Nini Suluhu ya tatizo la foleni barabarani mvua zikinyesha

DISPLEI

Member
Oct 17, 2012
70
46
Tatizo la foleni barabarani limekuwa likijirudiarudia kila mvua kubwa zikinyesha. Ukiangalia, chanzo kikubwa ni baadhi ya njia za kuingia na kutoka maeneo mengi hasa mjini kutopitika kutokana na kujaa maji hivyo kufanya magari kutegemea njia chache. Ikishakuwa hivyo kila mtu anakuwa na uharaka kiasi cha kutotaka kusuburiana hasa kwenye makutano ya barabara. Ukweli madereva wakiwa na subira kwenye makutano ya barabara, ugumu unaojitokeza wa magari kufungana unaweza husiwe kama itokeavyo wakati wa mvua.

ukiangalia kazi ya Traffic Police kwenye makutano huwa wanaruhusu mapishano ya magari kwa zamu hivyo kusaidia kutokuwa na foleni za ajabu. Bahati mbaya wakati wa mvua wanakuwa hawapo kitu kinachosababisha magari kufungana kwenye makutano mwishowe hakuna gari linalokuwa linaenda popote. Hiki ndiyo kilichotokea juzi na huwa inakuwa kila mvua kubwa zikinyesha.

Maofisa usalama barabarani wangetoa mwongozo wa watu kujiongoza wakati wa dharula kama hizi na kuusambaza kwenye mitandao ili madereva wajenge ustaalabu utakaopunguza tatizo hili wakati wa mvua. Ukiangalia wakati huu ndiyo mvua zinaaanza kwa hiyo tukio la juzi bila kufanya chochote litajirudia tena. Tusadiane kuelimishana ili tupunguze matatizo kama hayo yasijirudie.
 
Back
Top Bottom