Nini sababu za wapiga kura kupungua na nini kifanyike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini sababu za wapiga kura kupungua na nini kifanyike?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abduel paul, Nov 25, 2010.

 1. a

  abduel paul Senior Member

  #1
  Nov 25, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Idadi ndogo ya watu kujitokeza kupiga kura!

  kadiri ya siku zinavyo zidi kwenda swala hili limeanza kusahaulika na pengine kuonekana lilikuwa la kawaida, lkn madhara yake ni makubwa, ktk ka uchunguzi kangu nilichofanya mtaani kwangu, na ofisini kwangu niligundua wengi ambao hawakujitokeza kupiga kura wameathirika na mfumo wa upigaji kura, ya kwamba hawana imani tena na KURA YAO MOJA kwani wengi wamekua wakisema hata kama akipiga kura kiongozi anajulikana, na hii ilitokana na either kuachwa kwa taasisi kutoa matokeo ya utafiti na watu kuyaamini (haya ni maoni yangu) au kukosekana kwa imani na tume ya uchaguzi. wewe unafikiria nini?
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Click hiyo button ya search uitafute manake hii thread ishajadiliwa hapa jamvini!
   
 3. T

  Thesi JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jana nilikuwa naongea na ndugu yangu m1 ambaye ameonekana kupata pesa hivi karibuni nikamuuliza pesa umetoa wapi ndugu yangu! Bila kumung'unya maneno akaniambia "UCHAKACHUAJI WA KURA" na akaendelea mbele kunieleza mpango huo ulivotekelezwa. Alichoniambia ni kuwa hapa nilipo ambako ni mkoa mpya huu CCM wametumia zaidi ya milion 100 kufanikisha mpango huo haramu kwenye jimbo moja tu hapa. Walichokuwa wanafanya ni kwenda maeneo ambako wanajua CHADEMA wana nguvu. Wakifika maeneo hayo wanakutana na viongozi wa mashina na hao wanawapeleka au wanawaelekeza kwa wananchi ambao wanajua hawataipigia kura CCM. Hao wananchi wanapewa pesa kwa makubaliano kisha kadi zao zinachukuliwa mpaka baada ya uchaguzi.
  Mpango huo uliwahusisha vyombo vya usalama na TAKUKURU ambao walizima namba zao za simu karibia na uchaguzi au siku ya uchaguzi.
  Lazima watu tunaoitakia mema nchi yetu tujiandae kupambana na hawa watawala wahalifu. Tujue tunatawaliwa na wahalifu ambao wako tayari kufanya chochote ili wawe madarani. Nimekuwa nikiamini Dr. Slaa alipata kura zaidi ya JK lakini lazima kuna mbinu ilitumika kuzima ushindi wa Dr.
  Tatizo watanzania wengi hatujajua nani tunapambana naye. Tunafikiri ni mtanzania mwenzetu. Ndiyo ni wtanzania hawa lakini ni wahalifu wa kutupwa kama kweli walifanya vitendo hivi ambavo kwa asililimia 90 uwezekano upo vilifanyika. Hii itakuwa ni njia 1 kati ya nyingi zilizotumika lakini hizi njia za kupunguza wapiga kura ina athari kubwa zaidi make kama kufanikiwa imefaniwa sana. Mathalan siku zote tangu uhuru turn out haijawahi kuwa chini ya asilimia 70. Ikiwa 30% imetumika zengwe kuwazuia kupiga kura na ikiwa hawa walikuwa wafuasi wa upinzni ndo walilengwa ni dhahri JK alikuwa ameshindwa uchaguzi vibaya.
  Bila tume huru ya uchaguzi na wananchi na vyama vya kisiasa kutofatilia uchaguzi kwa njia zao makini hata nje ya vyombo vya usalama ambavo haviwezi kuchukua hatua wakati huo ni dhahri tutaendelea kuimba mabadiliko bila mabadiliko.
  Uchaguzi wa mwaka huu nina imani watu walihamasika kupiga kura kuliko chaguzi zote zilizopita na haiwezekani kamwe kuwa waliopiga kura ni 42% tu.
   
 4. D

  Derimto JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hatuna elimu ya kutosha baada ya kubanwa miaka 50 tangu uhuru unadhani tutashindwa kulaghaiwa na wapenda madaraka wanaotununua kwa fedha zetu wenyewe!? Lazima kufanyike jambo hapa vinginevyo huko tunapokwenda hakutakua na ndoto za mabaliko ya maana ya kidemokrasia
   
 5. H

  Haika JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Tafadhali usikose usingizi, tunakwenda huko,
  Hakuna kurudi nyuma
  Hatumuogopi mtu, Si Kikwete, Slaa, wala fisadi, sauti ya watu ni Sauti ya Mungu.
  Tunataka katiba ambayo itamuwajibisha kiongozi yoyote madarakani, awe CCM, CDM, CUF, au binafsi,
  asiwepo yoyote juu yetu na katiba yetu.
   
 6. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hamasa ya watanzania katika upigaji kura umekuwa ukipungu siku hadi siku. Nimekuwa nikifuatilia idadi ya wapiga kura katika chaguzi mbalimbai kuanzia 2005 hadi leo hii. Trend inaonyesha kuwa kunasignificant decrease ya idadi ya wapiga kura. Zipo sababu nyingi zinazopelekea hali hii.

  Nape Nnauye kupitia kipindi cha asubuhi kinachorushwa na Clouds Fm ametoa sababu nyingi ila hii imenifurahisha, amesema sababu ya kupungua kwa idadi ya wapiga kura ni kwamba kunabaadhi ya vyama vya siasa (akimaanisha vya upinzani) kuwa vinatishia wakina mama ili wasipige kura na hivyo idadi kupungua. Je wewe unasemaje???Wapo wachangiaji waliosema kuwa hakuna elimu ya kutosha kwa wapiga kura, wengine walisema matokeo yanakuwa yameshajulikana kabla ya watu kupiga kura hivyo kuondoa umuhimu wa zoezi zima, wapo waliorusha lawama kwa tume ya uchaguzi kwa ujumla wake, wapo waliosema kuwa uboresheshaji wa daftari la wapiga kura ni kikwazo na wengine walisema hawana imani na viongozi waliosimamishwa kugombea ndo mana hawapigi kura. Wapo waliosema wizi wa kura ndio chanzo. Je wewe unasemaje???

  Ndugu zangu, hata kama chama flani kitakubalika sana kwa wananchi, lakini kama wananchi wanaokikubali chama hicho hawana sifa ya kupiga kura ni kazi bure. Mimi nashauri nguvu tunazotumia kwenye kampeni za uchaguzi, pia tutumie nguvu za caliber hiyo hiyo kwenye kushauri/kushawishi watu kujiandikisha ili kuongeza mtaji wa wapiga kura.

  Kwa mfano, vyama vingi vya upinzani vinakubalika na vijana ambao inawezekana miaka mitano iliyopita hawakutimiza umri wa kupiga kula au hawakuwa na mwamko wa kufwatilia siasa zetu, wengi we vijana hao inawezekana hadi sasa hivi bado hawajajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura au wamehamia sehemu walipopata kazi. Hivyo mchango wao kwenye kumchagua kiongozi wa chama wanachokipenda ni zero. Hivyo harakati za kuboresha mivuto ya vyama vyetu ziende sambamba na harakati za kushawishi wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura sehemu wanapoishi ili huo uwe ni mtaji per se, kukusanyika kwa wingi, kumshangilia mgombea wkt wa kampeni hakutakuwa na tija kama hupigi kura.!!Nashauri kuwepo na kampeni maalum ya vyama vya siasa kuhimiza watu kujiandikisha, kwani kazi hii tukiiachia tume peke yake ni kwamba tunajikomoa wenyewe. Kura yako ni muhimu kwa maendeleo ya Taifa lako. Kura yako inatosha kuifanya Tanzania unayoitaka.
   
 7. M

  Mayu JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  moja ya sababu ni movement ya watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine na uvivu wa kufanya uandikishaji sehemu waliyohamia

  Watu kutokuwa makini kutunza vitambulishao vya kuwa, wanapoteza
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  Lini waliongezeka?Takwimu unazo?ukweli ni kuwa majina mengi yaliyopo katika daftari hili ni feki na yaliwekwa makusudi na ccm ,kama unakumbuka wakati wakuandikisha watu mara ya kwanza vyama pinzani vili lalamika sana kuhusu tume kuandikisha idadi ya watu kubwa kupita hata record za takwimu za taifa. au mmesahau hili?
   
 9. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaulize tume
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Sababu kuu wananchi wamekata tamaa,sisiemu wanaiba kura sana ndio maana wanaona hata wakiipigia cdm,sisiemu wanaiba kura wanashinda,ila kwa kipindi hichi cdm inbidi ifanye mikutano mingi kuwaelimisha watu elimu ya uraia na kuwapa somo jinsi wizi wa kura unavyofanyika ili waweze kukabiliana nao kwa mfano wizi ulivyodhibitiwa arumeru!
   
 11. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Tume haina majibu ndo mana haina inachofanya kubadilisha hii hali. wewe kama mwananchi mzalendo unapaswa ulione hili kuwa ni muhimu sana kwa mustakabali wa Taifa lako.
   
 12. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Unahitaji takwimu zipi Kibanga ili ujiridhishe kuwa idadi ya wapiga kura is tremendously dwindling???
   
Loading...