Nini maana ya dhana Tunataka Mabadiliko?

Nini maana ya dhana Tunataka Mabadiliko?

Hivi kumbe huko Lumumba bado wanawalipa hiyo 7500? By the way sijui Dr Watson umemsoma lini. Kuna watu wanaitwa Uncle Tom and that is what you are. Wakikaa na wazungu siku mbili wanajiona kama na wao rangi inabadilika.
Nimeshaeleza juu huko kuwa kama nataka hela saivi ningekuwa nampigia debe Lowassa humu na kila mtu analijua hili kuwa mwaka huu wa uchaguzi fedha zinamwagwa kwa Lowassa.

Najisikia vibaya kukwambia ndugu kuwa napata ushawishi kuamini kuwa nawe upo kwenye sample ya wale watu aliowazungumzia Dr. Watson.
 
Kukuza uchumi kwa kwa kufanya mapinduzi ya viwanda kwamikakati ipi na funds za wapi ili tuone tofauti kati yake na mipango ya CCM ili tuyatarajie kweli hayo mabadiriko????
Kama kusema kukuza uchumi kwa mapinduzi ya viwanda hata wewe unaweza sema hapo.

kwanza kabisa ccm haina mipango na viwanda kwa hiyo cjui utatofautisha vip? kazi ya ccm ni kumaliza kabisa vile vilivyoachwa na ccm.

cha ajabu hata train ya mkolon mmeshindwa kuiboresha zaid zaid ni kufanya ufisad wa mabehewa...

alafu kwa taarifa yako usijidanganye kwa hizo propaganda zenu sijui mmetumwa na nani mseme lowassa anatoa pesa.... lowasa hatoi pesa wala chadema hawatoi pesa na hawawezi kutoa pesa na hawana pesa za kuwatosheleza wanachadema wote kwasababu tupo wengi... sijawah kupokea hata sent tano kutoka chadema wala kwa lowasa...

sasa turudi kwenye hoja za msingi... kama ccm ambayo imeshindwa kutengeneza serikali ambayo imeshindwa kutatua mambo ya msingi kama vile:-
1. usafirishaji kwa njia ya treni... njia ambayo ingesaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo a kupunguza mfumuko wa bei hususan mikoan na vijijin.

2. viwanda. hapa sisem sana coz kila mtu anajua na anaona ccm wamekuwa wa hovyo katika eneo hili.

3. rushwa.

4. elimu ya hovyo. ajabu sana eti sasa hivi tuna div 5 na hii imekaa kisiasa zaid na sio vinginevyo.

5. na mengine mengi.

hapa mtawezaje kutushawishi kuwa mnastahili kurudi madarakani? mnataka kura za wabunge, ili wakaendelee kulala bungen au wakaitikie ndiyo hata kwenye mambo wasiyoyaelewa?
 
Nimeshaeleza juu huko kuwa kama nataka hela saivi ningekuwa nampigia debe Lowassa humu na kila mtu analijua hili kuwa mwaka huu wa uchaguzi fedha zinamwagwa kwa Lowassa.

Najisikia vibaya kukwambia ndugu kuwa napata ushawishi kuamini kuwa nawe upo kwenye sample ya wale watu aliowazungumzia Dr. Watson.

kwa taarifa yako hku utaishia kupakatwa tu na senti hupat... endelea kulipwa pesa za escrow mlizozibeba kwenye masandarusi.
 
Amani iwe nanyi wadau,
Kwa kipindi sasa kuna jambo limekuwa likiniwazisha sana hasa Kwa wapenzi wa Chadema, ukawa na baadhi ya washabiki wao pale wanapolitumia kwenye kujenga ushawishi neno Tunataka mabadiliko. Hili ni neno ambalo wamekuwa wakilisema kwa kipindi sasa wakiwa wanatarget kuwa wanapolisema tu basi maana yake kuu ni kuiondoa CCM madarakani.

Napenda kutoa historia fupi ya umaarufu wa hili neno ambayo najua wengi wenu humu mnaifahamu. Neno hili kwa lugha nyingine CHANGE lilipata umaarufu hasa pale raisi wa sasa wa Marekani Barack Obama alipolichagua kama kaulimbiu yake kwenye mchakato wake wa kisiasa katika kuutafuta uraisi wa Marekani mnamo mwaka 2008. Neno hili alilichagua na kulitumia akiwa hamaanishi kuwa wamarekani wanataka change ya kubadiri chama kwa sababu alianza kulitumia tangu kwenye mchakato wa ndani wa chama chake yaani Democrats akiwa anamaanisha wamarekani wanaitaji mabadiriko ya kisera za kiuchumi, kijamii, kiulinzi na usalama na hata za kimaisha. Huu ndo msingi wa neno CHANGE/MABADILIKO KWENYE SIASA. Hata mwalimu Nyerere aliposema watanzania wanataka mabadiriko wasipoyapata CCM watayapata nje ya CCM ukiangalia ile hotuba kuna vitu aliviongelea na vilikuwa vinne kikiwemo Rushwa na vingine vitatu, na ndo baadae akasema kuwa watanzania wanaitaji mabadiriko kwenye ivo vitu wa wasipovipata CCM watavitafuta nje ya CCM. Hii inamaanisha mabadiliko kwenye siasa sio kubadirisha vyama.

Nimeamua kutoa haya maelezo mafupi nikiwa naionea huruma jamii hii ya watanzania huku nikiwa nawaza mawazo ya Yule Dr wa kizungu anayejulikana kama Dr. Watson aliyesemaga kuwa ana wasiwasi na akili ya mtu mweusi.
Ninasema haya kwa sababu kwa jinsi wafuasi, wapenzi na wanachama wa Chadema wanapolitumia hili neno wao wanachowaza kikubwa ni kuwa maana ya mabadiriko ni kukiondoa chama kinachotawala madarakani wakati kiuhalisia hali haiko ivo. Inaniuma zaidi eti wanaposema hawa wamekaa miaka 50 na sasa tuweke wengine as if uongozi ni kujaribu hasa wan chi. Kweli Africa we have a long way to go.

Dhana ya mabadiliko/ change inapotumika kisiasa inamaanisha ni mabadiriko KWENYE SERA HASA ZA KIUCHUMI, KIJAMII NA KISIASA, INAMAANISHA MABADIRIKO KWENYE MTINDO WA KUENDESHA MAMBO HASA YA KIUTAWALA ILI JAMII IONE KITU TOFAUTI HASA KWENYE MAISHA YAO YA KILA SIKU NA SIO KUHUSU KUBADIRI CHAMA TU.

Kuna watu watatu nimewasikiliza wiki hii, wa kwanza ni Ndugu Humphrey Polepole na wa pili na Dr Kitila Mkumbo na wa tatu ni Jenerali Ulimwengu ambaye nimemsoma kwenye gazeti la leo la Raia Mwema. Humphrey amezungumzia kwa mapana sana tangu wiki iliyopita na hadi wiki hii na kusema kweli nimefarijika sana kuona jamii ya Tanzania ina mtu mwingine mwenye upeo wa tofauti na ulio mbali kama wake(wa kwanza kwangu ni Prof Muhongo) huyu mtu bila kumung’unya maneno ameweza kuelezea kwenye vipindi alivoalikwa kinagaubaga kuwa Tanzania inaitaji mtu wa aina Fulani na mwenye uwezo Fulani. Kwa Dr Kitila alisema wazi kuwa vyama vya upinzani vinaonekana kuwa dhumuni lao kuu ni kushika madaraka tu yaani kukamata dola ndo mana wanasema tutumie silaha yeyote ile( kwa hapa nikapata picha kuwa kumbe hawa viongozi lengo kuu sio kuja na sera mbadala zinazoonyesha ni kwa jinsi gani watamkomboa mtanzania na nchi yetu mama Tanzania). Kwa Jenerali Ulimwengu amegusia kwa jinsi gani ushabiki usio na maono na upenzi wenye kupapalikia mambo unaoliangamiza taifa letu na siku ya mwisho hatupati kitu tunachotakiwa kupata.

Hawa wachambuzi watatu wameugusa sana moyo wangu na kwa uzoefu wangu nimegundua kuwa nchi hii inaharibiwa na wanasiasa kwa sababu fikra zao ndo zinaiharibu wafuasi wao ambao ni sehemu ya jamii ya watanzania. U chambuzi wa hawa watu umenifanya nitafakari sana maneno ya Dr Watson kuwa mtu mweusi ana matatizo Fulani kwenye akili yake. Kwa sababu kiuhalisia Chadema/Ukawa hawajajipambanua kisera, Lowassa hajajipambanua kisera hasa kujibu how question yaani atafanya nini na kivipi na hata fedha atapata wapi zaidi ya kusema tu Fulani kakuta sukari bei Fulani, kakuta kitu Fulani bei Fulani na sasa ivi kaacha kikiwa bei Fulani alafu wapenzi wake wanashangilia tu raisi raisi raisi bila kupembenua vizuri ni nini kasema ni kwa nini iwe yeye kwa sera zake/utekelezaji wake tofauti na mwingine.

Kitu kinachoniumiza zaidi ni pale ninapojiuliza kama tatizo kuu la nchi hii ni ufisadi, utumiaji mbaya wa madaraka, uvivu, porojo, kuabudu wenye mali, wizi, porojoporojo na unafiki hivi mtu ambaye kwa miaka yake tuliyomfahamu na kumuona kuwa ana mambo mengi sana ambayo ni matatizo kwa Tanzania yet u ndo huyu apewe nchi yetu aiongoze?????? Kama jibu ndio basi kweli Dr Watson atakuwa yuko sahihi asilimia 100 kuwa ana matatizo na akili ya mtu mweusi.

Nawatakia siku mpya njema wadau.
Mungu awabariki.
Lord Denning...as noble as ur name suggests, nimekuwa nikiuliza hili swali kwa ndugu zetu bila kupata majibu staha sanasana watakutukana. Sisi Watanzania tunatia huruma na hasa tunaporuhusu ulofa utawale akili zetu. Tumerogwa walahi
 
kwanza kabisa ccm haina mipango na viwanda kwa hiyo cjui utatofautisha vip? kazi ya ccm ni kumaliza kabisa vile vilivyoachwa na ccm.

cha ajabu hata train ya mkolon mmeshindwa kuiboresha zaid zaid ni kufanya ufisad wa mabehewa...

alafu kwa taarifa yako usijidanganye kwa hizo propaganda zenu sijui mmetumwa na nani mseme lowassa anatoa pesa.... lowasa hatoi pesa wala chadema hawatoi pesa na hawawezi kutoa pesa na hawana pesa za kuwatosheleza wanachadema wote kwasababu tupo wengi... sijawah kupokea hata sent tano kutoka chadema wala kwa lowasa...

sasa turudi kwenye hoja za msingi... kama ccm ambayo imeshindwa kutengeneza serikali ambayo imeshindwa kutatua mambo ya msingi kama vile:-
1. usafirishaji kwa njia ya treni... njia ambayo ingesaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo a kupunguza mfumuko wa bei hususan mikoan na vijijin.

2. viwanda. hapa sisem sana coz kila mtu anajua na anaona ccm wamekuwa wa hovyo katika eneo hili.

3. rushwa.

4. elimu ya hovyo. ajabu sana eti sasa hivi tuna div 5 na hii imekaa kisiasa zaid na sio vinginevyo.

5. na mengine mengi.

hapa mtawezaje kutushawishi kuwa mnastahili kurudi madarakani? mnataka kura za wabunge, ili wakaendelee kulala bungen au wakaitikie ndiyo hata kwenye mambo wasiyoyaelewa?
Hoja ni kuwa maana ya dhana mabadiliko sio kukiondoa CCM madarakani. Maana yake ni hoja mbadala, sera mbadala na mikakati ya sera mbadala inayoelezeka kirahisi yenye nia ya kumkomboa mtanzania kweli na kulikomboa taifa kwa ujumla.
Unarudia yaleyale niliyoyasema juu huko kuwa nyie mnaelezea tu matatizo bila kuelezea sera zenu na mikakati ya kufanikisha hizo sera kwenye how, na pia kwenye kusema funds za kufanya yote hayo mtatizoa wapi????? Ili tuseme kweli haya ndo mabadiriko ya kuwachagua.
Kwa kukuaga tu ndugu umeendeleza porojo tu na tantalia tu na kuzidi kuthibitisha maneno ya Dr. Watson.
Alafu huoni aibu kuiweka hoja ya rushwa kwa ukawa saivi??????? Hivi hujui watoa rushwa wote na mafisadi ndo wako safari ya matumaini???????
 
Lord Denning...as noble as ur name suggests, nimekuwa nikiuliza hili swali kwa ndugu zetu bila kupata majibu staha sanasana watakutukana. Sisi Watanzania tunatia huruma na hasa tunaporuhusu ulofa utawale akili zetu. Tumerogwa walahi
Hawawezi kukujibu ndugu, na hili ndo janga kubwa tulilo nalo nchini mwetu saivi yaani ni siasa za jazba, mihemko, tantalila, matusi huku watu wakikimbia kujibu hoja za msingi za maswali magumu yanayotoa majibu mazuri kwa mustakabali wa nchi yetu.

Africa tuna shida sana ndugu yangu amini usiamini, na hawa watu ndo wanathibitisha kuwa tatizo la africa sio kunyonywa na wazungu bali ni fikra zetu kutopevuka kisawa sawa na kutuwezesha kufikiri kisawa sawa.
 
Hoja ni kuwa maana ya dhana mabadiliko sio kukiondoa CCM madarakani. Maana yake ni hoja mbadlra, sera mbadala na mikakati ya sera mbadala inayoelezeka kirahisi yenye nia ya kumkomboa mtanzania kweli na kulikomboa taifa kwa ujumla.
Unarudia yaleyale niliyoyasema juu huko kuwa nyie mnaelezea tu matatizo bila kuelezea sera zenu na mikakati ya kufanikisha hizo sera kwenye how, na pia kwenye kusama funds za kufanya yote hayo mtatizoa wapi????? Ili tuseme kweli haya ndo mabadiriko ya kuwachagua.
Kwa kukuaga tu ndugu umeendeleza porojo tu na tantalia tu na kuzidi kuthibitisha maneno ya Dr. Watson.
Alafu huoni aibu kuiweka hoja ya rushwa kwa ukawa saivi??????? Hivi hujui watoa rushwa wote na mafisadi ndo wako safari ya matumaini???????

Hizo ndio sera za chama. na wananchi wanaziona zina tija. sio kuwaahid waalim laptop wakati ili kuboresha elim waalim hawahitaj laptop.

swala la rushwa ni nyeti sana... na hao unaosem wapo kwenye safar ya matumain ni akina nani? kwa ushahidi upi?
 
Nani aliye mwadilifu ? Magufuli na Kikwete ndio hao hao. Kwenye serikali hii ya Kikwete zimechuliwa billions kwa kutumia magunia kutoka bank na hakuna chochote kilichofanyika....obviously Kikwete anahusika na Magufuli kwa jinsi anavyomsifia inaonekana Kikwete ni mmoja wa role model wake.

Tunapochagua kiongozi, nakubali uadilifu lazima uwe moja ya vigezo, lakini katika choices tulizo nazo, wote hawana uadilifu !. Wanaweza wakatofautiana kwa level, lakini sioni kama ina-make any difference, viongozi wetu wengi hawana uadilifu !. Njia nzuri ya kudeal na hili ni kuweka utaratibu wa kushughulikia mambo haya pamoja na mengine ya msingi kwa taifa letu. Rasimu ya Warioba ingekuwa msingi mzuri kuelekea huko lakini hao hao unaoona waadilifu ndio walioichakachua na watu pekee ambao wana possibility ya kuirudisha Rasimu ya Warioba ni UKAWA....

Analysis za mechi huwa zinatolewa na wataalamu waliobobea kwenye mambo ya soka kwa kutumia uzoefu wao na mazingira ya mechi husika. Kuna wakati wanapatia na kuna wakati wanakosea tena mara nyingine wanakosea sana !. Hayo ndio maisha, binadamu tuna limitations na hatujui future hivyo tunafanya maamuzi kwa uzoefu, taarifa tulizo nazo na common sense...

Kwa uzoefu wangu mimi katika maisha hapa Bongo na hali halisi ya kisiasa naona kwamba CCM ikipewa madaraka ni business as usual, hakuna jipya. With UKAWA naona uwezekano mkubwa wa possibilities kama nilivyozieleza kwenye post yangu uliyoijibu. Je, nina uhakika wa asilimia miamoja kwamba watafanya exactly kama ninavyotaka wafanye ?! Ofcourse not !. Mungu tu ndie anayejua exactly kitakachofanyika......Lakini mimi inabidi nifanye uamuzi kwa kutumia akili Mungu alizonipa na taarifa nilizo nazo na uzoefu wa maisha yangu......

Ni Either CCM yenye Magufuli au UKAWA yenye Lowassa. Kwangu mimi the choice is very clear......UKAWA !


Mabadiliko chanya huletwa na watu waadilifu wenye nia njema kwa maslahi ya watu wote. Kama tunakubaliana kwamba katiba iliyopendekezwa haifai kwa sababu ya kuchakachua maoni ya wananchi lakini pia kwa ushiriki wa Chenge? Basi itakua ni sahihi kwamba perspective ya mabadiliko kwa mujibu wa UKAWA ina walakini kwa kuongozwa na Lowassa asiye mwadilifu. Nadhani mlete mada hajagusia jambo hili, lakini kwa jinsi alivyowasilisha nadhani amelenga kuonyesha Watanzania wanashida kutolitambua jambo hili. Ikiwa lengo ni kuing'oa CCM madarakani hata ikimaanisha wanaofuata watafanya hovyo zaidi ya CCM, basi kweli tutakua waafrika wengi tuna shida vichwani mwetu. Mashabiki ni wengi na si wavumilivu. Kwa wanaopenda kuangalia match za mpira wa miguu hasa za Ulaya, mara nyingi kunakua na wasaa wa pre match analysis. Wasaa huu hutoa mweleko wa nani atashinda na namna gani kwa kuzingatia kikosi kinachocheza kati ya timu mbili. Wasaa huu unafaa pia utumike kwenye siasa zetu ili tupate yupi wa kumuunga mkono na tuweze kushinda vita dhidi ya UFISADI, KUMOMONYOKA KWA MAADILI na mengine mengi.
 
Mabadiliko chanya huletwa na watu waadilifu wenye nia njema kwa maslahi ya watu wote. Kama tunakubaliana kwamba katiba iliyope7ndekezwa haifai kwa sababu ya kuchakachua maoni ya wananchi lakini pia kwa ushiriki wa Chenge? Basi itakua ni sahihi kwamba perspective ya mabadiliko kwa mujibu wa UKAWA ina walakini kwa kuongozwa na Lowassa asiye mwadilifu. Nadhani mlete mada hajagusia jambo hili, lakini kwa jinsi alivyowasilisha nadhani amelenga kuonyesha Watanzania wanashida kutolitambua jambo hili. Ikiwa lengo ni kuing'oa CCM madarakani hata ikimaanisha wanaofuata watafanya hovyo zaidi ya CCM, basi kweli tutakua waafrika wengi tuna shida vichwani mwetu. Mashabiki ni wengi na si wavumilivu. Kwa wanaopenda kuangalia match za mpira wa miguu hasa za Ulaya, mara nyingi kunakua na wasaa wa pre match analysis. Wasaa huu hutoa mweleko wa nani atashinda na namna gani kwa kuzingatia kikosi kinachocheza kati ya timu mbili. Wasaa huu unafaa pia utumike kwenye siasa zetu ili tupate yupi wa kumuunga mkono na tuweze kushinda vita dhidi ya UFISADI, KUMOMONYOKA KWA MAADILI na mengine mengi.

Uadirifu wa kiuongozi hujengwa Kwa misingi miadirifu. Katiba na sheria adirifu.

Katiba ya wananchi MTU asiye mwadirifu aliikataa pale dodoma.

MTU asiye na uchafu anaongozwa na miongozo isiyo michafu.
Alipokuwa ccm mlishindwa kumwadilisha.
 
RIPOTI ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imeibua ufisadi mkubwa katika mamlaka za Serikali za mitaa,mashirika ya umma na serikali kuu.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutoa ripoti ya ukaguzi mjini Dodoma jana,Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad alisema ukaguzi huo umefanywa katika taasisi 176 za Serikali kuu, halmashauri 163 na mashirika ya umma 109.
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad.
Alisema usimamizi wa bajeti kwa mamlaka ya Serikali za Mitaa ulibaini kuwapo upungufu wa fedha za maendeleo Sh bilioni 312. 04, Serikali kuu Sh bilioni 1.8, fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambazo hazikutumika lakini hazikutolewa ni Sh bilioni 417.
Fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambazo hazikutumika ni Sh 203.13, alisema.
Alisema ripoti hiyo imebaini ukiukwaji wa matumizi ya utoaji wa misamaha ya kodi, kuendelea kwa mishahara hewa, usimamizi mbovu wa mipango miji,madeni ya Serikali katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).
Kuhusu misamaha ya kodi, Profesa Assad alisema iliyotolewa kwa mafuta yanayotumika migodini imefikia Sh bilioni 22.33 kati ya yale yaliyotakiwa kutumiwa na makampuni ya Geita Gold Mine na Resolute Tanzania Ltd na yalipelekamafuta hayo kwa wakandarasi wasiostahili msamaha wa kodi.
“Matumizi ya misamaha ya kodi kwa malengo tofauti na yasiyokusudiwa na kusababisha upotevu wa Sh milioni 392.7, iliyosababishwa na Kampuni ya Kiliwarrior Expenditions Ltd. ya Arusha iliyokuwa imesamehewa kodi ya Sh milioni 465.2 kuingiza magari 28 ambako kati ya Sh milioni 465.23, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeambulia kukusanya Sh milioni 72.5.
“Misamaha ya kodi ya Sh milioni 53.4 ilitolewa kwa Kampuni ya Kilemakyao Mountain Lodge Limited kwa ajili ya mradi wa ujenzi na upanuzi wa hoteli katika Kijiji cha Changarawe wilayani Meatu. Kampuni hii iliagiza magari matatu kwa kutumia msamaha wa kodi wa gari moja ya Hyundai Santa.Magari mengine ni BMW X5 na Toyota Land Cruiser Prado hayakufahamika yalipo,” alisema.
Alisema amebaini kudorora kwa uwekezaji wa Serikali kwenye makampuni mbalimbali ambako Serikali ina hisa kutokana na kuchelewa kuongeza mtaji, wakati inapohitajika kufanya hivyo kama ambavyo inataka kutokea katika benki ya NBC Ltd.
Mashirika ambayo yamegubikwa na kusuasua kwa usimamizi wa uwekezaji wa Serikali ni pamoja na Shirika la Ndege Tanzania (ATC),Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na Shirika la Reli Tanzania (TRL) ambayo yote yanahitaji ruzuku kutoka serikalini.
Mashine za EFD’s
Katika ukaguzi wa malipo, CAG amebaini kampuni binafsi hazitumii mashine za elektroniki za kutolea stakabadhi na hivyo kusababisha Sh bilioni 4.4 kutokuwa na stakabadhi hizo wakati taasisi za Serikali zimefanya malipo yenye thamani ya Sh bilioni 4.6 bila kutumia mashine hizo, mbali na halmashauri 22.
“Katika suala hili, TRA ilitoza faini ya Sh milioni 440.8 kwa wafanyabiashara walioshindwa kutumia EFD’s ambako milioni Sh 72 zililipwa na hivyo kufanya bakaa ya Sh milioni 369 ambayo haikulipwa,” alisema Profesa Assad.
Mapato ya ndani
Ukaguzi wa mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2014, ulibaini taasisi zilizo katika mpango wa kubakiza maduhuli na hazikurejeshwa zilikuwa Sh bilioni 32.74, hivyo kuathiri utekelezaji wa kazi zilizokuwa zimepangwa na taasisi husika.
Mishahara hewa
Ukaguzi wa CAG umebaini wafanyakazi walioacha kazi na kustaafu wameendelea kulipwa mishahara kupitia akaunti zao, licha ya Serikali kuwekeza katika mfumo wa Lawson kama njia ya kudhibiti hali hiyo.
Pia fedha za makato ya mishahara yao zimeendelea kupelekwa kwenye taasisi kama vile Bima ya Afya, TRA na mifuko ya hifadhi ya jamii.
Kutokana na hali hiyo mpaka sasa fedha zilizolipwa ni Sh milioni 141.4.
Alisema katika halmashauri 36, Sh bilioni 1.01 zililipwa kwa watumishi waliotoroka kazini.
Wizara ya ujenzi
Ripoti hiyo imeitaja Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Waziri Dk.John Magufuli kuwa inaongoza kwa kudaiwa na wakandarasi.
Alisema mpaka anatoa ripoti hiyo wizara hiyo inadaiwa Sh bilioni 800.
Lakini jambo la kushangaza wizara hiyo pia imetumia Sh bilioni 250 nje ya bajeti husika.
UKAGUZI WA MIRADI
Alisema ukaguzi wa miradi ya maendeleo mwaka 2013/14 ulihusu miradi mikubwa mitano.
Miradi hiyo ni Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP), Mfuko wa Afya (HBF), Mfuko wa Barabara (RF), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) na miradi mingine ambayo inatekelezwa wizara, idara na mashirika ya umma.
“Katika ukaguzi wa hesabu za halmashauri 162, tulibaini Sh 52.7 zilizoidhinishwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo hakikutolewa hivyo kuathiri utekelezaji wa miradi iliyokusudiwa.
“Hii imechangia malipo yaliyocheleweshwa kulipwa mwaka wa fedha 2013/14,” alisema.
Alisema ukaguzi ulibainia fedha zilizotolewa na kutotumika ndani ya mwaka wa fedha 2013/14, ni Sh bilioni 495.9 ikiwa ni asilimia 25.45 ya fedha zote za miradi.
“Sababu kubwa ya bakaa hii ni pamoja na ucheleweshaji wa kutoa fedha kwa wadau wa maendeleo na mchango wa Serikali, mchakato mrefu wa taratibu za ununuzi, uwezo mdogo wa halmashauri wa kutumia fedha za miradi na wafanyakazi wachache wenye utaalamu katika kusimamia fedha za miradi.
Ocean Road
Alisema Taasisi ya Ocean Road inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa vya uchunguzi na matibabu kwa wagonjwa wa kansa.
“Mahitaji halisi ni mashine 36, wakati zilizopo ni mashine 11 tu ambazo kati ya hizo, mashine tatu zimeshapitwa na wakati zinangoja kuondolewa na mashine nne zinahitaji kufanyiwa ukarabati.
“Hali hiyo inasababisha ucheleweshaji wa matibabu hususan mionzi kwa wagonjwa ambako humchukua mgonjwa zaidi ya miezi mitatu kutibiwa wakati viwango vinavyokubalika kimatibabu ni chini ya wiki mbili,” alisema.
Aliishauri Serikali kuchukua hatua za haraka kupunguza ama kuondoa kabisa tatizo la vifaa katika taasisi hiyo.
Mipango Miji
Alisema ripoti yake imethibitisha halmashauri 148 ambazo ni asilimia 80 zinaendelezwa bila kuwa na mipango kabambe inayoweza kutoa miongozo wa shughuli zote za uendelezaji wa miji nchini.
“Halmashauri 96 au asilimia 65 kati ya halmashauri 148, hazijawahi kuandaa mipango kabambe tangu zianzishwe,” alisema.
Alisema maeneo mengi yanaendelezwa bila kufuata mipango kabambe iliyopo.
Usambazaji dawa
Alisema kwa mujibu wa ukaguzi, imebainika tathmini ya makadirio ya uhitaji wa dawa na vifaa tiba muhimu katika vituo vya afya haufanyiki kwa uhakika.
Alisema hali hiyo inatokana na asilimia 50 ya ripoti zinazohitajika za makisio ya dawa za vifaa tiba muhimu kutoka halmashauri za wilaya kutowasilishwa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kama inavyotakiwa.
“Imebainika asilimia 54 ya oda zinazopokelewa na MSD kutoka bohari za kanda ni kuanzia muda wa siku 14 kulingana na muongozo wa MSD.
“Hii imesababisha kutetereka kwa mtaji kushuka kwa zaidi ya asilimia 69 kutoka Sh bilioni 81 mwaka 2008 hadi Sh bilioni 25 mwaka 2013.
“Hii imechangiwa na ongezeko la deni la Serikali ambalo limeongezeka zaidi ya mara nne kutoka Sh bilioni 14 mwaka 2008 hadi Sh bilioni 69 mwaka 2014,” alisema CAG.
Kutokana na hali hiyo, CAG alipendekeza uboreshaji wa upatikanaji wa dawa na vifaa muhimu katika vituo vya huduma ya afya.
“Ninapendekeza Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na MSD kutathimini hali ya mtaji wa uendeshaji wa mfumo mzima wa makisio na usambazaji wa dawa na vifaa tiba muhimu kwa lengo la kutatua tatizo la uhaba wa dawa,” alisema.
Wastaafu,watumishi
Kuhusu wastaafu, ripoti yake imegundua Sh milioni 5.43 zimelipwa kama posho na pango kwa watumishi walioko ubalozini nje ya nchi.
“Hii ni kinyume na kanuni za kudumu za utumishi, fedha hizo zinazoendelea kulipwa kwa wastaafu hao ambao hawafanyi kazi si zingeweza kulipwa kwa wafanyakazi?” alihoji Profesa Assad.
Majengo ya Serikali
Alisema ukaguzi huo umebaini majengo mengi yanayomilikiwa na Wakala wa Majengo yalijengwa kwa zaidi ya miaka 25 iliyopita, hali inayosababisha majengo hayo kuwa katika hali isiyoridhisha.
“Ilibainika hakuna utaratibu madhubuti wa usimamizi wa ukarabati wa majengo ya Serikali, hii ni kwa kuwa mikoa mingi haifuati taratibu zilizopo za ukarabati wa majengo ya Serikali.
“Kati ya mikoa sita iliyotembelewa hakukuwa na mkoa hata mmoja ulioweza kufanya marekebisho ya viwango vilivyowekwa vya ukarabati wa majengo ya Serikali.
“Pia hakukuwa na nyaraka kama vile vitabu vya rejista vya kuweka kumbukumbu ya hali ya ukarabati wa majengo katika ofisi zao na pale ukarabati unapotekelezwa, hutekelezwa bila kuwa na mpango kazi uliowekwa,” alisema.
CAG alipendekeza Wizara ya Ujenzi na Wakala wa Majengo kuweka sera ya ukarabati wa majengo yanayomilikiwa na Serikali na kufuatilia utekelezaji wake ikiwa ni pamoja na kuweka kumbukumbu sahihi ya majengo hyo.
Mifumo ya uhifadhi
Alisema katika ukaguzi uliofanyika ilibainika mipango ya usimamizi wa mazingira iliyoandaliwa na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC), haitilii mkazo suala la viashiria hatarishi.
“Ilibainika NEMC halikutoa adhabu stahiki kwa mujibu wa sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 kwa makampuni mbalimbali ya migodi inapokiuka sheria hiyo.
“Na hata pale adhabu zinapotolewa hakukuwa na ufuatiliaji mzuri kuweza kubaini kama adhabu husika imetekelezwa ipasavyo,” alisema.
Alisema pia halmashauri hazifanyi ufuatiliaji wa shughuli katika migodi hali inayosababisha NEMC kushindwa kuwa na picha halisi juu ya utunzaji mazingira katika migodi nchini.
“Vilevile imebainika kuwa hakuna utaratibu wa shughuli za usimamizi wa mazingira migodini, NEMC ilishindwa kuratibu kwa ufanisi ushirikiano wa wadau mbalimbali katika usimamizi wa mazingira migodini,” alisema.
CAG amependekeza NEMC kutathmini utekelezaji wa mfumo ulipo pamoja na kuanzisha uandaaji wa taarifa itakayoonyesha hali ya mazingira katika sekta madini na kutoa adhabu stahiki kuzuia uvunjaji wa sheria kutojirudia.
Huduma za ugani
Alisema katika uchunguzi huo, Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika hawajasambaza kwa ukamilifu miongozo inayohusiana na utoaji wa huduma za ugani kwa maofisa ugani.
“Pia hakuna vitabu vya rejista na ratiba zinazoonyesha utendaji kazi wa maofisa ugani hali inayosababisha utekelezaji usioridhisha wa mipango na miradi ya mendeleo ya kilimo,” alisema.
Alisema ripoti hiyo pia ilibaini kuwapo teknolojia duni za shughuli za ilimo, ucheleweshaji wa fedha na kusababisha huduma duni za ugani na ufuatiliaji na tathimini za utoaji wa huduma za ugani kutofanyika ipasavyo.
“Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika zifanye tathmini ya huduma ya ugani na kuangalia na jinsi gani hizo zinaweza kuboreshwa katika maeneo ya uandaaji wa mipango, uratibu, uwezeshaji, ufuatiliaji na utoaji wa mrejesho ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo,” alisema.
Kauli ya PAC
Akizungumzia ripoti hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Amina Mwidau alisema inaonyesha mapato ya serikali bado yanapotea na kulitaka Bunge lijalo lipambane na hali hiyo.
“Kwa ujumla hali ni mbaya, kwa mfano Wizara ya Ujenzi ililidanganya Bunge lililopita, angalia Tanroads (Wakala wa Barabara Tanzania), wanaongoza kwa madeni. Lakini pia Kitengo cha Maafa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kimetumia fedha vibaya na hili lazima tulishughulikie haraka” alisema Mwidau.
(CHANZO: MTANZANIA)

RIPOTI YA CAG IMEIBUA UFISADI MKUBWA – Global Publishers
 
Mkuu Abunuas umesoma Tosamaganga...? Hilo neno nyumbu tumelitumiaga sanaaa Tosaa ndugu umenikumbusha mbali sanaa teh teh

mkuu hata sijasoma tosa japo nimewahi kuishi maeneo karibu. hata hivyo ninamarafiki wengi tu waliosoma tosa. hilo neno nyumbu nimelipata humuhumu. siunajua tena kwenye mitandao kila moja na vionjo vyake. Anyway, hata hivyo nikatika kuburudishana tu. sina maana mbaya kivile maana huku mitaani tunaishi kwa amani na furaha bila kujali itikadi zetu kivyama, kidini, kikabila wala kikanda. tunafurahi pamoja tukiwa na furaha kama maharusi nk na tunahuzunika pamoja tukiwa kwenye misiba.
ya humu mitandaoni huwa nayaacha humuhumu.
 
Ubinafsishaji, kuuza Nyumba za serial I n.k
vitu kama kuuza nyumba za serikali sio sera za chama bali maamzi ya kipuuzi ya watu. na hata sera za ubinafsishaji sio mbaya, tatizo watekelezaji wengi wao ni ovyo. labda ninachoweza kukuambia ni kuwa ccm kunawachumia tumbo na wabinafsi wengi kuliko wazalendo. hapo ningekuelewa.
 
Back
Top Bottom