Inawezekana ikawa ni miujiza ya Mungu kwa vile anayetenda ni Mungu sio wao. Neno la Mungu linasema siku ya mwisho wengi watanililia wakisema nilikuwa nahubiri sana au nilikuwa naponya wagonjwa kwa jina lako au kazi yeyote ile lakini Bwana atasema siwajui ninyi!! Kikubwa ni kuishi maisha ya utauwa. Mungu anaweza akakutumia ufanye kazi yake lakini matendo yako yakienda kinyume na mapenzi yake siku ya mwisho ni hukumu tu! Kama hao uliowataja hawatendi mapenzi ya Mungu Mungu mwenyewe anajua. Mwachie yeye aamue. We shika neno na ulitende period. Usimkashifu mtumishi wake maana Mungu hapendi. Kasome kitabu cha Hesabu 12: 1-15 utaona jinsi Mungu alivyomuadhibu Miriam kwa ajili ya kumsema mtumishi wake Musa.
Wanajamvi,
Mimi ni muumini wa dini ya kikristo, dhehebu langu nitataja nikihitajika kufanya hivyo.
Naomba ufafanuzi kwa wale wenye uelewa zaidi kuhusu hawa viongozi wa dini wanaoibuka siku hizi hapa nyumbani mpaka kwingineko ulimwenguni!
Hapa nyumbani tunao wengi, kuwataja wachache ni Kakobe, Mwingira, Mama Rwakatare na Mzee wa Upako (Lusekelo)
Naomba tofauti ya mitume/watumishi hawa; Mwingira wa Tanzania na TB Joshua wa Nigeria.
Kwa uelewa wangu, hawa wote na wengineo wanatumia neno la Mungu kujitajirisha! Ni nini kinamfanya TB Joshua awe maarufu zaidi?
Miujiza wanayoitenda ni kweli ina mkono wa Mungu au ni mapepo?
Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums