Nini tofauti na uhusiano uliopo kati ya Yesu, Allah na Yehova.?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,894
155,917
Kuna wanaosema Yesu ni Mungu, na wapo wanaosema Allah ni Mungu. Pia kuna wengine wanaosema kwamba Yehova ni Mungu.

Je tunaweza kuwa na miungu watatu na wakawa na nguvu moja?

Je nini uhusiano uliopo kati ya watatu haWa?

Mimi naona hawa ndio chanzo cha ukosefu wa amani duniani.
 
Hao ni miungu feki hawajawahi kuwepo. Wametengenezwa tu na wanadamu kwa malengo ya kiuchumi na kiutawala.
 
Kwa kiarabu neno mungu ni illah. Lakini wao wanaspecify Mungu wanayemwabudu anaitwa Allah maana wapagani wa wakati huo walikuwa na illah wengi, Mtume (SAW) akapewa specification ya huyo mungu anayepaswa kuabudiwa badala ya hao other deities.

Hata hivyo, description ya Allah ni tofauti sana na description ya Mungu wa sisi Wakristo, kwakuwa Mungu wa Wakristo ni anaishi katika utatu mtakatifu yaani Mungu baba, Mwana ambaye ni Yesu na Roho mtakatifu, one in 3 and each ikiwa na specific role wakati huo ni kitu kimoja.

"Na tufanye mtu kwa mfano wetu" alisikika Mungu akiongea akiwa katika process ya kumuumba binadamu wa kwanza, note hapo aliongea katika uwingi.

Sisi Wakristo hatupendi sana kuchunguza kupata tafsiri ya utatu mkatatifu, maana ni ngumu kwa binadamu unayeishi katika nafsi 2 yaani roho na mwili, kufikiria uwepo wa nafsi ya 3, wengine wakishindwa kabisa hata kujiconnect na roho zao wenyewe wanaishi kama makopo (mwili) isiyo na content ndani yake (roho).

Good news ni kwamba hiyo nafsi ya tatu ya Mungu huweza pia kuishi baina yetu pale tunapoishi maisha ya usafi wa nafsi zetu. Yesu aliahidi hilo wakati anatoa zile speeches zake zilizoenda shule katika vitabu vya injili. Roho wa Mungu atakuelekeza namna sahihi ya kuishi, na ukiwa na uwezo wa kuisikia na kufuata maelekezo. Huyu Mungu ni mysterious sana!

Mungu atuongoze katika njia ya kweli na uzima. Amina
 
Back
Top Bottom