Nionavyo: Ccm inategemea huruma za Chenge, Lowassa na Rostam kujivua gamba

Kwa hali ilivyo sasa hivi ni Kwamba CCM haiwezi kumfukuza Chenge, Lowasa wala Rostam, kitu kilichokuwa kinapanfwa ni wao kuwaomba hao Jamaa wajitoe. Huu ni Mchezo wa Kuigiza ambao CCM wameshaona itakula kwao maana Pamoja na Kuja na Staili ya Kujivua Gamba naona Sasa wanaitwa Chama Cha Magamba

CCM wanaendelea kunegotiate na RA, EL na AC, wajivue Nyadhifa zao je hii Itasaidia? Asante Dr. Slaa kuliona hili Mapema na Kutibua Mpango Mzima


Huo ni utumwa wa fikra. Kila kitu Dr. Slaa! Tumechoka bootlicking hii iliyopitiliza.
 
Chenge na Lowasa: muungwana ni kitendo
Tumeona jinsi RA alivyopewa heshima kiasi cha kuitwa kufungua kampeni na bwana mkapa huko igunga...itakuwa pia jambo la busara kwa chenge na lowassa kujiudhuru fursa zao ili kujiwekea heshima ndani ya chama badala ya wanavyoonekana sasa kama wapangaji ndani ya chama..nawasilisha
 
Wajiuzulu wamerogwa hao..mmoja anautaka urais, mmoja anatumia ubunge kama kinga kuficha uchafu wake wa mikataba ya ufisadi na mauaji.
 
Mziki wa Igunga ulivyokuwa mzito sijui kama hata hao neo-CCM watawakubalia wajiuzulu
 
Pale hakuna wakujiuzulu. Unafikiri zile posho za ubunge hawazipendi, ufisadi wanaoufanya kupitia vyeo vyao. Dhubutu.
 
Mbona yalikuwepo maneno kuwa mpango wa kujivua gamba ulikuwa unachagua majina, na kwamba hao ambao jina/majina yao hayahusiki sio walengwa wa huo mpango.Ngoja tusubiri tuone ccm c wanaweza kutoa tamko
 
sidhani ka Lowasa ukimwambia hili atakuelewa ka huwa anaenda kwa TB joshua nigeria kusali n akufanyiwa maombi akiamini atakua Rais unadhani antaka kujiharibia ssa
 
Hawavui gamba hao maana hata intelijensia ya magamba sasa imesitisha zoezi hilo baada ya kazi ngumu iliyofanyika Igunga. Huko Songea sasa kuna pressure ya kuwafukuza madiwani waliopiga kura ya hapana ila nalo wanajiuliza mara kumi kumi tutazikomnboa hizo kata? Maana wanajua CDM ni moto wa kuotea mbali
 
Chenge na Lowasa: muungwana ni kitendo
Tumeona jinsi RA alivyopewa heshima kiasi cha kuitwa kufungua kampeni na bwana mkapa huko igunga...itakuwa pia jambo la busara kwa chenge na lowassa kujiudhuru fursa zao ili kujiwekea heshima ndani ya chama badala ya wanavyoonekana sasa kama wapangaji ndani ya chama..nawasilisha

Mpango wa Kujivua ghama umeonekana hauna faida kwa CCM na NAPE very soon ataoneshwa mlango kwa kubadilishiwa kazi. Uchaguzi wa mbinde wa Igunda ni kicheko kikubwa sana kwa LA and EC. Neno gamba kwa sasa hivi hutalisikia tena toka kinywani mwa NAPE et al. Uchaguzi wa Igunga ulikuwa ni mtihani mkubwa kwa uongozi mpya wa CCM na kushinda ilikuwa ni kwa vyovyote kama walivyofanya, kusupress turn up kwa kuvuruga daftari la wapiga kura Igunga.
 
Dhana ya kujivua gamba na ilivyotekelezwa ndio imeiweka pabaya zaidi ccm kuliko ilivyokuwa awali kabla ya mpango huo!
Kuna uwezekano wa vijana wengi viongozi wa chama hiki kuachana nacho hali ikiendelea kama ilivyo sasa, nikiwemo mimi mwenyewe
 
CCM Wanamwogopa Lowasa? Mbona naona kama wanakesha Wakiomba Jamaa ajing'atue ili Watangaze kwamba Wamamvua Gamba? Kwa nini Wasimtimue?

Hivi CCM na kuwa na Polisi, Mahakama, Jeshi, Magerereza wanamuogopa hivo Lowasa? Mbona Lowasa ni Mwepesi jamani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom