BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Ben aliacha kiinua mgongo cha Mbunge kikiwa 35M. JK awamu ya kwanza akakitoa 35M to 90M na awamu ya pili akapandisha kutoka 90M hadi 240M. Bila shaka hapo ndipo ubunge ulipoacha kuwa utumishi ukageuka fursa ya kiuchumi.
Yohana hajaongeza hata mia. Ameacha kama alivyokuta. Lakini kumekuwa na mjadala kuwa maslahi ya wabunge yapunguzwe kikiwemo kiinua mgongo ili kufanya ubunge kuwa utumishi. Hapo ni nje ya mshahara wa 12M kwa mwezi, mkopo wa gari 90M, bima ya afya inayoweza kumpatia matibabu hadi ya 250M yeye na familia yake, pasi ya kusafiria ya kidiplomasia, mafuta ya gari lita 1,000 kila mwezi etc.
Nini maoni yako? Maslahi ya wabunge yapunguzwe, yaongezwe au yaachwe yalivyo?
Malisa GJ