Nini tofauti ya nchi zilizoendelea na zile ambazo bado?

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Nashukuru nilipata bahati ya kutembelea baadhi ya nchi zilizoendelea na zile ambazo bado. Safari hizo zilinipa fursa ya kutafuta jibu la maswali yaliyosumbua kwa miaka mingi:
1. Mataifa yaliyoendelea yana nini kilichofanya yaendelee ambacho sisi hatuna?
2. Kwa nini wao waendelee na sisi bado?
3. Nini tofauti ukilinganisha nchi zilizoendelea na ambazo bado?

Safari hizo zilinipatia majibu kwa maswali yote matatu. Kwa leo, majibu ya swali la tatu yatawasilishwa.

Nchi ZilizoendeleaNchi Ambazo Bado Zinaendelea
1. Wajibu wa mtu binafsiWajibu wa serikali
2. Muda uheshimiweWazungu zao saa, lakini muda wote duniani ni mali yetu
3. Mifumo ya taarifa karibu kwa kila kitu. Na mifumo 'inaongea' yenyewe kwa yenyewe.Mifumo michache ya taarifa. Mifumo haiongei yenyewe kwa yenyewe -- hata ndani ya taasisi moja
4. Mifumo ya uendeshaji (business processes) inalenga kulinda muda wa mteja.Mifumo ya uendeshaji (business processes) ni sumbufu kwa wateja.
5. Wananchi ni wachapakazi. Kazi ni msingi wa maendeleo.Wananchi huona kazi ni adhabu.
6. Mali ya umma -- ikiwemo kodi inavyokusanywa na inavyotumika -- ni suala la kila mmoja.

7. Uwazi wa taarifa
Mali ya umma -- ikiwemo kodi inavyokusanywa na inavyotumika -- si suala la kila mmoja.

Usiri wa taarifa
 
Hiyo Number mopja i0ongezee Nyama, sijuhi unazungumzia wajibu upi?

Wajibu wa mtu binafsi vs Wajibu wa Serikali.

Tuangalie maeneo saba yafuatayo, kama kielelezo:kwa nchi zilizoendelea:
1. Afya (ikiwemo matibabu)
2. Elimu (Ikiwemo mafunzo kuanzia chekechea mpaka elimu ya juu)
3. Usalama (wa hali na mali)
4. Miundombinu, ardhi na makazi
5. Bei (za bidhaa muhimu na zisizo muhimu)
6. Ajira
7. Mafao ya uzeeni

1. Afya ni jukumu la mtu binafsi. Hii ikiwemo matibabu. Raia anategemewa kupata bima ya kwake mwenyewe au aingie madeni makubwa kujitibu iwapo hana hela za kujitibu bila bima. Anaweza kukosa baadhi ya huduma.

2. Elimu ni jukumu la mtu binafsi. Mzazi anaweza kuamua kumuelimisha mtoto wake bila kumpeleka "shule ya umma" zenye propaganda. Au anaweza kumpeleka shule binafsi.

3. Usalama wa raia ni jukumu la mtu mwenyewe. Serikali ipo kuingilia kati pale mtu mmoja anapotumia nguvu dhidi ya mwingine. Jukumu la kulinda taasisi fulani ni la taasisi hiyo. Usalama wa mji, mkoa au jimbo ni wa eneo husika. Rasilmali za mahali fulani hutumika sehemu hiyohiyo.

4. Reli binafsi. Barabara binafsi. Ardhi binafsi. Maliasili, mfano mafuta na gesi kwenye eneo binafsi ni mali ya mtu binafsi. Serikali haiwezi kumnyang'anya ardhi mtu mmoja binafsi na kumpa mtu binafsi mwingine "kwa maslahi ya taifa". Kila mtu anatakiwa kujiwezesha kupata makazi. Anayeshindwa anakuwa msimakazi ("homeless").

5. Bei za bidhaa muhimu na zisizo muhimu huongozwa na ushindani wa soko.

6. Kupata ajira au kukosa ni suala la mtu binafsi. Hakuna kumlilia Big Daddy Government (BDG) kwamba kwa nini sina ajira na nimesoma nina digirii.

7. Fainali uzeeni. Ukijiwekea mafao ni vema. Wewe tu. Usipojiwekea Wewe tu. Hakuna mwenye wajibu wa kumtunza mtu mzee isipokuwa mzee mwenyewe (kupitia ushiriki wake wa hifadhi ya jamii au kodi zake).


Cha msingi, ni kwamba serikali inabaki na wajibu wa kutunga sera na kuzisimamia kama refarii, na kuwaachia watu binafsi kuingia uwanjani kucheza. Hukuti serikali ni refa-mchezaji. Ndio maana utaona serikali ni ndogo -- wenye madaraka wachache, vyombo vya serikali vichache, idadi ya watumishi wa umma ni ndogo, bajeti ya serikali haina nakisi, na mziki mzima wa organized chaos.

Kibanga Ampiga Mkoloni nyama hiyo!

EDIT1: UFUPISHO: Vitu vingi ambavyo ni wajibu wa mtu binafsi kwenye nchi zilizoendelea, utavikuta ni wajibu wa serikali kwenye nchi zinazoendelea.
 
Mlenge

Ni ngumu sana kubishana na watu wa Propaganda ambao wanalipwa kwa kazi hiyo.
BUT ALL IN ALL ALL THE BEST , HOPE FAMILIA YAKO NA UKOOO WAKO NA NDUGU ZAKO WANAFAIDIKA NA HII KAZI YAKO,

OTHERWISE UNACHOKIFANYA NI DHAMBI TU.
 
Mlenge

Ni ngumu sana kubishana na watu wa Propaganda ambao wanalipwa kwa kazi hiyo.
...

Kibanga Ampiga Mkoloni ,

Sioni uhusiano wowote wa nilichoandika hapa na ubishi wa propaganda. Kwani nimeandika propaganda ipi? Nabishana na nani? Maandishi yangu yako neutral kwa vile ni mawazo binafsi yaliyowasilishwa kwa jamii.

Mlenge

...
BUT ALL IN ALL ALL THE BEST , HOPE FAMILIA YAKO NA UKOOO WAKO NA NDUGU ZAKO WANAFAIDIKA NA HII KAZI YAKO,

Hata mimi sielewi wananufaikaje. Mimi binafsi nanufaika kwa vile naposti humu kama burudani binafsi na endapo litakuwepo la maana katika ninayoposti basi hadhira nayo itanufaika. Ndio maana naposti humu JF, na hasa kwenye jukwaa la Great Thinkers, mahali ambapo mambo ya kufikirika ndio mahala pake. Consider any discussion here as academic.

Mlenge

OTHERWISE UNACHOKIFANYA NI DHAMBI TU.

Haswaa. Ninayo dhambi ya kutolipwa pesa mimi, wala ndugu na ukoo wangu kwa kuposti mambo ya kufikirika humu kama burudani binafsi kwangu. Pana tatizo mkuu katika ninayoposti? Burudani kwangu haitakiwi kuwa bugdha kwa wengine. Ikiwa wapo wanaobughuwa na niandikayo, nitaacha.

Ps. KUANDIKA MANENO KWA HERUFI KUBWA MTANDAONI HUHESABIKA UNASHOUT!
 
Mkuu Mlenge
Hayo uliyoanisha ni ''subset'' ya kitu kimoja, Elimu. Tofauti yetu na nchi zilizoendelea ni kuhusu elimu ambayo kwa kila mtazamo, uwe wa kijamii, uchumi, utamaduni n.k. huongoza

Ukitaka kulibaini hili, tafuta nchi iliyoendelea, inayoendelea na nchi masikini kama zetu angalia kitu kinaitwa elimu. Hiyo ni factor kubwa sana katika kujitambua na kutambua mazingira ya mtu

Kodi: Nchi zilizoendelea wananchi wana ufahamu na kodi zao kutokana na elimu
Katika nchi zinazoendelea wananchi hawana ufahamu na wala hawajui kodi zao ni za nini
Factor kubwa ni elimu

Afya: Nchi zilizoendelea afya ni ya mtu binafsi kwa vile anatambua umuhimu wa afya katika maisha yake ya kila. Kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira ambayo si kazi ya mtu binafsi
Katika nchi zinazoendelea afya haina umuhimu kwa wananchi, ndiyo maana bado kuna maambukizi ya magonjwa. Watu hawaelewi kuwa kuhara kunazuilika kwa kuosha mikono, kula vitu visafi na kuishi katika mazingira mazuri
Factor ni elimu

Usalama: Nchi zilizoendelea kila mtu anajua gharama za usalama wake na kwamba serikali inashughulikia usalama katika ngazi ya juu.
Nchi zinazoendelea usalama si jambo la muhimu kwa mtu, na wala serikali zake hazijihusishi
Factor ni elimu

Orodha inaendelea na nimalize kwa mfano mdogo tu wa mtaani. Hivi kwanini kipindupindu kipo buguruni siyo masaki na maeneo ya karibu?
Hivi inashindikanaje watu kupanga mstari kupanda dala dala?
Hivi kwanini watu hawatambui maji yanayouzwa yamechotwa mtaroni na kuchujwa tu?
Hivi kwanini mtu ale kitumbua cha mkononi au samaki asiojua wamepikwa wapi?

Hayo yote yanafanywa na watu wasio na elimu. Na hayo hayaishii hapo, yanaendelea hadi katika nyanja nyingine kama siasa, utawala n.k. Kwamba, wananchi hawajui haki zao, hawajui kuhoji , hawajui kudai kwasababu hawana elimu inayowapa ufahamu wa ku approach mambo hayo
 
Mkuu Nguruvi3,

Elimu kweli ni jambo la msingi. Naamini hapo huzungumzii elimu kwa maana ya mafunzo ya madarasani pekee. Maana siku hizi ile kaulimbiu ya enzi za Nyerere "Elimu Haina Mwisho" inatekelezwa kwa vitendo na UNESCO na wadau wengine wa kimataifa.

Umezungumza mengi, na itabidi kuyajadili kipekee, na huenda, kwa posti tafauti.

Orodha inaendelea na nimalize kwa mfano mdogo tu wa mtaani. Hivi kwanini kipindupindu kipo buguruni siyo masaki na maeneo ya karibu?
Hivi inashindikanaje watu kupanga mstari kupanda dala dala?
Hivi kwanini watu hawatambui maji yanayouzwa yamechotwa mtaroni na kuchujwa tu?
Hivi kwanini mtu ale kitumbua cha mkononi au samaki asiojua wamepikwa wapi?

Kwa nini kipindupindu hakiishi Buguruni? Nakumbuka siku moja kwenye TV walionyesha wananchi wenye ghadhab Buguruni wakitaka kumsulubu mwenzao aliyeunganisha bomba la majitaka toka nyumbani kwake kwenda kwenye bomba la majisafi yanayotumiwa na wengine. Nadhani taswira hiyo ni patigazeti ya picha nzima.

Kupanga mstari -- Civilization is the ability to queue. Kujipanga mistari ndicho kipimo cha ustaarabu. Siyo kwenye daladala tu -- wapi kwengine tunakopanga foleni? Ukikuta foleni angalia pembeni. Utaona askari anayesimamia foleni au utakuta vizuizi vya kuswaga watu kwenye foleni. Pana tatizo kwenye ustaarabu wa foleni.
 
"Mlenge, post: 32247370, member: 450"]
Elimu kweli ni jambo la msingi. Naamini hapo huzungumzii elimu kwa maana ya mafunzo ya madarasani pekee. Maana siku hizi ile kaulimbiu ya enzi za Nyerere "Elimu Haina Mwisho" inatekelezwa kwa vitendo na UNESCO na wadau wengine wa kimataifa.
Elimu ya ufahamu na si ya darasani tu. Lakini pia ninaamini kukaa darasani hata kama hakuna matokeo mazuri bado ni sehemu ya elimu ya ufahamu. Kuwasikiliza wengine wanaoelewa ni sehemu ya elimu ya ufahamu. Kuona wengine wanavyotenda ni sehemu ya elimu.
Kupanga mstari -- Civilization is the ability to queue. Kujipanga mistari ndicho kipimo cha ustaarabu. Siyo kwenye daladala tu -- wapi kwengine tunakopanga foleni? Ukikuta foleni angalia pembeni. Utaona askari anayesimamia foleni au utakuta vizuizi vya kuswaga watu kwenye foleni. Pana tatizo kwenye ustaarabu wa foleni.
Hapa kuna hoja nzuri sana. Ustaarabu hutangulia mambo mengi ikiwemo elimu. Historia inaonyesha sehemu zilizokuwa na ustaraabu ziliendelea kielimu tangu miaka dahari. Pamoja na hayo, elimu hufanya Ustaarabu kuwa bora zaidi
Kwa maana eneo lenye elimu ustaarabu wake unakuwa juu kuliko ustaraabu huo pasipo na elimu

Nikuchekeshe kidogo, kwamba utamaduni wetu Waafrika ni tohara (kutahiri) kwa sehemu kubwa
Imedhihirika ni jambo jema na juzi tu serikali ya Kenya imeamua kuwasaka wasiotaka tohara
Huu tunaweza kusema ni ustaarabu mzuri

Lakini tohara katika zama hii imekuwa dhahma na kuwa chanzo cha maambukizi ya maradhi ya damu kama Hepatitis na Ukimwi kutokana na matumizi hovyo ya vifaa yasiyozingatia elimu

Kumbe basi pangalikuwa na kaelimu ka ufahamu, mfanyiwa tohara angechukua tahadhari za vifaa vyake na mto tohara angechukua tahadhari kwa wateja wake, ustaarabu ungetamalaki

Elimu ya ufahamu inatoa tofauti kubwa sana katika maendeleo na tofauti za maendeleo baina ya mataifa.
 
Elimu ni pamoja na technology, nchi zilizoendelea zilianza kutoa mafunzo ya internet na IT kwa raia wake wote takriban miaka 15 iliyopita.

Wenye ajira lilikuwa jukumu la mwajiri kufunza IT kwa wote na wasio na ajira ilikuwa sehemu ya mafunzo ya kutafuta ajira. Kuandika CV kuisambaza ni elimu iliyotolewa bure library kwa raia wote wanaopenda.

Sasa hivi ni rahisi kuwafikia wananchi wote, wenye matatizo.

Mix economy pia husaidia kuweka sawa hali ya uchumi. Sehemu kama Masaki ni muhimu kuwa na affordable homes ambazo watu wa kipato cha kawaida wanaweza kuishi.

Hii itawasaidia waliowekeza kwenye biashara kubwa kupata wafanyakazi wakuhudumia biashara zao ambao hawakai mbali na ajira zao.
 
Ni sahihi hizo tofauti lakini sidhani kuwa watu wanazaliwa nazo au ni utamaduni unaowafanya kuendelea bali ni tabia zinazotokana na sera za serikali. Mfano serikali ikisema itatoa elimu ya juu bure kuna mtu atathubutu kuserve kwa elimu ya juu? Kama sera za serikali zinajali sekta binafsi basi haiwezi weka mifumo sumbufu kwa wateja. Na itawashirikisha matumizi ya kodi zao.

Kama sera za serikali hazijaji private proprerty usitegemee wananchi wawe wachapakazi. Nitoe mfano, mtanzania kalima chai na anatakiwa kuuza kupitia ushirika ulioundwa na serikali huku bodi ya chai ikimuangalia. Matokeo yake anapata bei nusu ya mkulima wa Kenya, unafikiri nani atakuwa mwenye kuchakazi kwa bidii na nani atajali muda zaidi? kuna uhusiano mkubwa wa juhudi na kipato(rewards). Kenya haijaendelea lakini uwiano huo umeenda mpaka kwa nchi zilizoendelea zaidi.

Mi naona tofauti kubwa ya nchi zii zoeendelea na zisizoendelea ni sera za serikali. Nafikiri tukicheki sera za serikali tunawza predict iwapo nchi itaendelea au la. Sera za serikali ya Mao ziliua wachina kwa njaa na magonjwa., Sera za Deng Xinping zimefanya wachina kutajirika kwa kasi.
 
Kiongozi Red Giant,

Asante kwa mchango wako wa mawazo. Umeenda hatua moja mbele zaidi kwa kujadili chanzo cha tofauti baina ya nchi zilizoendelea na zile ambazo bado.

Umezungumzia fofauti ya kisera kama ndicho chanzo. Kwa nini sera zisizoleta kasi ya maendeleo hutungwa na kutumika? Jibu kwa swali hilo lilipata kutolewa na Mwanafalsafa Ayn Rand. Mama Ayn Rand anasema, sera zinazoleta matokeo magumu, aghalabu hutungwa kwa nia njema kabisa (altruistic inclinations). Sera hizo zinapokwama ni kwenye mahali zilikoegemea (premises) dhaifu. Tofauti kubwa ya sera msingi wake ni ya falsafa zinakotokea.

Falsafa za Kijamaa

Falsafa za Kibepari

Falsafa za Huria

Binafsi nazipenda falsafa huria, kwani ndizo zinazohusishwa na maendeleo makubwa ya haraka.

Kwa harakaharaka:

Nchi zilizoendelea sana zinafuata (kwa sehemu kubwa) misingi ya Falsafa Huria.

Nchi zilizoendelea kwa wastani hutumia falsafa za kibepari.

Nchi zilizoendelea kidogo hutumia falsafa za kijamaa.


Kiukweli uwiano wa mchanyato maalum wa falsafa mbalimbali huweza kufanya taifa husika lipige hatua kubwa za maendeleo.
 
Pengine na mimi ni changie hapa kuhusu tofauti ya nchi zilizoendelea na zile ambazo hazijaendelea.
Naamini tunapozungumzia maendeleo hapa tunazungumzia material things.
So tunapaswa kwenda deep hapa kidogo na kutafakari kwa kina.
Na hatuwezi kuepuka kuongelea evolution of the mind kutoka katika ile mind ambayo inafanana na wanyama na kuwa na hii inayoitwa creative mind. Mind ambayo inauwezo wa ku form ideas na ku create things. Tofauti kati ya nchi tajiri na maskini ni gunduzi walizofanya. Mataifa yaliyofanya gunduzi ndio yaliyoendelea kwa kasi. Kwahiyo nchi za ulaya na marekani wamekuwa na scientist wengi na wanafalsafa wengi wakifanya research kugundua na kuunda mambo. So development imeanzia hapo kwenye gunduzi bila gunduzi hakuna maendeleo. Infact gunduzi ndizo zilizotenganisha mataifa maskini na mataifa tajiri na wale wanaotawala mataifa mengine ni wale wenye technologia ya hali ya juu. Mind is the source of everything we see. Kwahiyo inategemea ubora wa minds za watu wa mataifa husika na jinsi gani wame organize watu wao, kujiletea maendeleo yao wanyewe. So kama watu wamegawanyika hawana direction moja ni ngumu wao kuendelea. So we must invest in research and development. Hata malighafi tunazojidai nazo na kujiita matajiri bila gunduzi zao wazungu malighafi zetu ni nothing ! Sababu ya gunduzi zao demand ya malighafi ikapanda juu. Ukizungumzia petrol, dhahabu au chuma ni gunduzi zilizofanya vitu hivyo kuwa na value. Before wakoloni sijui kama wasukuma walikuwa wanajua value ya almasi? Kwasababu ya gunduzi kwamba unaweza kuichonga ikang’aa ikapanda value bila gunduzi wa magari petrol isingekuwa na thamani. Kwahiyo kitu cha value kuliko kitu kingine ni mind. So watu wetu wana mind nzuri kiasi gani? Kwasababu ndio source of development? Je wanafukiri sawa sawa?
But in nature hakuna maskini, umaskini umeletwa na binadamu kwasababu they think na kugundua na hapo ndipo paka watenga wenye nacho na wasio nacho, mataifa maskini na matajiri. In nature hakuna maskini. Umaskini umeletwa na binadamu wenyewe kwa sababu ya ability yao ya kufikiri na kugundua. In nature all are equal, ndio maana hakuna simba maskini, ngedere maskini au pundamilia maskini kwasababu tunafikiri, umaskini na utajiri umekuja! So mind is the source of all these things. In nature all we are equal. Kilichotutofautisha ni mind zetu. So creative mind is the source of all these things. So infact there must be some fault in the way we think and behave ndio maana hatuendelei haraka. Pengine tunakumbatia ujinga na kupiga teke werevu na maarifa. Kwahiyo tunabaki wajinga.
 
Pia hivi vitabu viwili vinaeleza kirefu sana kuhusu hii mada.
Hiki cha kwanza kinaeleza kuwa tofauti zimetokana na tofauti za sera.
tumblr_m9ultsWTaB1qjkc8xo1_1280-685x1024.jpg
Hiki kitabu cha pili kimejikita zaidi kwenye sababu za kijiografia. Kipo deep sana hiki.
Ggas_human_soc.jpg
 
Back
Top Bottom