Nini Mantiki ya Matangazo ya Vifo Redioni?

Ndugu Nyanshani Ngabire wa Nshamba muleba, anasikitika kutangaza kifo cha mjomba wake Samaki Kiruru kilichotokea ziwani kwa ajali ya mtumbwi. Habari ziwafikie;
-Ndg Mapuli Kandambili wa Marekani
-Ndg Lusato Malyatabu wa Afrika ya Kusini
-Bi Hawa Mwampambuli wa Naijeria

Hilo tangazo hao watu kweli watalisikia au wanaolengwa kusikia ni watu gani? Zamani wakati mawasiliano ya simu yalikuwa mtihani ilikuwa inaingia akilini, lakini ulimwengu wa sasa mimi sioni umuhimu wa Tangazo la kifo redioni, labda kama kuna sababu nyingine.

Hata watu waliotajwa kwenye tangazo wana habari ya msiba uliotokea lengo maana yake nyingine n kuwafahamisha watu wengine kuwa watajwa hapo wamepatwa na msiba. Ni jinsi ya kuwataarifu watu kuwa, marehemu alikuwa baba wa fulani a Afrika kusini,mjomba wa fulani Kibohehe na wengieneo wengi,na wala sio ujiko.
 
Waulize Wachaga na Wahaya ndiyo wanaoongoza kwenye matangazo ya vifo radioni

Utasikia habari ziwafikie
1. PROF. RUNYORO ANAYEISHI NEW YORK
2. ENGINEER KWESIGABO ALIYEKO AMSTERDAM
3.BWANA RWEYMAMU ALIYEPO SAFARINI CHINA
yaani ni sheedaah
 
Kwani we unakufa lini tukutangaze?
Mheshimiwa Mnyaa unaanza kuchanganyikiwa.
Subiri ufe tukutangaze

hahhaa, mimi nikifa sitangazwi mkuu, ndugu zangu wa muhimu wote watajua kwa muda, kwetu tuna baiskeli ziko fast vibaya mno!
 
Utasikia habari ziwafikie
1. PROF. RUNYORO ANAYEISHI NEW YORK
2. ENGINEER KWESIGABO ALIYEKO AMSTERDAM
3.BWANA RWEYMAMU ALIYEPO SAFARINI CHINA
yaani ni sheedaah

hahaha, halafu wote hao ndiyo watoaji wa pesa za matibabu hivyo wanajua siku hiyohiyo kuwa wamefiwa, sasa kwenye redio tena kutafuta nini?
 
Kuna umuhimu sana... Pindi upatavyo matatizo. Huta weza kuwapa taarifa watu wote.. Wanatafutwa ndg zake ambayo wanafahamika kwenye jamii eg walio ulaya na nk. For sure mtt wa mtani kwenu akienda ulaya lazima mtaa mzima wajue.. Hivyo wakitumia njia hiyo kwa wale watakao sikia tangazo na hawajapata information kwa njia nyingine.. Watajumuika pia.. Chukulia mfano mzuri tu wa harusi.. Watu huwa wanasahau watu wa karibu.. Unakutwa na pete na wanashangaaa umeoa lini!!! Sasa upate matatito.. Simu inakuwa nzito hata kupokea kuachilia mbali kutuma msg

🙏🙏🙏🙏
 
Hata watu waliotajwa kwenye tangazo wana habari ya msiba uliotokea lengo maana yake nyingine n kuwafahamisha watu wengine kuwa watajwa hapo wamepatwa na msiba. Ni jinsi ya kuwataarifu watu kuwa, marehemu alikuwa baba wa fulani a Afrika kusini,mjomba wa fulani Kibohehe na wengieneo wengi,na wala sio ujiko.

sasa mkuu hauoni kwamba wewe ukipata habari ya msiba haraka unawajulisha jamaa zako wa karibu, au unasubiri wataskia tangazo redioni?!
 
Kuna umuhimu sana... Pindi upatavyo matatizo. Huta weza kuwapa taarifa watu wote.. Wanatafutwa ndg zake ambayo wanafahamika kwenye jamii eg walio ulaya na nk. For sure mtt wa mtani kwenu akienda ulaya lazima mtaa mzima wajue.. Hivyo wakitumia njia hiyo kwa wale watakao sikia tangazo na hawajapata information kwa njia nyingine.. Watajumuika pia.. Chukulia mfano mzuri tu wa harusi.. Watu huwa wanasahau watu wa karibu.. Unakutwa na pete na wanashangaaa umeoa lini!!! Sasa upate matatito.. Simu inakuwa nzito hata kupokea kuachilia mbali kutuma msg



sasa kwa nini harusi hazina matangazo redioni?!!
 
sasa mkuu hauoni kwamba wewe ukipata habari ya msiba haraka unawajulisha jamaa zako wa karibu, au unasubiri wataskia tangazo redioni?!

Nafikiri watu wanafanya kama mazoea tu lakini kwa hali halisi watu wanapata habari mapema kabla ya tangazo redioni.
 
hahaha, halafu wote hao ndiyo watoaji wa pesa za matibabu hivyo wanajua siku hiyohiyo kuwa wamefiwa, sasa kwenye redio tena kutafuta nini?

haa haa haaa wakitumia simu tu sie wengine hatutajua
 
Ndugu Nyanshani Ngabire wa Nshamba muleba, anasikitika kutangaza kifo cha mjomba wake Samaki Kiruru kilichotokea ziwani kwa ajali ya mtumbwi. Habari ziwafikie;
-Ndg Mapuli Kandambili wa Marekani
-Ndg Lusato Malyatabu wa Afrika ya Kusini
-Bi Hawa Mwampambuli wa Naijeria

Hilo tangazo hao watu kweli watalisikia au wanaolengwa kusikia ni watu gani? Zamani wakati mawasiliano ya simu yalikuwa mtihani ilikuwa inaingia akilini, lakini ulimwengu wa sasa mimi sioni umuhimu wa Tangazo la kifo redioni, labda kama kuna sababu nyingine.

Aliyekufa siyo mbuzi. Ikitangazwa kuwa mtu kafa vile vile siyo kosa. Ukitaka kuangalia kila kitu kina faida gani basi hata kununu jeneza zuri ni kosa.

Lakini yote kwa yote, waache watu wafanye vitu wanavyoona ni muhimu kwao. Kama ungechunguzwa na wewe madude ya kipumbavu unayofanya mbona tungeandika vitabu
 
mi nataka kujua umuhimu tu, zamani lengo ilikuwa kufikisha taarifa, sasa nataka kujua sasa hivi lengo ni nini, maana kama ni taarifa walengwa wanazipata mapema zaidi kwa simu. btw, mbona umekuja juu sana mkuu wakati ni mjadala tu?!
 
Oh samahani kwa ukali.

Watu wanatangaza vifo wakiwa katika hali ya uchungu na kuchanganyikiwa. Kwa watu wasio na mila ya kutangaza, huwa wana fanya vitu vingine. Kwa watu wenye mila hiyo, kukimbia radio one kutangaza ni moja ya njia ya kudumisha mila kwa ajili ya marehemu pamoja na kujifariji mwenyewe.

Ni complex kidogo, ndiyo maana nikasema waache watu wafanye vitu wanayoona ni muhimu kwao
 
sasa mkuu hauoni kwamba wewe ukipata habari ya msiba haraka unawajulisha jamaa zako wa karibu, au unasubiri wataskia tangazo redioni?!

Hakuna ubaya kwa wale wengine nitakao sahau kuwajusha wakisikia kwenye matangazo ya radio.
 
Zamani ilikuwa logical lakini kwa sasa ni show off tu na mazoea.
 
Mkuu CYBERTEQ

Unahoji umuhimu wa matangazo ya vifo au mashauzi katika matangazo ya vifo?

There is a case to be made kwamba kutangaza majina ya ndugu walio nje ni mashauzi, hata kama vile vile kuna case ya kusema kwamba hiyo ni namna ya kutangaza nasaba, watu wakiwa na shaka waweze kuunganisha kwamba yule ni Pandu Vuai Faki mwenye ndugu zake Denmark waliojilipua miaka ile na kadi za CUF.

Matangazo ya vifo ni sehemu moja ya ceremony ya mazishi, hata kama kuna simu. Naelewa wewe mtu wa tech unaelewa "broadcast" ni nini na faida zake ni nini.

Uki uliza sana hizi habari unaweza kuuliza kwa nini watu wakusanyane kumzika mtu? Kwa nini kusiwe na funeral homes tu, watu wanne wakapeleka mwili hapo, wakaukabidhi, watu wenye kazi maalum ya kuzika wazike.

Kwani si mtu kashajifia zake tayari? Ya nini kukusanya watu kibao waache shughuli zao wende mazikoni, wakienda wengi ndo atafufuka au?

Kuna babu mmoja WW2 veteran, alikuwa jirani yangu Gotham hapo. Alifariki, tumeenda kumzika mimi.na mama mmoja Mjamaica, wote majirani tu. Mke wake na watoto (granted enstranged) waliishia funeral home. Babu tumemsitiri majirani wawili, ama sivyo angezikwa na watu wa funeral home tu. But should that matter? Si ameshafariki na anazikwa?

Kwa hiyo, ni ceremony, part of a tradition kumuenzi aliyekufa na kuwapasha habari waliobaki.
 
Last edited by a moderator:
Sioni nafasi yake kwa ulimwengu huu wa digitali. Yanasaidia tu kutunisha mifuko ya radio.
 
Back
Top Bottom