Ninaomba tujadiliane kwa hoja na umakini mkubwa.
Serikail yetu imejibainishwa kupendwa na kuungwa mkono na Watanzania asiliamia kubwa kama siyo wote. Serikali hii inaundwa na chama kinachopendwa na kukubalika kila mahala ndani na nje ya nchi kiasi kwamba katika kila chaguzi, chama hiki kimekuwa kikishinda kwa asilimia za juu kwa wastani wa 80%.
Kwa nini sasa inakuwa na hofu ya kuangushwa na watu wachache tu wasioichagua ambao hata si zaidi ya 20%? Ninasema hivi kwa mshangao kwa nini nguvu kubwa mno zitumike kuwazuia hawa wachache wasiokuwa hata na silaha wala influence kufanya mikutano yao?
Zaidi sana kumekuwa na sintofahamu kubwa inayoonyeshwa na hofu za viongozi wa hii serikali pale wanaposikia kuna watu wanataka kuandamana kwa amani ili kufikisha ujumbe wao kwa masuala wanayohitaji yafanyiwe kazi. Hii hofu na taharuki inatoka wapi? Kwa nini serikali isitumie jehsi la polisi kusimamia usalama wa hayo maandamano ili yafanyikie kwa amani ? Hizo nguvu za kuua waandamanaji, zisingezaa matunda mema na ya amani kama zingelitumika kulinda usalama wa hao waandamanaji na wadau wengine pasipo kufanya mauaji?
Inakuwaje serikali pendwa inaogopa maandamano na mikutano ya hao 20% ambao wala hawawezi kufanya hatari yoyote?
Zaidi sana ninaomba tujadiliane hii dhana ya kutafsiri kwamba maandamano ya amani ni mapinduzi, inatoka wapi? Kuna kivuli kibaya kinacholeta ndoto mbaya zinazoopelekea watu wakimbie usingizini pasipo sababu?
Ninatamani viongozi wa nchi yangu, wangekubali kuongoza kwa kufuata katiba ya nchi, kuwaruhusu wanaotaka kuandamana waandamane ili mradi hawafanyi fujo, iwaruhusu watu wakusanyike kwenye mikutano ya siasa kama chama kilichopo madarakani kinavyofanya ili mradi hawavunji sheria. Serikai iendelee na kufanya maendeleo ya taifa bila matusi, ubaguzi, na kitu kinatiwa unyanyasi wa ki itikadi na kuimarisha uhusiano wa viongozi na watu wa kawaida.
Nini maoni yako?