1. Libeneke: Kwa ufahamu wangu neno ili ni Kiswahili cha mtaani (Lugha ya msimu), na maana yake ni Kung'ang'ania jambo bila sababu ya maana.
2. Msaada katika Tuta/Tutani: Huu msemo umepatikana kipindi kile matuta ya barabarani ndio kwanza yamewekwa, abiria wengi wa mabasi ya daladala, walikuwa wakiomba msaada wa kushuka kwenye hayo matuta au jirani ya hayo matuta kwani mara zote mabasi yakifika karibia na hayo yalikuwa yakipunuza mwendo...!