Nini maana ya Kusimika?

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Ninapokutana na sentensi kama hili "Katika sherehe za kumsimika ofisini", huipita mbiombio kiaina nikidhani ni tusi. Wewe unalionaje?
 
Kusimika ina maana nyingi. Neno moja maana nyingi.

Mbali na viungo vya uzazi,kike/kiume kusimama

Kusimika inatumika sana katika msamiati wa kanisa katika kuwateua na kuwakabidhi vyeo/ majukumu ya kiuongozi watumishi wa kanisha.

Maana nyenginezo ni: Dictionary - Definition of kusimika. .. sow (kusimika), set up (kusimika), plant (kusimika), appoint (kusimika).

Wigo na matumizi ya maneno katika lugha yananyambulika/yanakua na wakati. Kiswahili cha leo,sio cha jana, mkuu.

Kusimika pia ni jina la mtu. link http://www.facebook.com/lumbani.kusimika

au Kusimika Chatterjee
 
Asante sana Mkuu Nonda kwa maelezo na ufafanuzi. Ni kweli Kiswahili kinakua na wengine kinatuacha njiani.
 
Last edited by a moderator:
kwa upande wa wakwetu pba kusimika ni kusimama kwa uume (kudisa)
 
.
Mkuu MAMMAMIA ... kwa mujibu wa Kamusi ya TUKI


Neno Simika lina maana mbili:


1. simika = erect, set up. maneno mengine simikia; simikika; simikwa.

2. simika = install in office, appoint. maneno mengine simikia; simikana; simikika; simikwa.

.
 
Kundinda pia sio matusi, BBC na radio za Kenya huwa wanatamka live, mfano,,Madocta waidindia serikali.

Tanzania kwasababu akili zetu zipo masaburini, huwa haiwezekani kutamkwa kwenye vyombo vya habari kihivyo.
 
Kusimika ilitokana na ile kisu ya kimasai (Simi) ambapo unapuichoma ardhini (kusimisha) unakuwa umeweka mamlaka juu ya kitu fulani

Afbeelding429.jpg
 
Back
Top Bottom