Usithubutu kujenga Wala kuoa, kwanza nakushauri uuze hicho kiwanja uende kitambaa Cheupe ukale Bata maisha mafupi haya.
Unasema story za kujenga vipi Kama ukienda kununua bati afu kwa bahati mbaya zikakukata ukaumia utamlaumu Nani? Achana na hizo mambo we kula Bata life is too short.


Daah umenifany nicheke kweeeel yaaan!Naam sijapata mchumba,,,maana nishawahi kupata mchumba kipindi cha nyuma lakini akawa hajatulia nikajiweka pembeni tangu hapo nimesubiri MUNGU atakae nipa!!Jenga kwanza kijana wanawake wapo tu,alafu si umesema hujapata mchumba au?
Aminaaa,,,ntalifanyia kazi mkuu maana kweli ukijenga Uhuru unakuwepoUmri wako huo kibongobongo ukiingia kwenye NDOA Kuna changamoto utazipata, Fanya maendeleo Kwanza mf Jenga Kwanza utaona tu NDOA hiyo hapo
Achana na Hao wazushi wanasema eti oa Kwanza na milango ya baraka itafunguliwa, baraka zipi hizo zinatokana na NDOA?
Wakupe mifano ya watu walipooa tu basi wakajenga majumba ya kifahari na sio kupanga tofali,
Baada ya kuoa tu, basi wakaweza Kununua mandinga Kama ma BMW na Mercedes Benz brand new kutokana na baraka za NDOA![]()
Umenifumbua macho aiseeJenga kwanza Ili mke aje akute una nyumba,mkizinguana anasepa peke yake.Lakini ukisema uoe halafu uje kujenga,mkizinguana atadai mlijenga wote na nyumba ipigwe bei mgawane pesa.Ndio ishu ambayo imenikuta Mimi,inanitesa mbaya sana.
Sijasoma content.Wapendwa Habari za wakati huu!!
MUNGU ni mwema anazidi kutupigania siku zote.
Sifa na utukufu vimrudie yeye
Kuna kitu naomba ushauri wenu wapendwa katika hili, nipo na umri miaka 27 sijaoa na wala sina mchumba nipo nimepanga ,, MUNGU kanisaidia katika kupambana katika kazi huku na kule nimefanikiwa kupata kiwanja japo ni kidogo lakini cha kuanzia maisha,
Niliwaza saana kuhusu kodi ninazo mpa mwenye nyumba nikapata uchungu hapa namfaidisha mwenye nyumba japo naishi kwake,,Basi ndo hivyo MUNGU akanijalia kwa mapenzi yake.
MSAADA:
Nimewaza na kuwazua kati ya haya mawili lipi litangulie,,japo sina kipato kikubwa saaana cha kusema naweza kufanya kati ya kimoja wapo kwa mkupuo hapana bali ni kujichanga taratibu maaana ni mimi kama mimi najitagemea.
Na mnavyojua ujenzi ni taratibu na hasa kama kipato ni cha kuunga
Je, wakuu niendelee kupambana tu ili nijenge hata chumba kimoja cha kuanzia ama nioe kabla sijajenga?
Ushauri wenu wakuu ili nifanye maamuzi sahihi kwanza.
MUNGU awabariki!