Nini Tofauti ya TB Joshua na Mwingira??

Nini Tofauti ya TB Joshua na Mwingira??

Shika neno wana Wa Mungu...sisi wafuasi Wa mtume Na nabii Eliya Wa Siloam tuna washauri Muje huku kwani kuna Mungu Wa ukweli. Hapo ulipo jaribu kuulizia mahali lilipo Kanisa LA Siloam naomba jumuika nasi upate kumuabudu Mungu Wa Kweri. Amina
Kanisa ni IMANI yako tu ayomengine majengo tu
 
Mambo ya ujuzi wa Neno la Mungu ni magumu sana kwa wale ambao wameathiriwa na kuwa katika kaasisi za kidini.

Nataka nimwambie ndugu yangu anayekuwa na mashaka na watumishi wa Mungu hawa, kuwa Mungu anatenda kazi pamoja na watumishi wa Mungu, hatendi kazi yake na taasisi. Zamani nami nilipokuwa katika taasisi mojawapo ya kidini nilikuwa nabeza sana juu ya watumishi wa Mungu ambao Mungu kwa namna moja ama nyingine alikuwa amewaita.

Tunaposoma katika maandiko hatuoni popote kwamba Mungu alikuwa anatenda kazi na taasisi fulani kama ilivyo leo; Katoliki, Anglikana, Lutheran nk. Lakini tunaona kuwa Mungu alikuwa na; Daniel, Mussa, Ibrahim, Yakobo nk. Sawa na siku hizi, tunaona kuna Mwingira, TB Joshua, Kakobe, Anthony Lusekelo, Rwakatale nk. Ndugu zangu, tumeathiriwa na mapokeo ya wazee, tuyachunguze maandiko na kuona je ndivyo ilivyo?

Neno la Mungu ni gumu na ni rahisi sana kwa wanaomtafuta, Mungu ni wa haki angeacha Neno lake liwe kama elimu zingine, basi wenye elimu ndio ambao wangemjua Mungu lakini wapi! Amewanyima wenye hekima na akili na kuwafunulia watoto wachanga. Tumwache Mungu aitwe Mungu, roho zote ni mali yake, wenye kumtafuta watamwona.











kevy.jpg


Wanajamvi,

Mimi ni muumini wa dini ya kikristo, dhehebu langu nitataja nikihitajika kufanya hivyo.

Naomba ufafanuzi kwa wale wenye uelewa zaidi kuhusu hawa viongozi wa dini wanaoibuka siku hizi hapa nyumbani mpaka kwingineko ulimwenguni!

Hapa nyumbani tunao wengi, kuwataja wachache ni Kakobe, Mwingira, Mama Rwakatare na Mzee wa Upako (Lusekelo)

Naomba tofauti ya mitume/watumishi hawa; Mwingira wa Tanzania na TB Joshua wa Nigeria.

Kwa uelewa wangu, hawa wote na wengineo wanatumia neno la Mungu kujitajirisha! Ni nini kinamfanya TB Joshua awe maarufu zaidi?

Miujiza wanayoitenda ni kweli ina mkono wa Mungu au ni mapepo?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Shika neno wana Wa Mungu...sisi wafuasi Wa mtume Na nabii Eliya Wa Siloam tuna washauri Muje huku kwani kuna Mungu Wa ukweli. Hapo ulipo jaribu kuulizia mahali lilipo Kanisa LA Siloam naomba jumuika nasi upate kumuabudu Mungu Wa Kweri. Amina

Du!!hii kali
 
Mada yako ni tofauti na ulichokiandka, hii inamaanisha kua, you have a message behind the message. Lengo lako si kujua tofauti zao kwa kua tofauti zao zko wazi. Ushauri wangu kwako ni huu: Swala la hukumu kwa watu, wakiwamo watumishi wake,libaki kwa Mungu mwenyewe, coz yeye ndo anajua, ipi nyeusi ipi nyeupe. Ni tahadhari kwako coz watu wengi ambao wamekua wakiwanyooshea vidole watumishi wa Mungu, bila kua na uhakika, wameishia pabaya
 
ukimchunguza sana bata hutakula nyama yake.

sikiliza mahubiri yao achana na matendo yao na utajiri wao

utajiri wao au wingi wa watu makanisani sio sababu ya wewe kukukuza kiimani

chukua za kwako changanya na zakupewa uende mbinguni
 
Jf bwana..!! Yaan mtu unaweza kuanzisha uzi kwa nia nzuri ya kupata elimu..na kwa mategemeo kuwa utapata majibu mazuri...lakin matokeo yake huwa kinyume kabisa na matarijio ya muanzisha mada
 
Hawa waumini wa madhebu wanaojiita waanzilishi ndio matatizo yao haya yani wanafikirigi Mungu ni wao peke yao na kwamba Yesu wamemuweka mfukoni kama wangeweza nafkiri wangechukua haki miliki ya jina la Yesu na Bible watumie wao peke yao.

Yani kwao yeyote ambae havai wala hafuati utaratibu wa kuendesha ibada kama wao utasikia wakimuita tapeli mchumia tumbo mwizi nabii/mtume wa uongo hata kama anahubiri KWELI ya MUngu.

Lakini ashukuriwe Mungu asitazama kama wanadamu tunavyotazama zaidi wanavyozidi kuwasema vibaya zaidi sana Mungu anazidi kuwainua na makanisa yao yanabaki tupu.

Hakuna kanisa la kipentecoste lililotupu marekani au ulaya ila kaangalie kwa wale wanaojiita wajuzi na waanzilishi wa kanisa?

Angalia mataifa kama China India na Asia Africa ni kanisa gani linalo pamba moto sana utasikia ni Pentecoste.
 
Mungu wetu ni wa ajabu huwezi kuwalinganisha watumishi wa Mungu ila Mungu aliyewapa kazi ndiye anawajua katika Mat 25:14-25 Yesu anatoa mfano wa msafiri aliyewapa watumwa wake dinari wafanyie kazi majibu yake unayaona aliyepewa nyingi anadaiwa nyingi.Kwa habari ya kuhukumu Paulo anasema si kazi yetu kuhukumu ni kazi ya Baba(Mungu) Lakini kwa habari ya huduma ni kitu ingine Yohana mbatizaji alikuwa na huduma yake na Yesu Kristo alikuwa na huduma yake lakini tazama watu hawa walivyojishusha japokuwa mmoja alikuwa ni Mungu Yoh 1:23-27,Yoh3:30 Lakini Yesu anamfuata Yohana ili abatizwe Mat 3:14 si hivyo angalia Yesu anavyomsifia Yohana mbatizaji Mat11:11 Huduma ya Mungu ni ya kutiana moyo wala si kushindana angalia Paulo anavyosema 1Kor 3:4-9 hao wote ni wafanyakazi katika shamba la Mungu kila mtu atavuna kwa staili yake 1Kor3:11-15 mleta hoja kuwa sasa usiendelee kunywa maziwa jaribu kula makande
 
wakati mwingine mtu
anauliza swali ili apate msaada kwa wana jamvi kakini najibu mengine
yanasikitisha
du mollel hajambo nabii wa karne ya 21 geodavie na ule mchakato wake wa kuandika biblia yake amekamilisha vitabu vingapi? naskia biblia yake anajielezea yeye na wanyilamba wenzie tu biblia yote
 
Mkuu maswali ya ajabu ajabu hujibiwa kwa hoja za ajab ajab.
Mtoa mada hakutaka kujua tofauti zao,alitaka kuwakashfu hao wachungaji(mi sio muumini wao),sio vizuri kutoa kashfa na hukum kwa vitu huna uhakika navyo.

napenda na mimi kuuliza. hv unakuwaje mtume halafu una baki dar? kwanin asiende somalia uarabun au maeneo ambayo ukristo ni hadith nzito kusikika?
 
acha ushabiki usio na mantiki kwa watumishi wa Mungu hata kama huwakubali ucje ukaanza kupata matatizo mana hata kwenye biblia kumeandkwa ni vibaya kuwawazia watumishi kwanza ni Mkristo gani una mawazo finyu hivo only God can judge them[/QUOImeanfikwa kitabu gani mkuu
 
Back
Top Bottom