Nini msimamo wa Tanzania juu ya Sahara Magharibi?

Nini msimamo wa Tanzania juu ya Sahara Magharibi?

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,347
Sahara Magharibi ilikuwa koloni la Hispania baada ya mataifa ya Ulaya kugawana makoloni kwenye ule mkutano wa Berlin wa mwaka 1884. Hispania walipoondoka Morocco iliikalia Sahara Magharibi kimabavu huku ikida kuwa eneo hilo ni sehemu ya himaya yake kwa sababu ukoo wa kifalme wa Morocco ulitokea eneo hilo kabla ya ukoloni. Hatua hiyo ilisababisha wananchi wa Sahara Magharibi kuingia katika harakati za ukombozi kwa kuanzisha kikundi cha Polisario cha kudai uhuru kwa njia ya mapambano.

Kati ya mwaka 1966 hadi 1973, Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha maazimio kama saba hivi yaliyotambua umuhimu wa Sahara Magharibu kujiamulia mambo yake. Aidha mnamo mwaka 1975, Mahakama ya Kimataifa ya Haki (International Court of Justice), katika hukumu yake, ilitupilia mbali kuwa Sahara Magharibi ilikuwa sehemu ya Morocco.

Mapambano yalisitishwa mwaka 1991 na Umoja wa Mataifa ulitaka ifanyike kura ya maoni ili kuamua hatma ya taifa hili. Hata hivyo, mpaka sasa kura ya maoni yaijafanyika kutokana na mgogoro wa kutambua wanaostahili kupiga kura. Mfano, Morocco inataka wavamizi wake kwenye eneo hilo nao waruhusiwe kupiga kura. Jitihada za kusuluhisha mgogoro wa Sahara Magharibi kwa njia wa amani bado zinaendelea.

Kwa muda mrefu Tanzania imekuwa katika mtari wa mbele kidiplomasia katika kudai uhuru wa Sahara Magharibi. Tanzania haina uhasama na Morocco, lakini kwa muda mrefu imekuwa ikipinga kitendo cha Morocco kuendelea kuikalia Sahara Magharibi kimabavu. Pia Tanzania imekuwa ikiishauri Morocco kurejea kwenye Umoja wa Afrika (ambao Sahara Magharibi ni mwanachama) na kukubali kura ya maoni ili wananachi wa Sahara Magharibi waamue hatima yao wenyewe.

Hata hivyo, hivi karibuni kumekuwa na ziara za viongozi wa Tanzania nchini Morocco na habari zitokanazo na ziara hizo aidha zinaleta utata juu ya msimamo wa sasa wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi au labda hatuambiwi kwa uwazi dhamira yetu na nini hasa kinachozungumziwa na kukubaliwa na serikali ya Morocco kila viongozi wetu wanapoenda huko. Pia huwa huwa wanaenda tuu Morocco au wanaenda kujadiliana pia na viongozi wa Sahara Magharibi?


tanzanie.jpg


Katibu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana akiwa na Spika wa Bunge la Morocco, Rachid Talbi Alami, juzi Jumatatu nchini Morocco.

Habari zilizoripotiwa na tovuti ya lugha ya Kifaransa ya Le360 zinadai kuwa Tanzania inasonga mbele na majadiliano yake na Morocco kutoitambua tena Sahara Magharibi (Sahrawi Arab Democratic Republic) kama nchi inayotakiwa kujitawala yenyewe. Tovuti inadai kuwa jana Jumatatu, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alifanya mazungumzo na spika wa Bunge la Morocco Rachid Talbi Alami jijini Rabat, Morocco.

Vyanzo vya habari vya Le360 kutoka Bunge la Morocco ambavyo havikutaka kutajwa majina yao vimedai kuwa majadiliano yanaendelea vizuri kati ya Tanzania na Morocco kutoitambua tena Sahara Magharibi kama nchi inayotawaliwa kimabavu na Morocco. Aidha Le360 inadai Tanzania inataka kuboresha uhusiano wake na Morocco kwa kutambua pendekezo la Morocco la kuipa Sahara Magharibi mamlaka ya utawala wa ndani tuu wa eneo hilo.

Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi, Polisario, kimekuwa kinalitaka jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa, MINUSRO, kuandaa kura ya maoni ili kuamua kuhusu mustakabali wa himaya hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta. Morocco inakubali tuu kuwepo kwa mamlaka ya utawala wa ndani eneo hilo. Morocco inadai kuwa kujitawala eneo hilo la Sahara Magharibi si suluhisho la kudumu la mgogoro wa eneo hilo. Inadai kuwa Sahara Magharibi inapaswa kuacha mapambano ya kupigania uhuru wa eneo hilo.

picha%2Bnamba%2B3%2B.jpg


Lowassa na kamati yake ya Bunge walipozuru Morocco mwaka 2012.

Itakumbukwa kuwa Mwaka 2012, Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, ikiwa chini ya Mwenyekiti Edward Lowassa ilifanya ziara nchini Morocco ambapo vyombo vya huko viliripoti kuwa aliunga mkono pendekezo la Morocco la kuipa Western Sahara mamlaka ya ndani bila kuwa nchi huru. "Tanzania hopes to see a settlement of the Sahara issue and welcomes Morocco's autonomy proposal," anadaiwa kusema Lowassa alipokutana na Naibu Spika wa Bunge la Morocco Deputy Speaker Mohamed Yatim.

Vyombo vya habari Morroco vilidai kumnukuu Lowassa akisema,
"Tanzania is satisfied with the autonomy proposal to the southern provinces put forward by Morocco as a solution to the Sahara issue" and "The Moroccan autonomy plan must be supported by all African countries and we will defend the proposal and convey the reality of this issue to our partners, because our goal is to see the Sahara in good hands as part of a united Africa."

Lakini aporejea nchni na kuongea na waandishi wa habari Dodoma Lowassa alinukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kuwa "Sisi kama Bunge la Tanzania tunaunga mkono msimamo wa Morocco wa kuitisha kura ya maoni, ambao ni msimamo wa Umoja wa Mataifa". Hata hivyo, nukuu hii ina utata kwa sababu, tofauti na Sahara Magharibi, Morocco haitaki kuwe na kura ya maoni kwa sababu tayari inajua matokeo yatakuwaje. Labda Manyerere Jackton atafafanua walikuwa na maana gani walivyoripiti vile.

Chombo kingine cha habari cha ndani kilidai kuwa Kamati hiyo ya Bunge kamati_ya_bunge_yalikoroga inadaiwa "kukubaliana" na utawala wa Morocco juu ya kuinyima Sahara Magharibi uhuru kamili. Inadaiwa wajumbe wa kamati waliombwa na serikali ya Morocco kuipigia chapuo katika vikao vya Umoja wa Afrika (AU) ili Sahara isipate uhuru kamili. Kamati ya bunge iliombwa na serikali ya Morocco kushawishi serikali ya Tanzania na baadaye serikali kushawishi nchi za Kusini mwa Afrika na baadaye Umoja wa Afrika (AU) kukubaliana na Morocco kuwa Sahara ni sehemu yake.[/URL]

IMG_7294.JPG


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard K. Membe (MB), akitoa msimamo wa Tanzania kuhusu suala la Sahara Magharibi na Morocco, wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Baada ya Lowassa kuyasema hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alitoa msimamo wa serikali ya juu ya mgogoro baina ya nchi za Morocco na Sahara Magharibi kwamba haiko upande wa Morocco kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari vya nchi za Magharibi. Alisema msimamo wa serikali umeafikiana na Umoja wa nchi za Afrika (AU) kwamba Sahara Magharibi inafaa kujitawala yenyewe hivyo yaitishwe makubaliano na watu waweze kupiga kura ili ijulikane kama inajitawala yenyewe au inakuwa pamoja na Morocco.

Membe aliongeza kuwa, Tanzania itaheshimu maamuzi yoyote ya wananchi wa Sahara Magharibi kwa vile "tunaamini wataamua kujitawala wenyewe na siyo kuwa kama kile Kisiwa cha Mayote nchini Comoro". Wananchi wa Kisiwa hicho waliamua kuwa sehemu ya nchi ya Ufaransa, ingawa kipo Afrika.

President-Jakaya-Kikwete.jpg


Rais Kikwete akihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa

Akihutubia Baraza la Umoja wa Mataifa mwaka 2011, Rais Kikwete alisema kuwa uhuru wa Sahara Magharibi ni "outstanding" issue na kutaka Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kuwawezesha watu wa Sahara Magharibi kupata haki yao ya kujitawala wenyewe kama nchi huru.

Rais Kikwete alisema "It is heart-warming indeed, to see our efforts, sacrifices and contributions having been rewarded so handsomely with the independence of all African countries and apartheid having been dismantled in South Africa. Only Western Sahara remains outstanding. I hope the United Nations will expedite the process so that people of Saharawi can determine their future peacefully."

Wakati wa kuadhimisha miaka 50 tokea Tanzania ipate uhuru wake, Rais wa Sahara Magharibi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama cha Polisario Mohamed Abdelaziz, alimtumia Rais Kikwete salamu zake. Salamu hizo zilisema "As our brothers in Tanzania celebrate- with deserved pride- the 50th Anniversary of their independence, it is a great honour for me to express to you and through your Excellency to the people of Tanzania, our warmest congratulations on behalf of the Saharawi people, the government of the Saharawi Arab Democratic Republic and on my own behalf as well as our best wishes for success".

Abdelaziz aliongeza "Since its independence, Tanzania became a shrine for all Liberation Movement and Freedom Fighters of Africa" huku akinukuu maneno ya Mwalimu Nyerere kuwa "For, the right to freedom either exists throughout Africa, or it does not exist anywhere in Africa". Alimalizia salamu zake kwa ku-reiterate "our high appreciation and profound gratitude for the support and solidarity constantly extended by Tanzania to the just struggle of the Saharawi people for freedom and independence".

cc kwa waliokwishafuatilia hili zuala huko nyuma Sheba, FJM, harbab, Mbopo, Raia Fulani, petrol, POLITIBURO, fige, andishile, KIM KARDASH, Kiona, NasDaz, SURUMA, Tumaini Makene, Halisi, Filipo, Kimbunga, JokaKuu, Kichuguu, Mag3, omujubi, Njaare, TUJITEGEMEE, MgonjwaUkimwi, Sangarara, mtotowamjini, MTAZAMO, Nguruvi3, mlagha, TUNTEMEKE, Phillemon Mikael, Kiranga, Tume ya Katiba, Pasco, Precise Pangolin, Njoka Ereguu, Abdillahjr, BAK, Jasusi, Ben saanane, OTIS, ocampo four, DSN, Ogah, Viol, Alinda, Ubongo Silaha, Tina, The Boss, Jagermaster, alles, bucho, Keil, Bongolander, Candid Scope, Sheba, Sniper, manucho, Mpui Lyazumbi, Synthesizer, Tiote, Mkandara, Iza, kalokolaVIII, Sikonge, mharakati, Ukwaju, Chakaza, Mzalendo, Ndahani , W. J. Malecela, JacksonMichael, Njoka Ereguu, TIMING, newazz, KIDUNDULIMA, Kiduku, Mtumishi Wetu, mpujufu, mkomatembo, Kizotaka
 
Last edited by a moderator:
Mbona msimamo wa Tanzania uko wazi, Sahara Magharibi wapige kura ya maoni ili kuamua hatma yao. Na msimamo wa tokea enzi za awamu ya kwanza ni kuitambua Sahara magharibi na PORISARIO.

Achana na siasa za ndani ya Nchi yetu kama ambavyo imeonekana tofauti ya mtazamo baina ya Kamati ya mambo ya nje na Waziri wa mambo ya nje.

Moja ya mambo ambayo yanasikitisha juu ya misimamo yetu katika medani za Diplomasia ni uelewa mdogo au uzembe wa baadhi ya senior officials kwenye ofisi zetu za umma ama Siasa. Mambo kama haya si kila mtu anaweza kuamua aseme nini juu ya mahusiano yetu mahsusi na tawala za nje. Wakati mwingine hii misaada midogo midogo au privilege ndoogondogo imepofusha Watawala wetu.
 
Kuna wakati viongozi wetu kwa tamaa zao wanafanya maamuzi si kwa maslahi ya taifa ila kwa ubinafsi wao wenyewe. Kuna wakati wanajikanyaga ila wakifungua macho wanatakiwa watoe tamko kama nchi ma sio mtu binafsi hapo ndo wengi wanaumbuka.
 
Morocco wamegundua kuwa viongozi wa Tanzania wanatawaliwa na njaa. Kwa hiyo huwa hawajali kuwa jet in kina Lowassa na wanakamati wengine ili kupata support ya key members wa AU. Sema kitu kbaya kimewatokea puani kwa sababu hii AU ya Mugabe imenuia kulivalia njuga suala la Western Sahara.

Ila Tanzania officially ni supporter wa Sahrawi.
 
Bulldog, Kobello ndio maana katiba ya Warioba inakataza kiongozi kuhongwa eti zawadi!!
Kiongozi anpewa rushwa anapotosha ukweli, Moroco should stop colonizing Saharawi!!
Sahara should be free, achana na wala rushwa kina Lowasa rushwa inapofusha macho na ufahamu!!
 
Last edited by a moderator:
EMT,

Sidhani ikiwa msimamo wa Tanzania juu ya Morocco na Western Sahara utakuwa umebadilika tangu kuasisiwa kwa msimamo huo wakati wa utawala wa awamu ya kwanza wa kuunga mkono harakati za oppressed states kujitawala wenyewe kama ilivyokuwa na bado ilivyo kwa Palestine dhidi ya Israel. Pamoja na kwamba mara kwa mara Israel imekuwa ikiisaidia Tanzania huku tukiwa hatupati chochote cha maana kutoka kwa Palestine, lakini msimamo wa Tanzania umebaki pale pale wa kutambua harakati za Palestine katika kujitawala!

Kinachoshangaza ni kauli ya Lowassa kwamba Tanzania inaunga mkono pendekezo la Morocco la kutoa uhuru wa ndani peke yake kwa Sahara Magharibi! Huu ni msimamo wa Lowassa na sidhani kama ni wa Tanzania! Msimamo wa nchi kwa masuala ya nje ni ule unaotolewa na Rais wa nchi ambao umeunukuu hapo juu na ule unaotolewa na Waziri wa Foreign Affairs! Kuonesha kwamba msimamo wa Tanzania haujabadilika, pamoja na hiyo kauli ya Rais, Membe nae akiwa New York September 28, 2012 alitamaka: "With regards to Western Sahara, Tanzania calls upon the UN Secretary General to continue his mediation efforts of bringing together the government of Morocco and the leadership of Western Sahara to resolve the crisis. In this regard, my delegation encourages Morocco to rejoin the AU so that together we can find a durable solution on the independence of Western Sahara." Kwahiyo issue ya uhuru wa Westen Sahara lipo pale pale: Statement of Hon. Membe at UN General Assembly – Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation, Tanzania. Na hata ukija kwa kauli ya Membe Bungeni: “Our position remains the same, we are still supporting the AU’s position on independence of Western Sahara but that does not mean that we cannot have diplomatic relations with Morocco” Kauli hiyo nayo inaenda kinyume na madai ya Lowassa!

Hapa ni muhimu sana kuzingatia hapo kwenye RED juu... hivi sasa we're no longer working on International Relations but we work on International Cooperation! Masuala ya Uhusiano wa Kimataifa yameshapitwa na wakati na kilichopo dunia ya leo ni Ushirikiano wa Kimataifa! Tofauti ipo wapi! Inawezekana nina mdogo wangu baba mmoja, mama mmoja (Uhusiano) lakini namuona ni mtu aliye hopeless, haeleweki eleweki! Katiak situation kama hiyo kunakuja business deal... mdogo wangu anataka nifanye nae kazi na wewe EMT unataka tufanye kazi with the same business deal! Ikiwa nakuona you're more smart than my own brother, I'll definitely choose you (Cooperation) over my brother but that doesn't mean kwamba naweza kuwa tayari kukuona unamfanyia my brother wrong doings!

In those old politics or diplomacy, tulikua tayari ku-loose everything for our brothers but that doesn't apply any longer and anywhere in a modern world! Ndio maana unakuta pamoja na uhasama wa enzi na enzi kati ya China na US (no uhusiano) lakini hawajaacha kufanya biashara between them (it's all about cooperation)! Kutokana na hilo, ndio maana bado Tanzania(sio Kamati ya Lowassa) inaendelea kuunga mkono harakati za Sahara Magharibi kuwa Taifa Huru (uhusiano) lakini hiyo haitufanyi tusiwe na ushirikiano na Morocco ikiwa tunaona kuna manufaa... hapo ndipo inapokuja hoja ya uhusiano wa kidiplomasia ambao ndio consequently una-facilitate cooperation among nations... sawa na ambavyo tunavyoendelea kuunga mkono harakati za Palestine kuwa taifa huru lenye mamlaka kamili lakini huku tukiendelea kushirikiana na Israel kwa hili na lile! Na ndio maana miaka michache iliyopita kulikuwa na mpango wa Israel kufungua fully-fledged embassy hapa Dar es salaam badala ya kutegemea ule wa Nairobi!

c.c JokaKuu, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Mleta mada kama katiba mpya imetushinda ndio itakuwa kutoa misimamo ya nchi za wenzetu!? Hebu mtoa mada ungeomba msimamo wa Tanzania katika katiba mpya kama hujapata majibu zaidi ya matano tofauti toka kwa viongozi wa tume na serekali. Hizo enzi za misimamo ilikuwa ni wakati tuko chini ya uongozi dhabiti wa Mwl.Nyerere sio wakati huu wa viongozi mabepari uchwara.
 
Mbona msimamo wa Tanzania uko wazi, Sahara Magharibi wapige kura ya maoni ili kuamua hatma yao. Na msimamo wa tokea enzi za awamu ya kwanza ni kuitambua Sahara magharibi na PORISARIO.

Achana na siasa za ndani ya Nchi yetu kama ambavyo imeonekana tofauti ya mtazamo baina ya Kamati ya mambo ya nje na Waziri wa mambo ya nje.

Moja ya mambo ambayo yanasikitisha juu ya misimamo yetu katika medani za Diplomasia ni uelewa mdogo au uzembe wa baadhi ya senior officials kwenye ofisi zetu za umma ama Siasa. Mambo kama haya si kila mtu anaweza kuamua aseme nini juu ya mahusiano yetu mahsusi na tawala za nje. Wakati mwingine hii misaada midogo midogo au privilege ndoogondogo imepofusha Watawala wetu.

nadhani kuna wakati tunatakiwa kutambua ukweli kuwa akili zetu na mawazo yetu kwenye mambo ya kimataifa yanatakiwa yaendane na maslahi ya nchi. Moroccans of both sides are same people, they are much more close to each other than they are to Tanzanians.

Kwa hiyo mkuu EMT huwa naina kichefuchefu pale viongozi wetu wanapoongea mambo kwa ajili ya sifa na sio kwa ajili ya maslahi yetu. angalia damu tuliyomwaga na jasho lililovuja kwa ajili uhuru kusini mwa Afrika, what did we get out of it? kejeli tu na asante za mdomini.
 
Mleta mada kama katiba mpya imetushinda ndio itakuwa kutoa misimamo ya nchi za wenzetu!? Hebu mtoa mada ungeomba msimamo wa Tanzania katika katiba mpya kama hujapata majibu zaidi ya matano tofauti toka kwa viongozi wa tume na serekali. Hizo enzi za misimamo ilikuwa ni wakati tuko chini ya uongozi dhabiti wa Mwl.Nyerere sio wakati huu wa viongozi mabepari uchwara.

Imewashinda wale waliotaka kuileta. Wamejichanga wenyewe big time
 
EMT, sasa hivi tunacheza kama timu ya mpira isiyo na formation. Sitarajii tofauti ya nini tunafanya huko nje na haya tunaofanya kwa ajiri yetu hapa ndani.
 
Last edited by a moderator:
Bulldog, Kobello ndio maana katiba ya Warioba inakataza kiongozi kuhongwa eti zawadi!!
Kiongozi anpewa rushwa anapotosha ukweli, Moroco should stop colonizing Saharawi!!
Sahara should be free, achana na wala rushwa kina Lowasa rushwa inapofusha macho na ufahamu!!

Njaa zetu zinaliyumbisha taifa kupitia viongozi njaa
 
Last edited by a moderator:
TANZANIA ni dude moja la ajabu
tunagongana Sahara magharibi na Morocco wakati tulishakula YAMINI na POLISARIO
kwanza tusafishe nyumbani tuwaruhusu WAZANZIBAR nao wapige KURA yao ya maoni kabla ya Sahara Magharibi kupiga yao
la sivyo ni njaa zetu tu ili tupatiwe vijizawadi na allowance za safari
 
..kwanza mkumbuke kwamba Morocco siyo mwanachama wa AU.

..sina uhakika kama in 1984 walijitoa wenyewe, au walifukuzwa. lakini chanzo cha kutokuwa mwanachama wa AU ni huu mgogoro wa Sahara Magharibi.

cc EMT, Kimbunga, NasDaz, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
..kwanza mkumbuke kwamba Morocco siyo mwanachama wa AU.

..sina uhakika kama in 1984 walijitoa wenyewe, au walifukuzwa. lakini chanzo cha kutokuwa mwanachama wa AU ni huu mgogoro wa Sahara Magharibi.

cc EMT, Kimbunga, NasDaz, Nguruvi3
Huu mgogoro wa Polisario ulikuwa na nguvu sana wakati wa golden generation (Huari Boumediene, Samora, Nyerere, Kaunda, Saddat, William Tolbert, Leopad Senghor, Dauda Al Jawari

Ukombozi wa Africa ulikuwa sambamba na suala la Morocco.

Hakuna wakati msimamo wa Tz uliwahi kubadilika kuhusu Polisario.

In fact Sahara magharibi wameanza kuja tena Tz baada ya kuzorota kwa jitihada za UN.

Wameangalia nyuma na kuona kuna ombwe la msukumo waliloliacha akina Nyerere, wanajribu kuja wakidhani kila mmoja ni Nyerere!

Nadhani Morocco inapata support ya nchi za magharibi, angalia suala la Mali lilivyoshughulikiwa, inakuwaje kuna kusuasua kwa suala la sahara magharibi tena likiwa mbele ya UN?
 
..sitasema mengi lakini nahisi pesa za kampeni za CCM mwaka huu zitatoka Morocco.

..kuna madai kwamba uchaguzi wa 2005 na 2010 pesa za kampeni zilitoka Uarabuni[Qatar & Oman].

..tena kumuona Kinana huko Morocco ndiyo kunaniacha na maswali mengi zaidi. nasema hivyo kwasababu CCM inajitambulisha kama chama cha ukombozi barani Afrika. Sasa Katibu Mkuu wa CCM anapofanya ziara Morocco ambao wanaitawala kimabavu Sahara Magharibi kunatoa taswira inayokanganya kidogo, na baadhi yetu tunaweza kuhoji kama CCM bado inaamini ktk ukombozi wa bara zima la Afrika.

..nadhani kuna lack of coordination ktk utekelezaji wa siasa zetu za mambo ya nje, au kama siyo hivyo basi tumeingiliwa na special/personal interests.

..kwa mfano, haiyumkiniki kamati ya BUNGE iwe inazungumza lugha tofauti na SERIKALI ktk suala hili la Sahara Magharibi.

..pia kwa kuzingatia kauli ya Raisi[mwenyekiti wa CCM] ktk kikao cha UN, ziara ya Katibu Mkuu Kinana inakwenda kinyume na msimamo wa Tanzania ambao unaeleweka kwa miongo kadhaa, na umekuwa validated majuzi ktk hotuba ya Raisi[mwenyekiti wa CCM] UN.

cc NasDaz, Kasheshe
 
Last edited by a moderator:
..kwanza mkumbuke kwamba Morocco siyo mwanachama wa AU.

..sina uhakika kama in 1984 walijitoa wenyewe, au walifukuzwa. lakini chanzo cha kutokuwa mwanachama wa AU ni huu mgogoro wa Sahara Magharibi.

cc EMT, Kimbunga, NasDaz, Nguruvi3
Mkuu kuna mambo najaribu kujikumbusha kabla sijachangia hapa. Hii issue ya Sahrawi ina unafiki mkubwa sana wa kidiplomasia. Polisario ni chama cha zamani sana cha ukombozi. Miaka hiyo nikisikia SWAPO, POLISARIO, nk.
 
Msimamo wa nchi uko wazi,bora waziri umetilia mkazo upya suala hili!Tumekusikia,tumekuelewa.
 
JokaKuu,


Suala la Sahrawi Arab Democratic Republic (SADR) na Morocco sio suala la kivyama bali ni la kiserikali kwahiyo CCM na taasisi ambayo iliitambua SADR sio CCM bali ni serikali ya Tanzania kwahiyo ikiwa CCM wanaenda huko kwa nia ya ku-side na Morocco na kuipa kisogo SADR, hiyo itakuwa ni aibu yao wao! Binafsi nisingependa kujimaliza moja kwa moja kwavile it's just a matter of time lengo la Kinana na chama chake kuhusu ziara hiyo litafahamika tu! Ingawaje media ya Morocco imetoa habari kwamba lengo la ziara hiyo ni kufanya negotiation ambayo lengo lake ni kuifanya Tanzania iache kuitambua SADR bado habari hiyo nitaichukulia kama tetesi hasa nikizingatia tabia za Moroccan medias linapokuja suala la SADR... mara nyingi zimekuwa zikieneza propaganda kama ilivyo kwa baadhi ya media za Israel dhidi ya other Mid-Eastern States, particularly Iran and Palestine! Kwa sasa nitachukulia ziara ya Kinana kama yenye lengo la kuzikutanisha nchi hizo mbili hadi pale nitakapokuwa na taarifa zinazotoka kwenye source isiyofungamana na upande wowote!

Kwamba nia ya Morocco ni kuikamata Tanzania ili hatimae itumike kuzishawishi African Union states binafsi naona hoja hii haina nguvu sana hususani nikizingatia kwamba majority of AU states ambazo hapo awali zilikuwa zinaitambua SADR hivi sasa ama zime-withdrawal, suspend au zime-freez recognition of SADR. Eneo pekee la Africa ambalo bado wamekaza ni SADC na EAC countries excluding Burundi ambayo iliacha kuitambua SADR mwaka 2010. Apart from Burundi, hata Kenya wakati wa Kibaki ilisimamisha kwa muda kuitambua SADR... inaelekea walipigwa mkwara na Morocco ambayo ina ubalozi wake Nairobi, being the only fully-fledged embassy ni East Africa. Hata hivyo, Kenyatta alipoingia madarakani akarudisha status ya zamani ya Kenya kuitambua SADR.

Kutokana na hilo, labda kama lengo la Morocco ni kuitumia Tanzania kuzishawishi ama EAC states, or SADC states (kwangu ndiyo hoja yenye nguvu zaidi kv ni politically powerful block in Africa) au zote kwa pamoja na sio Afrika kwa maana ile ile kwamba, most of African states excluding SADC na EAC zimeshaana na SADR... na nyingi kama sio zote zilisitisha kuitambua SADR miaka kadhaa iliyopita... majority in mid 1990's and mid 2000's. Kama ndivyo, basi CCM na ama viongozi wa serikali wanatakiwa kuwa na akili ya kipumbavu iliyokosa aibu pale watakapoanza kuwashawishi radicals kama akina Mugabe, Zuma, Kagame, Kenyatta na wengine kama hao... sijui wataanza anza vipi!

Tukija upande mwingine, narudia hoja ile ile ya awali... isionekane kwamba ni crimes kushirikiana na Morocco... si Morocco wala SADR ambae ni ndugu zetu. Tuna-side na SADR only because ni oppressed country; nothing less nothing more! Ikiwa lengo la serikali ama CCM kukuza ushirikiano na Morocco huku ikiendelea kuunga mkono uhuru wa SADR mimi nawaunga mkono kwa 100%... tuache siasa za ujima za kuwa tayari kupoteza kila kitu kwa ajili ya nchi zingine... we've done a lot and enough is enough! Huko ambako tulipoteza kila kitu kwa ajili yao hakuna tunachopata zaidi tu ya kuishia kujisifia kwenye sherehe za misiba mikubwa za nchi husika huku hata wananchi wa nchi hizo zikiwa hazifahamu kwamba Tanzania ilifanya nini kwenye nchi zao! Ikiwa Morocco kuna opportunities, let's establish diplomatic cooperation huku tukiendelea kuwaunga mkono SADR... an oppressed state or organism need to be protected and defended na ndio maana hata tunapopita mitaani na kukuta baba zima linamdhuru innocent guy, tunasimama upande wa huyo anayeonewa!
 
Last edited by a moderator:
..kwanza mkumbuke kwamba Morocco siyo mwanachama wa AU.

..sina uhakika kama in 1984 walijitoa wenyewe, au walifukuzwa. lakini chanzo cha kutokuwa mwanachama wa AU ni huu mgogoro wa Sahara Magharibi.

cc EMT, Kimbunga, NasDaz, Nguruvi3
Mwaka 1984 ndio ambao SADR walipata uanachama kamili wa OAU... kutokana na hilo, Mororocco wakasusa na kujitoa... kwahiyo walijitoa wenyewe kama njia ya kupinga SADR kupewa hadhi ya uanachama kamili wa OAU/AU.
 
Mkuu kuna mambo najaribu kujikumbusha kabla sijachangia hapa. Hii issue ya Sahrawi ina unafiki mkubwa sana wa kidiplomasia. Polisario ni chama cha zamani sana cha ukombozi. Miaka hiyo nikisikia SWAPO, POLISARIO, nk.
Wala sio unafiki wa kidiplomasia bali, ikiwa ni unafiki basi ni unafiki wa kimaslahi! Enzi ambazo Sahrawi ilipata uungaji mkubwa mkono ni zile enzi ambazo, kwa huku Afrika hatukuwa tunaongozwa na maslahi ya kiuchumi bali maslahi ya kisiasa... kwamba, kwavile sisi tumekandamizwa na mabeberu kwa miongo kadhaa basi mwingine yeyote anayekandamizwa popote pale duniani nae ni mwenzetu na hivyo tusimame nae bega kwa bega katika kumuunga mkono katika harakati zake za kujinasua na ukandamizaji! Enzi hizo, Afrika tulikuwa tayari kwa jasho na damu kusimamia hilo!

Hivi sasa, Afrika nayo inaangalia nitapata na ama kupoteza nini! Na ndio maana, kwa mtazamo wangu linapokuja suala la Sahara Magharibi na Morocco, ni ujinga kusema hatutakiwi kuwa na ushirikiano na Morocco kwa sababu ya Sahara... ikiwa Waafrika wenzetu majirani wanashindwa kutambua mchango wetu itakuja kuwa hawa wa mbali... hakuna mambo ya tenda wema uende zako kwenye masuala ya nchi coz' Mungu hajaandaa thawabu kwa ajili hiyo! Rational decision making ni kuendelea kuunga mkono harakati za Sahara Magharibi kujitawala as a part of maintaining our national sovereignty but at the same time tukikuza ushirikiano na Morocco for the very same reason provided tunaona ushirikiano huo una maslahi kwetu... kama ambavyo tunavyoendelea kushirikiana na Israel huku tukiendelea kuunga mkono harakati za Palestine!
 
Back
Top Bottom