Ninunue kipi gari au nijenge nyumba?

Ninunue kipi gari au nijenge nyumba?

Naishi singo sijaoa mkuu

Halafu kuna kosa kubwa huwa linafanyika.Kabla ya kufanya lolote kama una wazazi kijijini hakikisha kwanza hao wanaishi mzingira mazuri.Nakumbuka wakati ndiyo nimeanza kazi nilienda kijijini kwetu na siku hiyo mvua kubwa ikanyesha usiku.Nilikuwa na mama yangu na wadogo zangu kwenye ile nyumba.Ile nyumba ilikuwa inavuja mvua balaa.Usiku kucha tulikuwa tumesimama tunajikinga sehemu ambayo haivuji.Nilichokifanya niliamua kumjengea mama yangu nyumba nzuri ya kuishi kabla sijafanya jambo lolote.Angalia mambo mengi usikurupuke.Kuna watu mijini wanatanua na magari,lakini huko kwenye source ni balaa.Kila la kheri kijana.
 
Mkuu ukishanunua gari nipm nikupeleke kiwanja chenye mademu wazur
 
Nunua gari.Gari n habari ya mjn wewe.Kazi usafir muhimu, ukijenga nyumba utapanda punda?

Tafuta pesa kwa hiyo gari.Ukiwa na pesa nyumba unamvua hata mtu.

Kujenga nyumba ni sawa na kuizika pesa Milion 10 yako saiv.Acha woga.
Ushauri m bovu
 
Kama kiwango chako cha elimu kinaanzia digrii moja na umri wako ni chini ya miaka 45, nunua gari...
 
Kwa maoni yangu na ushauri inategemea lengo la kununua gari ni nini? Unaweza nunua gari kwanza ikiwa litakuwa ni ''Asset'' kwa maana ya kuwa itakuwa inakuingizia kipato utakachotumia kujenga. Lakini kama litakuwa ni ''Liability'' kwa maana ya kwamba haliingizi kipato zaidi ya kudraw pesa kutoka mfukoni mwako basi anza na kujenga nyumba kwanza. NB: Huu ni ushauri tu unaweza zingatia au laaaa. 😀😀
 
Kama nyumba muhimu iendeshe tukutane posta acha maneno nunua ndinga wewe u pimp town.
nb (mawazo yangu sio sheria)
 
mkuu kwani ushawahi Kulala nje kisa huna nyumba ya Kulala hapa jibu ni lazima hapana.

Ila ni mara ngapi ushatembea na miguu umbali mrefu kisa huna gari....ukicheki hapo utaona kabisa kuwa umeteseka mara nyingi kwa kutokuwa na gari kuliko kwa kutokuwa na nyumba.

Wakati ndio huu fanya maamuzi ya busara jenga heshima mjini.

Umemjibu vizuri sana!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom