Nini msimamo wa Tanzania juu ya Sahara Magharibi?

Nini msimamo wa Tanzania juu ya Sahara Magharibi?

Sahara Magharibi ilikuwa koloni la Hispania baada ya mataifa ya Ulaya kugawana makoloni kwenye ule mkutano wa Berlin wa mwaka 1884. Hispania walipoondoka Morocco iliikalia Sahara Magharibi kimabavu huku ikida kuwa eneo hilo ni sehemu ya himaya yake kwa sababu ukoo wa kifalme wa Morocco ulitokea eneo hilo kabla ya ukoloni. Hatua hiyo ilisababisha wananchi wa Sahara Magharibi kuingia katika harakati za ukombozi kwa kuanzisha kikundi cha Polisario cha kudai uhuru kwa njia ya mapambano.

cc kwa waliokwishafuatilia hili zuala huko nyuma Sheba, FJM, harbab, Mbopo, Raia Fulani, petrol, POLITIBURO, fige, andishile, KIM KARDASH, Kiona, NasDaz, SURUMA, Tumaini Makene, Halisi, Filipo, Kimbunga, JokaKuu, Kichuguu, Mag3, omujubi, Njaare, TUJITEGEMEE, MgonjwaUkimwi, Sangarara, mtotowamjini, MTAZAMO, Nguruvi3, mlagha, TUNTEMEKE, Phillemon Mikael, Kiranga, Tume ya Katiba, Pasco, Precise Pangolin, Njoka Ereguu, Abdillahjr, BAK, Jasusi, Ben saanane, OTIS, ocampo four, DSN, Ogah, Viol, Alinda, Ubongo Silaha, Tina, The Boss, Jagermaster, alles, bucho, Keil, Bongolander, Candid Scope, Sheba, Sniper, manucho, Mpui Lyazumbi, Synthesizer, Tiote, Mkandara, Iza, kalokolaVIII, Sikonge, mharakati, Ukwaju, Chakaza, Mzalendo, Ndahani , W. J. Malecela, JacksonMichael, Njoka Ereguu, TIMING, newazz, KIDUNDULIMA, Kiduku, Mtumishi Wetu, mpujufu, mkomatembo, Kizotaka
Mkuu, kwanza asante kulichambua hili jambo kwa udani wake, mimi maoni yangu yatakuwa tofauti na wengi, ila huu ndio ukweli halisi!. Wakoloni walipotutawala sio tuu walijigawia maeneo yetu, bali pia walichukua na akili zetu na kuzitawala, kiasi kwanza hata baada ya kuisha kwa ukoloni, bado akili zetu nyingi zinatawaliwa na kitu kinachoitwa 'the colonial mentality', na nchi nyingi zilizokuwa colonized, hata baada ya kupata uhuru, zinaendelea kutawaliwa na the former colonial bosses kupitia neo colonialisim, na hii ndio basis ya msimamo wa UN kwenye suala na Western Sahara na AU is simply nothing but a puppet of UN ambayo imeshikwa na wale wale colonial masters!.

Ukweli ambao ni ukweli halisi, Western Sshara was part of Morroco before 1884 na wazungu washenzi hawa kuna nchi wamezigawa hata kati kati ya koo, na kuwafanya baadhi ya wana ukoo wako nchi moja na wanaukoo wengine wako nchi nyingine!. Sisi wa Afrika baada ya kila nchi kujitawala, tungepaswa tukae chini na kuifutilia mbali the colonial legacy ya washenzi hao waliotugawa na kufanya re patitioning ili zile koo zilizokatwa na colonia partitioning, zirejeshwe!. Eritrea irejeshwe Ethiopia na kufanyike consolidation ya himaya yote ya Abysinia. Baganda Kingdom irejeshewe maeneo yake ambayo Tanzania tungekubali kuwapoteza Wahaya na Wahangaza chini ya Bahima Kingdom, huku Warundi wangerudi kwetu!. Kule Arusha Wakenya wakubali kuwapoteza Wamasai na kulichukua eneo lote la Maasai Mara kulirudisha Tanzania, huku tukiwaachia Wajaluo wajirudie kwao!. Kule kusini tungepaswa kuwaachia Wamakonde waende kwao Msumbiji, na Wanyasa kuwa ni sehemu ya Malawi na hata Ziwa Nyasa kiukweli kabisa sio la kwetu!.

Wazungu hawa hawa waliotutawala kwa kupitia huko huko UN wanafanya double standard ya hali ya juu sana kupitia ujinga unaotwa Referendum, eti kisiwa cha Mayotte ni sehemu ya Ufaransa!. Leo unawapa masikini wa kutupwa option ya kupiga kura ya maoni kuchagua upande kati ya shida na heri!. Mfano umezaliwa kwenye familia masikini ya kutupwa, hohe hahe!, kisha Bill Gate aje na referendum upewe uhuru wa kuchagua unataka kulelewa familia gani kati ya familia yako ya asili, au assimileted family ya Bill Gates?!, nakuhakikishia kuna watu wata opt kuziacha familia zao za asili na kujiunga na Bill Gates huku wakijipongeza "to hell with umasikini"!. Hiki ndicho kinachofanyika kwenye hizo referendum za UN!. Leo ukiitisha referendum kwa Zanzibar kuhusu muungano, amini usiamini, wengi watasema no!, na ukiwa Zanzibar option ya kuchagua kama wanataka kuendelea kuwa part of URT na kujiunga na Ottoman Empire!, amini usiamini wata opt kujiunga na Oman!.

Mimi naunga mkono msimamo wa Morocco kuipa Sahara Magharibi mamlaka ya ndani kama ilivyokuwa kwa Palestina hapo mwanzo, lakini eneo hilo likabaki kuwa ni sehemu ya Morroco kama ilivyofanya kwa Taiwan, Hong Kong na Macau!. Kwenye vita vya Falkland mimi nilisimama na Argentina!.

Tena Waafrika ni watu wa ajabu sana!, Ghadafi alikuja na roadmap ya kuunda United States of Afrika na kushauri tuikate mizizi yote ya ukoloni kwa kuanzisha WB ya Afrika, IMF ya Afrika, mashirika ya mawasiliano na kila kitu kama ulaya kwa kupigia hesabu jumla ya rasilimali zetu zote za Afrika zikiwa consolidated, sisi ni matajiri mara 10 ya wazungu, why kila siku tubishe hodi kwenda kuwapigia magoti washenzi hawa?!. Wazungu walitishika na msimamo huu, kilichofuatia sote tunakijua!.

AU is just a barking dog! seldom bite!, ni toothless kabisa!.

Pasco
 
Uwezekano Wa serikali ya awamu ya NNE kuwa imebadirisha msimamo ni mkubwa sana hasa ukizingatia haiendeshi mambo yake kiharakati.

Rais amekuwa akisema Mara zote kwamba safari anazofanya nje ya nchi ni za kututafutia hela, sass labda morocco nao wameishaeleweka.
 
NasDaz,

..hii nadharia yako ni ngumu kweli kumeza kwa watu kama mimi ambao tumebwia chumvi nyingi.

..hivi miaka ile ya harakati za ukombozi tungesema tunapinga utawala wa makaburu, lakini hilo halituzuii kushirikiana nao kiuchumi, leo tungekuwa tunazungumzia Afrika Kusini huru?

..ni vizuri kama taifa tukawa na mambo fulani-fulani ambayo tunayasimamia wakati wote. hili la kupinga UKOLONI nilitegemea liwe kati ya mambo hayo.
 
Last edited by a moderator:
Nadhani Morocco inapata support ya nchi za magharibi, angalia suala la Mali lilivyoshughulikiwa, inakuwaje kuna kusuasua kwa suala la sahara magharibi tena likiwa mbele ya UN?

Au kama ilivyokuwa East Timor.
 
..kwanza mkumbuke kwamba Morocco siyo mwanachama wa AU.

..sina uhakika kama in 1984 walijitoa wenyewe, au walifukuzwa. lakini chanzo cha kutokuwa mwanachama wa AU ni huu mgogoro wa Sahara Magharibi.

Mwaka 1984 ndio ambao SADR walipata uanachama kamili wa OAU... kutokana na hilo, Mororocco wakasusa na kujitoa... kwahiyo walijitoa wenyewe kama njia ya kupinga SADR kupewa hadhi ya uanachama kamili wa OAU/AU.

Yes, walijiondoa wenyewe baada ya OAU kuikubali Sahara Magharibi kama mwanachama. Rafiki mkubwa wa Morocco alikuwa ni Zaire na Mobutu alipinga vikali Sahara Magharibi kuwa mwanachama wa OAU kiasi cha kuugomea umoja huo kati ya mwaka 1984 na 1986.

Hata hivyo, Morocco wana "special status" kwenye AU na wanafaidika na kazi za AU kama ilivyo kwa wanachama. Mfano, inafaidika na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

940px-Current_relations_of_SADR.svg.png


Current relations of the Sahrawi Arab Democratic Republic (SADR):
RED: SADR, as claimed
GREEN: Diplomatic relations and recognition of SADR
LIGHT GREEN: Recognition of SADR only
 
EMT,

..ina maana hii serikali ya sasa ina fikra kama za Mobutu Sese Seko?

..I hope I am not over reacting here.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu kuna mambo najaribu kujikumbusha kabla sijachangia hapa. Hii issue ya Sahrawi ina unafiki mkubwa sana wa kidiplomasia. Polisario ni chama cha zamani sana cha ukombozi. Miaka hiyo nikisikia SWAPO, POLISARIO, nk.

Wakati ukiendelea kijikumbusha nakumbuka mwaka 1987 Morocco iliomba kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya lakini ikakataliwa kwa sababu haikuwa nchi ya Ulaya. Pitia W. Europe Bloc Bars Morocco as a Member

Kitu kingine ni ule ukuta wa Morocco aka the Moroccan "Wall of Shame" ulijengwa kwa ushauri wa nani?
 
Sababu zipi zinakataza Zanzibar kuwa huru na sababu zipi zinakataza Zanzibar kujitenga kama Sahara magharibi? mabingwa wa double standard approach karibuni huku tuendelee kujadili mada hii muhimu!!! BTW nilidhani misimamo ya Tanzania nje ya Tanzania yalikoma baada ya Utawala wa awamu ya pili!!! Sasa hivi si kila kitu tunaamrishwa na WB, IMF na nchi wahisani? Tunashuhudia Bunge likiridhia mikataba ya kishenzi yenye kuendeleza unyonyaji wa blacks ... as a nation we are almost done! ... CCM Must go!!
 
Mimi naunga mkono msimamo wa Morocco kuipa Sahara Magharibi mamlaka ya ndani kama ilivyokuwa kwa Palestina hapo mwanzo, lakini eneo hilo likabaki kuwa ni sehemu ya Morroco kama ilivyofanya kwa Taiwan, Hong Kong na Macau!.

Kwa vile Western Sahara nao wana msimamo kwa nini Morocco wasikubali kura ya maoni ili mgogoro huu wa muda mrefu utatuliwe once and for all?

Kuna haja gani ya kulazimisha watu kuishi na wewe wakati wao hawataki. Wao hawataka internal self-determination. Wanataka external self-determination.

Ghadafi alikuja na roadmap ya kuunda United States of Afrika na kushauri tuikate mizizi yote ya ukoloni kwa kuanzisha WB ya Afrika, IMF ya Afrika, mashirika ya mawasiliano na kila kitu kama ulaya kwa kupigia hesabu jumla ya rasilimali zetu zote za Afrika zikiwa consolidated,

Gadaffi was doing that for his personal interests.
 
EMT,

..ina maana hii serikali ya sasa ina fikra kama za Mobutu Sese Seko?

..I hope I am not over reacting here.

Serikali imesema msimano bado ni ule ule, ila ziara za wanasiasa huko Morocco labda hazitolewi ufafanuzi wa kutosha.

Hata MwanaDiwani anayeripoti ziara za Kinana hapa JF, hajaripoti ziara ya Kinana huko Morocco let alone hata kuweka picha.
 
Last edited by a moderator:
NasDaz,


..hii nadharia yako ni ngumu kweli kumeza kwa watu kama mimi ambao tumebwia chumvi nyingi.


..hivi miaka ile ya harakati za ukombozi tungesema tunapinga utawala wa makaburu, lakini hilo halituzuii kushirikiana nao kiuchumi, leo tungekuwa tunazungumzia Afrika Kusini huru?


..ni vizuri kama taifa tukawa na mambo fulani-fulani ambayo tunayasimamia wakati wote. hili la kupinga UKOLONI nilitegemea liwe kati ya mambo hayo.
JokaKuu,

Mi nadhani si mgeni sana kwako na mara zote I hope unafahamu nini naweka kipaumbele kwenye mijadala kama hii... faida za kiuchumi kwanza, mengine yatafuata!

Aidha, tusisahau kwamba, kila zama na kitabu chake... hizo zama unazotaja wewe ni zama za harakati za ukombozi na hatuna budi kukubali kwamba zama hizo zimepita ingawaje haimaanishi ukombozi umeshapatikana kila pembe ya dunia na/au hatuna tena wajibu wa kusimama bega kwa bega na mataifa yanayokandamizwa, HAPANA! Hizi ni zama za ukombozi wa kiuchumi... si tena zama za kuwa tayari kupoteza mambo ya msingi kwa ajili ya "ndugu yetu" anayeishi mtaa wa saba tusiyemjua mama wala baba ake! Ikiwa kuna uwezekano wa sisi kuendelea kumsaidia huku tukiendelea kupata mkate wetu wa kila siku, haidhuru hata kama ni kupitia kwa adui wa ndugu yetu! Hapa narudia tena na tena; Mungu hajatenga thawabu maalumu kwa ajili ya nchi kwamba Tanzania tukiendelea kujitoa mhanga kwa ajili ya ndugu zetu ndo basi tena pepo mwanana inatusubiri huko tuendako, HAKUNA!

Labda niseme jambo moja. Itikadi yangu ni ya kijamaa ingawaje nikitulia ni kama huwa najiuliza hivi mimi ni mjamaa wa aina gani... lakini ni MJAMAA! Hata China nayo ni taifa la kijamaa! US akitaka kumtwanga mtu, China atapiga kura ya veto kumzuia US asifanye uharamia wake lakini wakitoka kwenye vikao vya UN, China hao hao wanafanya order ya Boeing 20 kutoka kwa US kwenda Uchina... hizo ndizo zama za leo! And don't forget, hakuna jipya hapa kwa siasa za Tanzania na Afrika (in fact world politics as a whole) kwa ujumla. Wakati ule wa zama za harakati za ukombozi, nchi nyingi za Afrika zilivunja uhusiano na Israel. Ilipofika mid-1990's nchi nyingi ambazo zilivunja uhusiano huo hatimae zikaurejesha including Tanzania ambayo ilirejesha uhusiano huo 1995 wakati wa utawala wa Mwinyi! And thanx God, ambae alirudisha uhusiano na Israel alikuwa Mwinyi ambae ni Mwislamu manake angefanya Mkapa, na kwa upuuzi wa nchi hii basi tungesikia mengi ya kipuuzi kama sio ya kipumbavu! Na kama ambavyo nilisema hapo awali, hivi sasa Israel wana mpango wa kufungua full-fledged embassy in Dar es salaam! Na kama isingekuwa tayari wana ubalozi wao pale Nairobi, huenda tayari zoezi hilo lingekuwa limeshakamilika!

Ukweli na uhalisia ndio huo, ambao hata kama ni mchungu kwako, basi jitahidi tu kuumeza hivyo hivyo hata kama ni kwa kuushushia na Fanta baridi! Na kama wakati unaumeza ukweki huo utakushinda na kulazimika kuutema, basi usiuteme kwa chuki na hasira manake sooner or later utalazimika tu kuumeza kwa mara nyingine na kukubali matokeo! Na si ajabu hayo yakajwa kutekelezwa na yule ambae wala hukumtarajia... najua utasema huyu nae ameshaanza kuhongwa!!! Na kutokana na hilo, ndio maana sioni na wala sitakuja kujisikia soni kusema kwamba bado tunapaswa kuwaunga mkono wana-Sahara Magharibi katika harakati zao za kupigania uhuru kamili lakini hili lisitufanye tuache kabisa kushirikiana na Morocco hata kama tunaona kuna maslahi makubwa ya kiuchumi. Tunaweza kuwa tayari kuacha maslahi ya kiuchumi au yoyote yale katika ushirikiano na Morocco IF AND ONLY IF Morocco watatulazimisha kwamba endapo tunataka ushirikiano maslahi na wao basi ni lazima tuvunje uhusiano na Sahara Magharibi... HILO HALIWEZEKANI WALA KUKUBALIKA... Tanzania is a free state ambayo wakati wote inatakiwa ku-practice her power of sovereignty and maintain her dignity at all cost!
 
Gadaffi was doing that for his personal interests.
Vitu vingine ni kuelimishana, vinginevyo wazungu wametufanya vibaya sana kwenye eneo la indoctrination!.

Wamemvamia Saadam kusaka rasilimali mafuta zake, malipo ya war reparations na tenda za reconstruction lakini wakauambia ulimwengu tunasaka WMD, tukawakubalia, no WMD, na hakuna aliyeuliza kwa nini Bush hajafikishwa The Hague kujibu mashitaka ya kivita?!. Bush killed 100 times more Iraqis in just one year, than the total number Saadam aliyowaua at his entire life!, no one cares!.

Wameivamia Libya kwa sababu zile zile na kuua maltitude!, katika kumpasue Osoma, Americans wameua 100 times more innocent lives kuliko walioperish kwenye September 11, and yet the world rallies behind Americans!.

All this is indoctrination!. Niliwahi kupandisha uzi humu kuhusu "The American Puppets!", ukinielimisha kuhusu Gadafi doing all that for his own interest, labda nitakuelewa!.

Pasco
 
EMT Mbona hii inafaamika toka enzi ya Mwalimu JK, kuanzia pia kama swala la BIAFRA, japo alikwenda ilivyopaswa lakini msimamo wetu ulibaki vilevile na swala la SAHARA MAGHARIBI, msimamo kama TAIFA ni ule wa dhama zilizo asisiwa na Mwalimu JK, ambao Rais Jakaya na Waziri Wa Mambo ya Nje Bernald Membe wameusimamia.Lakini hii maneno ya Kamati haa si ndio maneno yetu ....heshima na niadhamu ya kimamlaka inapoguswa na walioguswa na mguswaji wana nasaba zao binafsi wengine kutafuta mitaji Kimataifa na hakuna NIDHAMU YA MISIMAMO YA KITAIFA ...basi vululu...

Ndio maana Baraza la Maaskofu linasema msimamo wetu ni huu, anakuja Askofu ndani ya Baraza nae anasema hapana sio hivyo....

Ndio kusema matamshi ya watu wawili yamesimamia wigo mmoja, lakini mtu mmoja ndani ya mfumo huo huo mmoja anaibuka na kusema vinginevyo nje ya msimamo ya wenye DHAMANA NA TAIFA basi wenye dhamana na TAIFA ndio wanaopaswa kulaumiwa kwa kuacha Tafsiri zitoke tofauti na matarajio kama tathimini ya TAIFA.

Hapo zamani tulikuwa HATUYUMBI na kwa kutokuyumba huko TULIHESHIMIKA DUNIANI SANA SANA. Maswala kama Palestine na Israel, Nigeria na swala la Biafra, South Africa na Ubaguzi n.k.Tuliposima na kusema msimamo wa Taifa letu hapa ni hivi basi MATAIFA makubwa na madogo waliheshimu matakwa yetu kwa kuwa ndani ya maamuzi hayo hatukuwa na INTEREST yoyote bali tulisukumwa na UKWELI kwa faida ya wote wahusika wa swala husika, sisi kama Taifa na Wanaadamu wowote wale Duniani.

Tulipokea watu toka Mataifa mengine yoyote pale kusihi Tanzania wakati watu hao hao wasingeweza kuruhusiwa kuingia badhi ya MATAIFA...kumbuka issue za PAN, ANC, SWAPO, FRELIMO nk. Yote hiyo ilikuwa ni swala la misimamo.Leo hii watu wanajua ukiwa Raia wa Tanzania Botswana, Msumbiji, Angora, Zimbabwe na South Africa ruksa kuishi na kufanya biashara na kazi Nchi husika ili mradi Watanzania hao wafuate sheria za Taifa husika na sheria za Nchi yake Tanzania.Heshima hiyo wanayopata Watanzania kwenye Mataifa mbalimbali Duniani inatokanao na zao la kusimamia misimamo sahahi ya Taifa husika iliyoleta HAKI na USTAWI wa mataifa husika na hatima yake ni tuzo ya heshima kwa Raia wa Tanzania.

Msimamo wa TANZANIA swala la Sahara Magharibi ni ule ule toka enzi ya marehemu Baba wa TAIFA..

Taarifa nyingine zinazosikika nje na zile halisi, lawama ziende kwa waliopewa dhamana kusimamia Taifa ...manake Mwalimu Nyerere alisema Wananchi wakimpa dhamana Mtanzania mwenzao AWAHAKIKISHIE USALAMA WAO NA TAARIFA ziwafikie kwenye majumba yao wajue kwa hakika kuwa kuna Mtu anawasimamia Mambo yao kwa uhakika anayatenda hayo kwa uhakika na wako salama.
 
Kwamwelekeo huu wa hawaviongozi wapo watakao tuchanganisha na nchi nyingine kwa kauli tata
 
Msimamo wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi ni ule uliotolewa na Bernard Membe, na kukomelewa na Rais Kikwete. Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania kwa mambo mengi haijabadilika, ukiacha ongezeko la safari za viongozi ughaibuni ambalo kwa Awamu hii ya Nne limefanywa 'sera'. Sahara Magharibi wana haki ya kujitawala wenyewe.
 
ukinielimisha kuhusu Gadafi doing all that for his own interest, labda nitakuelewa!.

Gaddafi established himself as an enemy of the unification of the peoples of Africa for over 40 years. He exceeded his conservative instincts when he stated before a group of young students that Nigeria should be split in two.

Instead of motivating the students to work for the transformation and unification of the peoples of Nigeria as one prerequisite for the unification of Africa, Gaddafi called for the country to be divided on religious grounds.

He exposed his ignorance of African religious and spiritual traditions because there was no room for followers of African religious beliefs in his call for the division of this society.

This call for the division of Nigeria is one more effort to break up Nigerian society so that this society is weakened and its people subjected to more exploitation and manipulation.

For 40 years Gaddafi had supported the butchers and dictators in Africa. Starting with his military support for Idi Amin of Uganda and other murderers such as Foday Sankoh and Charles Taylor, this militarist in Libya was an obstacle to African liberation.

For a short while after Nelson Mandela rescued him from obscurity, Gaddafi had sought to use his wealth to buy the leadership of the African Union (AU). He was made to understand that the unity of Africa was more profound than the meeting of leaders of states.

You cannot put Gadaffi on the same foot as Marcus Garvey, W.E.B. DuBois, Kwame Nkrumah, Amílcar Cabral, Cheikh Anta Diop, Frantz Fanon, Patrice Lumumba, Samora Machel, or even Nyerere who were strong advocates of African unity.

Source: Gaddafi Was an Obstacle to African Unity | Think Africa Press
 
Gaddafi established himself as an enemy of the unification of the peoples of Africa for over 40 years. He exceeded his conservative instincts when he stated before a group of young students that Nigeria should be split in two.

Instead of motivating the students to work for the transformation and unification of the peoples of Nigeria as one prerequisite for the unification of Africa, Gaddafi called for the country to be divided on religious grounds.

He exposed his ignorance of African religious and spiritual traditions because there was no room for followers of African religious beliefs in his call for the division of this society.

This call for the division of Nigeria is one more effort to break up Nigerian society so that this society is weakened and its people subjected to more exploitation and manipulation.

For 40 years Gaddafi had supported the butchers and dictators in Africa. Starting with his military support for Idi Amin of Uganda and other murderers such as Foday Sankoh and Charles Taylor, this militarist in Libya was an obstacle to African liberation.

For a short while after Nelson Mandela rescued him from obscurity, Gaddafi had sought to use his wealth to buy the leadership of the African Union (AU). He was made to understand that the unity of Africa was more profound than the meeting of leaders of states.

You cannot put Gadaffi on the same foot as Marcus Garvey, W.E.B. DuBois, Kwame Nkrumah, Amílcar Cabral, Cheikh Anta Diop, Frantz Fanon, Patrice Lumumba, Samora Machel, or even Nyerere who were strong advocates of African unity.

Source: Gaddafi Was an Obstacle to African Unity | Think Africa Press

Mkuu
EMT, naona tuna different perspective kumhusu Gaddafi wewe ukimwangalia Gaddafi yule aliyemsaidia Nduli Amini kuivamia Tanzania, mimi nikimuangalia Gadaffi huyu aliyetaka kulikomboa bara la Afrika toka ukoloni mambo leo na ubeberu wa Ulaya na Amerika!.

Mimi namzungumzia Gadafi huyu aliyetupatia zile Benzi 100 S-Class za Ikulu yetu!. Yule Gaddafi aliyepandisha African Communication Satelite, ili Ukitaka kupiga simu Kenya, Uganda lazima kwanza iende London ndipo ije Nairobi!, Ukitaka kupiga simu Rwanda or DRC, Lazima kwanza iende London, itoke London iende Paris, ndipo ije Rwanda au DRC!. Ukitaka kupiga simu Burundi, lazima kwanza iende London, kisha Brusells ndipo ifike Burundi!. Ukitaka kupiga simu Msumbiji na Angola, lazima kwanza iende London, kisha Lisbon ndipo ishuke Angola!. Kote huko simu zinapopita ni mirija tuu ya kutunyonya Waafrika!. Gaddafi kataka kuikata, wakamkata!.

Namzungumzia Gaddafi aliyeamua tuanzie African Monetary Fund, tuachane na IMF!, Namzungumzia Gadaffi aliyetaka tuanzishe African Bank tuachane na WB!. Namzungumzia Gaddafi aliyetaka tuanzisha United States of Africa, tuwe a strong nation, African Super Power, wenye Veto kwenye Security Council!. Maadui wa kitisho hiki, wakaamua kumuwahi huku sisi Waafrika wenyewe tukishangilia!.

Ama kweli African continent ni dark continent na sisi watu wake tumelogwa, kama sisi Watanzania tulivyologwa kuichagua CCM!, mwaka hadi mwaka na mwaka huu tunaichagua tena!.

Kwa vile hapa tunawazungumzia Gaddafi wawili tofauti, then tuko parallel hatuwezi kukutana, the best way ni kukubaliana kutokukubaliana!.

Pasco
 
Tatizo kubwa liloipata nchi yetu ni wimbi kubwa la wasemaji. Toka katika vyama hadi Kitaifa yaani hakuna sura ya TAIFA kama ilivyokuwa wakati wa Mwalimu. Ukitazama nchi za wenzetu iwe US au UK dunia inamsikiliza mkuu wa nchi ama waziri wake wa mambo nje kwisha, hakuna mwanasiasa sijui wa chama tawala kenda kushawishi au kutoa suluhu za nchi. Chama na Utaifa wapi na wapi..Ukiona mtu kenda basi katumia influence yake yeye kama kina Carter wanavyofanya pale serikali imeshindwa.

Hili swala la Sahara kusema kweli mimi ndio kwanza nalisikia kwa undani na sijui historia yake wala sijaisoma. Kwa hiyo sina mchango zaidi juu ya nchi hiyo isipokuwa tu naweza zungumzia msimamo wetu umebadilika vipi.. Ni ile kutokana na kwamba NCHI yetu leo haina mfumo bora wa Uongozi. Kuna wakati utadhani Lowassa au Kinana wana nguvu kuliko rais au Jussa anagopwa, au zungu fulani ni untouchable!..
 
..sitasema mengi lakini nahisi pesa za kampeni za CCM mwaka huu zitatoka Morocco.

..kuna madai kwamba uchaguzi wa 2005 na 2010 pesa za kampeni zilitoka Uarabuni[Qatar & Oman].

..tena kumuona Kinana huko Morocco ndiyo kunaniacha na maswali mengi zaidi. nasema hivyo kwasababu CCM inajitambulisha kama chama cha ukombozi barani Afrika. Sasa Katibu Mkuu wa CCM anapofanya ziara Morocco ambao wanaitawala kimabavu Sahara Magharibi kunatoa taswira inayokanganya kidogo, na baadhi yetu tunaweza kuhoji kama CCM bado inaamini ktk ukombozi wa bara zima la Afrika.

..nadhani kuna lack of coordination ktk utekelezaji wa siasa zetu za mambo ya nje, au kama siyo hivyo basi tumeingiliwa na special/personal interests.

..kwa mfano, haiyumkiniki kamati ya BUNGE iwe inazungumza lugha tofauti na SERIKALI ktk suala hili la Sahara Magharibi.

..pia kwa kuzingatia kauli ya Raisi[mwenyekiti wa CCM] ktk kikao cha UN, ziara ya Katibu Mkuu Kinana inakwenda kinyume na msimamo wa Tanzania ambao unaeleweka kwa miongo kadhaa, na umekuwa validated majuzi ktk hotuba ya Raisi[mwenyekiti wa CCM] UN.

cc NasDaz, Kasheshe
JokaKuu unajivunjia heshima achia watu wa mipasho hayo mambo !!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom