stev30sudi
Member
- Feb 3, 2012
- 48
- 18
Amani iwe nanyi wadau,
Kwa kipindi sasa kuna jambo limekuwa likiniwazisha sana hasa Kwa wapenzi wa Chadema, ukawa na baadhi ya washabiki wao pale wanapolitumia kwenye kujenga ushawishi neno Tunataka mabadiliko. Hili ni neno ambalo wamekuwa wakilisema kwa kipindi sasa wakiwa wanatarget kuwa wanapolisema tu basi maana yake kuu ni kuiondoa CCM madarakani.
Napenda kutoa historia fupi ya umaarufu wa hili neno ambayo najua wengi wenu humu mnaifahamu. Neno hili kwa lugha nyingine CHANGE lilipata umaarufu hasa pale raisi wa sasa wa Marekani Barack Obama alipolichagua kama kaulimbiu yake kwenye mchakato wake wa kisiasa katika kuutafuta uraisi wa Marekani mnamo mwaka 2008. Neno hili alilichagua na kulitumia akiwa hamaanishi kuwa wamarekani wanataka change ya kubadiri chama kwa sababu alianza kulitumia tangu kwenye mchakato wa ndani wa chama chake yaani Democrats akiwa anamaanisha wamarekani wanaitaji mabadiriko ya kisera za kiuchumi, kijamii, kiulinzi na usalama na hata za kimaisha. Huu ndo msingi wa neno CHANGE/MABADILIKO KWENYE SIASA. Hata mwalimu Nyerere aliposema watanzania wanataka mabadiriko wasipoyapata CCM watayapata nje ya CCM ukiangalia ile hotuba kuna vitu aliviongelea na vilikuwa vinne kikiwemo Rushwa na vingine vitatu, na ndo baadae akasema kuwa watanzania wanaitaji mabadiriko kwenye ivo vitu wa wasipovipata CCM watavitafuta nje ya CCM. Hii inamaanisha mabadiliko kwenye siasa sio kubadirisha vyama.
Nimeamua kutoa haya maelezo mafupi nikiwa naionea huruma jamii hii ya watanzania huku nikiwa nawaza mawazo ya Yule Dr wa kizungu anayejulikana kama Dr. Watson aliyesemaga kuwa ana wasiwasi na akili ya mtu mweusi.
Ninasema haya kwa sababu kwa jinsi wafuasi, wapenzi na wanachama wa Chadema wanapolitumia hili neno wao wanachowaza kikubwa ni kuwa maana ya mabadiriko ni kukiondoa chama kinachotawala madarakani wakati kiuhalisia hali haiko ivo. Inaniuma zaidi eti wanaposema hawa wamekaa miaka 50 na sasa tuweke wengine as if uongozi ni kujaribu hasa wan chi. Kweli Africa we have a long way to go.
Dhana ya mabadiliko/ change inapotumika kisiasa inamaanisha ni mabadiriko KWENYE SERA HASA ZA KIUCHUMI, KIJAMII NA KISIASA, INAMAANISHA MABADIRIKO KWENYE MTINDO WA KUENDESHA MAMBO HASA YA KIUTAWALA ILI JAMII IONE KITU TOFAUTI HASA KWENYE MAISHA YAO YA KILA SIKU NA SIO KUHUSU KUBADIRI CHAMA TU.
Kuna watu watatu nimewasikiliza wiki hii, wa kwanza ni Ndugu Humphrey Polepole na wa pili na Dr Kitila Mkumbo na wa tatu ni Jenerali Ulimwengu ambaye nimemsoma kwenye gazeti la leo la Raia Mwema. Humphrey amezungumzia kwa mapana sana tangu wiki iliyopita na hadi wiki hii na kusema kweli nimefarijika sana kuona jamii ya Tanzania ina mtu mwingine mwenye upeo wa tofauti na ulio mbali kama wake(wa kwanza kwangu ni Prof Muhongo) huyu mtu bila kumungunya maneno ameweza kuelezea kwenye vipindi alivoalikwa kinagaubaga kuwa Tanzania inaitaji mtu wa aina Fulani na mwenye uwezo Fulani. Kwa Dr Kitila alisema wazi kuwa vyama vya upinzani vinaonekana kuwa dhumuni lao kuu ni kushika madaraka tu yaani kukamata dola ndo mana wanasema tutumie silaha yeyote ile( kwa hapa nikapata picha kuwa kumbe hawa viongozi lengo kuu sio kuja na sera mbadala zinazoonyesha ni kwa jinsi gani watamkomboa mtanzania na nchi yetu mama Tanzania). Kwa Jenerali Ulimwengu amegusia kwa jinsi gani ushabiki usio na maono na upenzi wenye kupapalikia mambo unaoliangamiza taifa letu na siku ya mwisho hatupati kitu tunachotakiwa kupata.
Hawa wachambuzi watatu wameugusa sana moyo wangu na kwa uzoefu wangu nimegundua kuwa nchi hii inaharibiwa na wanasiasa kwa sababu fikra zao ndo zinaiharibu wafuasi wao ambao ni sehemu ya jamii ya watanzania. U chambuzi wa hawa watu umenifanya nitafakari sana maneno ya Dr Watson kuwa mtu mweusi ana matatizo Fulani kwenye akili yake. Kwa sababu kiuhalisia Chadema/Ukawa hawajajipambanua kisera, Lowassa hajajipambanua kisera hasa kujibu how question yaani atafanya nini na kivipi na hata fedha atapata wapi zaidi ya kusema tu Fulani kakuta sukari bei Fulani, kakuta kitu Fulani bei Fulani na sasa ivi kaacha kikiwa bei Fulani alafu wapenzi wake wanashangilia tu raisi raisi raisi bila kupembenua vizuri ni nini kasema ni kwa nini iwe yeye kwa sera zake/utekelezaji wake tofauti na mwingine.
Kitu kinachoniumiza zaidi ni pale ninapojiuliza kama tatizo kuu la nchi hii ni ufisadi, utumiaji mbaya wa madaraka, uvivu, porojo, kuabudu wenye mali, wizi, porojoporojo na unafiki hivi mtu ambaye kwa miaka yake tuliyomfahamu na kumuona kuwa ana mambo mengi sana ambayo ni matatizo kwa Tanzania yet u ndo huyu apewe nchi yetu aiongoze?????? Kama jibu ndio basi kweli Dr Watson atakuwa yuko sahihi asilimia 100 kuwa ana matatizo na akili ya mtu mweusi.
Nawatakia siku mpya njema wadau.
Mungu awabariki.
Watanzania bado si waelewa wa nini wanachohitaji, watakipataje na changamoto za kufikia maendeleo. Wamekaririshwa nyimbo kuimba "tunataka mabadiliko" bila hata kuelezwa sera za kufikia mabadiliko.