kwani uongo?mkandara,
hili la marc na dc kuchaguliwa kwa kura alilisema freeman mbowe mwaka 2005 wakamwita mkabila. Ccm walimwita mkabila kwa kauli hiyo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwani uongo?mkandara,
hili la marc na dc kuchaguliwa kwa kura alilisema freeman mbowe mwaka 2005 wakamwita mkabila. Ccm walimwita mkabila kwa kauli hiyo.
Katiba haisababishi uongozi bora na uongozi wenyewe hausababishi katiba bora. Wananchi ndio huchagua uongozi na wakichagua uongozi mbaya matokeo yake yako wazi; wakichagua uongozi mzuri basi uongozi huo utaweza kusimamia kuandikwa kwa Katiba bora ambayo wao viongozi bora watakuwa tayari kuilinda na kuwa chini yake.
Hivyo, wananchi bora huleta viongozi bora na ambao huongoza kuandika Katiba bota itakayowafaa wote; na ikishaandikwa, wote wanakuwa chini ya Katiba hiyo bora.
Ndio maana Katiba yetu inasema "wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali
itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;".. kumbe msingi wa mamlaka yote siyo viongozi, katiba n.k bali ni wananchi! So.. kama wananchi wakiwa wazembe mamlaka zitakuwa zembe..
Kumbe mkuu ulidhani nataka CCM wabadili katiba? kwani Zanzibar Katiba wamebadioli CCM? mabadiliko ya katiba yanaletwa na nia, nguvu na mshikamano wa wananchi, hata siku moja CCM hawawezi kukubali hilo. Vyama vaya siasa should dedicate their resources in mabadiliko ya katiba. Ogaha tusitegemee zur5i lolote kutoka CCM! mabadiliko yanaletwa na wananchi kupitia vyama, bila mabadiliko CCM watatawala milele study zimeonyesha hivyo.
Sio rahisi ni nguvu na kujitoa vinatakiwa hapo ikiwa na kuwa tayari kudhalilishwa na kulazwa polisi, na hili hatulitaki! na hao wanaosema wapinzani hawataki hili!
Webby............sitegemei kuwa CCM wataleta mabadilikoya katiba.......kama nilivyokwishaeleza...............suala la Katiba nakuambia heri hata ya sisi hapa JF tulilipigia kelel wee mapka CCM wakakja na majibu kuwa.....eti tuwaeleze mapungufu yako wapi ili warekebishe..............hivi vyama vya upinzani ukiondoa juhudi binafsi za Mtikila.......sitegemei sana si kwa CHADEMA au CUF bara................
CCM Zanzibar wanalazima kufanya baadhi ya mambo kwa sababu ya upemba na uunguja....... period!.........otherwise visiwa havitawaliki idadi ya wawakilishi wa upinzani ni kubwa.............halafu kumbuka kwa wao zinapokuja issue za Muungano..........ukiangalia kwa undani (i.e. behind the curtain) utaona wako pamoja (CCM, CUF and the rest)...............kupatana kwa Seif na Karume wala si kitu kingine..............ni common interest ya Wazanzibari.........if you know what i mean..............
............and trust me kama kuna kosa la kiufundi CCM walifanya kuhusu Zanzibar ni kukataa ushauri wa JKN kuhusu serikali ya Mseto............ilikuwa ni mbaya kwa CCM......lakini ilikuwa ni nzuri kwa mageuzi...............kwani pressure yake umeiona na matokeo.........ndio hayo............
Kwa hiyo utaona kuwa Zenji........nguvu ya mabadiliko yao imetokana na mgawanyiko wa uongozi uliopo i.e. Pemba na Unguja..............hii kitu bara HAIPO.............labda mapinduzi yatokee..........otherwise it will take bara centuries..........kama mwendo wa upinzani ndio huu...........trust me...........
Kwamba wananchi wameshawishika na kuaminishwa (wamedanganywa) kuwa nchi haina hela, isituzuie kuwaeleza ukweli. Kuwaeleza tu kuwa fedha zimetumika vibaya, na kuficha kuwaeleza kuwa EPA zimeibiwa fedha nyingi ambazo zingewaletea maendeleo, si jambo la busara sana.Monoko Mushi,
Leo ukiwaambia Wananchi kuwa bajeti na fungu la bajeti iliyopaswa kuleta Hospitali au kujenga barabara, Uongozi wa Wilaya umezitumia visivyo, ni rahisi kwa wao kuelewa kuliko kuanza kuwaelezea kuhusu EPA.
Kwanza tukianza kuwaambia Wananchi kuhusu EPA na kusema pesa zimeibiwa, ni rahisi wao kutupuuzia maana kila siku kauli wanazozisikia kutoka kwa Viongozi ni kuwa Tanzania haina pesa na wameshawishika vizuri kuamini kuwa hakuna fedha.
Ndio maana unakuta wanashangilia pale mtu anapokuja na kudai ati ana Wafadhili au marafiki ulaya ambao watatuletea misaada. Hii ni kutokana na wao kuamini Tanzania haina uwezo na Serikali yao bado inajaribu kujikwamua tangu tamko la Mwalimu Nyerere baada ya vita vya kagera aliposema tujifunge mkanda!
Monoko Mushi,
Mfumo bora ni mfumo shirikishi, mfumo huru wenye kutoa usawa na haki na zaidi kuwajenga wananchi kuwa huru na kuishi katika Demokrasi ya kweli.
Kilichofanyika Zanzibar 1992 ni mazingaombwe ambayo yaliishia kujaza maduka bidhaa za kuagiza na kuanzishwa kwa mfumo butu wa kisiasa.
Katiba haikubadilishwa, Sheri ahazikubadilishwa na bado CCM inaendelea kuongoza eti katika mfumo wa Vyama vingi lakini Katiba, Sheria na mengine mengi ni ya mfumo wa zamani uliokuwa ni wa Ki-TANU na CCM.
Ndio maana leo hii TISS wanahangaika kwa vitu vidogo visivyo na maana, lakini vile vya msingi hawavioni, tatizo ni mfumo tulionao.
Leo hii walioko CCM wanajifanyia wanachotaka, hakuna wa kuwashikisha adabu. Wakivunja sheria, wanaogopewa kwa kuwa Polisi na Mahakama bado zinatawaliwa na kuongozwa kutoka mfumo wa awali na katiba inayovifunga vyombo hivi.
Hata Bunge, linapaswa kuwa lenye nguvu huru, lakini kwa kuwa CCM haijiamini na wana wasiwasi kila siku, basi kudhibiti hata mapinduzi ndani ya Chama kutoka kwa Wabunge wake, wameendeleza mfumu butu ambao wabunge ni kama galasa kwenye karata!
Tukibadilisha mfumo tutapata nafasi mpya na kuvua zile nguvu za mabavu za CCM na wateule wake wanaojiona wako juu ya sheria.
Rev Kishoka,
Op Sangara ilianza baada ya CHADEMA kushinda uchaguzi mdogo uliofuatia kifo cha Wangwe. Mafanikio yake yanaweza kupimwa kwa kuangalia chama hicho kilivuna nini kwenye chaguzi ndogo zilizofatia Op hiyo za Busanda na Biharamulo. Hapa JF tunaweza tusijue mafanikio ya Op hiyo, lakini watawala wanayafahamu sana na yanawatisha kwelikweli!
Gag,
Kama OS ingekuwa effective, TAMISEMI 2009 ingemeguka japo kwa 45% na kwenda Upinzani! Lakini almost 98% ya TAMISEMI imerudi CCM, utasemaje Watawala wametishika?
Rev.Kishoka usipime ufanisi wa OS kwa kutumia kigezo kimoja tu cha matokeo ya TAMISEMI jaribu kuangalia na vigezo vingine hiyo ni kasumba ya wengi kwamba mwanafunzi kushinda mtihani ni hadi afaulu mtihani wa mwisho, mtihani wa mwisho si kipimo tosha cha uelewa wa mwanafunziGag,
Kama OS ingekuwa effective, TAMISEMI 2009 ingemeguka japo kwa 45% na kwenda Upinzani! Lakini almost 98% ya TAMISEMI imerudi CCM, utasemaje Watawala wametishika?
Luteni na Shalom,
Mtazamo wenu uko kwenye sehemu finyu ambayo ni Ubunge na Urais.
Serikali bora na siasa mbadala hujengwa kwanzia vijijini kwenda juu na si kutoka juu kwenda chini. Kosa la Upinzani mpaka leo hii ni kukimbilia ngazi za juu na si ngazi za chini ambako ujumbe wao utashika moto na kusambaa kwenda juu.
Sasa kama CHADEMA waliona hakuna maana ya TAMISEMI je wamejiuliza kilichotoke 2004 kwenye TAMISEMI na kukiwezesha CCM kushinda kwa kishindo 2005?
Hao wa TAMISEMI ndio wakala wa uchaguzi, wahamasishaji, watafuta wapiga kura, wanakata mbuga kutoka kijiji, kata, tarafa mpaka wilayani kuhamasisha. Hii ndio mbinu tulitumia kudai Uhuru wetu na kufanikiwa kumng'oa mkoloni. Hoo ni mbinu CCM wanaitumia mpaka leo hii kuendelea kuchaguliwa na kutawala.
Kosa lenu ni kufikiri kinachohitajika ni kushika Ikulu na Bunge pekee. Tanzania ya leo kubadilika ni kuanzia mitaani, vijijini, kwenye kata hadi tarafa na huko watu wakishaelimika, basi huku juu ni kazi rahisi.
Labda niwaulize moja la mwisho, kama ilikuwa ni gharama sana, mbona hata kwenye miji mikubwa ambako vyama ya upinzani inafahamika hakuna hata iti ya kutosa iliyoenda kwao kwenye TAMISEMI 2009 pamoja na watu wa mijini kuwa ndio wenye redio, magazeti, luninga na mifumo kebekebe ya kupashwa habari?
KishokaLuteni na Shalom,
Mtazamo wenu uko kwenye sehemu finyu ambayo ni Ubunge na Urais.
Serikali bora na siasa mbadala hujengwa kwanzia vijijini kwenda juu na si kutoka juu kwenda chini. Kosa la Upinzani mpaka leo hii ni kukimbilia ngazi za juu na si ngazi za chini ambako ujumbe wao utashika moto na kusambaa kwenda juu.
Sasa kama CHADEMA waliona hakuna maana ya TAMISEMI je wamejiuliza kilichotoke 2004 kwenye TAMISEMI na kukiwezesha CCM kushinda kwa kishindo 2005?
Hao wa TAMISEMI ndio wakala wa uchaguzi, wahamasishaji, watafuta wapiga kura, wanakata mbuga kutoka kijiji, kata, tarafa mpaka wilayani kuhamasisha. Hii ndio mbinu tulitumia kudai Uhuru wetu na kufanikiwa kumng'oa mkoloni. Hoo ni mbinu CCM wanaitumia mpaka leo hii kuendelea kuchaguliwa na kutawala.
Kosa lenu ni kufikiri kinachohitajika ni kushika Ikulu na Bunge pekee. Tanzania ya leo kubadilika ni kuanzia mitaani, vijijini, kwenye kata hadi tarafa na huko watu wakishaelimika, basi huku juu ni kazi rahisi.
Labda niwaulize moja la mwisho, kama ilikuwa ni gharama sana, mbona hata kwenye miji mikubwa ambako vyama ya upinzani inafahamika hakuna hata iti ya kutosa iliyoenda kwao kwenye TAMISEMI 2009 pamoja na watu wa mijini kuwa ndio wenye redio, magazeti, luninga na mifumo kebekebe ya kupashwa habari?
Kishoka
Ukitaka mafanikio ya haraka haraka jaribu wizi,
Lengo la chama cha siasa si kushinda uchaguzi peke yake lengo ni kuona yale unayoyataka yanatokea au kutekelezwa hata kabla ya kushinda uchaguzi, unaweza kushinda na kuingia madarakani ukashindwa ku deliver
CCM wako madarakani kwa muda mrefu wana resources nyingi wanamtandao mkubwa hadi vijijini kutaka kuilinganisha na Chadema ya juzi eti kwanini haikushinda TAMISEMI ni ufinyu wa kufikiria kutegemea kesho tu Chadema itande nchi nzima ni ndoto za alinacha kwa hiyo kupima matokeo ya TAMISEMI kati ya CCM na Chadema bila kuangalia hali halisi(reality) ni umasikini wa utafiti
Kishoka unaweza kuniambia mwaka 1994 Chadema ilikuwa inaongoza vijiji/mitaa na Halimashauri ngapi nafikiri ilikuwa haina hata kijiji, Halimashauri zote zilikuwa chini ya CCM tuambie hizo Halimashauri za Chadema na hiyo mitaa ya CUF imetoka wapi Kenya au ilikuwa ya ODM Kenya, sometimes tujifunze ku appreciate what opps parties are doing hata kama si kwa speed unayotaka wewe mipango huendeshwa kwa ustaarabu na taratibu ndiyo maana hapo juu nilisema ukitaka mafanikio ya haraka haraka jaribu kuwa mwizi hata wizi wa kura ni wizi kitu ambacho vyama vya upinzani ikiwemo Chadema hawakifanyi