Nini maana na matumizi ya neno ''mrahaba''

mzeemitomingi

JF-Expert Member
Aug 3, 2014
267
74
Habari zenu wadau ,hope mnasonga salama.

Naomba kufahamu kwa wenye uelewa juu ya neno mrahaba kama linavotumika sehemu mbalimbali.

Mimi sijawahi kukutana na hili neno huko shuleni.

Mwenye tafsiri msaada.
 
Neno sahihi ni MRABAHA. Hii ni sehemu yafaida ambayo analipwa mtu na yule anayetumia kitu chake. Kwa mfano, Accasia wanatumia migodi yetu, kwa hiyo wanatakiwa kulipa serikali kiasi fulani cha faida wanayopata. Ukiandika kitabu, ukapeleka kwa publisher, huyo publisher atakapouza, atakulipa sehemu ya faida anayopata. Huo ndio mrabaha (sio mrahaba).
 
sante sana kwa marekebisho na tafsiri ujinga umepungua tayari
sante sana

Sent from my HUAWEI MT7-L09 using JamiiForums mobile app
 
mapato =faida ? kwa mantiki hiyo apo juu

Sent from my HUAWEI MT7-L09 using JamiiForums mobile app
Hapana! Yani mfano wamechenjua dhahabu yenye thamani ya bilioni moja, wakatupa mrabaha wa 4% hapo tutapata milioni arobaini. Sasa hizo milioni 960 walizobakiwa nazo ndipo watatoa gharama zao za uendeshaji, then wakipata faida watalipa corporate tax inayotokana na faida ambayo huwa ni kati ya 25%-30%...
 
duuu sante unajua kwenye hi sector %kubwa ya akina mie hatujui calculation zinaendaendaje ...yaani mi ndio leo najuzwa apa ...sante sana

Sent from my HUAWEI MT7-L09 using JamiiForums mobile app
 
Neno sahihi ni MRABAHA. Hii ni sehemu yafaida ambayo analipwa mtu na yule anayetumia kitu chake. Kwa mfano, Accasia wanatumia migodi yetu, kwa hiyo wanatakiwa kulipa serikali kiasi fulani cha faida wanayopata. Ukiandika kitabu, ukapeleka kwa publisher, huyo publisher atakapouza, atakulipa sehemu ya faida anayopata. Huo ndio mrabaha (sio mrahaba).
kumbe??
 
Neno hili ukosewa hata na wasomi badaka ya MRABAHA wao utamka na kuandika MRAHABA ambayo siyo sahihi.
Mrabaha ni sehemu ya faida au gawio la faida kutokana na biashara au uwekezaji fulani. Mara nyingi uhusiana na uwekezaji au makampuni makubwa ya uwekezaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Murabaha ni mauzo ambayo yana makubaliano ya faida. Kiufundi, ni mkataba ambayo muuzaji anaweka bayana gharama na faida.

Murabaha hutumika kama moja ya njia za kuwezesha kifedha katika mabenki yanayofata mfumo wa kibenki wa Kiislam (Islamic Banking).

Soma zaidi: Murabaha - Wikipedia
 
Back
Top Bottom