fredito13
JF-Expert Member
- Sep 3, 2012
- 213
- 146
Wanajamvi,
Mimi ni muumini wa dini ya kikristo, dhehebu langu nitataja nikihitajika kufanya hivyo.
Naomba ufafanuzi kwa wale wenye uelewa zaidi kuhusu hawa viongozi wa dini wanaoibuka siku hizi hapa nyumbani mpaka kwingineko ulimwenguni!
Hapa nyumbani tunao wengi, kuwataja wachache ni Kakobe, Mwingira, Mama Rwakatare na Mzee wa Upako (Lusekelo)
Naomba tofauti ya mitume/watumishi hawa; Mwingira wa Tanzania na TB Joshua wa Nigeria.
Kwa uelewa wangu, hawa wote na wengineo wanatumia neno la Mungu kujitajirisha! Ni nini kinamfanya TB Joshua awe maarufu zaidi?
Miujiza wanayoitenda ni kweli ina mkono wa Mungu au ni mapepo?
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums