Nini tutaifishe, nini tuwe na hisa kubwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini tutaifishe, nini tuwe na hisa kubwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 11, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kutokana na hali ya kiuchumi ya dunia na mwitiko wa nchi tajiri kukabiri hali hizo ni wazi kuwa kuna vitu ambavyo serikali inapaswa kuvifanya na kutoviacha soko huru. Mwaka 1967, tulitangaza azimio la Arusha na kutaifisha (kuviweka kwenye himaya ya serikali) vitu vingi. Baadaye miaka ya tisini vitu hivyo vingi vilianza kurudishwa kwa wananchi katika kile kinachoitwa ubinafsishaji.

  Mabenki, Bima, makampuni ya uzalishaji n.k yakaanza kuuzwa na kuondolewa mikononi mwa serikali. Leo hii hali ya uchumi ya dunia inatufanya tuhoji je kuna vitu ambavyo tuviweke moja kwa moja mikononi mwa serikali, na ni vitu gani hivyo na kwa nini? Na ni vitu gani ambavyo vinaweza kuwa bado chini ya watu binafsi lakini serikali ikiwa na hisa za kikamkakati (strategic shares) kama UK kwenye BAE na nchi nyingine?
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Utaifishaji ni ujambazi, serikali kama inataka kujiingiza katika uchumi, which is against the prevailing free market ideology, ijenge vyake.

  Hatuwezi kuwa tuna alternate perpetually between kutaifisha and kubinafsisha.This will do more harm than good.Serikali iwe inasimamia mazingira ya biashara tu, lakini isijiingize katika biashara.

  Na inapotokea kwamba ni lazima ijiingize katika biashara kwa kufuata mtindo wa mixed economy, isitaifishe bali ijenge vyake.

  Kutaifisha licha ya kutufanya tu-flip flop, kutachangia kudhoofisha uchumi kwa kuogopesha wawekezaji serious, hata kama tungejua jinsi ya kufanya nao biashara, which we don't.Which is worthy of a thread of its own.
   
 3. M

  Mkora JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu tutafika kweli kwa kugeza maana hapo tutaiingiza serikali gharama za bure
  Unafahamu kwamba hayo mashirika yaliuzwa kwa bei ya kutupa
  Sasa tutayanunua katika market value
  Hilo Azimio la Arusha halikutakiwa kufutwa anyway
   
 4. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hilo haliwezekani kwa sasa mpaka pale watakapo ondosha Azimio la ZANZIBAR ,kitu ambacho viongozi hawapo tayari kukifanya ,kutokana na mwanya walio upata wa kuanzisha biashara zao binafsi.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hizo nchi za kibepari mbona zinabinafsisha kila kukicha.. au ni bora kutumia sera za kijamaa kuukoa Ubepari? Leo hii US inaweka hisa kwenye kampuni binafsi ya magari ya Chrysler, inaweka fedha za walipa kodi kwenye makampuni ya fedha kama ruzuku, sisi ni kipi tunashindwa?

  Badala ya kuibinafsisha ATCL serikali iweke umiliki wa asilimia angala 70 na hisa nyingine wauziwe wananchi wa kawaida kwa mfano.. NBC irudishwe serikalini kwa asilimia kubwa na hata hiyo MNB yao.. Bima ndiyo kabisa..
   
 6. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji,
  Tungefanya kama walivyofanya marafiki zetu wa India. Tungebaki na benki yetu wenyewe badala ya kuwauzia makaburu NBC. Hii ni benki iliyokuwa imesambaa kote vijijini Tanzania. Tungeiita Benki ya Watanzania halafu tukaribishe ushindani. Reli definitely is a no, no, kama ukiangalia mfano hata wa Marekani. Na hata zile kampuni na mashirika ya umma tuliyogawa bure tungeendelea kuwa major share holders. Huo ndio mtazamo wangu.
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Hebu niambiaeni: hata NMB ilokuwa na faida tu kubwa ya 10's of billions kila mwaka serikali imeuza tayari!

  Why???
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  May 12, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mzalendohalisi,
  Unauliza why? 10% na corruption vitatuangamiza. Wakuu wakishaona kuna % na mshiko basi hata kama wangeweza kuuza Ikulu wangeiuza.
   
 10. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #10
  May 12, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu Je wewe ni mjamaa au mjima.
  Siasa za ujamaa zilishindwa na haziwezi tena kufanikiwa sio tu tanzania na washiriki wake bali sehemu yeyote duniani.
  Serikali kuendesha biashara haiwezekani hasa tanzania kwenye nchi ya kujuana na kukumbatia ujinga na wajinga , ujomba , ukaka ndio unatawala.
  Kuanguka kwa uchumi wa dunia sio swala la nani anamiliki au alimiki nini bali lilikuwa ni swala la mfumo, na kuna swala jingine la kukua kwa uchumi duniani na demand yake na shift of economy powers btn traders.
  Serikali kuachia uendeshaji wa uchumi sio kitu kibaya ila ni vipi wanafanya hivyo na mfumo gani na kwa sheria zipi hapo ndio kizazaa kinazuka.
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  May 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Serikali duniani ambazo ni magwiji ya ubepari (siyo ujamaa wala ujima) wanazirudisha serikali zao kwenye kuendesha mashirika na makampuni na nyingine hazikuachia mashirika hayo. Kwa sababu wanajua na kugundua kuwa serikali ina maslahi katika uzalishaji mali.

  La maana ni jinsi gani serikali inajiingiza katika makampuni, ni yapi na kwa mtindo gani. Mbona tunaiga mengi tu ya nchi hizo na tunaogopa kuiga kile ambacho sisi wenyewe tulikifanya miaka zaidi ya 40 iliyopita..
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  May 12, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kinepi_nepi,
  Siyo hivyo. Marekani imelazimika kuingilia mfumo wake wa kibepari baada ya kudidimia kwa uchumi. Ufaransa inamiliki asilimia 50 ya hisa za Renault, kampuni ya utengenezaji magari. Waafrika tusiwe mabwege. Tunaambiwa kuwa tuache market forces ziamue mambo wakati tunajua kwamba market forces ni ukoloni mamboleo. Angalia Tanzania ya leo nani anamiliki kila kitu. Ukisema ubinafsishaji unasema makaburu, wahindi na wazungu. We Mwafrika uko wapi? Acha hayo. Wajapani waliyagundua hayo siku nyingi ndio maana mpaka leo Marekani analalamikia sera za Japan kuhusu free market.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  May 12, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Mimi naona kabla watu hawajakurupuka na kusema mengi yasiyo kuwa na maana au faida kwetu ni bora sana tutazame tulikotoka na tunakoenda kisha tuangalie mifano ya wenzetu waliokwisha pita njia hizo hizo tunazopita sisi sio kutazama wanakopita wao kwani hatujaingia Highway..

  Nasema hivi kwa sababu hatuwezi kuingiza gear namba tano tukakanyaga mafuta kwa mwendo wa 100 miles/hr kwa sababu tu Marekani wako ktk Freeway na wanakwenda speed kali basi nasi tufanye hivyo wakati tunaendesha ktk barabara ya makorongo mbali na hivyo uwezo wa uwezo wa gari letu (Bajaj) ni mdogo..

  Ningeomba sana watu wapitie hapa Wikipedia, tuwasome wenzetu walifanya kitu gani na wapi walifanya makosa kisha ndio tuje na hoja zenye kujenga...Bofya hapa

  Pia wanaweza kutazama kwa undani ni zipi Commanding Heights za uchumi wetu ambazo inabidi tuwe makini sana ktk kutoa maamuzi au mawazo kulingana na mazingira yetu.. Sii lazima kinachofanyika Marekani kifanyeke Bongo kwa sababu Marekani wenyewe chini ya Free Market economy walikutana na Great depression ambayo Frankilin Roosevelt alifanya hivi hivi kama Obama na wakaweka regulations uchumi ukarudi na kukua, kisha walipokuwa sawa wakarudisha tena free market wakaanguka kidogo wakati wa Reagan wakatangaza buy American only ambazo ni pinzani ya mfumo huu wa free market economy na Globalisation.. wakarudi tena kuwa sawa wakaondoia tena baadhi ya regulations na yamewakuta tena ya depression na safari hii serikali imenunua hisa ktk Commanding Heights za uchumi ili kuepuka nchi kuporomoka kiuchumi..pia wamerudisha tena regulations ambazo ziliondolewa baada ya mafanikio ya Roosevelt. Pia unaweza kubofya hapa..

  Sasa tunangalie wao hizo regulations ziko vipi maanake tusije sema hawana kabisa control ya uchumi wao..na sii kweli kwamba kila kitu US na nchi za kibepari ni Private owned..Bila shaka mimi kama Bepari naamini kabisa in invisible hand na hakika Utajiri wa mtu mmoja ni utajiri wa nchi nzima lakini mtu mwenyewe asiwe mgeni anayechukua mafao nje ya nchi..Je, imani kama hii inanifanya mimi niwe Mjamaa?
   
Loading...