Nioe au nijenge kwanza?!

Nioe au nijenge kwanza?!

Umesema hauna mchumba!! Utamuoa nan! Sasa

Na achana na walee wachumba wa kutafuta, mchumba wa kweli analetwa na M:Mungu inabidi utulivu mwingi sanaa mkuu
 
Usithubutu kujenga Wala kuoa, kwanza nakushauri uuze hicho kiwanja uende kitambaa Cheupe ukale Bata maisha mafupi haya.

Unasema story za kujenga vipi Kama ukienda kununua bati afu kwa bahati mbaya zikakukata ukaumia utamlaumu Nani? Achana na hizo mambo we kula Bata life is too short.
 
Umesema hauna mchumba!! Utamuoa nan! Sasa

Na achana na walee wachumba wa kutafuta, mchumba wa kweli analetwa na M:Mungu inabidi utulivu mwingi sanaa mkuu
Aminaa mkuu,Barikiwa saaaana
Mke mwema mtu hupewa na Bwana

Mithali 19:14
 
lipia twisheni ya kutongoza Kama upo tayari nikupe control number ada ni laki mbili tu ila unalipia kwa installment ukishajua kutongoza na ukapata demu ndo uamue unajenga au unaoa kwanza
Wee mkuu!
 
Umri wako huo kibongobongo ukiingia kwenye NDOA Kuna changamoto utazipata, Fanya maendeleo Kwanza mf Jenga Kwanza utaona tu NDOA hiyo hapo

Achana na Hao wazushi wanasema eti oa Kwanza na milango ya baraka itafunguliwa, baraka zipi hizo zinatokana na NDOA?

Wakupe mifano ya watu walipooa tu basi wakajenga majumba ya kifahari na sio kupanga tofali,

Baada ya kuoa tu, basi wakaweza Kununua mandinga Kama ma BMW na Mercedes Benz brand new kutokana na baraka za NDOA 😂
 
Wapendwa Habari za wakati huu!!
MUNGU ni mwema anazidi kutupigania siku zote.
Sifa na utukufu vimrudie yeye

Kuna kitu naomba ushauri wenu wapendwa katika hili, nipo na umri miaka 27 sijaoa na wala sina mchumba nipo nimepanga ,, MUNGU kanisaidia katika kupambana katika kazi huku na kule nimefanikiwa kupata kiwanja japo ni kidogo lakini cha kuanzia maisha,
Niliwaza saana kuhusu kodi ninazo mpa mwenye nyumba nikapata uchungu hapa namfaidisha mwenye nyumba japo naishi kwake,,Basi ndo hivyo MUNGU akanijalia kwa mapenzi yake.

MSAADA:
Nimewaza na kuwazua kati ya haya mawili lipi litangulie,,japo sina kipato kikubwa saaana cha kusema naweza kufanya kati ya kimoja wapo kwa mkupuo hapana bali ni kujichanga taratibu maaana ni mimi kama mimi najitagemea.
Na mnavyojua ujenzi ni taratibu na hasa kama kipato ni cha kuunga

Je, wakuu niendelee kupambana tu ili nijenge hata chumba kimoja cha kuanzia ama nioe kabla sijajenga?

Ushauri wenu wakuu ili nifanye maamuzi sahihi kwanza.
MUNGU awabariki!
Oa utakuja kunishukuru baadae
 
Back
Top Bottom