Naombeni elimu ya kiroho kuhusiana na hili suala, je ni kawaida au?

vanus

JF-Expert Member
May 27, 2017
1,149
2,842
Habari wakuu

Kuna hii hali huwa naipitia mara kwa mara inanipa mshangao na maswali mengi!

Yaani nimekuwa na uwezo fulani wa kufikiri kitu na kikatokea baada ya muda fulani.

Kuna siku nilikuwa kwenye mkusanyiko mkubwa wa watu, baada ya kuwaangalia wale watu kwa muda mfupi nikajikuta nawaza na naona wale watu wakikimbia kwa kuinama chini.

Haikupita dakika 10, watu wakaanza kukimbia kwa kuinama na kujificha baada ya nyuki wengi kutokea eneo hilo.

Kuna mshikaji wangu nilimuachia mzigo dukani kwake nikamwambia nitakuja kuchukua siku fulani, nikasahau sikuenda ikapita kama wiki moja

Sasa jmos moja nimetulia home nikakumbuka nimesahau kufata mzigo wangu, huwezi kuamini haikupita dakika 2 baada ya kufungua data, naona sms whatsapp ananikumbusha kuhusu mzigo.

Hili swala la kumkumbuka mtu na kupigiwa simu au kutumiwa sms baada ya muda kidogo kwangu ni swala la kawaida sana, au kukutana na mtu ambaye nilikuwa namfikiria kichwani ni jambo la kawaida sana

Na ukimwambia mtu anakataa anasema acha uongo bana hujanikumbuka wala nini.

Je hii ni kwangu tu wakuu, au na nyie mnapitia mambo kama haya? Kiroho imekaaje?
 
Manabii wengi mjini wanatumia hiyo kama fursa ya kujaza waamini makanisani mwao 🐒

Utaskia nabii anaibuka anasema,kuna mtu anafikiria kuja kutoa sadaka ya laki moja hapa mbele muda huu, kwasabb kuna mahali ana appointment ya pesa nyingi anahitajika muda huu 🐒

Hebu ñjoo na sadaka yako hapa mbele, nikuombee na uwahi kikao maana wewe ni mtu muhimu sana pale na kikao hakianzi mpaka ufike wew 🐒

Hata wew ndugu yangu, Inawzekana Mungu anakuita, hebu fungua maskio ya moyoni mwako uweze kuskia sauti ya wito wa Mungu katika maisha yako 🐒

Huenda anataka kukutuma au kukutumia mahali kwa watu wake 🐒

ni karama ya kipekee hiyo..
 
Je wewe ni dini gani?

Je wewe ni mchamungu unafanya ibada sana?

Je wewe ni mtu wa kusema kweli?

Je kwenu kuna historia ya waganga?

Kupitia maswali hayo huenda tunaweza ku-figure out jibu la swali lako.

Kingine ni kuwa hali kama hizo ndio huwa zinawakuta watu japo ni wachache katika wengi.
 
Sijajua vizuri kuhusu historia ya familia yangu

Ila siku chache kabla sijazaliwa kulikuwa na nyoka mkubwa sana ndani kwetu akizunguka juu ya paa

Wazazi walijaribu kumuua kwa kumpiga lakini haikuwezekana maana alikuwa anapotea

Wakaitwa mpaka majirani na wazee wa heshima lakini ilishindikana na hakuwa kuzuru mtu

Baada ya mama kupata uchungu kwenda kujifungua hospitali, wakarudi nyumbani na hawakuwahi kumuona tena huyo nyoka.

Hii nilisimuliwa na mama hata watu wazima pale mtaani wananiogopa kwasababu wanajua hilo tukio, nyoka alikuwa mwekundu hivi mkubwa
 
Manabii wengi mjini wanatumia hiyo kama fursa ya kujaza waamini makanisani mwao

Utaskia kuna mtu anafikiria kuja kutoa sadaka ya laki moja hapa mbele muda huu, kwasabb kuna mahali ana appointment ya pesa nyingi anahitajika muda huu

Hebu ñjoo na sadaka yako hapa mbele, nikuombee na uwahi kikao maana wewe ni mtu muhimu sana pale na kikao hakianzi mpaka ufike wew

Inawzekana Mungu anakuita, hebu fungua maskio ya moyoni mwako uweze kuskia sauti ya wito wa Mungu katika maisha yako

Huenda anataka kukutuma au kukutumia mahali kwa watu wake

ni karama ya kipekee hiyo..
Kama jana nilienda sehemu fulani ile kufika pale nje nataka niingie ndani akili ikaniambia ukiingia huko utaweza kukutana na mtu fulani

Yaani ile natia mguu nakutana na mshikaji ikabidi nivunge tu, na huyu mshikaji nilitoka kumota juzi yake
 
Sijajua vizuri kuhusu historia ya familia yangu

Ila siku chache kabla sijazaliwa kulikuwa na nyoka mkubwa sana ndani kwetu akizunguka juu ya paa

Wazazi walijaribu kumuua kwa kumpiga lakini haikuwezekana maana alikuwa anapotea

Wakaitwa mpaka majirani na wazee wa heshima lakini ilishindikana na hakuwa kuzuru mtu

Baada ya mama kupata uchungu kwenda kujifungua hospitali, wakarudi nyumbani na hawakuwahi kumuona tena huyo nyoka.

Hii nilisimuliwa na mama hata watu wazima pale mtaani wananiogopa kwasababu wanajua hilo tukio, nyoka alikuwa mwekundu hivi mkubwa
Umejibu swali moja tu vipi kuhusu dini , uchamungu na ukweli?
Kuhusu tukio la kuzaliwa kwako linamaelezo yake ila yanategemea pia majibu ya hayo maswali matatu ambayo bado hujayajibu.
 
Je mkuu ukihitaji aina Fulani ya kazi unaipata?

Hiyo ni nguvu ambayo huwa inaendana na manifest and manifestation ,vibration and frequency

Ukisoma mambo ya law of Attraction katika universe law utaelewa kwa kina.
 
Hii Hali hata Mimi Huwa inanitokea
👇
Hili swala la kumkumbuka mtu na kupigiwa simu au kutumiwa sms baada ya muda kidogo kwangu ni swala la kawaida sana, au kukutana na mtu ambaye nilikuwa namfikiria kichwani ni jambo la kawaida sana

Na ukimwambia mtu anakataa anasema acha uongo bana hujanikumbuka wala nini.
 
Umejibu swali moja tu vipi kuhusu dini , uchamungu na ukweli?
Kuhusu tukio la kuzaliwa kwako linamaelezo yake ila yanategemea pia majibu ya hayo maswali matatu ambayo bado hujayajibu.
Siamini katika dini mkuu japokuwa nimezaliwa katika ukristo
 
Je mkuu ukihitaji aina Fulani ya kazi unaipata?

Hiyo ni nguvu ambayo huwa inaendana na manifest and manifestation ,vibration and frequency

Ukisoma mambo ya law of Attraction katika universe law utaelewa kwa kina.
Kwenye maswala mengine sijaona matokeo itabidi nisome hizo law of attraction labda ntapata kitu
 
Sijajua vizuri kuhusu historia ya familia yangu

Ila siku chache kabla sijazaliwa kulikuwa na nyoka mkubwa sana ndani kwetu akizunguka juu ya paa

Wazazi walijaribu kumuua kwa kumpiga lakini haikuwezekana maana alikuwa anapotea

Wakaitwa mpaka majirani na wazee wa heshima lakini ilishindikana na hakuwa kuzuru mtu

Baada ya mama kupata uchungu kwenda kujifungua hospitali, wakarudi nyumbani na hawakuwahi kumuona tena huyo nyoka.

Hii nilisimuliwa na mama hata watu wazima pale mtaani wananiogopa kwasababu wanajua hilo tukio, nyoka alikuwa mwekundu hivi mkubwa
Acha fikra za ushirikina
 
Hii Hali hata Mimi Huwa inanitokea

Hili swala la kumkumbuka mtu na kupigiwa simu au kutumiwa sms baada ya muda kidogo kwangu ni swala la kawaida sana, au kukutana na mtu ambaye nilikuwa namfikiria kichwani ni jambo la kawaida sana

Na ukimwambia mtu anakataa anasema acha uongo bana hujanikumbuka wala nini.
Kwangu imezidi sana mpaka najishtukia, kuna demu wangu yupo huko pwani

Tulizinguana kitambo sana, sasa siku 2 nyuma nikawa namuwaza sana nakumbuka zile best moments

Huwezi amini mkuu juzi naingia IG nakuta sms yake
 
ˌdeɪʒɑː ˈvuː/

noun

a feeling of having already experienced the present situation.

"a feeling of déjà vu"
 
Back
Top Bottom