Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,291
Nashukuru nilipata bahati ya kutembelea baadhi ya nchi zilizoendelea na zile ambazo bado. Safari hizo zilinipa fursa ya kutafuta jibu la maswali yaliyosumbua kwa miaka mingi:
1. Mataifa yaliyoendelea yana nini kilichofanya yaendelee ambacho sisi hatuna?
2. Kwa nini wao waendelee na sisi bado?
3. Nini tofauti ukilinganisha nchi zilizoendelea na ambazo bado?
Safari hizo zilinipatia majibu kwa maswali yote matatu. Kwa leo, majibu ya swali la tatu yatawasilishwa.

Nchi Zilizoendelea | Nchi Ambazo Bado Zinaendelea |
---|---|
1. Wajibu wa mtu binafsi | Wajibu wa serikali |
2. Muda uheshimiwe | Wazungu zao saa, lakini muda wote duniani ni mali yetu |
3. Mifumo ya taarifa karibu kwa kila kitu. Na mifumo 'inaongea' yenyewe kwa yenyewe. | Mifumo michache ya taarifa. Mifumo haiongei yenyewe kwa yenyewe -- hata ndani ya taasisi moja |
4. Mifumo ya uendeshaji (business processes) inalenga kulinda muda wa mteja. | Mifumo ya uendeshaji (business processes) ni sumbufu kwa wateja. |
5. Wananchi ni wachapakazi. Kazi ni msingi wa maendeleo. | Wananchi huona kazi ni adhabu. |
6. Mali ya umma -- ikiwemo kodi inavyokusanywa na inavyotumika -- ni suala la kila mmoja. 7. Uwazi wa taarifa | Mali ya umma -- ikiwemo kodi inavyokusanywa na inavyotumika -- si suala la kila mmoja. Usiri wa taarifa |