Kitila, Muhongo, Ulimwengu, Polepole nao ni watu weusi, kwa hiyo kwa theory yako hiyo wana matatizo ya akili ! Na wewe ingawa sikufahamu, naamini ni mtanzania na ni mtu mweusi vile vile.......kwa theory unayoiamini, wewe utakuwa na matatizo ya akili.....
Change ni neno la kiingereza (mabadiliko kwa kiswahili) lilikuwepo kabla ya Obama na Nyerere hawajazaliwa !. Linaweza likatumika kwenye maeneo mengine ambayo sio ya kisiasa au linaweza likatumika kwa namna tofauti katika siasa. Obama
aliamu a kulitumia kwa namna hiyo na Nyerere naye kama ulivyoeleza. Wao hawalimiliki hili neno, na hivyo haina maana kwamba yeyote anayetaka kulitumia basi lazima alitumie au amaanishe kile alichokisema Obama au Nyerere.....
Kwa members wengi tu wa UKAWA (sio wote), wanapolitumia hili neno wana maana kuiondoa CCM madarakani, hivyo kwa sasa hivi na kwa uchaguzi huu, Change kwao ni kubadili chama kilichopo madarakani (CCM) na kuwaweka UKAWA (CHADEMA kwa JMT na CUF kwa upande wa Zanzibar). Kama unaona wamekosea kutumia neno hilo, hebu wewe sema watumie neno gani ambalo linafit zaidi.....
Kitu ambacho, mimi binafsi ningependa kwa Tz, ni sisi wananchi waTz tuwe na uwezo ambao uko wazi kabisa wa kuiwajibisha serikali yetu au viongozi wetu. Itakapofika mahali ambapo, kila mtu anajua kabisa kwamba kura yake ina-count then hapo mimi nitaridhika..... Hili bado ni tatizo hapa kwetu (kura ina-count kwa sehemu tu, ila uchakachuaji una nafasi pia) na hata kwa nchi nyingine za kiafrika !. Tukiwa na uwezo huo, then viongozi watakuwa na discipline na watawajibika kwa wananchi kwani watakuwa wanajua kwamba mamlaka yao yanatokana na wananchi na wakiboa wananchi watawaweka kando....
Nilifarijika tulipoanza mchakato wa katiba, nikitegemea at least tungeweka msingi wa kuelekea kuwapa wananchi mamlaka yao, lakini CCM wakavuruga mchakato na kuamua kwamba mawazo yao ndio mawazo ya watanzania...
Mimi nataka UKAWA wachukue nchi kwa sababu ninaamini wataweza kutupatia vitu vifuatavyo vya msingi katika nchi yetu....
1. Katiba mpya yenye maoni ya wananchi
2. Kuimarishwa kwa mifumo ambayo itasaidia kukuza demokrasia hapa nchini
- Tume huru ya uchaguzi
- Mahakama
- Bunge
etc
With CCM, ni mambo yale yale, hakutakuwa na chochote kipya.......Hawatufai, inabidi wakae kando !