Nini umuhimu wa semina ya viongozi inayofanyika Arusha?

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
2,515
4,231
Wakati wananchi wakiendelea kuteseka na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali pamoja na gharama za maisha kiujumla, inasikitisha kuona jicho la serikali linazidi kuelekea katika matumizi ya hovyo ya fedha za umma.

Mpaka kiongozi anateuliwa, maana yake anafahamu majukumu ya kiuongozi na mambo anayopaswa kusimamia. Mbali na hayo, vipo vikao vya ndani vya mabaraza ya mawaziri, kamati tendaji za mikoa, wilaya n.k. Je, kulikuwa na haja gani kukusanya mawaziri na misafara ya viongozi kwa ajili ya semina huko Arusha?

Kiongozi anasema hadharani kwamba anaogopa na hawezi kumsimamisha mteule wake kazi kwa kuhofia familia yake pamoja na wale wanaomtegemea! Hivi dhana nzima ya uwajibikaji inaeleweka? Je, vipi kuhusu familia za wananchi masikini waliotendewa vibaya na kiongozi huyo, vipi wao hawaathiriki na utendaji mbovu? Kwa hiyo, waziri anapohujumu miradi ya maji, ni heri aendelee kuwepo ili kuepusha dhahma kwake na kwa familia yake kuliko wanakijiji wapate huduma ya maji?

INASIKITISHA INASIKITISHA INASIKITISHA

20230302_094623.jpg
 
View attachment 2534472
Sukuma gang mtanyooka tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom