Ninunue kipi gari au nijenge nyumba?

Ninunue kipi gari au nijenge nyumba?

Nunua ndinga mzee,nyumba yenyewe utajenga then itaishia njiani kwa hiyo pesa uliyonayo.
 
Jenga nyumba, nyumba ni asset isiyohamishika na unaweza kuchukulia mkopo bank ila gari unaweza kulinunua likapinduka Hata ndani ya week ukala hasara ya vimilion vyako.

NB. Wanaume wanaitwa baba mwenye nyumba sio baba mwenye gari
 
Kama unaishi kwenye nyumba ya kupanga nunua gari uendelee kulipia kodi,gari lako utakuwa unaegesha kwenye viwanja vya shell kwa kodi yako mwenyewe pamoja na kutoa fedha za mlinzi atakayekuwa ana linda gari lako
 
Jenga nyumba, nyumba ni asset isiyohamishika na unaweza kuchukulia mkopo bank ila gari unaweza kulinunua likapinduka Hata ndani ya week ukala hasara ya vimilion vyako.

NB. Wanaume wanaitwa baba mwenye nyumba sio baba mwenye gari
Naheshim mawazo yako
 
Kwa wewe nunua gari kwakuwa kipato chako kitaongezeka,hicho kitakachoongezeka basi ukipeleke kwenye ujenzi

MUHIMU:hicho kipato kitakacho zidi hakikisha unajenga kweli.

Kila la kheri...
 
Kwa wewe nunua gari kwakuwa kipato chako kitaongezeka,hicho kitakachoongezeka basi ukipeleke kwenye ujenzi

MUHIMU:hicho kipato kitakacho zidi hakikisha unajenga kweli.

Kila la kheri...
Sante
 
Habari vipi wakuu,

Najua katika maisha ya vijana hua kuna mitazamo tofauti ya mfumo wa maisha mtu atakavyo kuishi sina nyumba naishi nimepanga hapa Dar, lakini nina kiwanja Mbezi.

Mpango wangu ninunue gari MUNGU akisaidia mbeleni nitajenga tuu sasa hili suala la kutangulia kununua gari kabla ya kujenga, baadhi ya watu wameanza kuona eti napotea njia, wananiona sasa nimeanza kuchanganyikiwa.

Ushauri wenu wana JF ninunue gari au nitangulie kujenga nyumba.

NB: Endapo nitanunua gari kipato changu kitaongezeka Mara 2 ya nilichokua napata kwa mwezi.
Mi nishauri kitu kimoja...vyote ni muhim kwa ustawi wa maisha yako ila kikubwa cha kuangalia hapo ni je fan yako au mishe zako zaweza ongeza speed ukiwa na hiyo gari? Kama ndio nunua gari il uongeze thaman
Pili ni je hiyo hela ulonayo ya kununua gar ina thaman ya kusimamisha vyumba viwil kama tu una kiwanja tayari..?
Kama ndio jenga nyumba ila kikubwa ni kuangalia mishe zako zinahitaj sana gari.
Fanya litakaloongeza kipato
 
ushauri wangu: kwa kuwa vyote unavitaka, fanya ivi; kiasi cha pesa ulichonacho gawanya mara 2. Nusu yake kanunue gali nusu nyingine jengea nyumba.
 
jenga nyumba maana nyumba kila siku hata ukiuza ina banda thamani.gari baadae maana gari lina shuka thamani
Hats mtoto wa primary atachagua Nyumba,kama gari unaweza kopa kwa kutumia Nyumba ukaipata ila best choice nyumba
 
Gari ni liability na nyumba ni asset usipo iona hiyo basi tena!
 
Chukua hii kutoka kwangu,jenga nyumba kaka,nililijaribu hilo,nikaja kujuta,usafiri ninao lakini kodi bado inanitesa mno,nimeanza kujenga lakini natamani niliuze nikamalizie tu nyumba,jenga nyumba usafiri utapata tu
 
Watu wana maisha yao na wewe una maisha yako; usiwaruhusu wakuvuruge we fuata kipaumbele chako!!
 
Mtafute Madame B atakusaidia namna ya kuitumia hiyo hela nymbafu
 
Una sh.ngapi usije ukaanza kujenga ukaishia kwenye msingi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom