Mbunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Gidel Kiswaga akizungumza leo Aprili 2, 2026 kwenye Bunge la 13 Mkutano wa 3 kikao cha 3 Dodoma, ameeleza kuwa kulingana na hali ya kukosekana kwa mafuta duniana kufuatia mgoggoro unaondelea mashariki ya kati inabidi watanzania wakubali bei ya mafuta iliyoongezewa na serikali ni ndogo ukilinganisha nchi jirani Kenya huku akisitiza wananchi kupunguza mambo ya mitandao kuwa hayana maana." Nimeona maneno mengi kwenye mitandao kuhusiana na bei za mafuta ndugu zangu Watanzania kwanza mkubali kabisa kwamba sisi kama nchi serikali yetu imeongeza bei za mafuta kidogo ukilinganisha na namna majirani mfano Kenya Petroli wameongeza sasa inafika 5450 na diesel ni 5056 na mafuta ya taa ni 4400" Amesema Mbunge Jakcson Kiswaga