Nini maoni yako kuhusu kusitishwa kwa mchakato wa Katiba Mpya?

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
250
Mchakato wa Katiba mpya ulisimamiwa vyema na iliyokuwa Tume ya Marekebisho ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba, ambao waliandaa rasimu ya Katiba iliyokabidhiwa Desemba 30, mwaka 2013.

Jaji Warioba na wenzeke walijikuta katika wakati mgumu, kwa kuvamiwa na kushambuliwa na watu ambao inadaiwa hawaikubali Rasimu hiyo bali wanaunga mkono Katiba pendekezwa ambayo ilitengenezwa na Bunge la Katiba.

Kutokana na kutoelewana ndani ya Bunge hilo, Aprili 16, mwaka 2014 wajumbe wa Bunge hilo wa upinzania zaidi ya 200 waliunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) walisusia vikao kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo ikiwamo kutozingatia maoni ya wananchi yaliyopo kwenye Rasimu ya Warioba.

Wajumbe waliobaki ndani ya Bunge hilo waliendelea hadi ikapatikana Katiba pendekezwa Oktoba 2014 na kubaki hatua ya kupigiwa kura ya maoni ambayo hufanywa na wananchi kwa mujibu wa sheria. Katiba inayopendekezwa chini ya uenyekiti wa Samuel Sitta, ilikabidhiwa kwa Rais wa Muungano na Zanzibar kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, na kubaki kupelekwa kwa wananchi kupiga kura ambayo ilipagwa Aprili 30, mwaka 2015, lakini haikufanyika.

Hadi sasa Katiba hiyo ni kiporo ambacho haijulikani lini kitapashwa moto.

Je wewe kama mwananchi una maoni gani kuhusu kusimamishwa kwa mchakato huu?

Je unadhani maoni ya wananchi yalichukuliwa ipasavyo?

Unadhani ni sahihi kwa mchakato huo kufufuliwa hivi sasa na je ifanywe kwa njia gani.

MAONI YAKO MUHIMU.

KARIBU.

SzWConstitutionFlyer-EN-page-001.jpg
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,648
2,000
Mkuu hapo unatafuta kupata vidonda vya tumbo tu. Hebu jaribu kuongea na Kabudi au Polepole kwani wao ndio walikusanya maoni ya wananchi uone kama wanauthubutu wa kuyatetea maoni waliyokusanya wenyewe toka kwa wananchi. Kwa wananchi makondoo wanaoimbishwa wimbo wa amani wanapewa chochote toka kwa watawala bila kukataa.
 
makinikia 101

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
491
1,000
Kama iliyopo tu na inakanyagwa, hata ikija katiba ya marekani hakuna kitu hapa. Tuna tatizo kubwa la viongozi na marekebisho ya katiba iliyopo
 
SAI-ELECTRICIAN

Senior Member
Jun 29, 2016
170
225
Katiba ni jambo muhimu sana kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu,naamini kwa hekma za mh Rais swala hili atahakikisha linakamilika kabla hajamaliza muda wake wauongozi
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,550
2,000
Jaji Warioba na wenzeke walijikuta katika wakati mgumu, kwa kuvamiwa na kushambuliwa na watu ambao inadaiwa hawaikubali Rasimu hiyo bali wanaunga mkono Katiba pendekezwa ambayo ilitengenezwa na Bunge la Katiba.

Kumbe unajua kuwa maoni ya wananchi ambayo yalichukuliwa na Jaji Warioba hayakusikilizwa bali ni kundi jingine lililoundwa na anayejua mambo yake lililoleta katiba pendekezwa sio. Basi, Mungu ameyakataaaa mawazo hayo ya wajumbe wenye nia zao kinyume na wananchi.
Hakukuwa na katiba mpya baada ya kuyafutilia mbali mawazo ya wananchi. Kama vipi, ule muda na resources zote zilizotumiwa na kina Warioba ni ufujaji wa pesa za kodi. Wangeunda bunge hilo la katiba likakae litengeneze hiyo katiba bila kupoteza nguvu za kina Warioba.
Namuunga mkono rais wetu. Kiporo chenu sio kipaumbele kwetu kwa sababu ni kitu kipya sio kile tulichokuwa tunakitaka.
 
Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,777
2,000
Je wewe kama mwananchi una maoni gani kuhusu kusimamishwa kwa mchakato huu?
Kitendo cha kusimamisha mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya kwangu naona ni sawa kabisa, kwa sababu si vizuri kuendelea na stage ya kura ya maoni huku hakuna maridhiano baina ya wadau muhimu (wanasiasa)

Je unadhani maoni ya wananchi yalichukuliwa ipasavyo?
Ndio maoni ya wananchi yalichukuliwa ipasavyo

Unadhani ni sahihi kwa mchakato huo kufufuliwa hivi sasa na je ifanywe kwa njia gani.
Binafsi napenda sana kuona Katiba Mpya ikipatikana chini ya uongozi wa Raisi Magufuli
Lakini iwe baada ya 2020, na si sasa hivi
Kwa sasa ngoja Serikari isifashe nchi
Na hio 2020 ikifika tuanze upya, na tutumie utaratibu wa Kenya wa kutumia watalaamu wachache
Tuachane na utaratibu wa bunge la katiba, ambao ndio ulioleta shida

maonomakuu

JF-Expert Member
Jul 24, 2015
2,522
2,000
Katiba ni matakwa ya viongozi ambao wakichaguliwa wanakuwa watawala wa waliowachagua.Hakuna katiba mpya ya matakwa ya wananchi bali katiba ya wanachokitaka wanaotutawala.Wakiamua hata kesho mnapata katiba mpya ya watawala. Hakuna Hatua tutakayoruka kwenye maendeleo....
 
Adolph Sendeu

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
269
250
Katiba ni jambo muhimu sana kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu,naamini kwa hekma za mh Rais swala hili atahakikisha linakamilika kabla hajamaliza muda wake wauongozi

Naomba clip moja ya raisi wa sasa kwa wakati huu akizungumziz katiba ndipo tuanzie hapo, ukishindwa niambie nikupe nondo zako!!!
 
Isa khamisi

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
431
500
Mchakato wa Katiba mpya ulisimamiwa vyema na iliyokuwa Tume ya Marekebisho ya Katiba chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba, ambao waliandaa rasimu ya Katiba iliyokabidhiwa Desemba 30, mwaka 2013.

Jaji Warioba na wenzeke walijikuta katika wakati mgumu, kwa kuvamiwa na kushambuliwa na watu ambao inadaiwa hawaikubali Rasimu hiyo bali wanaunga mkono Katiba pendekezwa ambayo ilitengenezwa na Bunge la Katiba.

Kutokana na kutoelewana ndani ya Bunge hilo, Aprili 16, mwaka 2014 wajumbe wa Bunge hilo wa upinzania zaidi ya 200 waliunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) walisusia vikao kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo ikiwamo kutozingatia maoni ya wananchi yaliyopo kwenye Rasimu ya Warioba.

Wajumbe waliobaki ndani ya Bunge hilo waliendelea hadi ikapatikana Katiba pendekezwa Oktoba 2014 na kubaki hatua ya kupigiwa kura ya maoni ambayo hufanywa na wananchi kwa mujibu wa sheria. Katiba inayopendekezwa chini ya uenyekiti wa Samuel Sitta, ilikabidhiwa kwa Rais wa Muungano na Zanzibar kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011, na kubaki kupelekwa kwa wananchi kupiga kura ambayo ilipagwa Aprili 30, mwaka 2015, lakini haikufanyika.

Hadi sasa Katiba hiyo ni kiporo ambacho haijulikani lini kitapashwa moto.

Je wewe kama mwananchi una maoni gani kuhusu kusimamishwa kwa mchakato huu?

Je unadhani maoni ya wananchi yalichukuliwa ipasavyo?

Unadhani ni sahihi kwa mchakato huo kufufuliwa hivi sasa na je ifanywe kwa njia gani.

MAONI YAKO MUHIMU.

KARIBU.

View attachment 611722
Tatizo aliyekamata rungu hana haja ya katiba mpya na tatizo tulilonalo katika nchi yetu rais ndo kila kitu yaani yeye ni katiba na yeye ndo sheria
 
KiuyaJibu

JF-Expert Member
Aug 29, 2007
830
250
Yaani ni kichefuchefu; wananchi maoni yao yamepuuzwa hali baadhi ya watu wachache wamewaka yao nakutoa yale ya wananchi halafu wanatuletea iliyochakachuliwa. Kwa maana hiyo hakuna haja ya kuwa na katiba ambayo iko kwa maslahi ya wachache ( fake).
Warudishe ile original halafu ndiyo tuipigie kura ya maoni. Hiyo fake wakaitumie kwenye chama chao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom