Mtumishi Mkuu
JF-Expert Member
- Mar 31, 2011
- 259
- 93
Ndugu wanajukwaaa, heshima kwenu! Kwa muda sasa nimekuwa ninajiuliza maana ya haya matangazo ya vifo kwenye radio haswa kwa nyakati hizi ambazo teknolojia ya mawasiliano imeboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Mtakubaliana name kwamba kwa sasa unapotokea msiba mahali, ndani ya nusu saa ndg wengi wa marehemu watakuwa wamepata taarifa hizo za msiba. Kilichonifanya niulize swali hili ni hapa majuzi kuna jirani yangu alifiwa na mama yake ambaye alikuwa anaishi nae hapa mjini.
Kesho yake msiba ule ukatangazwa na ndugu zake wakajulishwa kupitia tangazo redioni.
Nikashangazwa mdogo wake na huyu ndugu aliyetuma tangazo kuwajulisha ndugu zake nae akatangaza tena na kati ya waliotajwa kwenye tangazo ni yule ndg mkubwa ambaye msibwa umetokea nyumbani kwake, kwamba nae anapewa taarifa ya msiba!
Hii imekaaje wadau?

Ndugu Nyanshani Ngabire wa Nshamba muleba, anasikitika kutangaza kifo cha mjomba wake Samaki Kiruru kilichotokea ziwani kwa ajali ya mtumbwi. Habari ziwafikie;
-Ndg Mapuli Kandambili wa Marekani
-Ndg Lusato Malyatabu wa Afrika ya Kusini
-Bi Hawa Mwampambuli wa Naijeria
Hilo tangazo hao watu kweli watalisikia au wanaolengwa kusikia ni watu gani? Zamani wakati mawasiliano ya simu yalikuwa mtihani ilikuwa inaingia akilini, lakini ulimwengu wa sasa mimi sioni umuhimu wa Tangazo la kifo redioni, labda kama kuna sababu nyingine.