Lowassa, Chenge na Rostam - Nini hatma yao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa, Chenge na Rostam - Nini hatma yao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mshikachuma, Apr 15, 2011.

 1. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Heshima yenu wana jamvi!

  Waswahili usema mwisho wa ubaya ni aibu, na malipo ni hapahapa duniani. Siyo siri HOT NEWS ndani ya wiki hii ilikuwa ni ccm na kujivua gamba. Baada ya vutanikuvute huko Dodoma....ikaishia kwa wah.Lowassa,Chenge na Rostam kuvuliwa nguo hadharani na kutupwa nje ya CC ya ccm kwa tuhuma za ufisadi uliokubuhu bin sugu.

  Chenge :alipokuwa mwanasheria mkuu wa serikali alihusika na ufisadi kwenye Rada,na aliita mabillions yake aliyoficha nje ya nchi kuwa ni vijisenti tu! Pia huyu ndiye waziri alieongoza kwa kusaini mikataba fake kwa uroho wa fedha....haitoshi hapa majuzi aliendesha gari yake ambayo haikuwa na bima na ikaishia kuuwa wadada 2 na kesi yake ilighubikwa na mazingira ya rushwa na ikaishia yeye kuachwa huru.

  Lowassa :alipokuwa waziri mkuu wa serikali alihusika na ufisadi kwenye project ya Richimond,na inasemekana ana mabiashara makubwamakubwa ndani na nje ya nchi zilizotokana na wizi wake wa kuliibia Taifa....mfano mdogo ni hizi biashara zake zinazoanzia kwa majina ya Alpha....

  Rostam :huyu ndiye fisadi nguli papa a.k.a Rais wetu. Alipo kuwa mpambe wa marais wetu na huku akiwa mtunza hazina wa ccm,alihusika na ufisadi ndani ya B.O.T kwa kujichotea mabillions ya EPA na kuyaingiza kwenye kampuni ya kagoda. Pia alihusika na Richimond na sasa yupo hata kwenye Dowans.

  Kama tulivyoona na kusikia jana kwenye vyombo vya habari kuwa hawa jamaa 3 hawatakiwi tena ndani ya ccm. -Sasa Je,
  1. watarudisha kadi za uwanachama wa ccm na kuachana na siasa moja kwa moja?

  2.Hawa wote ni wabunge - ni nini hatma ya majimbo yao na wapigakura wao?

  3.Je, wanauthubutu wa kuanzisha chama chao cha siasa na wakakubalika kwa jamii?

  4.Je,kuna chama chochote cha upinzani kinachoweza kuwapokea hawa jamaa?

  5.Au wafilisiwe tu na kufungwa jela?

  Nakaribisha mgongano wa kimawazo na kimtizamo - Ahsanteni
   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wanaweza kuanzisha chama, ila hawawezi kwenda kwenye chama ambacho tayari kipo hai.
  Chama tawala kitoapo kauli...angalia nyuso za viongozi wao waongeapo ndipo utajua alama 'iashiriayo'
   
 3. M

  Marytina JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kwa nini waanzishe chama wakati CCM ipo?
  Nani mwenye udhubutu wa kuwafukuza ccm wakati wote magamba (JK RICHMOND,Mkapa Kiwira au Meghi)
  Mimi naona watanue kwa raha zao na kama JK atajidanganya kuwaweka pembeni ataumbuka sana .

  EL RA AC musijiuzulu tuone nani wa kuwashika uchawi hapo CCM
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Wasibughudhiwe, wafilisiwe kwa stail ya Kigoma Malima.
   
 5. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Lakini pia kuna swala lingine ambalo tunapaswa kujiuliza. Je uchaguzi ujao wa mwaka 2015 hawa jamaa watatetea majimbo yao au watakaa kando tu kusubili huruma ya chama chao cha ccm?
   
 6. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Hao Jamaa watatu tu Wakiamua kuimaliza CCM wanaweza, wana wafuasi na wameweka mizizi ya ajabu. CCM wawaombe msamaha kwa kuwaita MAFISADI bila ushahidi wa kisheria.

  Pili CCM Ihakikishe inayalinda maslahi yao na familia zao, wasisumbuliwe na mtu yoyote, vinginevyo wakiamua kuimaliza CCM WANAWEZA tena less than 7 days. NAPE hawezi ubavu wa EL, RA NA CHENGE. Bado bwa mdogo sana.
   
 7. F

  FUSO JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Hakuna mtu ana ubavu huo, kama nilivyosema wakiamua kisambaratisha chama wanaweza in less than 7 days. Kwanza kuna ushahidi gani wa kisheria kwamba ni Mafisadi?. CCM ijiangalie sana.
   
 8. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa nakubaliana na wewe kabisa....hawa jamaa wanamambo mazito sana (siri) zinazoihusu ccm,so wakiamua kuimaliza basi ni ndani ya siku 7 tu na ccm inakuwa kwishney
   
 9. Mswahilina

  Mswahilina Senior Member

  #9
  Apr 15, 2011
  Joined: Apr 7, 2008
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe unachekesha kweli, eti wafilisiwe kwa stail ya Prof. Kighoma Ali Malima, hii haitawezekana, hata Malima mwenyewe tuliyemfilisi leo Mtoto wake wa kutoka kwenye damu yake mwenyewe ndiye naibu waziri anayeshughulikia madini. Je tutafika?
   
 10. i411

  i411 JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  kweli maisha ni double standars kila mahali yani wao ni wezi na wanapete tuu hivi hivi na hatuwezi kuchukua hayo mali zao
   
 11. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #11
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watatoka lkn si hivihivi tu kwanza watamalizia kukiua ni ka kuku wa kideli kummalizia kwa kumchinja huna hata kazi ya kumkimbiza!
   
 12. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,454
  Trophy Points: 280
  1. Warudishe haraka mali walizoiba na kupora pamoja na riba.
  2. Wasimame kizimbani na kuwataja waliohsirikiana nao kuihujuma Tz muda wote
  3. Watubu na kuacha mambo na mawazo yoyote ya kifisadi
  4. Wawekwe chini ya karantini ktk jamii zinazowahusu, wakifuzu....
  5. Wapewe nafasi ya kuishi Tz ila wasikae (never ever) wapewe cheo au dhamana yoyote hadi mauti yao.
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,134
  Trophy Points: 280
  Nimeonewa sana....nimesemwa sana.......hii yote ni sababu ya uwaziri mkuu....(sijui km atathubutu kusema upuuzi km huu kwa mara hii)
   
 14. F

  FUSO JF-Expert Member

  #14
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  JK kawatosa wenzie waliomsaidia kuingia ikulu - sio freshi ingetakiwa aondoke nao tu.
   
 15. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Jamani ukweli ni kwamba uhai au kifo cha CCM kipo mikononi mwa Lowassa na Rostam Azizi. Hawa wana siri nyingi sana kwani ni vema ujue ufisadi hawakufanya peke yao bali kwa ushirikiano na vigogo wengi wa chama na serikali. CCM labda haijafanya utafiti ijue uamuzi wanaotaka kuufanya unaweza kumkuta Rais wa nchi haswa pale watuhumia watakapoamua kujitetea kama mtu binafsi na si kama wanachama wa CCM.

  Lazima watakapokuwa wanakata roho za kisiasa wataongea maneno ya mwisho na kupaza sauti kabla ya pumzi ya mwisho na hapo ndo JK atarudi zero katika kusafisha chama. Na huuu mchakato utakigharimu tena chama mwaka 2015. Hekima inatakiwa itawale hapa wasichukulie kuwafukuza EL, RA na Chenge itakuwa rahisi kama kurusha karatasi kwenye dustbin halafu inatulia humo mpaka ichomwe. Hawa hata wakifukuzwa lazima wapambane.
   
 16. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Huyo jamaa hapo kwenye red inasemekana gazeti lake la mtanzania toleo la leo limehujumiwa ili lisiingie mitaani....inaelekea kunahabari ambayo ilikuwa mbaya zidi ya ccm
   
 17. m

  matawi JF-Expert Member

  #17
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwa kuwatosa hawa jamaa Kikwete keshajiweka kupata support ya umma. Hawa jammaa ndo kwiisha habari yake
   
 18. m

  matawi JF-Expert Member

  #18
  Apr 15, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Inawezekana pia hii ya kuwatosa chenge,el na RA ni danganya ya public ili kupunguza power ya upinzani yaani ionekane ccm haipendi ufisadi lakini wenyewe kwa wenyewe wanawasiliana na wako poa
   
 19. F

  FUSO JF-Expert Member

  #19
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  yeah lakini wamemuharibia sana EL sababu ndoto zake ilikuwa siku moja kuja kuongoza nchi hii. Tangu zamani hata wakati ule baba wa taifa bado hai alionyesha utashi huo, nafikiri safari yake imeishia hapa rasmi, unless afanye Move kali ambayo itashangaza nchi sababu ana wafuasi wengi sana nyumba yake.
   
 20. F

  FUSO JF-Expert Member

  #20
  Apr 15, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  RA ni mfanyabiashara lakini kumhukumu yeye na wengine wachache tu ni kosa, madili mengi walikula na watawala na mengine yalisaidia kuwaweka madarakani, leo hii ndiyo mtake kumfanyizia?

  Njia iliyotumika na CCM kujisafisha ina walakini - Black Market.
   
Loading...