Nionavyo Udhaifu wa Operesheni Sangara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nionavyo Udhaifu wa Operesheni Sangara

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Mar 27, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Nilitarajia Operesheni sangara ingeingia kila Wilaya na Mkoa si kujiuza kuhusu CHADEMA na kupiga vita CCM na kuioanisha na UFISADI, bali ni kuwatikisa Wabunge na Serikali za Wilaya.

  Naangalia hii Karamu ya Chai ya Wamarekani wanavyoisakama Serikali na Wawakilishi kwa kuwa mambo kadhaa hayafanyiki kwa manufaa ya Taifa au hao Wanakaramu wa Chai.

  Kwangu mimi Operesheni Sangara nilitegemea ingeingia kwenye kila Wilaya ya CCM na kuwauliza wananchi, kwa nini wanaendelea kuiamini CCM na huyo mwakilishi wa CCM?

  Ningewauliza tangu wamchague huyo Mbunge wa CCM:

  1. Maisha yao yameboreshwa kwa kiasi gani katika miaka mitano au kumi ya mbunge huyuhuyu?
  2. Wanafunzi wangapi wa Darasa la Saba wamefaulu na kwenda Shule za Sekondari na kufaulu Kidato cha nne?
  3. Zahanati ngapi zimejengwa?
  4. Vifo vya Watoto na Mama Wajawazito vimepungua kwa kiasi gani?
  5. Je kila nyumba, kijiji, kata na tarafa zina Maji, Umeme na simu?
  6. Je kila familia ina nyumba bora?
  7. Je Wilaya hizi zina shughuli za kiuchumi ambazo zinatoa ajira ukiachia biashara ndogondogo na kilimo?
  8. Je hali za maisha za Wakulima na shughuli za kilimo zimeongezeka kiasi gani?
  9. Je wakulima wana pembejeo, nyenzo, maghala na soko la uhakika kwa mazao yao?
  10. Je kuna waalimu, wauguzi na watendaji wa kutosha wenye uwezo wa kitaaluma na kiufanisi?
  11. Je Wilaya ina miundo mbinu imara, kama barabara za kutosha kuunganisha vijiji, tarafa na kata? mifereji, madaraja na vivuko imara?
  12. Je magonjwa kama Malaria, Kichocho, Utapiamlo, Kipindupindu na magonjwa mengine yanatokea mara ngapi na takwimu zinazokusanywa zinafanyiwa kazi gani kuhakikisha kuwa kuna kampeni imara kupiga vita maradhi?
  13. Je Wazee, Wajane, Wastaafu, Walemavu na Wasiojiweza wanapewa huduma gani na Serikali na maisha yao yana hali gani?
  14. Je Watoto, Wazee na hata watu Wazima wanapata Lishe bora kila siku na kwa uhakika?
  15. Je Kilimo ni cha kisasa na chenye kuwapa Wakulima Uwezo wa kuongeza kipato chao kwa kutumia Ukulima stadi na wa Kisasa bila kutafuta shughuli nyingine kujiongezea kipato?
  16. Je Wilaya hizi zinapiga vita kwa kiasi gani ajira kwa watoto walio chini ya umri wa kuajiriwa?
  17. Je Wilaya zina programu gani za kuwaendeleza watoto na vipaji iwe ni katika masomo, michezo, sanaa na sayansi?
  18. Je Wilaya ina mfumo gani wa kuchochea ubunifu na msukumo wa kueneza Sayansi na mifumo ya kisayansi katika shughuli za uzalishaji mali na nyenzo za uzalishaji mali?
  19. Je Wilaya, Vijiji, Kata, Tarafa na Mitaa zina shughuli za kukuza elimu ya Uraia, Demokrasia na ushirikishi kwa nia ya Kujenga Taifa, bila msuguano wa kiitikadi?
  20. Je Wilaya, Vijiji, Kata, Tarafa na Mitaa zina Viongozi Bora na Siasa Safi na ziko wapi katika kujenga jamii inayojitegemea na yenye ufanisi?
  21. Je Watendaji waliohujumu, kuonea, kuzembea au kufuja mali wamechukuliwa hatua gani katika ngazi za kiuongozi kwatika Mitaa, Kata, Tarafa, Vijiji na Wilaya?
  22. Je Uongozi na Watendaji wa Wilaya wanafuata kanuni na Sheria na ni watiifu kwa Katiba, Sheria na kanuni za kazi na kijamii?
  Kama nilivyosema, haya ni maswali ambayo ningetegemea Operesheni Sangara ilipoanza hadi leo hii, ingekuwa inayatumia katika ngazi za Mitaa, Vijiji, Kata na Tarafa kuleta changamoto na kuwaweka Chama Tawala na Watendaji wake kiti moto kwanza ndipo wao wajitangaze kama chama Mbadala na chenye kuweza kuyafanya hayo ambayo Mbunge huyu na Serikali hii ya CCM imeshindwa kuyafanya kwa Miaka 20 iliyopita.

  Ndio maana nilitahamaki sana niliposikia kuwa Vyama vingi vya Upinzani havikushiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na hasa CHADEMA ambayo ilikuwa na uwakilishi mdogo kwa kuwa wao wameekeza macho na akili zao kwenye Ubunge na Urais kupitia Uchaguzi Mkuu wa 2010!

  Kampeni hii ya kuhoji Wabunge na Serikali si kitu cha kunyemelea majira ya Uchaguzi Mkuu pekee, ni suala la kila siku kujikumbusha na kukosoa ili Watanzania waweze kuanza kuwa na upeo wa kufikira nje ya ahadi za Wanasiasa na Serikali ambazo hazitimizwi au zinanufaisha wachache!

  Ni maswali ya kwenda kuwabana kila Mbunge na Mkuu wa Wilaya ambaye ni wa CCM, bila kujali yeye ni Mpiganaji au ukaribu wake kwa Rais au bila kujali eti yeye ni kigogo au kizito wa chama.

  Bila kuanza kampeni hii kuhoji na kuonyesha udhaifu na mapungufu ya CCM na si kuzungumzia EPA, Richmond na mambo ya magazeti, itakuwa ni vigumu kujiuza kama chama kinachojua kinachofanya na chenye uwezo wa kurekebisha kasoro zilizofanywa na CCM na Serikali yake.

  Hivyo kama CHADEMA na Operesheni Sangara inakosa nguvu na ladha ya kuhoji haya, je tutegemee vipi kuwa watauzika na kuwa watakuwa Chama makini wakipewa dhamana ya kuongoza nchi?
   
 2. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #2
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Rev.Kishoka,
  Nakushukuru sana kwa maswali yako. Pamoja na kwamba ningependa kuona hoja yako inachangiwa ili tupate utajiri wa michango, ningependa kuweka awali kabisa kuwa hayo yote uliyoyasema ndiyo yanayofanywa na Operation Sangara. Ni dhahiri lugha na namna ya kusema tunatofautiana sana.

  Pili naamini hutegemei kuwa hotuba za vijijini haziendi kama unavyofanya research kwenda na Questionnaire, yaani listi ya mambo unayotaka kuyahoji.

  i) Operation Sangara mazingira yanatofautiana sana. Kwa kila Wilaya, Kata na kijiji inayoenda ina maswali ambayo inahoji CCM, na Mbunge wake wamefanya nini? kuna mahali inahojiwa Serikali yenyewe kwa maana ya DC iwapo malalamiko ya mahali yanaonyesha kuwa DC ni kikwazo katika eneo hilo kama ambavyo tumekuta kila mahali. Nakushukuru sana kwa focus yako, lakini ningelipenda wale ambao kwa "masikio yao" wamesikia hotuba za viongozi mbalimbali wakati wa Operation Sangara watupe feed back yao, na kutukosoa kwa kadiri inavyowezekana.

  ii) Ukiihukumu Operation Sangara kwa kile kinachoandikwa na magazeti, sidhani kama utapata picha kamili. Gazeti linatoa para chache tu kwa hotuba ya masaa kadhaa. Pia magazeti huchukua kile ambacho kwao wanaona ni "habari". Swala la elimu kwa Watanzania kwa magazeti mengi siyo habari. Nadhani ushahidi wa jinsi watanzania wanavyoitikia ni jinsi wanavyoitikia kwenye vibwagizo mbalimbali katika picha ambazo zimeonekana sana katika Operation Sangara ya Dodoma.

  iii) Operation Sangara ya Chadema haipo tu wakati wa Kampeni. Kumbuka Chadema ilianza 2007 mara baada ya kubadilisha Katiba na kuja na Kauli mbiu " Chadema Tumaini Jipya" tulifanya Ziara ya shukrani kwa zaidi ya mikoa 7. Tulipoanzisha mapambano dhidi ya Ufisadi, tuliwashirikisha wenzetu katika mapambano kwa kuzuguka tena mikoa kadhaa12. Kati ya mwaka 2003-2009 Chadema imekuwa ikitekeleza program yake inayoitwa " Chadema ni Msingi"( ambayo wengi ambao hawakufikiwa na programu hiyo hawaijui. Lakini kwa sisi tunaona matunda yake katika vijiji na vitongoji vingi tuliyopata mwaka huu. Tunaona kabisa tofauti kati ya maeneo tuliyofika na yale ambayo hatukuyafikia (inawezekana kabisa kuwa kati ya Op.Sangara na Chadema ni Msingi).

  iv) Inategemea wewe unavyoiona EPA, Richmond na ufisadi wote uliofanywa na Serikali ya CCM. Kwetu sisi, msingi mkubwa wa umaskini wa Watanzania ni ufisadi. Hivyo, huwezi kuzungumzia swala la Mbunge/DC/ RC na au hata JK na Serikali yake bila kugusia jinsi utajiri mkubwa wa nchi ulivyopokwa na kundi dogo la watu wachache walafi. Watanzania wanaelewa sana ukiwaeleza Billioni 155 za Meremeta zilivyoyeyuka na wao kukamuliwa na CCM kila kukicha kwa michango ya Shule(Sekondari na Msingi) au Zahanati, au hata Barabara. Siku hizi Wameanza hata kuwakamua wananchi kuchangia Mahakama. Haya yanaeleweka sana Brother, labda iwapo wako tu ambao hayo mambo yasizungumziwe kwenye Operation Sangara kwa kuwa yanaiumiza sana CCM. Hakuna anayeogopwa katika ukweli, Yatasemwa tu, hadi yatakapoeleweka. Ningependa nikukaribishe Operation Sangara ili siku moja uisikie mwenyewe bila kuambiwa....Kuona ni kuamini na vivyo hivyo kusikia kwa masikio yako ni kuamini pia.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  mchungaji maswali yako na nadharia yako ni tamu sana. Lakini sisi ni nchi ya amani, umoja, mshikamano na utulivu. Kutafuta majibu ya maswali hayo ni sawa na kupandikiza mbegu za chuki na mgawanyiko katika jamii hasa majibu yatakapotolewa kuwa serikali "iko mbioni", "ina nia", "imeanza mchakato" na "ina makusudio" ya kuyashughulikia masuala hayo yote "pindi wafadhili wakipatikana".

  Sasa Chadema ikianza kuyapush maswali hayo inaweza kuwafanya waonekane wanataka kuleta mgawanyo na wao wenyewe siyo watu wanaopenda confrontation za kisiasa. Ni kwa sababu hiyo usitarajie kwenye OS kuona wakibeba mabango ya kuwapinga wabunge mbalimbali au CCM au wanachama wao kuandamana hadi kwa mbunge wa CCM kutaka asigombee tena.

  Msingi wa OS (niko tayari kusahihishwa) ni hoja za kisomi za kwanini hali ipo jinsi ilivyo. Hoja hizi zinaendana na uanishaji wa hali halisi kwa kutumia takwimu mbalimbali, vielelezo mbalimbali na mifano mbalimbali ambayo inalenga kushawishi akili. Kwa kiasi kikubwa siyo "siasa proper" kama mifano ya karamu za Chai.

  Kwa hiyo uelewa wangu wa OS imefanikiwa sana kuwavutia watu kujiunga na Chadema, sijui kwa kiasi gani watu hao watageuka kupigia kura hasa kama CCM itaamua kwenda full throttle kuwabana wapinzani na kuwavutia wananchi.
   
 4. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #4
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  MMJ,
  Asante sana. Wiki hii tumeshuhudia kauli ya Mbowe kuhusu Malecela.

  Haiwezekani umaskini wa Wananchi wa Mtera ukaelezwa vinginevyo zaidi ya kuwa Mbunge wao amewatelekeza. Amekuwa kila kitu katika nchi hii, bado wananchi wake ni maskini wa kutupwa. maji taabu, njaa kila kukicha, elimu ndiyo hivyo tena. kama siyo Hospitali ya Mvumi Mission hata matibabu ni balaa.

  Hivyo, ni kweli katika hali halisi huwa hatusiti katika Operation Sangara pale hali inapohitaji hivyo. Na hii siyo kuchochea hata kidogo. Ukweli ni lazima tufike mahali usemwe tu, hata kama una uma kiasi gani. Ni kweli baada ya Operation Sangara Bungeni huwa hapakaliki.

  Kuna watu hatusalimiani. Lakini hatutafuti kusalimiwa, tunatumikia wananchi. Full Stop. Hivyo, pamoja na kukubaliana na wewe, ni bahati mbaya kila kinachosemwa kwenye OS huwa hakiripotiwi, lakini asilimia 99 ya hoja za Kishoka zote zinatumika, ila siyo kwa staili yake.

  Kama ulivyosema, ametumia sana "nadharia", Operation Sangara ni Applied Political Science, kama ninaweza kutumia lugha hiyo, kwa sababu kuna analysis nyingi zinafanyika kabla ya kufika mahali, mahesabu ya Halmashauri husika yanatazamwa kwa kina na wananchi kuulizwa kwanini hayo yanafanyika kama siyo kwa sababu "wao ndio waliotuma panya kwenye halmashauri" bila hata "paka" mmoja. I hope the analogy is understood.
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Hapa sasa ndio napata tabu kumuelewa Katibu wetu huyu SHUJAA. Sasa akiwa "kila kitu" ndo rasilimali zote upeleke kwako? Wakifanya hivyo Katibu unakuwa Mbogo kweli kweli kuwa ni FISADI. Ikitokea vinginevyo unamzomea (maana kauli hiyo ni kama kuzomea hivi)

  Nashauri Malecela ahukumiwe kama Mbunge sio kama "aliyekuwa kila kitu".Otherwise Katibu utuambie kuwa wewe ukigombea urais( kama nia hiyo unayo) ukishinda tu, baada ya miaka mitatu Karatu itakuwa kama Washington....
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Baadhi ya sera ambazo CHADEMA walizifanya na kuona vile CCM wanaiga kama vile kujenga UDOM, na kuna tetesi kuwa wanataka kujenga hospitali ya Rufaa tanzania kule Dodoma na pia kwa wale watu na baadhi ya marafiki zangu waliiambia kuwa Mbowe alisema siasa ya MAHALI!! REV.

  Elewa kuwa kuna SIASA ya MAHALI na SEHEMU, .... yaani kama vile Policies at village level au national Level. Kila wakati Mbowe na viongozi walisema mambo mengi sana kuhusu hali mbaya ya Dodoma na kuhusu CDA. kama kungekuwa na baadhi ya sauti au kuweka kwenye youtube baadhi ya mikutano yake basi ingekuwa vizuri sana.

  CHADEMA wamefanya mambo mazuri na pia wameeleza yote haya ila kwa kauli tofauti na Lugha tofauti sana Rev
   
 7. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  unauona ukiwa ng'mbo kupitia vyombo vya habari............. hutaki hata kukanyaga nchiyako mwenyewe japo ushiriki siku moja..... u radhi kumaliza karne nyingi bila hata ya kupiga kura............ sasa unalilia haki ya kuchukua uraia wa nchi nyingine ili ufaidi memea ya nchi zaidi ya TZ..........

  hawa unaokosoa, hujawaunga mkono japo kidogo tu, wao wamethubutu.......... wamekenda hadi kule zinakopatikana mbigili, zimewachoma na zinaendelea kuwachoma.......... wewe baada ya kubeba box na kupata senti kidogo, unatafuta mvinyo na kuwasha PC yako unasoam JF na unaanza kupekua wapi pa kukatisha tamaa wapambanaji!!!!!!!!!............... hakika kama seriakli yetu ingekuwa na robo ti ya watu wa aina hii, hali ingekuwa mbaya zaidi ya sasa.......... tungeteamani ufisadi kwani hali ingekuwa mabaya zaiid ya ufisadi............

  Dr W. Slaa na chadema, nawashukuru sana kwa huduma yenu hii kwa uuma....... yatasemwa mengi lakini operation hii inatia uhai katika demokrsia ya TZ kila uchao....... japo nami sijawahi kwaunga mkono kwa kusimama mstari wa mbele katika mapambano yenu, lakini walau natambua umuhimu wa mapambano mnayoendesha.......... nawatakia kila la heri..................
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,625
  Likes Received: 2,003
  Trophy Points: 280
  Rev Kwenye highlights ndipo palikuwa pakigomba!Hata hivyo naona Dr. Slaa amesharekebisha,ukweli mkuu ni kwamba kati ya maswali yako yote 22 hakuna ambalo halina uhusiano na ufisadi as a whole kuhusiana na perfomance ya taifa letu,yani tulipokwama!

  Reverand,utaacha vipi kuhusisha ufisadi na umasikini tulionao?Ni lazima tujuwe kwanza wapi tumekwama,je utajiri wa wachache haswa viongozi na umasikini wa wengi havina uhusiano?Na je uhusiano huo si ufisadi?
   
 9. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ume-miss-understand............ jaribu kutafakari tena........ kuleta maendeleo hakuna maana ya "kuhamisharasilimali toka maeneo mengine kupeleka eneo la kiongozi" bali "kutumia zinazopatikana katika eneo husika " rasilimali......... kuwa kiongozi wa ngazi za juu kama malecela kwa muda mrefu kama wake madarakani na katika uwakilishi inatarajiwa kuwa comparativelly angekuwa na added advantage........... sasa kukosekana kwa maendelo japo ya mfano jimbomni mwake na huku akiendelea kuchaguliwa kla uchaguzi kunaashiria nni.......... unaweza ksema kwa hakika ana mtazamo sahihi na hatua anazochukua ni sahihi??...... anataka kuendelea na madaraka na uwakilishi hata akiwa zaidi ya umri wa kitwa babu, sasa anagombana na wajukuu kutafuta uongozi, ipi sifa ya ziada tuitumie kumuunga mmkono??....... tutumie mfano gani hai kumtetea?............ tafakari..............

  Washingtonsio kipimo cha maendeleo.......... hapo umedhihirisha kuwa waweza kuwa kabwela mzito sana kuelewa...............
   
 10. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #10
  Mar 27, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  MzittoKabwela,
  Hakuna popote niliposema apeleke kila kitu Mtera.

  Alichotakiwa kuwa nacho ni ubunifu kwa lengo la kuokoa jimbo lake. Ukiacha ubunifu, kusimamia vizuri fedha na rasilimali zinazoelekwa Wilayani kwake na Serikali. Uzoefu ninao wa kusema hivyo.

  Nikisema Tanzania leo CCM wanahangaika kujenga shule za Sekondari za Kata wakati Karatu tuko kwenye ngazi ya Sekondari za Vijiji. Hatukufanya miujiza tulisimamia vizuri fedha zile zile zinazoletwa na Serikali na zimezaa matunda. Katika nafasi yangu ya Mwenyekiti wa LAAC nimeona ni fedha kiasi gani zinapotea kwenye Halmashauri nyingi kwa kukosa usimamizi.

  Hivyo, ninamlaumu kwa kitu tested na wala sikuwa na nia ya kumtaka ahamishe kila kitu kwake. Hapo napo ningelikuwa mbogo kama unavyosema. Inatakiwa balance, huwezi kuwa kila kitu, na kisha kwako pakawa patupu. Nadhani nimeeleweka.
   
 11. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,625
  Likes Received: 2,003
  Trophy Points: 280
  Huwa ninajiuliza iwe vipi tukubaliane kuwa tatizo ni uongozi halafu solutions za tatizo hilo ziwe tofauti na uongozi?Kuna mwenye kujuwa ni kwanini?

  Kwa mfano umasikini ukikithiri kwenye maeneo ya mbunge flani ina maana yeye hayuko responsible kama wengine wanavyoonekana ku imply?

  Yani kuwa tuna tatizo kuu la uongozi viongozi si ufisadi?Duh,kazi ipo!

  Naomba kueleweshwa kama kuna aliyeelewa.

  Mzitto Kabwela anasema kila kitu kisipelekwe jimboni,ok lets say yuko sawa,sasa ukweli si ni kwamba vinapelekwa kwa mafisadi?Kama huvipeleki bungeni kwako then ni wapi unavipelekea?Wewe uwe kiongozi,utajirike kwa jasho la wananchi(kodi zao nk)halafu udai kuwa umasikini wao hauna uhusiano na uongozi wako,does it make ne sense?
   
 12. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #12
  Mar 27, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna baadhi ya vyombo vya habari sometimes vinakuwa vina bies na CHADEMA, tunayajua magazeti makini sana kwa ajili ya kusema ukweli na pia ndio maana reveland anasema hivyo
   
 13. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa Katibu. Hakuna kulala.....
  Kazi njema,
  Mzitto
   
 14. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Dr. Slaa,

  Naam umeamka na kurudi kwa mkuku na nafurahi japo kuna mmoja wa wana CHADEMA kaamka kuja katika malumbano haya.

  CHADEMA mwaka huu mnatimiza miaka 18 tangu muanzishwe. Mmetumia mbinu nyingi sana tena za upole lakin mnaendelea kuzabwa makofi na mara nyingine kama Mzee Mwanakijji alivyosema, mnaonekana mna Woga kwa kujenga hoja kwa udhaifu au kukwepa mambo kadhaa.

  Kibinafsi, niatkuambia wewe ni pekee pamoja na watu wachache sana ndani ya CHADEMA ambao hamna uoga. Lakini kwa kuwa hakuna Umoja katika vita vyenu, si nadharia au kisa kuwa nasoma magazeti, bali ni hali halisi kuwa vita vyenu vina Ubutu fulani na ndio maana hata kwenye chaguzi zilizopita, bado mmendelea kuchechemea.

  Umeongelea suala la kupigia kelele Ufisadi, je leo hii ni hatua gani za kisheria ambazo zimekwisha chukuliwa kutatua tatizo la EPA au Richmond? Ikiwa leo hii tunajiuliza iweje Mabenki ya Tanzania yameibiwa Shilingi Bilioni 300 hivi karibuni, huoni kuwa kuna tatizo kubwa na kelele na mayowe kuhusu Ufisadi ni sawa na kupigia Mbuzi gitaa?

  Mlikuwa na nafasi nzuri sana ya kuanza kuleta mabadiliko kwa kuanzia kuwafikia Wananchi wakati wa Chaguzi za TAMISEMI mwaka jana. Bahati nzuri nilikuwa nyumbani nikakutana na Kitila Mkumbo na hata Mheshimiwa Zitto, nikawauliza, iweje kule kijijini kwangu, wanaofanya kampeni ya Udiwani ni CCM pekee, majibu kutoka kwa Watu wengi wa Upinzani na hasa CHADEMA ni kuwa nyinyi CHADEMA mmewekeza nguvu kwenye uchaguzi mkuu 2010.

  Nikajiuliza, mwaka 2004, Mzee Malecela alizunguka Tanzania nzima na kurudisha karibu TAMISEMI nzima chini ya CCM, na kilichotoea mwaka uliofuata ni Kikwete na CCM kujitapa na ushindi wa Tsunami wa asilimia 80!

  Je hamkujifunza?

  Nakubali kuwa mnayauliza haya maswali, lakini mnayauliza kwa upole na kana kwamba kuna hofu ya Dola au hamtaki kushikana mashati.

  Mzee Mwanakijiji huniambia CHADEMA Politics is too academic and text book and not true confrotational, kama vile CUF wanavyofanya Zanzibar.

  Ndio maana maswali yangu ni yanaonekana ni ya ushari kama wengine wanavyodai. Lakini kwa nini tuendelee kuwa Wanyonge na kuburuzwa kisa Amani, Utulivu na Mshikamano?.

  Nikirudi tena kwenye suala la Ufisadi, tatizo na suluhisho lake si kutokuwepo kwa CCM madarakani. Hata nyinyi mkipewa Madaraka au CUF kama hatutakuwa na kichaa bin mwendawazimu katika usukuani na kuleta Uongozi imara, basi tutaendela kuwa na ufisadi.

  Leo Rais Kikwete anatangaza kushoto na kulia tunapigana na Ufisadi, nyinyi Bungeni mnabanwa pumzi, mnahamisha mlingoti nyuma mkituambia eti kumi na nane ni pale na si huku, hoja zinazikwa, sheria haziundwi, hamna ushirikiano wa kizalendo hata kama mnatoka vyama tofauti, je mimi kama raia ,nitegemee nini kuwa mtafanikiwa bila ya kuwa na mabadiliko ya kiungozi si ndani ya CCM pekee, bali hata kwenu Wapinzani?.

  Tatizo la Tanzania ni Uongozi, hatuna uongozi imara, hatuna uongozi unaowajibika na kila mtu anaogopa kutoa changaoto ya kweli (challnge) kwa Uongozi uwe ni wa Taifa au vyama. Ndio maana kila kitu kinafanywa kwa compromise at expense of Mtanzania.

  Nisingeyasema haya kama Chadema mngeonekana mna mwelekeo au kuna effectiveness ya kampeni zenu za Operesheni Sangara. Tena tangu muanze Operesheni Sangara ni jimbo moja tuu, lililowapa kura Tarime, lakini kwingineko Kiteto, Busanda, Mbeya na majimbo mengine huku Visiwani, CCM imeyachukua pamoja na baragumu na vinubi vya kudai CCM ni EPA na Richmond.

  Ikiwa mbinu mnazotumia Watanzania hawazisikilizi au kuzifanyia kazi kwa kupiga kura dhidi ya CCM (ungetegemea mnachosema kinge esonate na hovyo nusu ya kura za TAMISEMI 2009 zingekwenda Upinzani), je hamuoni kuna ulazima wa kuanza kuwasikiliza kina Mchungaji Kishoka na kundi lake ambalo linawapa msukumona mtazamo tofauti?

  Ukipata muda, naomba uisome ile thread ya CHADEMA must Reform na Focus 2010 nilizoziandika miaka kadhaa iliyopita.

  Nisalimie Mzee Makani na Mzee Mchatta!
   
 15. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Moniko Mushi,

  Wabunge in BUTU, hata leo CHADEMA wakija madarakani, Wabunge wataendela kuwa BUTU bila kubadilisha mfumo wa Serikali yetu.

  Wengi wenu mnaweza kuchukulia uchochezi wangu wa kuhoji haya mafanikio kwa ufupi sana bila kuangalia kuwa matokeo yake yanaweza kuwa yapi.

  Kwanza tukiangalia kauli na matendo ya Wabunge wengi, utaona kuwa kila mmoja anategemea kutafuta wafadhili au kikundi cha watu binafsi kuleta maendeleo na si kuishinikiza Serikali Kuu. Hili ni tatizo, na linapaswa kutatuliwa haraka sana na njia pekee ni kuanza kuwafundisha wananchi kupima matokeo na si ahadi. aidha kuna ulazima wa Wananchi kuanza kujua kodi zao zinatumika vipi na si kushangilia mbunge kuwanunulia Ambulance au kujenga kisima cha maji na kuwaletea madawati au vifaa vya zahanati walivyowenda kuomba kwa wafadhili na marafiki huko ulaya na Marekani kama si michango kutoka kwa marafiki.

  Maswali hayo yakiulizwa kila siku bila woga, yatawaweka Wabunge na Watendaji kiti moto wachape kazi na kuifanya Seikali Kuu ianze kulazimika kupeleka na kuratibu maendeleo kwa ufanisi kila siku na si kusubiri kila baada ya miaka mitano na ahadi hewa.

  CCM hawawezi kubadilika, wenye uwezo wa kuwawabasilisha ni CHADEMA< CUF, TLP na sisi kama jamii!

  Leo tunaweza kubadilisha mtawala na chama, lakini kama hatutabasilisha mfumo ambao utatuletea viongozi waadilifu, wachapakazi na wenye ufanisi, tatizo letu bado liko pale pale, hapatakuwa na nafasi ya kuunda na kutunga sheria achilia mbali kuhakikisha zinafanya kazi ambazo zitawabana Mafisadi na kutuondolea upuuzi wa EPA, RICHMOND na Ufisadi wote ambao hadi leo hii inaonnekanza wazi kuwa tumekuwa tukipigia gitaa mbuzi, iwe ni kwa Watanzania au Serikali.

  Ikiwa leo hii Watanzania wanaridhika kukosa maji na umeme (nasema wameridhika maana hawajakasirika na kuifanya Serikali iamke) au hata hili suala la mgomo tunaona wanapoozwa na kuna wanaoridhika jamani twende Ikulu tukajadiliane, na huku kila mtu anajua ataambiwa kuwa Mishahara mipya au suluhisho litakuwa 2012, lakini msisahu kutupigia kura, je tukiimba kama Mbilia Bell au Papa Wemba na Mr. Nice kuhusu Ufisadi wataelewa au Watanzania watasubiri matokeo 2012?

  Mbinu za Medani zinabidi kubadilika, hichi ndicho ninachojaribu kuwashawishi CHADEMA, lakini wanajiamini sana kwa mbinu zao ambazo leo hii miaka 18 tangu waanzishwe, tumeyaona matunda yake!
   
 16. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  mmmmhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndugu Slaa, nina ombi binafsi naomba unifikishie kwa Freeman Mbowe. Kama hana mpango wa kugombea ubunge jimbo la Hai nainamsihi abadilishe mawazo, yule kijana wa CCM aliye mbunge wa sasa hivi hajatusaidia lolote kiasi kwamba hata jina lake silikumbuki.
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Monoko Mushi,

  Hizi EPA zimeibiwa lini? je Richmond, IPTL, Rada na Ndege koko na upupu mwingine umeanza lini? Kama tutasema ulianza baada ya Azimio la Zanzibar mwaka 1992, hiyo ni miaka 30 tangu tuwe huru na bado tulikuwa na umasikini.

  Ufisadi nna kilichohujumiwa katika Ufisadi ni kiwango kidogo sana na si tiba kwa Umasikini wa Tanzania.

  Ukisoma ripoti ya CAG, utaona ni jinsi gani pesa zinatumika vibaya na zinaidhinishwa kibajeti, lakini ni mali bila daftari.

  Nimekujibu hapo juu, suala ni Uongozi. Kule kwenye mada ya Azimio na Vijiji vya Ujamaa, conclusion yetu wote ni Uongozi.

  Ukiwahoji hawa Viongozi kuhusu utendaji na ufanisi, wakashindwa kujibu na kuonyesha matokeo, ndipo utaanza kujenga mtaji imara wa kisiasa ambao utawezesha kupata kura Bungeni ambazo zitalazimisha kutungwa Sheria na hata kubasilisha Katiba.

  Focus yetu ya kuleta maendeleo tumeiwekeza kwenye kulilia mambo ya Richmond, huu ni mwaka wa nne sasa Tangu tujue tulihujumiwa na Richmond. tumeunda kmati, tumechunguza, lakini hakuna hatua za kisheria au kinidhamu zimechukuliwa. Sawa na suala la EPA, Mzee Balali katutoka, hakuna ambye yuko tayari kumkaba koo aliyekuwa Waziri wa Fedha hata Rais kujua iweje kulikuwa na uzembe na kukosekana kwa ufuatiliaji makini ambao usingetuletea EPA?

  Leo hii tunajiuliza, pamoja na kelele zote kuhusu Ufisadi, sijui EPA na upuuzi mwingine, Watu wamejichoeta Bilioni 300 kutoka mabenki ya Tanzania, je hatukujifunza kujenga mfumo bora wa kifedha baada ya EPA?

  Jibu lake ni moja, hatuna Uongozi Imara, hatuna Uongozi Makini na hivyo kushinda Umasikini wa Tanzania si vita vya UFISDI pekee, bali ni kuwa na Uongozi Fanisi na Imara unaojua kuchapa kazi na unaowajibika na kuwepo na chombo chenye uwezo wa kuwajibisha!
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Mar 27, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,610
  Likes Received: 3,911
  Trophy Points: 280
  Mimi pengine naweza kuwa na mawazo ya tofauti kwa kuangalia hali halisi ya nchi, tulikotoka tulipo na tunakoenda. It is known and proved kuwa wananchi ndio wanaoviangusha vyama vya upinzani vikichangiwa sana na wapinzani wenyewe.

  Honestly, speaking from bottom of my heart, SIONI na sitaona faida ya operation sangara, uchaguzi wa wabunge au lolote linalihusu hali ya siasa if and only if Katiba haitabadilishwa.

  Kwanza nchi hii siyo ya CCM huwa nasema hivi siku zote, wala si ya chadema wala haitakuwa ya CUF or NCCR! Kuwa na mfumo huu wa sasa kuendesha nchi kwa hizi nchi zetu ni wastage of time and resources.

  Sasa angalia kwa mfano, INTELLECTUAL, engines, propellers,brainy etc wengi wako upinzani, tena Chadema, which I am pretty sure ndio kwa namna moja au nyingine wanaliongoza taifa hili indirectly!

  I once said , chadema sio chama ni consultants, mawazo mengi ya chadema ndio wanatumia CCM na kuwapa wananchi, then what is CHADEM for, kama mkisema sera zenu na mawazo yenu CCM wakayachukua na kuyaweka kwenye practise? mwananchi wa kawaida in a long run hataona umuhimu wa kuchagua upinzani!

  Solution na kitu pekee kinachotakiwa kwa sasa na lazima kifanyike ni Mabadiliko ya katiba, kuwa na serikali ya mseto, serikali ambayo itakusanya vyama vyote na kuliongoza taifa kutokana na asilimia ya kura watakazopata. na HAPO NDIO WATANZANIA WATAKUWA ANALIONGOZA TAIFA LAO siyo CCM!

  I do believe . mabadiliko ya katiba ndio ukombozi kwa sasa , serikali ya mseto haiji kama zawadi we need to struggle and sit down and talk with CCM, ikishindikama mazungumzo then kuna namna nyingine watu watazipenda, tena mnaweza mkatumia nafasi hii ya hali ngumu ya maisha!

  Kinachoendelea sasa hivi ni kuwa vyama vyote vya upinzani vinakiri kwa namna moja au nyingine kuwa nchi hii ni ya CCM na CCM only should rule!

  Serikali ya Mseto ina stimulate vitu vingi sana kimojawapo ni kukua kwa demokrasia na ku-wa-convince watu kuingia chama fulani.

  Sorry to say this, Operation sangara, nyavu, ndoano, etc, uchaguzi wa wabunge n.k havileti maana yoyote kwa sasa hivi, bunge bado ni la chama kimoja. Kuzungumza wala hakuleti tija, CCM they will let you talk and talk and talk.......

  Tumelia na kuomboleza kuanzia mwembe yanga, still watu wanawatunza na kuwashabikia hao mafisadi, Rostam anaapishwa Igunga kama kamanda wa CCM, Lowasa, Karamagi, Chenge n.k hawa wote wanasifiwa na kuinuliwa na wananchi wenyewe! yet Operation Sangara mawapelekea watu waliotyari kuwabeba mafisadi!

  Operation sangara inalenga kuwabadilisha watu, contrary na hali halisi, mabadiliko ya watu yanaanzia mbali sana Chadema haitaweza hili peke yake, mabadiliko ya fikra yanaanzia mashuleni, makanisani, msikitini n.k!

  Pamoja na kuwa nimewasifia hapo juu kuna watu vichwa, lakini kuna eneo linasahauliwa sana nalo ni kujua saiokojia ya wananchi wa Tanzania, Mrema alibebwa na kuja kutahamaki wanaombeba hawapigi kura wala hawajajiandikisha! kumbe watu hata umuhimu wa kupiga kura hawauoni!

  Bila mabadiliko ya katiba, ili tuwe na serikali ya mseto any subsequent political activities will never be productive,

  Mabadiliko ya katiba yanawezekana, Zanzibar wameweza, this year alone ulikuwa mwaka mzuri sana kwa sababu wengi hamtaki ku-compete na JK! Mwaka 2015 CCM wakisema wanamsimamisha Magufuli! then wapinzani muwe mnahesabu maumivu tu

  CCM leaders are the only names ambayo watanzania wengi wanayajua, na CCM wanaringia hilo, hata leo hii thread nyingi humu JF watu wanawaza marais wa 2015, 2020 kutoka CCM!

  Dr. Slaa ulisema mmeshapiga kelele sana kuhusu Katiba, na serikali haitaki kusikia hilo!!!!??? I CCM hawatakubali kirahisi anahitajika kiongozi mwenye nguvu, hiyo ndiyo only barrier kwa sasa nchini mwetu, bila hivyo hesabuni(tuhesabu) kuwa lolote lile mfanyalo halina manufaa kwa watanzania wanaotaka ukombozi wa ujumla, mnachofanya ni kuwaletea manufaa watanzania kwa kuuza sera zenu kwa CCM , nyie sio consultant wa politics au chama cha policy makers you are opposition party for God sake.

  I stand to be corrected! However anayetaka kupinga aje na jibu zuri na la matumaini kwangu ni lini tutaweza kuindoa CCM madarakani kwa style ya siasa yetu hii, tusipoweza kujibu hapo then lets change tactics!
   
 20. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Guna mpaka utapike.......
   
Loading...