Ushauri: Serikali ya CCM iwakamate na kuwashtaki Rostam, Lowassa na Chenge

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Watajwa hapo juu,walishatambuliwa chamani kama Magamba Matatu. Yaani,walishatambuliwa kuwa ndiyo mizizi ya kuchafuka kwa CCM machoni mwa watanzania. Walitambuliwa na kuaminishwa kwa wanachama kuwa wamechafuka kwa rushwa,wizi na ufisadi. Kukaundwa hata mkakati dhabiti wa kichama wa kuvua gamba kwa ajili yao.

Mtemi Chenge aliwahi kukaririwa kuwa gamba lake limeishia kiunoni na halijavuka. Mambo yakaendelea. Rostam Aziz alijivua mwenyewe Ubunge na uongozi chamani. Lowassa hakuguswa hadi alipohamia CHADEMA mwaka jana. Hawa bado wanatajwa kama ni wachafu. Muda umefika.

Katika zama hizi za kutumbua majipu,Serikali makini ya chama makini cha CCM naishauri kuwakamata watajwa hawa kwa wizi,rushwa na ufisadi,kupitia polisi,TAKUKURU na Ofisi ya DPP, ili sinema inayowahusu ifike mwisho. Wote wapo na wanakamatika!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Nakala kwa:

Nape Nnauye,YEHODAYA alias HAMY-D,MwanaDiwani Mwigulu Nchemba,kababu alias stroke ,Mtela Mwampamba,Juliana Shonza,Wakudadavuwa alias singidadodoma Mzee Mwanakijiji na makada wengine
 
Mkuu VUTA-NKUVUTE hawa jamaa wanatakiwa wakamtwe ili sheria za nchi hii zivunjwe kwa sababu kuna waliojiwekea kinga wasikamatwe.

Acha nchi itikisike kwani itaanguka au?
 
Kwenye huu utatu tunamuacha Vipi Mzee Maarufu hapa Tanzania?

Kuna Ushahidi wa hizo Tuhuma au kuchafuana tu?
 
eti wamkamate rostam dah unamjua au unamsikia hujui kipindi chauchaguzi vodacom walipewa pesa wajenge minara fisiem wakazunguka nyuma
 
Ushahidi wa ufisadi wa lowassa upo chadema kwa kuwa wao ndio waliomtangaza kama fisadi kwa miaka nane. Naamini watatoa ushirikiano wa kutosha katika mahakama ya mafisadi itakayoanza muda si mrefu.
 
Back
Top Bottom