Nini mantiki ya Lowassa kuitisha mkutano na waandishi wa habari?

loiluda

Member
Jun 15, 2011
25
3
Mpaka muda huu sijafahamu haswa mantiki ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari, halafu asizungumze kuhusu Richmond, Dowans na mustakabali wa nchi yetu haswa katika kipindi hiki kigumu cha mgawo wa umeme.

Watanzania walitegemea azungumze kuhusu kulipwa kwa Dowans, kujivua gamba na msimamo wake khsu hisia kwamba anategemea kugombea urais 2015. Tetesi kuhusu uhusiano wake na yanayoendelea katika UVCCM Arusha.

Nifahamisheni mantiki ilikuwa ipi?
 
kila mtu anashangaa nini kimesababisha hali hii, haikubaliki kuwatoa waandishi makwao mpaka Monduli halafu uzungumzie ajira kwavijana na kusema mastomach yetu yameshashiba.
 
Mpaka muda sijafahamu haswa mantiki ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari,halafu asizungumze kuhusu Richmond,Dowans na mustakabali wa nchi yetu haswa katika kipindi hiki kigumu cha mgawo wa umeme,watanzania walitegemea azungumze kuhusu kulipwa kwa Dowans ,kujivua gamba na msimamo wake khsu hisia kwamba anategemea kugombea urais 2015,tetesi kuhusu uhusiano wake na yanayoendelea katika uvccm Arusha.Nifahamisheni mantiki ilikuwaipi?

Anza kusoma hii..........

"UJUMBE WA WAZI KWA MHE. EDWARD LOWASSA: "Uchaguzi ni wako"
Na. M. M. Mwanakijiji
Endapo aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa (CCM-Monduli) ataendelea na mwelekeo wake wa sasa wa kisiasa na mahusiano yake ya sasa ya kimkakati basi njozi zake za kuja kushiriki tena katika uongozi wa juu wa taifa letu zitakuwa zimefikia ukingoni bila kupiga kelele ya breki. Na endapo nitakachoandika hapa hatakipa uzito wake unaostahili naomba niwe wa kwanza kutanguliza habari mbaya kwake na wale wanaomuunga mkono kuwa atashindwa. He will lose.

Ninaandika kwa sababu kubwa tatu; kwanza ni kwa sababu ninaamini anapoteza muda kwa kuendelea na machungu ya matukio ya mwaka jana; pili, anapoteza kipaji chake cha uongozi kwa kukaa pembeni ya mijadala ya kitaifa na hivyo kuonekana yuko upande kinyume na maslahi ya taifa na tatu, ni kwa sababu naamini hakuna mtu mwingine anayeweza kumuambia kile nitakachomuambia hapa kwa heshima na taadhima kubwa. Wengine aidha wanamuonea soni, wanamuogopa au kwa namna fulani wanagwaya mbele yake.


Inaendelea katika attachment...

Nimeonelea nijitafsiri mwenyewe maana watu wengine wanatafsiri zaidi ya kile nilichosema.

a. Lowassa anawajibika kwa kujiuzulu kwake Uwaziri Mkuu. Hana wa kumlaumu.

b. Amechagua upande usio sahihi baada ya kuachia ngazi.

c. Hawezi kurudi kwenye uongozi wa kitaifa na hivyo ni bora aendelee kukaa upande huo mwingine. It is too costly."


Then njoo kwenye hii........


"Tafakuri yangu ya leo; Edward Lowassa sema neno moja tu

Na Nova Kambota

Ingawaje mimi sijawahi kusoma maswala unajimu wala utabiri naomba leo nitabiri mambo matatu kuhusu maisha ya waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Bw Edward Ngoyai Lowassa, kwanza nashawishika kuwa Lowassa ametoka familia ya kichifu au wazazi wake walikuwa matajiri, pili Lowassa ni msiri sana na tatu Lowassa anaishi kwa ahadi kuliko nyakati.

Kwa kawaida watoto wa kichifu au wa familia za kitajiri ni waoga tena wapo tayari hata kutoa fedha mradi wasikumbwe na dhoruba hata kwenye shule za bweni watoto wa kitajiri ni waoga kwelikweli, kwa jinsi Lowassa asivyopenda matatizo "ajali kazini" hapendi "kupambana jino kwa jino" yaelekea ni tatizo la kimalezi kuliko kisiasa, malezi ya Lowassa aliyolelewa katika familia yake ambayo ni ya kitajiri yamemfanya kuwa mwoga sasa amebaki kulalamika kuwa "anaonewa".

Chukulia sakata la Richmond ambalo lilimwondoa Lowassa kwenye kiti cha uwaziri mkuu, kamati ya bunge iliyoongozwa na Mwakyembe ilileta ushahidi mzito dhidi yake kwa kushindwa kusimamia mawaziri wake vizuri na Lowassa alipotoa ile hotuba yake ya …"nimetafakari sana , nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana kwa heshima ya chama changu…………………akaingizia na tuhuma kuwa kamati ya Mwakyembe imelidanganya bunge na akazidi kuongeza utata kwa madai kuwa tatizo ni uwaziri mkuu lakini yote haya yamebaki siri kubwa hayuko tayari kusema kinagaubaga na kutwambia kuwa tatizo lilikuwa uwaziri mkuu au kweli kamati ilidanganya bunge.

Halafu yaelekea Lowassa ni mtu anayeishi kwa ahadi kuliko kusoma alama za nyakati , tangu mwaka 1995 iliwahi kuelezwa kuwa Kikwete na Lowassa ni maswahiba wakubwa tena ikaelezwa kuwa iwapo mmoja wapo ataukwaa urais basi mwingine angeteuliwa kuwa waziri mkuu na hili halikupita kwani kufuatia ushindi wa "sunami" wa kikwete wa mwaka 2005 Lowassa akateuliwa kuwa waziri mkuu tena nakumbuka ile hotuba ya Kikwete siku ya uteuzi wake mara baada ya bunge kupitisha jina lake "mtaani watu wanasema ooh Lowassa ni rafiki yangu ni kweli rafiki yangu ila namfahamu Lowassa ni mtendaji mahiri asiyetetereka" haya yalikuwa ni maneno yake Kikwete sasa yaelekea kuwa si hivyo tu bali pia Lowassa aliahidiwa ndiye atakayekuwa mrithi wa Kikwete 2015 lakini licha ya yote yaliyomkuta naona bado kalala kwenye usingizi wa "fofofo" anategemea ahadi badala ya kuenenda kadri ya alama za nyakati zinavyomtaka.

Kama mwandishi mahiri wa habari za uchambuzi nchini maarufu kwa jina la Mwanakijiji alivyomshauri Lowassa kupitia makala yake iliyokuwa na kichwa cha "Edward Lowassa uchaguzi ni wako" , katika makala yake hiyo Mwanakijiji anamtaka Lowassa kurudi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa na mimi narudia tena kufanya siasa za chinichini kama anavyofanya Lowassa hivi sasa haimjengi chochote bali inabidi arudi rasmi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa tena atolee matamko mambo mazito bila woga, nashindwa kuelewa Lowassa anaogopa nini? kwa maana ushahidi wa nguvu na ushawishi wake unaonekana waziwazi mfano licha ya yeye kujiuzulu sambamba na Msabaha na Karamagi hawa wenzake wote "tupa kule" hawasikiki tena ila yeye bado anasikika kwenye vyombo vya habari (japo si kwa mema).

Bado hatujasahau vuta nikuvute kati ya Mwakyembe na Lowassa kiasi kwamba Mwakyembe aliwahi kuwapa changamoto kina Lowassa ili kupima iwapo wanakubalika kweli basi yeye na wao waende kuhutubia pale sokoni kariakoo kisha waone wananchi watafanyeje? Kama kweli Lowassa anajiamini tulitegemea ajitutumue hata kujibu au kufanya chochote kuonyesha kuwa anakubalika lakini wapi! Lowassa alikaa kimya hii maana yake nini? na inatafsiri gani? nini hitimisho la mvutano huu wa Mwakyembe na Lowassa?

Mvutano kati ya Samwel Sitta na Lowassa ulizua ya kuandikwa, kuna baadhi ya watu wakadai kuwa Lowassa aliposema kuwa …"tatizo ni uwaziri mkuu.." alikuwa akimaanisha mvutano wake na Sitta na hili likapewa uzito na kauli za Andrew Chenge "swahiba wa Lowassa" kuwa Sitta alitumia bunge kujeruhi wenzake kisiasa lakini licha ya yote haya Lowassa hakutia neno yeye kaka kimya, watu wanapotaka kufahamu uwaziri mkuu wake ulikuwa na uhusiano gani na Sitta? yeye "anajibu kisiasa badala ya kujibu ukweli" kuna nini hapa? Anamwogopa nani?

CHADEMA katika moja ya mapambano yao dhidi ya ufisadi waliwahi kumhusisha Kikwete na ufisadi tena baadhi ya magazeti yakadai kuwa iweje waziri mkuu Lowassa ahusike na Richmond kisha Kikwete ambaye kimsingi ndiye bosi wa waziri mkuu asihusike? Haya ni maswali ya msingi ambayo Lowassa hakupaswa kukaa kimya alitakiwa atwambie iwapo Kikwete alihusika au la? Na sio kutwambia tu bali aseme kwa nukta na mantiki kiasi tukipima maneno yake tuone yana ukweli na yamejengwa kwa mtiririko wa "logic".

Sasa kuna operation ya kujivua gamba ambayo ilielezwa kuwa mmoja wa walengwa alikuwa ni Edward Lowassa lakini sasa operation hii imekuwa butu kwa maana nyingine imeshindwa na watu wanamlaumu Kikwete kwa kushindwa kuisimamia, wengine wanahoji ingekuwaje kama angeisimamia? Lowassa angeathirika kwa kiwango gani? na je kwa kutoisimamia Lowassa kanufaika kwa kiwango gani? na je Kikwete anamwogopa Lowassa? Au Lowassa bado ni swahiba wa Kikwete? Haya ni maswali ya msingi na hakuna mtu mwingine wa kuyajibu zaidi ya Lowassa hapaswi kukaa kimya.

Lowassa anapaswa kuingia kwenye siasa za malumbano na minyukano bila kusita hata ikibidi kumjeruhi "swahiba" wake Kikwete potelea mbali ajali kazini hata ikibidi kulipua msuguano tena baina yake na Sitta na Mwakyembe sawa tu lakini ukweli pekee ndiyo utakaomweka huru Lowassa vinginevyo anajimaliza kisiasa kiasi kwamba hata kwenye historia ya taifa hili hatokumbukwa tena. Lowassa asiishie kusema pembeni kuwa yeye ni msafi anaonewa tu inabidi adhihirishe kauli yake kwa kuwataja wachafu pasipo kusita vinginevyo yeye ndiyo mchafu na anawasingizia wenzake kwa kusema wanamwonea.

Lowassa inabidi ajiamini kwani yeye si ndo alikuwa injinia mkuu wa mtandao uliomwingiza Kikwete 2005 kwa maana nyingine maadui Lowassa aliwapata wakati akimtetea Kikwete sasa anaogopa nini? kwa maana nyingine maadui wake pia ni maadui wa Kikwete hivyo asiogope sana! Kwa maana nani ana nguvu za kumshinda kiongozi wa nchi? Na kwa upande mwingine Kikwete na chama chake anachokiongoza CCM wanapaswa kuweka hadharani uchafu wa Lowassa kuliko kuendelea na minong'ono, mzee Chiligati, Nape Nauye na Mukama wamkane waziwazi Lowassa na Kikwete avunje urafiki na Lowassa iwapo kweli anaamini Lowassa ni "mchafu tena anamharibia kwa wananchi". Tunataka Mwakyembe, Sitta, Chenge na Rostam waseme ukweli kuliko kumung'unya maneno, tunataka ukweli "kindakindaki"

Tumechoshwa na siasa za mipasho na vijembe , hatutaki kusikia upuuzi wa "hao mafisadi" tunataka tuambiwe fulani na fulani ni mafisadi, hatutaki kusikia "mimi ni msafi" bali sina kosa kwasababu moja mbili tatu, hatutaki upuuzi wa "ni lazima CCM ijivue gamba" bali tunataka kusikia "fulani na fulani wamekiuka kanuni za chama sasa tunawatimua na kuwafilisi mali zao" , haya ndiyo matakwa ya watanzania.

Mtu pekee ambaye anaweza kutufikisha huko ni Lowassa , Lowassa ni lazima azungumze yeye ni "kichocheo" katika hili, aseme neno moja tu ! na alisimamie pasipo uwoga "UKWELI" huu ndiyo utamweka huru, atwambie bila kificho tena waziwazi basi mlolongo utafata kila mtu atasema ukweli, Kikwete, Chenge, Sitta, Rostam na Mwakyembe wote watasema ukweli mtupu na iwapo kweli Lowassa atajitokeza hadharani na kusema pasipo kumung'unya basi uamuzi wake huo usipokelewe kama amekuja kufukua kaburi bali atazamwe kama amekuja kuweka shada la maua juu ya kaburi…..A Luta Continua!

Nani bora anayeandika kwa taaluma yake au mimi nayeandika nachokiamini?
Nova Kambota Mwanaharakati,
Nipigie; 0717 709618 au +255717 709618
Niandikie kwenda;novakambota@gmail.com
kwa habari zaidi za uchambuzi nitembelee;www.novakambota.com
Tanzania, East Africa,
Jumamosi 11, Juni 2011."

Nadhani sasa baada ya kuzipitia makala hizo utakuwa umeshapata JIBU la swali lako!
 
anza kusoma hii..........

"ujumbe wa wazi kwa mhe. Edward lowassa: "uchaguzi ni wako"
na. M. M. Mwanakijiji
endapo aliyekuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa tanzania mhe. Edward lowassa (ccm-monduli) ataendelea na mwelekeo wake wa sasa wa kisiasa na mahusiano yake ya sasa ya kimkakati basi njozi zake za kuja kushiriki tena katika uongozi wa juu wa taifa letu zitakuwa zimefikia ukingoni bila kupiga kelele ya breki. Na endapo nitakachoandika hapa hatakipa uzito wake unaostahili naomba niwe wa kwanza kutanguliza habari mbaya kwake na wale wanaomuunga mkono kuwa atashindwa. He will lose.

ninaandika kwa sababu kubwa tatu; kwanza ni kwa sababu ninaamini anapoteza muda kwa kuendelea na machungu ya matukio ya mwaka jana; pili, anapoteza kipaji chake cha uongozi kwa kukaa pembeni ya mijadala ya kitaifa na hivyo kuonekana yuko upande kinyume na maslahi ya taifa na tatu, ni kwa sababu naamini hakuna mtu mwingine anayeweza kumuambia kile nitakachomuambia hapa kwa heshima na taadhima kubwa. Wengine aidha wanamuonea soni, wanamuogopa au kwa namna fulani wanagwaya mbele yake.


inaendelea katika attachment...

Nimeonelea nijitafsiri mwenyewe maana watu wengine wanatafsiri zaidi ya kile nilichosema.

A. Lowassa anawajibika kwa kujiuzulu kwake uwaziri mkuu. Hana wa kumlaumu.

B. Amechagua upande usio sahihi baada ya kuachia ngazi.

C. Hawezi kurudi kwenye uongozi wa kitaifa na hivyo ni bora aendelee kukaa upande huo mwingine. It is too costly."


then njoo kwenye hii........


"tafakuri yangu ya leo; edward lowassa sema neno moja tu

na nova kambota

ingawaje mimi sijawahi kusoma maswala unajimu wala utabiri naomba leo nitabiri mambo matatu kuhusu maisha ya waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya richmond bw edward ngoyai lowassa, kwanza nashawishika kuwa lowassa ametoka familia ya kichifu au wazazi wake walikuwa matajiri, pili lowassa ni msiri sana na tatu lowassa anaishi kwa ahadi kuliko nyakati.

kwa kawaida watoto wa kichifu au wa familia za kitajiri ni waoga tena wapo tayari hata kutoa fedha mradi wasikumbwe na dhoruba hata kwenye shule za bweni watoto wa kitajiri ni waoga kwelikweli, kwa jinsi lowassa asivyopenda matatizo "ajali kazini" hapendi "kupambana jino kwa jino" yaelekea ni tatizo la kimalezi kuliko kisiasa, malezi ya lowassa aliyolelewa katika familia yake ambayo ni ya kitajiri yamemfanya kuwa mwoga sasa amebaki kulalamika kuwa "anaonewa".

chukulia sakata la richmond ambalo lilimwondoa lowassa kwenye kiti cha uwaziri mkuu, kamati ya bunge iliyoongozwa na mwakyembe ilileta ushahidi mzito dhidi yake kwa kushindwa kusimamia mawaziri wake vizuri na lowassa alipotoa ile hotuba yake ya …"nimetafakari sana , nimedhalilishwa sana, nimeonewa sana kwa heshima ya chama changu…………………akaingizia na tuhuma kuwa kamati ya mwakyembe imelidanganya bunge na akazidi kuongeza utata kwa madai kuwa tatizo ni uwaziri mkuu lakini yote haya yamebaki siri kubwa hayuko tayari kusema kinagaubaga na kutwambia kuwa tatizo lilikuwa uwaziri mkuu au kweli kamati ilidanganya bunge.

halafu yaelekea lowassa ni mtu anayeishi kwa ahadi kuliko kusoma alama za nyakati , tangu mwaka 1995 iliwahi kuelezwa kuwa kikwete na lowassa ni maswahiba wakubwa tena ikaelezwa kuwa iwapo mmoja wapo ataukwaa urais basi mwingine angeteuliwa kuwa waziri mkuu na hili halikupita kwani kufuatia ushindi wa "sunami" wa kikwete wa mwaka 2005 lowassa akateuliwa kuwa waziri mkuu tena nakumbuka ile hotuba ya kikwete siku ya uteuzi wake mara baada ya bunge kupitisha jina lake "mtaani watu wanasema ooh lowassa ni rafiki yangu ni kweli rafiki yangu ila namfahamu lowassa ni mtendaji mahiri asiyetetereka" haya yalikuwa ni maneno yake kikwete sasa yaelekea kuwa si hivyo tu bali pia lowassa aliahidiwa ndiye atakayekuwa mrithi wa kikwete 2015 lakini licha ya yote yaliyomkuta naona bado kalala kwenye usingizi wa "fofofo" anategemea ahadi badala ya kuenenda kadri ya alama za nyakati zinavyomtaka.

kama mwandishi mahiri wa habari za uchambuzi nchini maarufu kwa jina la mwanakijiji alivyomshauri lowassa kupitia makala yake iliyokuwa na kichwa cha "edward lowassa uchaguzi ni wako" , katika makala yake hiyo mwanakijiji anamtaka lowassa kurudi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa na mimi narudia tena kufanya siasa za chinichini kama anavyofanya lowassa hivi sasa haimjengi chochote bali inabidi arudi rasmi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa tena atolee matamko mambo mazito bila woga, nashindwa kuelewa lowassa anaogopa nini? Kwa maana ushahidi wa nguvu na ushawishi wake unaonekana waziwazi mfano licha ya yeye kujiuzulu sambamba na msabaha na karamagi hawa wenzake wote "tupa kule" hawasikiki tena ila yeye bado anasikika kwenye vyombo vya habari (japo si kwa mema).

bado hatujasahau vuta nikuvute kati ya mwakyembe na lowassa kiasi kwamba mwakyembe aliwahi kuwapa changamoto kina lowassa ili kupima iwapo wanakubalika kweli basi yeye na wao waende kuhutubia pale sokoni kariakoo kisha waone wananchi watafanyeje? Kama kweli lowassa anajiamini tulitegemea ajitutumue hata kujibu au kufanya chochote kuonyesha kuwa anakubalika lakini wapi! Lowassa alikaa kimya hii maana yake nini? Na inatafsiri gani? Nini hitimisho la mvutano huu wa mwakyembe na lowassa?

mvutano kati ya samwel sitta na lowassa ulizua ya kuandikwa, kuna baadhi ya watu wakadai kuwa lowassa aliposema kuwa …"tatizo ni uwaziri mkuu.." alikuwa akimaanisha mvutano wake na sitta na hili likapewa uzito na kauli za andrew chenge "swahiba wa lowassa" kuwa sitta alitumia bunge kujeruhi wenzake kisiasa lakini licha ya yote haya lowassa hakutia neno yeye kaka kimya, watu wanapotaka kufahamu uwaziri mkuu wake ulikuwa na uhusiano gani na sitta? Yeye "anajibu kisiasa badala ya kujibu ukweli" kuna nini hapa? Anamwogopa nani?

chadema katika moja ya mapambano yao dhidi ya ufisadi waliwahi kumhusisha kikwete na ufisadi tena baadhi ya magazeti yakadai kuwa iweje waziri mkuu lowassa ahusike na richmond kisha kikwete ambaye kimsingi ndiye bosi wa waziri mkuu asihusike? Haya ni maswali ya msingi ambayo lowassa hakupaswa kukaa kimya alitakiwa atwambie iwapo kikwete alihusika au la? Na sio kutwambia tu bali aseme kwa nukta na mantiki kiasi tukipima maneno yake tuone yana ukweli na yamejengwa kwa mtiririko wa "logic".

sasa kuna operation ya kujivua gamba ambayo ilielezwa kuwa mmoja wa walengwa alikuwa ni edward lowassa lakini sasa operation hii imekuwa butu kwa maana nyingine imeshindwa na watu wanamlaumu kikwete kwa kushindwa kuisimamia, wengine wanahoji ingekuwaje kama angeisimamia? Lowassa angeathirika kwa kiwango gani? Na je kwa kutoisimamia lowassa kanufaika kwa kiwango gani? Na je kikwete anamwogopa lowassa? Au lowassa bado ni swahiba wa kikwete? Haya ni maswali ya msingi na hakuna mtu mwingine wa kuyajibu zaidi ya lowassa hapaswi kukaa kimya.

lowassa anapaswa kuingia kwenye siasa za malumbano na minyukano bila kusita hata ikibidi kumjeruhi "swahiba" wake kikwete potelea mbali ajali kazini hata ikibidi kulipua msuguano tena baina yake na sitta na mwakyembe sawa tu lakini ukweli pekee ndiyo utakaomweka huru lowassa vinginevyo anajimaliza kisiasa kiasi kwamba hata kwenye historia ya taifa hili hatokumbukwa tena. Lowassa asiishie kusema pembeni kuwa yeye ni msafi anaonewa tu inabidi adhihirishe kauli yake kwa kuwataja wachafu pasipo kusita vinginevyo yeye ndiyo mchafu na anawasingizia wenzake kwa kusema wanamwonea.

lowassa inabidi ajiamini kwani yeye si ndo alikuwa injinia mkuu wa mtandao uliomwingiza kikwete 2005 kwa maana nyingine maadui lowassa aliwapata wakati akimtetea kikwete sasa anaogopa nini? Kwa maana nyingine maadui wake pia ni maadui wa kikwete hivyo asiogope sana! Kwa maana nani ana nguvu za kumshinda kiongozi wa nchi? Na kwa upande mwingine kikwete na chama chake anachokiongoza ccm wanapaswa kuweka hadharani uchafu wa lowassa kuliko kuendelea na minong'ono, mzee chiligati, nape nauye na mukama wamkane waziwazi lowassa na kikwete avunje urafiki na lowassa iwapo kweli anaamini lowassa ni "mchafu tena anamharibia kwa wananchi". Tunataka mwakyembe, sitta, chenge na rostam waseme ukweli kuliko kumung'unya maneno, tunataka ukweli "kindakindaki"

tumechoshwa na siasa za mipasho na vijembe , hatutaki kusikia upuuzi wa "hao mafisadi" tunataka tuambiwe fulani na fulani ni mafisadi, hatutaki kusikia "mimi ni msafi" bali sina kosa kwasababu moja mbili tatu, hatutaki upuuzi wa "ni lazima ccm ijivue gamba" bali tunataka kusikia "fulani na fulani wamekiuka kanuni za chama sasa tunawatimua na kuwafilisi mali zao" , haya ndiyo matakwa ya watanzania.

mtu pekee ambaye anaweza kutufikisha huko ni lowassa , lowassa ni lazima azungumze yeye ni "kichocheo" katika hili, aseme neno moja tu ! Na alisimamie pasipo uwoga "ukweli" huu ndiyo utamweka huru, atwambie bila kificho tena waziwazi basi mlolongo utafata kila mtu atasema ukweli, kikwete, chenge, sitta, rostam na mwakyembe wote watasema ukweli mtupu na iwapo kweli lowassa atajitokeza hadharani na kusema pasipo kumung'unya basi uamuzi wake huo usipokelewe kama amekuja kufukua kaburi bali atazamwe kama amekuja kuweka shada la maua juu ya kaburi…..a luta continua!

nani bora anayeandika kwa taaluma yake au mimi nayeandika nachokiamini?
nova kambota mwanaharakati,
nipigie; 0717 709618 au +255717 709618
niandikie kwenda;novakambota@gmail.com
kwa habari zaidi za uchambuzi nitembelee;www.novakambota.com
tanzania, east africa,
jumamosi 11, juni 2011."

nadhani sasa baada ya kuzipitia makala hizo utakuwa umeshapata jibu la swali lako!


umepiga ndipo! Mwenye tatizo hapa la kuficha uchi ni lowassa! Longa lowassa longa kama wewe mwanasiasa mkweli! Sina shaka utalipua fataki za sitta na mwakyembe. Ukikaa kimya na porojo za "hatukukutana barabarani", tutajua unaogopa missiles za uhakika kutoka kwa wapambanaji!
 
Mpaka muda sijafahamu haswa mantiki ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari,halafu asizungumze kuhusu Richmond,Dowans na mustakabali wa nchi yetu haswa katika kipindi hiki kigumu cha mgawo wa umeme,watanzania walitegemea azungumze kuhusu kulipwa kwa Dowans ,kujivua gamba na msimamo wake khsu hisia kwamba anategemea kugombea urais 2015,tetesi kuhusu uhusiano wake na yanayoendelea katika uvccm Arusha.Nifahamisheni mantiki ilikuwaipi?

Mpelekee sms muulize moja kwa moja akueleze mantiki kaka ndiyo uje na hoja .Kwa sasa hutapata jibu maana hapa ni JF na hakuna Lowasa wala msaidizi wake .Na mantiki inatoka akilini mwake au moyoni sasa hapa pagumu mno kuijua Mantiki yake kama hajasema tukaiona .
 
anawakimbusha kina nape wasipige kelele sana silaha zake bado hajatumia na si wakati muafaka sasa kizitumia
 
Back
Top Bottom