Nini siri ya machale ya jambo litakalotokea?

Sokoro waito

JF-Expert Member
Nov 21, 2014
2,201
2,587
Kwanini watu wengine huwa na machale juu ya jambo baya liwezalo kumtokea au tayari linamtokea wakati huo huo. Hata wengine utasikia akisema "Moyo wangu unauma" wakati huo huo anadai kumkumbuka mtu wa karibu kama vile mke au mme wake akihisi kumfanyia jambo baya lolote.

Mtu mwingine utasikia akisema sina amani kabisa kusafiri leo, anaahirisha kusafiri lakini baadae utasikia basi ambalo angesafiria limepata ajari mbaya hata kuua au kuumiza watu. Maswali yangu ni,

1.Je Nguvu ya machale hutoka kwa Mungu au wapi?

2.Je Watu wote wana machale au ni baadhi tu ya watu wana uwezo huo.

3.Je kuna njia ya mtu kukuza uwezo wa machale yake.
 
...kuna watu wanafanya meditation bila kujua..na hii inategemea na utulivu wa hali ya juu wa mhusika na mazingira ya maisha kiujumla...BINADAMU KAMA WANYAMA WENGINE ANA MACHALE..NA NI KILA BINADAMU.
 
asante kwa mchango wako, nijibu pia maswali yaliyobaki hapo juu.
 
..Machale au intuition ni zawadi ambayo kila binadamu anayo.ishu ni jinsi gani unaweza kuifeel na kuitumia kiusahihi,hapa ndo inategemea mtu na mtu historia yake kwenye meditation either kwa kujua au kutokujua....

meditation ndio nini mkuu, wengne ni wageni kwa hilo.
 
Mimi imenitokea mwezi uliopita. Ilikuwa muda kama saa 1 hadi 2 usiku, umeme ulikuwa umekatika. Nimetoka zangu kijiweni nikaenda Mpesa shop kumtumia mtu pesa, bahati mbaya hakuwa na pesa za kutosha. Nikakata shauri kwenda duka jingine, ni mbali kidogo kutokea pale. Wakati nikiwa nishamaliza nusu ya safari, nikaghairi ghafla bila sababu za msingi na nikaamua kurudi kijiweni kwangu. Ndani ya dakika 15, nikapigiwa simu na jamaa yangu na kuniuliza nilipo. Muda mfupi akaja.

Akaniambia pale kwenye mpesa, muuzaji amepigwa risasi, mwili wake umelala pale, inaonekana amepigwa muda. Nilibaki nashangaa tu
 
Kwanini watu wengine huwa na machale juu ya jambo baya liwezalo kumtokea au tayari linamtokea wakati huo huo. Hata wengine utasikia akisema "Moyo wangu unauma" wakati huo huo anadai kumkumbuka mtu wa karibu kama vile mke au mme wake akihisi kumfanyia jambo baya lolote.

Mtu mwingine utasikia akisema sina amani kabisa kusafiri leo, anaahirisha kusafiri lakini baadae utasikia basi ambalo angesafiria limepata ajari mbaya hata kuua au kuumiza watu. Maswali yangu ni,

1.Je Nguvu ya machale hutoka kwa Mungu au wapi?

2.Je Watu wote wana machale au ni baadhi tu ya watu wana uwezo huo.

3.Je kuna njia ya mtu kukuza uwezo wa machale yake.

Jitahidi kupata muda wa kujitenga ukatulie mahali aidha porini, chumbani, au mahali popote ilimradi pasiwe na kelele/usisumbuliwe uanze kujihoji maswali kuhusu wewe tu.

MFANO.
Wewe ni nani?
Umetoka wapi na unaenda wapi?
Kwanini upo hapo ulipo?
Jiangalie ujishangae, ikiwezekana vua hata nguo ujiangalie kwa hisia kali na kwa UJASIRI! Wakati unajiuliza hayo uweke dini yako pembeni maana hukuja nayo, wala usiwaze mambo mengine nje yakoyako maana hukuja nayo.
Wakati ukijitazama utaona mwili wako ambao ni kama roboti tu. Sasa jiulize huo mwili/nyumba ambayo unayoitumia mbona kuna wakati inakucontrol wakati wewe ndio mwenye mamlaka ya kuamua iwe vipi kwanini ikudhibiti? Wewe sio huo mwili bali ni nguvu inayoishi.
 
duh! Hatari!
 
Mimi imenitokea mwezi uliopita. Ilikuwa muda kama saa 1 hadi 2 usiku, umeme ulikuwa umekatika. Nimetoka zangu kijiweni nikaenda Mpesa shop kumtumia mtu pesa, bahati mbaya hakuwa na pesa za kutosha. Nikakata shauri kwenda duka jingine, ni mbali kidogo kutokea pale. Wakati nikiwa nishamaliza nusu ya safari, nikaghairi ghafla bila sababu za msingi na nikaamua kurudi kijiweni kwangu. Ndani ya dakika 15, nikapigiwa simu na jamaa yangu na kuniuliza nilipo. Muda mfupi akaja.

Akaniambia pale kwenye mpesa, muuzaji amepigwa risasi, mwili wake umelala pale, inaonekana amepigwa muda. Nilibaki nashangaa tu

nguvu ya machale hiyo
 
Back
Top Bottom