Mkuu Wacha tu hayo matangazo yaendelee kuwepo
Sio watu wote wenye kumiliki simu,si ajabu wakati wa tukio la kifo kuna wahusika ambao msiba huo unawahusu na wakati huo huenda Simu zao ni mbovu,zimeibiwa,zimepotea,hazina chaji,hazina vocha na mengineyo,
Lakini tangazo la kifo linaweza kukuta hata ndani ya daladala au chombo chochote cha usafiri na ukapata taarifa,au mtu wako wa karibu anaweza kusikia tangazo hilo na kukujulisha,
Ikumbukwe pia mtu huwezi kuwa na namba za simu za watu wote ambao ungependa kuwajulisha habari ya msiba,na kumjulisha mmoja mmoja kwa simu nafikiri gharama ni kubwa zaidi uki compare na gharama ya kutangaza redioni,
Hayo ni maoni yangu tu.