kuwa hivyo daima.

Tungependa kumpa ujumbe mahususi Madabida kwamba, dawa ya kukwepa kuandikwa kwenye vyombo vya habari kwa mambo mabaya ni kukwepa kutenda mambo hayo, vyombo vya habari vina akisi yanayotokea katika jamii, havitengenezi habari, hufichua na kuweka hadharani yanayotekea mingoni mwa jamii, kwa maana hii suala la sukari mbovu ni jambo lililotokea na limezaa kesi ya jinai ambayo ipo mahakamani, lakini hatujui ni kwa nini hili Madabida hakutaka kuliambia Bunge kwamba wana kesi mahakamani kuhusiana na sukari mbovu.

Tangu mkutano huu wa Bunge uanze umma umeshuhudia mara nyingi tu baadhi ya wabunge wakikatazwa kuzungumzia mambo ambayo yapo mahakamani, tumeona hata hotuba zikirejeshwa kwenda kurekebishwa kwa sababu zinagusa mambo ambayo yapo mahakamani, katika mazingira hayo na Madabida akijua kwamba kanuni za Bunge zinamkataza kuzungumzia mambo ambayo yapo mahakamani, alitumia Bunge kama jukwaa la kujisafisha, huku akiwaumiza wengine ambao hawana nafasi ya kufika kwenye jukwaa hilo kujitetea.

Madabida anajua kwamba serikali iliingilia kati suala la kuzagaa kwa ARV feki nchini, anajua serikali imechukua hatua dhabiti, na anajua kuwa suala hili liko kwenye uchunguzi, na anajua kuwa kiwanda chao kilifungwa kwa tuhuma hizo, kama anafikiri ameonewa na kama anafikiri anaandamwa kisiasa na kulipwa kisasi kama anavyodai, ni vema akawasilisha malalamiko yake kwenye vyombo vinavyochunguza suala hilo, kutumia Bunge tu ili ajisafishe huku akiwatundika msalabani watu wengine siyo jambo la staha wala uungwana ambalo linastahi kufanywa na mbunge kama yeye tena anayetokana na chama tawala.

Tunamshauri Madabida na wabunge wengine kwa ujumla wao, wawe na ujasiri wa kusema ukweli wote bila kupindisha maneno, kwa kuwa kutofanya hivyo siyo wanajiabisha mbele ya jamii tu, bali pia wanashusha hadhi na heshima ya Bunge kama chombo muhimu cha kuisimamia serikali na kuwakilisha wananchi. Baada ya haya tunaamini sasa Madabida atasema ukweli wote.


CHANZO: NIPASHE
 
Nipashe mlichokiandika wakai huo ni cha kweli tena ni ukweli usio na mashaka, tunajua kwamba ARV feki alikuwa anatengeneza na ilibainika hivyo, lakini i kweli kwamba alikamatwa na sukari iliyokwisha muda,na ni kweli kwamba namna ambayo alikuwa akiongea bungeni hata mimi msomaji tu wa nipashe sikufurahishwa hata kidogo,lakini si hivyo tu nilikerwa zaidi pale nilipokuwa namona akiongea kwa jeuri, kiburi, dharau na majivuno wakati ufisadi wake,uhalif wake unagusa moja kwa moja afya za watanzania.

Yote kwa yote ni kwa sababu Madabida ni kada mwandamizi na kaenda mbali zaidi ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaa,upande wa pili mkewe Zarina ni Mbunge wa viti maalum kupitia CCM,sasa nani atawafanya nini hata kama walitengeneza dawa feki,nani atawafanya nini hata kama walikutwa na Sukari iliyoisha muda.

Hao wanatoka CCM! Naamini hata ninyi Nipashe mkiandika sana juu ya habari hii mwisho mtafungwa mdomo, mtake msitake, maana kuna tatizo la vyombo vya habari kujipendekeza kwa chama cha CCM
 
mara nyngi ukweli unauma tena saana.
ukijua maana ya conflict of interest uwez pata shida ya kuelewa kauli za mbunge huyo.
pia inasikitisha badala ya kuwa na hoja za msingi bungeni, mbunge huyo anajenga hoja za kupindisha ukweli anao husika.
nipashe kwa hili nawapa pongez, namzidi kutuletea kinachoendelea.
 
Dawa ya Watu kama hawa inakuja , ni kufuta VITI MAALUM , kwa mfano Zarina hana uwezo wa kushinda ubunge hata ndani ya familia yake , Sembuse Jimbo ? Thubutu yake ! Amuulize Mumewe kilichompata Lindi 2010 !
 
Kwamba huyun fisadi aliyenufaika kwa kuwauzia ARV fake watanzania anaweza kusimama mbele ya bunge na kujaribu kujisafisha kwa kashfa ambazo amezitaka mwenyewe.

Hata kama nipashe wasingetoa ufafanuzi wa suala hili lakini watanzania wanafahamu kwamba kiwanda chao cha TPI kimefungwa kwa sababu ya kutengeneza ARV fake na pia wamefunguliwa mashtaka ya kuhifadhi/kutumia sukari mbovu kwa ajili ya kutengenezea madawa kinyume na sheria.
 
nilimtazama huyo mama katika hiyo issue kwa kweli alilipaka sana hili gazeti huku akiwa nalo mkononi.

hili bunge sijui kwa nini?
 
Tufikie mahali tuamue kwa usahihi aina ya wabunge tunawachagua
 
Wabunge wanajifanya miungu watu sana siku hizi hasa wakiingia mjengoni hawajui kwamba anapotoa hoja yake ni kwa mtazamo wake yeye kama yeye kwani hawezi kushindana na mitazamo ya watu walio wengi maana kila mtu anaamngalia kwa upande wake na mwisho wa siku yanakuja maelezo ya paragraph moja ambayo yanammaliza yeye mwenyewe.
 
Kiukweli niliduwaa kumsikia mbunge yule akitumia muda mwingi kutukana gazeti kwa uwongo ambao mimi binafsi sikuuelwa, kumbe maslahi yake yaliguswa. Pole Madabida.
 
Chunguzeni mnaweza kuta bunge ni kichaka cha wabunge wa CCM na maovu yao kwa taifa hili.
 
Kweli achague moja kuwa fisadi au kuwa mbunge na ile point ya mwisho safi sana maana wabunge wengine hawajui kazi ya mbunge ni nini lazima wawe wa kweli sio kupitisha mambo kichama bila kuangalia maslahi ya taifa sasa inaonesha kabisa wabunge wengi wa ccm wapo kichama zaidi hasa hawa wakuteuliwa na kuwa mawaziri maana hakuna wanae mwakilisha isipokuwa boss
 
Chama Cha Mazingaombwe. Kuukana ukweli uliowazi huko ni kutuhadaa.
 
Vijana wa Lumumba mko wapi? Au ndo mshazidiwa nguvu humu mtandaoni? Au chama chenyewe hakibebeki tena? Au hamjalipwa posho? Au mna mgomo? Manake siwaoni kuwatetea makada wenu kwenye nyuzi kama hizi. Wapi Faiza Foxy, Mwita25, Rejao, et-al?
 
Madabida AMESHIBA UTAJIRI SASA ANACHEUA MATUSI! kiburi watu wasiosogelewa wala kuguswa!
 
Ubinafsi dhambi mbaya sana,huyu mwanamke badala ya kusikitikia watu waliokufa kwa sababu ya
kutumia ARV feki zilizotoka kwenye kiwanda chake na mumewe,anaibuka kulaumu gazeti lililoweka wazi juu
ya uhaini wa kutaka kutorosha sukari iliyoisha muda wake kupelekwa kiwandani kwao Arusha.
 
Huo ndo ujinga wa viti maalumu. Ukitupa jiww gizani atakaepiga kelele.......,!!!!!!????
 
Wapi mbunge wa kilwa kusini, seleman bungara maarufu b.w.e.g.e, njoo utuondolee huyu madabida wa kike mjengoni kama ulivyofanya 2010 kwa mumewe! Kwa kweli vyombo vya habari vya IPP mfano nipashe na itv ndivyo vyenye uafadhari mkubwa ktk kuleta habari zisizoegemea upande wowote. siyo kama ma tbc yao.hongereni sana nipashe na msiyumbishwe wa hawa mafisadi wa CCM.
 
Back
Top Bottom