Nini maana ya neno "Mtambuka"

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
18,020
Reaction score
24,971
Naomba msaada wa kiswahili: nifahamishemi kwa lugha nyepesi sana maana ya neno "Mtambuka"

Nimeskiliza jamaa huyun hapa chini, bado sikuweza kumwelewa sawasawa. Kuna rafiki yangu mzuri sana hapa anaitwa Magonjwa Mtambuka ; nadhani atanisaidia

 
1. Katika Jiometri (Hisabati)Huu ndio muktadha unaotumika zaidi.Mstari Mtambuka:

Ni mstari unaokata mistari mingine miwili au zaidi katika pointi tofauti.

Pembe Mtambuka: Ni pembe zinazoundwa pale mstari mmoja unapokata mistari mingine inayofanana.

2. Katika Lugha na Mawasiliano (Cross-cutting / Cross-disciplinary)
Huashiria jambo linalohusisha au kugusa nyanja, idara, au masomo tofauti kwa wakati mmoja.

Mada Mtambuka:
Ni mada ambazo hazifungwi kwenye somo moja tu, bali zinapaswa kufundishwa au kujadiliwa kila mahali.
Mfano: Masuala ya Jinsia, UKIMWI, na Mazingira ni mada mtambuka katika mitalaa ya shule.

3. Katika Jamii na Maisha (Intersectional / Horizontal)Inamaanisha kitu kinachoenda upande wa pembeni (horizontal) badala ya kwenda juu na chini (vertical).Hutumika kuelezea mahusiano au mifumo inayounganisha watu wa ngazi moja kutoka makundi tofauti.
 
maelezo yako yamezidi kunichanganya zaidi kuliko yule jamaa kwenye video ya Umoja wa mataifa
 
Cross cutting.

Kitu ambacho kinatokea sehemu nyingi mbalimbali kwa sababu ni cha msingi, hakiepukiki, kinatapakaa kila sehemu.
Umeeleweka kidogo; je nikitupa jiwe ndani ya dimbwi yale mawimbi yanayotokea ni "mawimbi mtambuka" kwani hayaeupikiki na yanatapakaa sehemu zote?
 
Tafsiri Sisisi.....

Neno mtambuka ni maana ya mambo mbalimbali/ au kadha wa kadha
 
"Mtambuka" ni mbalimbali sawa na iliyopo.
 
Cc Magonjwa Mtambuka
 
Neno Mtambuka nalo ni Neno Mtambuka.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…